Mambo juu ya mambo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo juu ya mambo...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Camfu, Jan 22, 2009.

 1. C

  Camfu Member

  #1
  Jan 22, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  wapenzii, naomba ushauri wenu. Nilifahamiana na dada x nilipokuw alikizoni tena ilikuwa kwa bahati tu, tukaachiana namba na kumbe kwa vile wote tulikuwa likizoni hatukuweza kukutana so kila moja akaendelea na safari yake. Tukawa na uhusiano mzuri wa kwa njia ya email na hivi pole pole kuanza kujuana, naye akawa ananielezakuhusu mchumbake ambaye kwa kweli inaonyesha hampendi tena. Sababu zilizomfanya asimpende tena ni kuwa akiwa Tanzania jamaa alikuwa na mshikaji mwingine kitu ambacho x alikitambua, achana na hilo, jamaa tayari anamtoto na yule mama mtoto bado anauhusiano naye, zaidi ya hayo huyo jamaa tayari amezaa na mdogo wake huyo mama mtoto wake, hayo yote x anayafahamu. Kwa kuongezea tu tofauti zao za kimadhehebu hazipokeleki katika familia zao. x alitokea kunipenda ghafla nami kwa kweli nampenda. X amemwambia jamaa kuhusu nia yake ya kuacha uhusiano naye lakini jamaa amekuwa akimtishia kumuua na ujiua mwenyewe, kadili yake y huyo jamaa ni mara kibao tu ameshachukua bunduki na kutaka kujilipua... nisiseme mengi kwani siwezi kuyasema yote, my issue is, huyu jamaa ameahidi kuja kumuua dada x na kisha kujiua mwenyewe, sasa bado yuko likizoni na mbioni kusafiri, je nifanye nini ili dada x asipoteze maisha? kingine dada x alishaanza kufanya mipango ya kuja kunitembelea kumbe jamaa kampiga mkwara na x hana nguvu tena, je nifanyeje ili kumotoa hofu x? zaidi ya hayo mimi na x bado hatufahamiani sana lakini tayari tuna nia kuoana kumbe kwa upande wangu naona tayari uhusianowake na jamaa yake ni kikwazo kikubwa kwangu, nifanyeje? Naomba ushauriwenu wadau!
   
 2. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  We Camfu... yale mengine 'yalookukuta' ushatatua??? mwanaweeeeeeeeee!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Sikiliza moyo wako unakuambia nini.
  Tishio la kujiua si la kweli...labda kama upeo wa huyu njemba ni mdogo sana au hana self esteem au ni mgonjwa wa akili.Chunguza vyote hivyo kisha amua.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hivi kumbe mtu akitaka kujiuwa huwa anasema??? We endelea na demu wako hakuna kitu hapo wauwaji huwa hawasemi bana eh!!!
  yaelekea jamaa analazimisha ma-love kimtindo!
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mara nyingi mtu anayetishia kujiua sababu ya mapenzi/etc ni mbinafsi ambaye, akilini mwake anaamini akijiua basi wewe ulomsababishia hayo utateseka mpaka mwisho wa maisha yako kwa ile Guilty conscience.

  Don't be a victim! kila mtu atakuwa accountable kwa matendo yake, kama anatishia kujiua/ akijiua, jua huna/hukuwa na uwezo wa kulizuia hilo...labda kama uataamua kuripoti polisi wamnyang'anye hiyo bunduki, lakini pia akitaka hata kwa kamba anaweza jinyonga!

  BTW, ni mapema mno kwako kuanza uhusiano na Bi x wakati hata bado hujapona majeraha ya yule wa mwanzo, mbona unapenda kuwa Victim wa matatizo wewe? Achana naye!
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  camfu anatunga hadithi.....well done.....
  Kumbe basi hakuna kumlaumu Gf wako kwa kukutanbulisha kwa mates zake kuwa weye ni ndugu na si bf.....wewe ndio uliyaanza.....
   
 7. C

  Camfu Member

  #7
  Jan 22, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hapa naona kuna upana wa mawazo na busara ndani yake, tuendelee kusaidiana vijana wngu, asanteni sana!!!
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,471
  Trophy Points: 280
  Vipi bado unaogopa bunduki usiyoiona?
   
 9. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Camfu naona kaka unatuletea hadithi hadithi njoo, utamu kolea!! hizi drama haziwezi kukumba wewe tu!! What a coincidence mara uachwe uitwe kaka na demu wako, mara una-demu na drama ya kuuawa!!!Man get a life!! Kama vipi soma hadithi za Shigongo zitakutoa!!
   
Loading...