Mambo haya yanaweza kuharibu battery ya gari yako. Ni vema kuyaepuka

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,321
Vitu vifuatavyo vinaweza kuharibu battery ya gari yako.

1. Kuweka battery yenye low capacity ukilinganisha na battery ambayo imekuwa recommended kwenye Specifications za manufacturer

Baadhi ya watu anaweza kuweka battery ambayo ni ya low capacity ukilinganisha na battery iliyokuwa recommended kwenye specifications za manufacturer wa hiyo gari. Ama mwenye gari mwenyewe anaweza kuweka ili kusave gharama au fundi anayemuwekea anaweza kuweka low capacity battery ili kupiga hela. Hii haitasaidia kwa sababu mwisho wa siku battery yako itaishia tu kuharibika haraka na utaishia kununua battery nyingine au kubadili battery mara kwa mara.

2. Kuongeza components za umeme kwenye gari yako bila kuupgrade capacity ya battery yako

Kuongeza vitu kama spotlights, winches, Aplifiers, Two-way radios na vingine vinavyofanana na hivyo kunaweza kuathiri battery yako. Vitu hivi vinaweza kuongeza matumizi makubwa kwenye battery yako na hivyo kupelekea battery yako kuharibika haraka sana. Sisemi watu wasifanye upgrades kwenye magari yao lakini unapokuwa unaongeza vitu kama hivyo vya umeme ni vizuri ukapata mtaalamu ambaye atakushauri masuala ya kuupgrade battery pia. Na pia hiyo battery kubwa utayoupgrade ni vizuri ikawa inaenea hapo kwenye sehemu ya kuwekea battery

3. Kuongeza Additives kwenye battery.

Hata siku moja asije mtu akakushauri kuongeza additive yoyote katika battery yako. Inaweza kuwork kwa muda mfupi lakini in a long run, it will ruin your battery to death.

4. Undercharging na Overchaging ya battery.

Hizi mara nyingi husababishwa na mtu kuwa na bad regulator kwenye alternator ya gari yake au alternator yenyewe kuwa na shida, driving habits na kadhalika. Overcharging inaweza kupelekea battery yako kuburst sababu ya formation ya Hydrogen na Oxygen gas ndani ya battery hasa kwa lead acid batteries ambazo ndio wengi wanatumia wakati undercharging hupelekea sulphocation kwenye battery na hivyo kuathiri performance ya battery na mwisho battery kufa. Hii overcharging na underchaging ni kipengele kirefu kidogo, I hope nitaifungulia uzi wake siku moja.

Pia unaweza kusoma.

Baadhi ya solutions za matatizo ya automatic gearboxes

Baadhi ya watu mnaofanya Computer diagnosis kwenye magari mnawamislead wateja wenu na kuwaingiza gharama zisizo za lazima

Kuna umuhimu mkubwa sana kufanya check up ya mifumo ya umeme na electronics kwenye gari yako
 
Dooo nahisi nimepata jibu,kuna gari nilipeleka kwa fundi hizi Noah siku naenda icheki gari wakasema battery iko chaji naenda cku nyingine naambiwa bettry imebutuka kimfuniko kimoja wapo kilitoka kabisa, sasa ndio nimepata jibu kwanini lilibust yaan watanilipa maan nilikuwa najiuliza ilikuwaje likabust??
 
Aiseeee pole sana mkuu.

Huenda walikuwa wanatumia charger yenye voltage kubwa kuliko charging voltage ya hiyo battery. With time accumulation ya O2/H2 gas ikizidi lazima battery iburst tu.
 
Aiseeee pole sana mkuu.

Huenda walikuwa wanatumia charger yenye voltage kubwa kuliko charging voltage ya hiyo battery. With time accumulation ya O2/H2 gas ikizidi lazima battery iburst tu.

Gari ilienda ina matatizo mengine imerudi inachemsha sijui hata walichokonoa wapi, tukawarudishia ndio wanahangaika nayo but inaonekan imeshawashinda haijakaa sawa tunaambiwa battery tena imebutuka.....yaani kuna mafundi unaweza ukawapika ulie ugali, ila watailipa tu hiyo battery
 
Mambo ya kumpelekea mtu gari halafu unamuachia yana changamoto sana. Labda kama ni sehemu inayoleweka. Otherwise unaweza kugombana tu na watu maana hutaitamani gari yako tena.
 
Mambo ya kumpelekea mtu gari halafu unamuachia yana changamoto sana. Labda kama ni sehemu inayoleweka. Otherwise unaweza kugombana tu na watu maana hutaitamani gari yako tena.
Ni kweli hawa mafundi wetu wa kugonga na nyundo ni tatizo kubwa, unapeleka gari kwa tatizo fulani linarudi na tatizo lingine. Tuendelee tu kununua magari used kutoka Japani hata ukimpelekea fundi akagonga kwa nyundo huumii sana kuliko kununua gari jipya halafu unampelekea fundi analigonga kwa nyundo inaumiza sana.
 
Ni kweli hawa mafundi wetu wa kugonga na nyundo ni tatizo kubwa, unapeleka gari kwa tatizo fulani linarudi na tatizo lingine. Tuendelee tu kununua magari used kutoka Japani hata ukimpekea fundi akagonga kwa nyundo huumii sana kuliko kununua gari jipya halafu unampelekea fundi analigonga kwa nyundo inaumiza sana.

Hahah...

Ila mkuu kugonga nyundo siyo shida. Kikubwa hiyo nyundo unayogonga iwe ni katika sehemu sahihi. Vinginevyo ni majanga tu...
 
Hizi Additives zinazoongezwa kwenye battery ni zipi? Ungezielezea kidogo

Na pia kuwasha radio huku gari umezima hii pia inachangia bettery kufa mapema

Na kama ikitokea utasafiri kwa mda wa mwezi ama zaidi na gari umeliacha nyumbani basi unashauriwa kudisconnect positive terminal
 
1. Additives zipo nyingi sana huko masokoni mfano kama hii.
images (1).jpeg

2. Haina shida. Ila shida ni pale ambapo unakuta labda mtu aliona radio ya gari haimtoshi amkaamua kuongeza na amplifier. Hapo lazima battery itakuwa nadrain faster na lazima ife haraka.

3. Kudisconnect positive terminal ya battery ni sahihi kabisa.
 
Ni kweli hawa mafundi wetu wa kugonga na nyundo ni tatizo kubwa, unapeleka gari kwa tatizo fulani linarudi na tatizo lingine. Tuendelee tu kununua magari used kutoka Japani hata ukimpekea fundi akagonga kwa nyundo huumii sana kuliko kununua gari jipya halafu unampelekea fundi analigonga kwa nyundo inaumiza sana.
Gari jipya linakuwa na warranty. Huumizi kichwa.
 
Back
Top Bottom