Mambo haya hayakuzi Uchumi wa Tanzamia


T

Toosweet

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Messages
1,593
Likes
1,140
Points
280
T

Toosweet

JF-Expert Member
Joined May 27, 2012
1,593 1,140 280
Heshima,

Kukua kwa uchumi wa nchi au kupata maendeleo kwa nchi lazima kuendane na hali za maisha ya watu kubadilika, kutoka duni kwenda bora.

Nimeangalia takwimu ambazo ni indicators for performance of financial institutions kwa uchumi wa nchi, nimeshangaa.
Hebu angalia,
Personal lending 2015,25.5%-personal lending 2017,8%
Business lending 2015,24.6%-business lending 2017,9%
Growth in Agriculture 2015 and before 6%,at present -9%(negative growth)
Growth in Manufacturing sector 2015 and before 30%,at present 3%.
Ukisoma magazeti karibu kila siku hukosi kukuta tangazo la kampuni kufungwa au kufilisika(voluntary winding up, liquidation)
VAT na PAYE, kodi ya ongezeko la thamani vimeshuka kuashiria biashara zimekufa na ajira zimepungua.

Kwa upande mwingine, mkulima ambaye amepata mavuno ya kutosha, anazuiwa kuuza mazao yake nje ya nchi, eti atasababisha njaa. Hivi chakula ni mahindi tu, mchele tu, maharage tu? Mkulima hana mahitaji mengine ya msingi kama ada za shule kwa watoto wake?

Mfanyabiashara maarufu wa sekta ya usafirishaji, hasa mabasi ya abiria, Sumry ameachana na biashara ya mabasi. Ameuza zaidi ya mabasi 80.Anasema kwa mwezi basi halifikishi zaidi ya milioni 10.

Kwa sasa Sumry ni mkulima mkubwa wa mahindi huko Katavi/Rukwa. Ana vifaa vya kisasa zikiwemo combine harvester. Ana godown kubwa sana la mahindi, kama tani 147,000.Hawezi kuuza kwa sababu ya zuio la serikali kuuza nafaka nje ya nchi. Ajabu ni kuwa Tanzania ni soko la mahindi kutoka Zambia. Tunanunua kutoka Zambia wakati tunalima ya kutosha. Serikali hainunui mahindi ya wakulima lakini inawakataza kupeleka soko lenye kuyahitaji...

Mbinu zetu za uchumi wa kutaka kukusanya kodi tu kwa kuwadhibiti wafanyabiashara ,ili kuzitumia kukamilisha miradi mikubwa, hazitatufikisha mbali.

Nakumbuka maneno yaKiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe,"Uchumi si fly over na Bombardier sita. Uchumi ni kipato kwa wananchi wa kawaida".
Uchumi wetu unaumwa.
 

Forum statistics

Threads 1,235,823
Members 474,742
Posts 29,237,182