Mambo JF Family

Kuna watu wanatusadikisha kuwa ukienda USA maisha ni matamu sana,hebu tueleze maisha yakoje na utamu huo ni vipi,watu wanapata pesa kiulaini bila ya kutoka jasho sana au pesa yake iko nje nje sana ukilinganisha na huku kwetu...?
Kwa pesa jasho linatoka kwa sana mzee. Na kulala haulali.
 
Karibu sana jukwaani mkuu.

Swali: Hivi wewe hapo ulipo unajiona ni tajiri au fukara? Kama ni fukara, Je, unadhani kwa nini wewe ni fukara? Kama tajiri, Je, unadhani kwa nini wewe ni tajiri?

KARIBU.
Kwa tanzania mimi ni fogo kwa kweli hata sehemu nimejenga ni mmoja ya watu walio juu kimaisha. Namshukuru Mungu. Kwa USA mimi sio tajiri kabisa. Watu huku wana hela aisee na mimi walaa sio mmoja wapo kabisa.
 
Vipi kwa nafasi za bidhaa za ngozi huko USA soko lake likoje

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngozi kama za wanyama pori au ng'ombe haziruhusiwi sababu ya poaching au sababu zao za kiafya kwamba ngozi itaingiza maradhi. Lakini vitu kama pochi ya ngozi, viatu kama safari boots, sandals nk inawezekana. Tatizo ni kwamba hata soko la USA lina products nyingi sana kutoka Asia kama Malaysia. Thailand, na China. Tena products za hali ya juu (quality) na bei ni chini. Sasa ukitafuta soko ya kitu kama hicho quality yake lazima iwe sawa na ya Asian products. Na ili wachukue ya Africa waachane na ya Asia inabidi utoe competitive price. Kwa hio inawezekana lakini kama nilivyosems awali African products ni kama hazipo USA sana sababu ya quality. Sana sana naona products from south africa hasa nguo au jeans, accessories, na jewelleries of course. Ila kwa tanzania hata tanzanite yetu haitoki moja kwa moja Tz. Utaona inasema made in India wakati ni hereni za tanzanite. Sad kwa kweli.
 
Du. Hata tanzanite haina ubora. Kwamba haiwezi katwa au polished vizuri hapa? Au bidhaa moja ikioza zote zimeoza.

Kwamba bidhaa yoyote toka Afrika au Tanzania ni takataka.

Huenda hata sisi wenyewe tunavumiliwa tu kuingia USA kwamba ni takataka tu. Safari tunayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du. Hata tanzanite haina ubora. Kwamba haiwezi katwa au polished vizuri hapa? Au bidhaa moja ikioza zote zimeoza.

Kwamba bidhaa yoyote toka Afrika au Tanzania ni takataka.

Huenda hata sisi wenyewe tunavumiliwa tu kuingia USA kwamba ni takataka tu. Safari tunayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana Trump ameita nchi zetu shiit hole countries. Hehehe. Na kwa sasa anarudisha waAfrika wengi sana makwao hasa wa Gambia, Sudan, Somalia, na Nigeria. Yap. Hata tanzanite haitoki Tz. Maybe pia ukataji na polish na uundaji wa final product unahitaji special skills na inabidi tuzipate hizo kwa ufanisi sana.
 
Uwekezaji kwa kweli USA kwa immigrants ni challenging kidogo sababu una-compete na corporations kubwa sana zenye billion of dollars. Kwa immigrants jambo zuri ni kufanya kazi na kulipwa dollars ambazo inaweza kuwa kati ya $5,000 na $10,000 kwa mwezi. Halafu unajitahidi ku-save ili uwekeze nyumbani tz sababu huko hata $10,000 inafanya kitu wakati kwa USA kuwekeza unahitaji hundreds of thousand of dollars au hata 1 million dollars na zaidi ili kufanya kitu at least cga kueleweka.
Duuh! Dollar 5000 hii Ni sawa na m10 si mchezo.
Kweli ukiamua kujilipua huko kama miaka mitatu inatosha kuja kuwachachafya wabongo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom