Mambo kadhaa yakumfanyia mwenza wako kumsaidia kuvishinda vishawishi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo kadhaa yakumfanyia mwenza wako kumsaidia kuvishinda vishawishi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,204
  Likes Received: 3,995
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kila mwanaume anapaswa kujua nini kinachomfanya mwanamke/msichana apagawe kunako sita kwa sita, hali kadhalika mwanamke anapaswa kufahamu mambo kadha wa kadhaa ambayo akimfanyia mwenza wake atamfanya avishinde vishawishi vya kumsaliti. Hii inamaanisha nini?

  Inamaanisha kuwa, kila mwanaume na mwanamke anapaswa kufahamu jinsi gani wanaume walivyo tofauti na wanawake.

  Mwanamke anapaswa kufahamu kwamba wanaume huamsha hisia za mapenzi kutokana na kile wanachokiona. Hivyo pindi anapoona msichana mwenye shepu akiwa amevaa nguo inayoiweka shepu yake bayana, ghafla hisia kali za mapenzi humjia, hata kama anajua baadhi ya utu ama tabia zake mbaya.

  Kuona tu jinsi binti alivyoumbika, hiyo ni tosha kwake kumfanya ahitaji kuwa naye faragha na hapo ndipo atakapoanza kupigana na mhemuko wa mwili wake kujizuia kuingia katika kishawishi cha kufanya ngono na mrembo aliyemuona.

  Kwa upande mwingine, wanaume wanapaswa kufahamu kwamba wanawake wapo tofauti. Hisia za mapenzi za mwanamke huamka pindi mwanaume anapomtimizia mahitaji yake ya moyo wake. Huhisi kupagawa pindi anapokutana na mtu ambaye anaweka kipaumbele mawasiliano baina yao na kujali hisia ama mawazo yake.

  Kwa mwanamke muelewa mara nyingi muonekano wenye mvuto pekee kwake haumuingizi kwenye vishawishi kwa kiasi kikubwa kama ilivyo kwa wanaume. Kitu pekee kwake kinachoamsha hisia zake za mapenzi kwa haraka zaidi ni kuwa na mwanaume anayeongea naye, kumsikiliza, kuthamini mawazo yake, na kufikiria mahitaji yake muhimu. Pindi mwanaume wa aina hii anapomwambia “ Nakupenda..muache mumeo tutumia usiku wa leo pamoja,” huhitaji kutumia busara na hekima kuweza kuvishinda vishawishi vya kutoa penzi kwa mwanaume wa aina hiyo!


  Aidha, watu wengi walio katika mahusiano hujikuta wakikumbwa na matatizo kadha wa kadha wawapo faragha kwa sababu tu mwanaume na mwanamke hawajui tofauti iliyopo baina ya mwanaume na mwanamke. Mfano, mwanamke anaweza kupanda kitandani akiwa amevaa pajama ambalo halioneshi shepu yake huku mwanaume akitamani kumuona mpenzi wake akiwa amevalia nguo ya usiku inayomtia hamasa ya mapenzi ama kumuona akiwa hajavaa chochote! Anahitaji kumuona mpenzi wake vema hivyo kumuona akiwa katika vazi lisilompa nafasi hiyo kunamkwaza.

  Hapa kosa kubwa lipo miongoni mwa wanawake wengi ni kuwa “ Ameshaniona mwili wangu zaidi ya mara 1000.” Hivyo kwao kumpa nafasi mwenza wake kuuona mwili wake hakuna umuhimu.

  Kimsingi wanawake wa namna hii ndio mara nyingi hujikuta waume zao pindi wanaporejea nyumbani huishia sebuleni na kusoma gazeti. Anajihisi kuchoka, hahitaji mkewe ama mtoto amsumbue na akikalibishwa mezani kwaajili ya chakula huongea maneno yasiyozidi kumi.

  Hufanya haya yote si kwa sababu anamchukia mkewe la hasha bali hugeuka kuwa mbinafsi anayetaka kutumia muda wake kujipumzisha na kufikiria mahitaji yake na si ya mwenza wake.

  Hatua hiyo ikijitokeza baina ya wapendanao mambo huharibika, hamasa ya mapenzi kwa mmoja wao hutoweka kwani inapofika wakati wa kwenda kujipumzisha kitandani. Mwanaume anapomuona mwenza wake akitoka bafuni akiwa na kanga moja iliyomshika vema maungo yake, mapigo ya moyo na damu humuenda mbio akitamani kumkumbatia bibie ili apate kitu roho inapenda!

  Wakati mwanaume akiwaza hayo, mambo huwa tofauti kwa mwanamke kwani hutawaliwa na maswali kadhaa kama “ Hivi ni kweli ananipenda? Namashaka. Haongei nami wala kunisaidia kwa lolote. Anachotaka ni kunitumia kama chombo cha starehe tu huyu.”

  Hivyo basi, mwanamke atamuachia mwenza wake mwili autumie atakavyo kutimiza haja zake, lakini hatafika kilele kamwe kwani hatahisi anapendwa bali anatumiwa kama chombo cha starehe.

  Hata hivyo, pindi mwanaume atakapokuwa akijipa raha toka kwa mwenza wake huyo, atatawaliwa na woga kwa sababu ataona wazi kuwa bibie hafurahii tendo la ndoa. Hivyo atajiuliza maswali mengi “ Kwa nini nimeshindwa kumpagawisha mamaa? Je, nyeti yangu ni ndogo?”

  Hapa ndipo mwanamke anapotakiwa kumueleza bayana kuwa, “ Uume wako upo sawa ila mawasiliano yako kwangfu ni finyu.”

  Kimsingi mwanaume anaporudi toka kazini anapaswa kuzungumza na mwenza wake, kujenga urafiki naye, kumuoneshe kuwa anamjali na kuthamini utu wake na usimfanye ajione kama mtu baki.

  Aidha, mwanaume anapaswa kumueleza mwenza wake kuwa, “ Unapokuwa kwenye jumuia, vaa nguo ambazo hazitaamsha hisia za mapenzi kwa watu baki, lakini unapokuwa nyumbani hakikisha unavaa nguo hizo kwaajili yangu tu.”

  Kufanya hivyo kutamueleza mumeo kuwa, “unampenda yeye tu na wanaume wengine hawana nafasi katika moyo wako!

  Mwisho nimalize kwa kusema kuwa, wanawake huamsha hisia za mapenzi kwa wanaume ambao huyapa kipaumbele mawasiliano, lakini mawasiliano hayo humpagawisha zaidi yakiwa ya kirafiki zaidi (fanya kama unawasiliana na rafiki yako, usiogope kumchombeza na utani inapobidi) na pia hukoshwa na wanaume wanaowajali.

  Kwa upande wa mwanaume, yeye hisia zake huamka pindi anapoona shepu (wapo wanaopenda wenye figa za kibantu na wengine za kimiss).

  Hivyo, kama mmefanikiwa kupata watoto wa wa kike hakikisheni mnawaeleza kuwa, nguo za aina fulani huamsha hisia za mapenzi kwa wanaume, kwa hivyo waache kuzivaa nyumbani hata mitaani kujiepusha na vishawishi.Mashosti: Mambo kadhaa yakumfanyia mwenza wako kumsaidia kuvishinda vishawishi!
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,586
  Likes Received: 762
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,944
  Likes Received: 5,091
  Trophy Points: 280
  Thanks!!!!!!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,369
  Likes Received: 34,094
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. B

  Bi nyakomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 387
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  well said. Thanx
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,194
  Likes Received: 1,590
  Trophy Points: 280
  Leo!
  Mhhh! Happy eid sheikh
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  hadi dakika hii sijapata mwaliko, leo patachimbika.

   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,617
  Likes Received: 38,941
  Trophy Points: 280
  Kaunga yaelekea una kiu na elimu dunia..............
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Root

  Root JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 22,434
  Likes Received: 7,961
  Trophy Points: 280
  heheheheh nice sana
  Kuna wengine wakiwa majumbani wanavaa nguo ambazo hata kuwatamani unashindwa ila wakitoka mmmmh huko barabarani whistles
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,114
  Likes Received: 2,216
  Trophy Points: 280
  Safi sana mkuu Mzizimkavu
   
 11. N

  Neylu JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,647
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Asante kwa darasa zuuri..
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,161
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Darasa zuri sana!!kuongezea wanaume wanapagawa na shape nzuri ikionekana kutokana na mavazi...siri kubwa kwa wenzetu ni mazoea na mwanaume,akishaweza kuwa nae karibu sana wana chat sana,mada mbali mbali,wanajadili mambo mengi kwa upana wake,,,wanapata kuwa karibu sana...hapo ndipo hatari inaposogelea..wataombana kutoka kwa dinner...taratibu wanajenga penzi la siri...na linakuwa imara sana....
   
 13. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekubali tatizo utekelezaji, we lack total committment
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,743
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Nimekukubali mkuu...............................................
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,447
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mkuu Mzizi Mkavu, nimekukubali uliposema mwanamume anatoka kazini hana muda na mkewe kweli hapo huwa inaleta picha sio nzuri
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ansate kwa somo mzizimkavu ni darasa lililojitosheleza kabisa
   
 17. peri

  peri JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  lol, mzizimkavu umetoa somo tosha sana.
  Ni kinadada wachache wanafaham hayo mambo, wengine wanazani kutembea nusu uchi mtaani ndo dili wakati kwa waume zao wanawavalia magauni.
  Big up mkuu.
   
 18. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 13,751
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  ah sa'anaa,mwanamke shurti uvutie na kuita unapoingia kulala na mumeo,nguo za stara wanawake tuvae tukiwa hadharani jamani,upo faragha na baba chanja unapiga gauni zitooooooo!ndani c*****i kuubwah,na sidiria juu kha!kisa nini eti mi nimeshazaa!hata huo mkono kukugusa aanzie wapi?manake ndo umejikoki mwili mzima!baba wa watu anaanza kufantasize na nyonyo la sekretari au aliloona kwneye foleni barabarn likiwa limeachwa jeuppeeeeeeeeee ndo analala.kuzaa na kuwa na ndoa ya muda mrefu si sababu ya kuacha kumtega mumeo.be sexy always,always haijalishi umbo lako ni la aina gani!manake utalilia hipsi ndo zinatega mwanaume angeziataka angemuo mwenye hipsi dada,jiamini na jikubali tht ur waht u r nad ur hubbie loves u the way u r.USE WHAT YU HAVE TO GET WAT YU NEED!unahitaji attention ya mume wako tumia mwili wako,huna hipsi ila una jicho,huna jicho basi una rangi,huna **** basi una mguu,huna sura nzuri kwa unavoamni basi una lipsi zinazompa wehu,huna miguu ya bia basi una kauli nzuri,huna ufundi wa kukata kiuno basi una ufundi wa kupika au kutandika kitanda,use them to capture ur man!haya mambo wala hayana degree.jipange mama jipange!mpe mumeo sababu ya kuwahi kurudi nyumbani!manake anajua atapokelewa nawe ukiwa unanukia mlangoni,yani jitie tashtiti za kike hapo mwenyewe ah !kesho anajua nikichelewa leo yale ya jana siyakuti!

  na nyie kina baba hebu kuweni na busara hiyo ndoa/mahusiano ni yenu wote wawili,ukiona mkeo anafanya visivyo jaribu kukaa nae chini kwa upendo na kumulekeza la kufanya,au mletee hivo vitu unataka akuvalie mnapokuwa kwa bed,lakini pia wasifieni wake zenu,tell her that she rock!tell her leo mke wangu uko bomba ile mby polepole atajifunza hakuna anayetaka kutokuwa na ndoa yenye amani jamani .wasaidieni wake zenu kujitambua.ukikaa na kusubiri ajue tu mwenyewe wengine sio wabunifu kiasi hicho na tayri ni mkeo!unafanyaje?ukinyamaza manake ni wewe unazidi kujikosesha furaha!
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,138
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Mkuu MziziMkavu asante sana kwa somo zuri
  Kwa wenza ni somo moja zuri sana maana
  Asante sana mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanza kabisa naomba nitumie fursa hii kukushukuru kaka MziziMkavu, pili naomba nijitupie misifa kwani haya yooote uliyoelezea namfanyia Mr Rocky na ndo maana hafukuti si eti bebiii eee??we wala ukiwaona wenye mishepu huwa damu haichemki.....lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...