Mambo haya yanaikwamisha CHADEMA, Maamuzi Magumu yanatakiwa Kabla ya 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo haya yanaikwamisha CHADEMA, Maamuzi Magumu yanatakiwa Kabla ya 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Apr 23, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wana chama wa Chadema,kwa hoja hii ni mhimu viongozi wakuu wa Chadema na Wajumbe wa kamati Kuu wayafanyie kazi. Sote tuna tambua kua Uchaguzi wa Mwaka 2010 ulikua na changamoto nyingi hasa kwa Chadema kuonekana ni Chama ambacho kinaelea juu tu ngazi ya Taifa! Hili limetokea kwa Chadema kuto kusimamisha Wagombea wa Ubunge baadhi ya Majimbo! Wito wangu ni sasa kujielekeza zaidi katika maeneo ya wilaya na hasa yale ambayo Chadema haikusimamisha wagombea katika majimbo hayo! Lakini jambo jingine ni mhimu kujitenga na mahusiano ya moja kwa moja na Kanisa Katoliki iwe mahusiano na Baraza la Maaskofu TEC iwe kwa wao kupenda kutoa ushauri kwa Chadema au Chadema kuomba Ushirikiano na TEC,pia Kadinal Pengo aache kutoa matamko pale tu anapo ona viongozi wa Chadema wanaongelea jambo fulani! Tatu,utaratibu uliotumiwa wa kutumia formula kupata Wabunge wa Viti Maalumu uangaliwe kwani unawapa zaidi nafasi wabunge wengi watoke Kilimanjaro! Nne,Imefika wakati sasa Chadema imulipe fidia Mzee Edwin Mtei kwa kuanzisha Chadema ili Chadema itoke kwenye mfumo wa Kampuni Binafsi na sasa kuwa Chama cha Wanachama! Tano,Mheshimiwa Freeman Mbowe sasa kuwapa nafasi wanachama wengine kugombea nafasi ya Uenyekiti na kuondoa taswira ya kuwa chama cha Ukoo. Mwisho, Matumizi ya Ruzuku ndani ya Chadema ni mhimu yaelekezwe Wilayani,Dr Slaa kulipwa 12 milioni kwa mwezi ni ufisadi ndani ya Chama.
   
 2. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  cdm hawahitaji mawazo yasiyo endelevu km haya yako
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Kampuni binafsi ni TLP ya Mrema Na UDP ya John CHEYO, ningekushauri peleka ushauri wako kwa vyama hivyo tajwa. na CHADEMA ina maconsultant wake ambao ni wasomi na haiwezi kushauriwa na mtu mwenye mawazo finyu ya kiwango chako. kama wewe si mnafki vyama ambavyo ni kampuni za watu ni hivyo nilivokutakutajia.
   
 4. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Je wewe umekataliwa kuwa MwanaCDM.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hii ni kawaida ya kunguru .... sikushangai
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ...mmmh!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  je ni kweli pengo wakati mwingine anaingilia maamuzi ya cdm? nilikuwa na hitaji kufamu hilo...
   
 8. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Niliwa kusema mlengo wa kati ww ni pimbi,narudia tena YOUR A NICE PIMBI
   
 9. M

  Mwamatandala Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tusiwe walevi wa siasa za upeo mdogo,mimi mwanachama na kada makini wa chadema,lkn aliyoyasema mwanzilishi wa thread hii ni vema na busara yakatazamwa kwa upeo mpana wa kufikiri na siyo kukurupuka tu.kwa mwenye mapenzi mema na chadema ni ataangalia upande wa pili wa shilingi haswa ule ambao unaelezea mapungufu ya chama chetu.vinginevyo wote mliochangia ktk thread hii mnaonekana hamna mapenzi mema na chama chetu.
  NAWAKILISHA.
   
 10. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  tuwekee kadi yako ya uanachama hapa kujihakiki
   
 11. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nina mashaka makubwa nawe,pamoja na mlengo wa kati,labda naomba nijibiwe(a)kuna uhusiano gani unaoufahamu kati ya katoliki na Cdm,(b)ni lini Mbowe alitangaza kwamba yeye ni mwenyekiti wa kudumu Cdm,NAOMBA UFAFANUZI,Maana wengi mnajiita makada wa chama kumbe........
   
 12. J

  Joshua Bukuru Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Mimi nizungumzie hili la kumlipa fidia Edwin mtei, mengine watakujibu wanaforum. Wakati anaanzisha chama hiki hakukianzisha kama kampuni binafsi na hakuwa na hisa za umiliki. Chadema na wanachama wake wanashukuru kwa mchango wa kuona mbali na kuona pia umuhimu wa kuwa na chama cha upinzani. Fidia anayostahili, ni kuenziwa kama mwasisi wa chama kwa vizazi vijavyo, nadhani ni fidia isiyokuwa na kikomo!
  Amekutuma umusemee kuwa anahitaji fidia? Ni mzee wetu, tunamheshimu na tutaendelea kumheshimu siku zote na hata kama atakuwa ametutangulia mbele ya haki.
   
 13. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  tokea kikao cha dodoma cha kuvaa gamba tumeshuhudia vibaraka wa ccm wengi waliotumwa na msekwa kuchafua harakati za ukombozi humu jf,..sasa huyu naye kwa nini asirudi hukohuko facebook alikotoka..
   
 14. M

  Mpanda Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana ukawa na hoja ya msingi ila umekosea kuiwakilisha... Ungefanya utafiti wa kutosha sana hasa kwenye mambo ya msingi kwa mfano wabunge wa viti maalumu unadai wanatoka Kilimanjaro takwimu unazo? Unajua utaratibu uliotumika kuwapata wabunge hao? Vipi uhakika ulionao kuhusu Muasisi wetu kuwa anaendesha CDM kama kampuni? Vipi kuhusu Mwenyekiti wetu wa Taifa Freeman Mbowe wapi amevunja katiba ya CDM? Usikurupuke katika kutoa maoni yako kamanda, naweza kukuunga mkono kwamba sasa tunatakiwa kwenda chini zaidi kwa maana ya kueneza chama wilayani, Katani na vijijini ila kwa kukumbusha ni kwamba kazi anayofanya Dr.Slaa kwa sasa ndiyo hiyo... Na ukumbuke mfumo mzima wa namna vyama vya siasa vinavyoanza siku zote zinaanzia juu halafu inakuja chini, na ndivyo CDM inavyofanya... Huwezi hata kidogo ukasema CDM ni Kampuni binafsi wala ya kiukoo, angalia kwa undani CDM ina uwakilishi wa kitaifa, vipi UDP ama TLP ipi kampuni binafsi? Hebu tupe ushahidi unaoonyesha kuwa CDM na Kanisa Katoliki ina mahusiano ya moja kwa moja vinginevyo utuambie kuwa una agenda nyingine...
   
 15. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Kamani msimalize chaji zenu sbb ya mtu huyu,mpaka hapo tumeshamstukia katumwa na arudi huko alitoka Kama ni facebook basi na arudi huko akajadili bethidei za kina Lily Wyne huku "hapamfai"anatuharibia upepo
   
 16. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,024
  Likes Received: 8,510
  Trophy Points: 280
  Mara sijui umetumwa,siku hizi jf imevamiwa ni dalili tosha kwamba mtu anashindwa kuwa na point za kuargue anakimbilia kashifa na kudai mtoa hoja katumwa.hata kama katumwa it is up to u to challenge him.
  Ukiderail it just show how inferior you are.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Mlengo wa Kati, kwenye posti yako hii, umechanganya ushauri, tuhuma na shutuma kama ifuatavyo.
  1. Chadema ni Chama ambacho kinaelea juu tu ngazi ya Taifa! Hili limetokea kwa Chadema kuto kusimamisha Wagombea wa Ubunge baadhi ya Majimbo!-Kumbe kutosimamisha wagombea majimbo yote ndio kuelea juu juu?
  2.Wito wangu ni sasa kujielekeza zaidi katika maeneo ya wilaya na hasa yale ambayo Chadema haikusimamisha wagombea katika majimbo hayo! -Huu ni wito mzuri!.
  3. Chadea kujitenga na mahusiano ya moja kwa moja na Kanisa Katoliki iwe mahusiano na Baraza la Maaskofu TEC- Fafanua mahusiano yepi na utoe mifano!
  4. TEC kupenda kutoa ushauri kwa Chadema -Elezea kuhusu ushauri huo na kutoa mifano.
  5. Chadema kuomba Ushirikiano na TEC-Kumbe chadema imeomba ushirikiano na TEC?!, hapa unaelezea ushirikiano huo uliiombwa.
  6. Kadinal Pengo aache kutoa matamko pale tu anapo ona viongozi wa Chadema wanaongelea jambo fulani!- Kumbe Kardinali Pengo huwa anatoa matamko pale tuu Chadema wanapoongelea jambo fulani?!, hizi ni tuhuma, zithibitishe!
  7. Utaratibu uliotumiwa wa kutumia formula kupata Wabunge wa Viti Maalumu uangaliwe kwani unawapa zaidi nafasi wabunge wengi watoke Kilimanjaro!-Hii ni hoja ya msingi, ila pia sikujua huo utaratibu umebiniwa ili kuwanufaisha watu wa Kilimanjaro tuu!
  8. Chadema imulipe fidia Mzee Edwin Mtei kwa kuanzisha Chadema. Kumbe Mzee Mtei anadai fidia ya nguvu zake alizotumia?!, hii pia uithibitishe!.
  9. Chadema itoke kwenye mfumo wa Kampuni Binafsi na sasa kuwa Chama cha Wanachama!- Kumbe Chadema ni kampuni binafsi sio chama cha wanachama?!, sasa hao wanaojidai ni wanachama kumbe status zao ndani ya kampuni hiyo ni zipi?, kumbe hata msajili wa vyama anasajili makampuni ya kisiasa?, au pia imesajiliwa Brella?. Hii ni tuhuma, inahitaji uithibitishe!.
  9. Mheshimiwa Freeman Mbowe sasa kuwapa nafasi wanachama wengine kugombea nafasi ya Uenyekiti. Kumbe ni Mhe. Mbowe ndio anazuia wanachama wengine kugombea uenyekiti?!, hizi pia ni tuhuma, zitahitaji uthibitisho!.
  10. Kuondoa taswira ya kuwa chama cha Ukoo. Hapa kuna hoja na sio ya kupuuzwa!.
  11. Matumizi ya Ruzuku ndani ya Chadema ni mhimu yaelekezwe Wilayani-Hii ni hoja ya msingi, kumbe ruzuku ya Chadema inakwenda wapi?.
  12. Dr Slaa kulipwa 12 milioni kwa mwezi ni ufisadi ndani ya Chama. Kumbe Dr. Slaa analamba milioni 12 kila mwezi?!. Kumbe mshahara wa Milioni 12 ni ufisadi?. Jee mishahara ya Wakuu wa TCRA, TICKS, TANROAD, BOT, EWURA, PPRA ETC ambayo inafikia Milioni 25 tuuiteje?!

   
 18. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huo ushauri wa Mlengo wa Kati ni Mzuri kwa CDM na wapenda demokrasia wengine, kinachotakiwa ni kuufanyia kazi na siyo kufikiria kuwa kila mtu anayewakosoa ni mwana CCM.
   
 19. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,024
  Likes Received: 8,510
  Trophy Points: 280
  Dah..!!25 million mtu mmoja?huo ni wizi hawafai
   
 20. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,024
  Likes Received: 8,510
  Trophy Points: 280
  Dah..!!25 million mtu mmoja?huo ni wizi hawafai
   
Loading...