Mambo Haya Kumi (10) Usiyojua Kuhusu Fedha Ndiyo Yanakufanya Uendelee Kuwa Masikini.

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Rafiki yangu mpendwa,

Tangu tunazaliwa mpaka tunakuwa watu wazima, kuna vitu vingi sana ambavyo tunafundishwa kwenye familia, kwenye jamii, shuleni na hata kwenye kazi au biashara.

Tunafundishwa jinsi ya kwenda vizuri na watu wengine, jinsi ya kufanya kazi au biashara zetu na umuhimu wa kufuata sheria mbalimbali. Yote haya yanalenga kutufanya kuwa watu wazuri kwenye jamii na kufanya shughuli zetu vizuri.

Lakini ipo elimu moja muhimu sana ambayo tunaikosa, elimu hii ambayo ndiyo inashika eneo kubwa la maisha yetu, hatuipati kwenye familia, hatuipati kwenye jamii, wala shuleni au kwenye kazi na biashara.

Elimu hii muhimu ambayo tumekuwa tunaikosa ni kuhusu fedha. Tumekuwa tunafundishwa mambo mengine yote, lakini inapokuja kwenye fedha, hakuna anayechukua muda wake kutufundisha. Na ni kwa sababu hata hao waliotutangulia hawakupata nafasi ya kufundishwa.

Hivyo chochote tunachojua kuhusu fedha imekuwa ni kwa kuiga. Tunaangalia wengine wanafanya kwa upande wa fedha na sisi tunafanya hivyo. Na haishangazi kwa nini watu wengi wana matatizo ya kifedha.

Nenda eneo lolote la kazi, na utakuta karibu wafanyakazi zote, moja mishahara yao haikutani, mbili, wana madeni. Hapo ni eneo la kazi ambapo watu wana mishahara tofauti, wapo wenye mshahara kidogo na wengine wenye mshahara mkubwa. Kinachoshangaza, wote wanaishia kuwa na matokeo sawa kifedha.

Rafiki yangu mpendwa, kwa kuona ukosefu mkubwa wa elimu hii muhimu ya fedha, na kwa kuona jinsi ambavyo watu wengi wanateseka inapokuja kwenye swala la fedha, nimetafiti kwa kina eneo hili na kuandika kitabu kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION).

elimu fedha 2


Hii ni elimu ya msingi kabisa ya kifedha ambayo ukipaswa upewe kwenye familia, kwenye jamii, shuleni na hata kwenye kazi au biashara. Lakini hakuna anayekupa elimu hiyo. Mimi kocha wako, kwa sababu najali sana kuhusu wewe, na kwa sababu kazi yangu kubwa ni wewe, nimekuandalia elimu hii kwa njia rahisi sana kuelewa kupitia kitabu.

Kwenye kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kuna mambo kumi muhimu sana niliyoyajadili kwa kina ambayo yamewafanya wengi kubaki kwenye umasikini kwa sababu hawajui.

Leo nakugusia mambo haya hapa kwa kifupi, na ili kujifunza kwa kina na hatua za kuchukua, nitakupa utaratibu wa kupata kitabu hiki kizuri sana.

Moja; FEDHA SIYO MAKARATASI.

Watu wengi wamekuwa wanafikiria fedha ni yale makaratasi au sarafu ambazo tunazishika. Na hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu wanakosa ule msingi muhimu kuhusu fedha. Kwa kukosa msingi muhimu kuhusu fedha, watu wanashindwa kuzipata kwa wingi na hata kuzitumia vizuri.

Fedha ni wazo ambalo lina thamani. Fedha ni matokeo ya mtu kuwa na wazo ambalo linaongeza thamani kwa wengine. Bila ya thamani hakuna fedha. Hivyo kama unataka fedha zaidi, lazima ujue thamani gani unatoa kwa wengine.

Kwenye sura ya kwanza ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, nimekufafanulia kwa kina kuhusu maana halisi ya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Bila kujua hii, huwezi kuondoka kwenye umasikini.

Mbili; KIPATO KIMOJA NI UTUMWA.

Kuwa na chanzo kimoja cha kipato pekee ni utumwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini kama unategemea kipato chako kitoke sehemu moja pekee. Kama umeajiriwa pekee, hata kama unalipwa kiasi kikubwa cha fedha, bado unabaki kwenye umasikini. Kama unafanya biashara na unategemea wateja wachache nayo pia inakuweka kwenye umasikini.

Utaondoka kwenye umasikini kwa kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Bahari huwa haikauki kwa sababu mito mingi inaishia kwenye bahari. Hiyo kama unataka usikaukiwe na fedha, kuwa na vyanzo vingi vya kipato.

Kwenye sura ya pili ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA nimekufundisha kwa kina kuhusu kipato, umuhimu wa kuwa na vyanzo vingi vya kipato na jinsi ya kuongeza kipato chako pale ulipo sasa.

Tatu; MATUMIZI NI BOMU.

Watu wengi wamekuwa wanaanza maisha na kipato kidogo, na yanaenda. Kipato kinaongezeka na matumizi yanaongezeka, kila kipato kinapoongezeka na matumizi pia yanaongezeka. Matumizi ni bomu kama hayatadhibitiwa. Matumizi yana tabia ya kuongezeka pale tu kipato kinapoongezeka.

Huwezi kuondoka kwenye umasikini kama huwezi kuyadhibiti matumizi yako. Haijalishi unatengeneza kipato kikubwa kiasi gani, matumizi ni bomu, usipolitegua litakulipua.

Kwenye sura ya tatu ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA utajifunza jinsi ya kudhibiti matumizi yako na hivyo kuruhusu kipato chako kukua na kuweza kuondoka kwenye umasikini.

Nne; MADENI NI UTUMWA.

Umesikia hapo, na najua huenda kimoyomoyo unakataa, unajiambia siyo kweli, kwa sababu huenda umeshalishwa sumu kwamba bila madeni maisha hayawezi kwenda. Unajua nini, wale wanaonufaika na madeni ndiyo wanasambaza propaganda za aina hiyo. Madeni ni utumwa, na huwezi kuondoka kwenye umasikini kama huwezi kuondokana na madeni.

Kuna madeni mazuri na mabaya, na masikini wote huwa wapo kwenye madeni mabaya. Madeni mabaya ndiyo yanawafanya watu kuwa watumwa, wanajikuta wanafanya kazi sana kulipa madeni, halafu wanakopa tena. Kwa hiyo maisha yao yote yanakuwa mzunguko wa kopa, lipa, kopa tena.

Kwenye sura ya nne ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA unakwenda kujifunza aina mbili za madeni, jinsi ya kuondoka kwenye madeni na mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kuingia kwenye madeni mazuri.

Tano; BIASHARA NI MKOMBOZI.

Zile zama za nenda shule, soma kwa bidii, faulu na utapata kazi nzuri na inayolipa zimeshapitwa na wakati. Kila mtu anaona wingi wa watu wenye sifa za kuajiriwa, lakini hakuna nafasi za ajira. Na hata walioajiriwa, mazingira ya kazi na hata kipato wanachoingiza hakiridhishi.

Kwa zama tunazoishi sasa, mkombozi pekee, kitu pekee kitakachokuwezesha kuwa na maisha mazuri ni kuwa na biashara yako. Hivyo ni muhimu sana uwe na biashara kama unataka kutoka kwenye umasikini.

Kwenye sura ya tano ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, utajifunza kwa nini kila mtu anapaswa kuwa na biashara, jinsi ya kuanzia biashara chini kabisa na kuikuza na biashara unazoweza kuanza kufanya hapo ulipo sasa.

Sita; UWEKEZAJI NI KIJAKAZI WAKO.

Inapokuja kwenye fedha, kuna mambo mawili, kuna kuifanyia kazi fedha, pale ambapo inabidi ufanye kazi ndiyo fedha iingie. Halafu kuna fedha kukufanyia kazi wewe, ambapo fedha inaingia hata kama hufanyi kazi moja kwa moja.

Ili kuondoka kwenye umasikini na kufikia uhuru wa kifedha, ni lazima fedha ziwe zinakufanyia kazi wewe. Na hapa ndipo unapohitaji kuwa na uwekezaji, ambao unafanya kazi ya kuuzalishia fedha, hata kama wewe umelala.

Kwenye sura ya sita ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, nimekuchambulia kwa makini sana kuhusu uwekezaji, aina kuu tano za uwekezaji, jinsi ya kuchagua uwekezaji sahihi kwako na uwekezaji unaoweza kuanza nao mara moja.

Saba; KODI NI UWEKEZAJI.

Kodi ni gharama unayolipa kwa kuishi kwenye jamii iliyostaarabika. Ni kodi tunazolipa ndiyo zinazoleta huduma mbalimbali tunazozitegemea kwenye jamii. Huduma za afya, huduma za elimu, ulinzi na usalama, miundombinu kama barabara na mengineyo ni matokeo ya kodi tunazolipa.

Hivyo kodi ni uwekezaji ambao kila mmoja wetu anapaswa kuufanya ili tuwe na jamii bora. Tunapaswa kuondokana na dhana potofu kwamba kodi ni kitu kibaya. Kwa sababu hebu pata picha, umekazana kutafuta fedha na ukawa tajiri, halafu unaishi sehemu isiyo salama, je utaweza kufurahia utajiri wako?

Kwenye sura ya saba ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA utajifunza umuhimu wa kodi kwenye jamii, kodi zinazokuhusu wewe moja kwa moja na jinsi ya kupata unafuu wa kodi.

Nane; BIMA NI MKOMBOZI.

Kuna hatari mbalimbali ambazo zinatuzunguka kwenye maisha, na kadiri unavyopiga hatua kifedha, ndivyo hatari zinakuwa kubwa zaidi. Hili limekuwa linazua hofu kwa wengi na wakati mwingine kuwazuia hata kufanikiwa.

Ili kuondokana na hatari zinazokuzunguka na kukuzuia kuanguka pale unapokutana na changamoto kubwa, unapaswa kuwa na bima. Kwa bima unachangia kiasi kidogo cha fedha, lakini unapopata tatizo, unalipwa kiasi kamili cha fedha au mali ulizopoteza.

Kwenye sura ya nane ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA unakwenda kujifunza umuhimu wa kuwa na bima, bima unazopaswa kuwa nazo kwenye maisha yako na mambo ya kuzingatia unapochagua bima.

Tisa; WATOTO WAKO HAWAHITAJI FEDHA ZAKO.

Wazazi wengi wamekuwa wanakazana kutafuta fedha na mali kwa wingi, ili kuwaachia watoto wao urithi na wasiwe na maisha magumu. Lakini wote tumekuwa tunaona nini kinatokea baada ya wazazi hao kufariki, utajiri na mali zote zinapotea, kwa kutumiwa vibaya na watoto walioachwa.

Watoto wako hawahitaji sana fedha wala mali zako, bali kikubwa wanachohitaji ni msingi muhimu wa kufuata na kusimamia inapokuja kwenye swala la fedha. Kuliko uwape watoto fedha bila ya misingi, ni bora uwape misingi bila ya fedha. Kwa sababu misingi itawawezesha kupata fedha zaidi wakati fedha pekee bila misingi zitapotea.

Kwenye sura ya tisa ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, utakwenda kujifunza jinsi ya kuwajengea watoto wako msingi sahihi wa kifedha ambao utawahakikishia kutokusumbuliwa kabisa na umasikini. Na kadiri unavyoanza mapema, ndivyo wanayonufaika zaidi.

Kumi; KUTOA NI UWEKEZAJI.

Mmoja wa watu matajiri sana kuwahi kuwepo hapa duniani, John D. Rockefelar amewahi kunukuliwa akisema unatumia nusu ya kwanza ya maisha yako kukusanya fedha, halafu nusu ya pili unaitumia kuzigawa fedha hizo kwenda kwa wengine.

Moja ya vitu vinavyowafanya matajiri kuendelea kuwa matajiri ni utoaji. Matajiri wengi wamekuwa watoaji wa misaada mbalimbali ya kijamii na hilo limekuwa linawasukuma kufanikiwa zaidi kifedha. Hivyo kutoa ni uwekezaji ambao unamlipa sana mtu baadaye.

Kwenye sura ya kumi ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, utajifunza umuhimu wa kutoa, njia bora za kutoa utajiri wako kwa wengine na pia sadaka na utoaji mwingine.

HITIMISHO; MAISHA YA KITAJIRI SIYO RAHISI.

Watu wengi kabla hawajapata fedha huwa wanafikiri wakishapata fedha basi maisha yao yatakuwa rahisi na hakutakuwa tena na changamoto. Wanachokuja kugundua baada ya kupata fedha ni kwamba fedha huwa zinakuja na matatizo na changamoto zake. Hivyo maisha ya kitajiri siyo rahisi kama yanavyoonekana kwa nje.

Kwenye hitimisho la kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, nimekushirikisha mambo kumi ya kuumiza sana kuhusu maisha ya kitajiri, ambayo unapaswa kuyajua na kusimama imara ili yasikuangushe.

Rafiki yangu mpendwa, kitabu ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ni kitabu ambacho hupaswi kukosa kukisoma, kwa sababu kina kila kitu unachopaswa kujua kuhusu fedha. Elimu iliyo ndani ya kitabu hiki itakuwezesha kuondoka kwenye umasikini na kukufikisha kwenye utajiri na uhuru wa kifedha.

JINSI YA KUPATA KITABU CHA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Kitabu cha elimu ya msingi ya fedha kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy) yaani kimechapwa na kinatumwa popote pale ndani ya nchi ya Tanzania.

Kitabu hiki kinapatikana kwa gharama ya shilingi za Kitanzania Elfu Ishirini (20,000/=) kwa nakala moja ya kitabu.

Lakini ipo ofa kwako wewe rafiki yangu, ya kukipata kitabu hiki kwa tsh elfu kumi na tano, (15,000/=) kama utakilipia kabla ya tarehe 31/07/2019.

Kupata kitabu hiki, tuma ujumbe kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha utaletewa kitabu ulipo kama upo dar au kama upo mkoani utatumiwa.

UZINDUZI WA KITABU CHA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Rafiki yangu mpendwa, kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ambao utafanyika jijini Dar es salaam siku ya jumamosi tarehe 03/08/2019.

Kwenye uzinduzi huu tutajifunza kwa kina mambo muhimu sana ya kifedha na jinsi ya kukitumia kitabu hiki kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Ada ya kushiriki uzinduzi wa kitabu ni tsh elfu kumi (10,000/=) na ili kupata nafasi ya kushiriki uzinduzi wa kitabu, tuma ujumbe sasa wenye majina yako kamili na namba ya simu ukisema utashiriki uzinduzi wa kitabu. Na uhakikishe umelipa ada ya kushiriki mpaka kufikia tarehe 31/07/2019.

Karibu sana rafiki yangu, usikose uzinduzi wala kitabu chenyewe.

Pia kuna kitabu kingine kimetoka, kinaitwa TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, ambapo kuna mambo matano ya kujifunza kwenye kila juma la mwaka, kuanzia siri za mafanikio, uchambuzi wa kitabu, makala za mafanikio, mafunzo ya kifedha na tafakari mbalimbali.

Kupata kitabu hiki tumia mawasiliano 0717396253 au 0755953887, karibu sana.

Vitabu vyote viwili vitazinduliwa siku moja, hivyo jipatie mapema na ushiriki uzinduzi ili uweze kujifunza na kuchukua hatua zitakazoyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

 
Hii ndio Tz tunayoitaka ,watu wawe na uwezo wa kuandika vitabu vingi na tafiti rukuki

Pig up sana Mkuu Mimi nitakusapoti ingawa najua kuwabadilisha watu wawe na mtazamo kama wako ni ngumu sana
 
Mkuu nitakaribia ngoja nimesevu details zako ntahtaji kitabu hicho maana its very inspiring and educational oriented

Soon ntakusikilizia...ila niko tarime can it be possible
Karibu sana mkuu,
Ndiyo, tunatuma popote Tanzania ambapo kuna basi inafika kutoka Dar,
Kitabu kinatumwa kwa ofisi za mabasi na hivyo unaenda kuchukua ofisini moja kwa moja.
Asante sana.
 
Hii ndio Tz tunayoitaka ,watu wawe na uwezo wa kuandika vitabu vingi na tafiti rukuki

Pig up sana Mkuu Mimi nitakusapoti ingawa najua kuwabadilisha watu wawe na mtazamo kama wako ni ngumu sana
Asante sana Mkuu,
Mabadiliko ni mimi na wewe, tukianza kubadilika sisi, na wale wanaotuzunguka watabadilika kidogo kidogo.
Hivyo kila mmoja wetu achukue hatua anayoweza katika mabadiliko, na haitapita bure.
Karibu sana ujipatie kitabu, ni hazina kubwa sana kwako na hata familia yako pia.
 
nimeudhuria semina nyingi za aina hii, nimesoma makala nyingi za aina hii nimeona kama Mungu hajakufungulia ni kazi bure. Ni sawa na kuhudhuria semina za ndoa wakati wewe ni hanisi!
Kuhudhuria semina pekee siyo tiketi ya kufanikiwa, unatakiwa uyafanyie kazi yale uliyojifunza ndiyo ufanikiwe.
Tatizo la watu wengi wanapenda kufanikiwa lakini hawataki kubadili maisha yao.
Mtu unataka uendelee kuamka muda unaotaka, uendelee kushinda mitandaoni, uendelee kufuatilia kila aina ya habari, uendelee kuendekeza starehe, uendelee kushabikia kila aina ya mchezo na hapo bado ufuatilie maisha ya wengine, halafu pia ufanikiwe. Ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.
Mafanikio yanakuja pale unapochukua hatua kweli, pale unapokuwa tayari kujitesa kwa kipindi kifupi ili kujenga msingi ambao baadaye unakufanya usiteseke kabisa.
Nakushauri sana upate kitabu hiki na ukisome, na fanyia kazi yale utakayojifunza kwa mwaka mmoja tu, na kama hutakuwa na mabadiliko yoyote kwenye maisha yako, niambie na nitakurudishia fedha mara mbili ya uliyolipa.
Karibu sana Mkuu.
 
Una utajiri wa kiasi gani baada ya kugundua hayo mambo???....Hayo ni maandishi tu na maandishi sio uhalisia....
Karibu ujipatie kitabu, ukisome na ufanyie kazi ndani ya mwaka mmoja tu, na kama hutarudisha mara kumi ya fedha uliyotoa kununua kitabu, basi nitakurudishia mara mbili ya fedha uliyolipia.
Maarifa haya yana nguvu sana ya kukuwezesha kuondoka kwenye matatizo ya kifedha, kama utayafanyia kazi.
Karibu.
 
Back
Top Bottom