Mambo gani umewahi kumuomba Mungu na akakujibu papo hapo?

mimi ilinitokea nilipewa mtihani mgumu kweli kweli chuoni sikujua naanzia wapi nikamwomba mungu nikasikia sauti inaniambia tizama ubaoni nikaona notisi za majibu yote ya maswali zimeandikwa ubaoni nikawa nanyanyua kichwa naangalia ubaoni nakopi kama ilivyo hadi msimamizi wa mitihani akawa ananikodolea macho ananishanga shangaa nikaibua na A KWENYE HILO SOMO

NILIPOMALIZA KUANDIKA YAKAFUTIKA YENYEWE
Uongo mwingine bhana!!!
 
Nimecheka sana hadi watu wananishangaa
Mungu acha aitwe Mungu

Ipo hivi, nilienda kuchakata demu wangu kwao si nkajisahau bwana hadi mida ya jioni ambapo hiyo mida mama yake ndo huwa anarudi kutoka job( huyu mama ni mkali balaa yani kukutia kisu hashindwi).

Mara tukamuona mdogo mtu anakuja mbio oooh mama anakuja, hatujajiandaa kwa lolote Mara huyo tunamuona kwenye dirisha anapita ili aingie ndani dah hiyo siku nilidata aisee!

Kilichofanyika pale demu kanichukua mpaka chumbani kwa mama yake kwenya mabegi akatoa manguo akanambia lala juu ya mabegi halafu akafunika juu zile nguo halafu demu hakuondoka hapo akajifanya kama anatafuta nguo.

Mama mtu kaingia chumbani kwake kamkuta mtoto mtu kama anatafuta nguo kumbe mimi nipo kwa ndani basi wakasalimiana halafu mama mtu akaanza yani wewe mbona nguo umeharibu hivyo mtoto kajibu nilikuwa natafuta nguo yangu ila sijafanikiwa na ndo naendelea kuitafuta dadeq yani ndani humo nililia machozi kwa Mungu, yani niliomba kila sala na nkaapa uzinzi naacha.

Mara mtoto akaanza mama amekuja hapa mama flani amenambia ukija tu uende anakuita (sasa hapa sijui alikuwa anadanganya au ilikuwa ukweli maana sikufanikiwaga kumuuliza) mama yake kaanza yani si aje tu mimi nimechoka kipindi hicho wapo chumbani nkasema leo nafia humu Mara nasikia anabadilisha nguo anamwambia mtoto wake aah ngoja tu niende daah aisee sikuamini yani alovyoondoka tu demu kanichomoa kanitoa yani miguu inatetemeka balaa aisee Mungu huyu acheni aitwe Mungu

Mungu ni mwema kila saa japo sisi binadamu tunamtenda kila kukicha ila haachi kutuonesha ukuu wake
 
Kuna muda bwana unaweza ukabanwa na mambo magumu katika maisha, na ukashindwa njia zote hatimae ukaamua kumuomba Mungu moja kwa moja na akakujibu?

Mimi kuna matukio kadhaa aisee naamini moja kwa moja Mungu ndiye alinisaidia.

1. Kukingwa na mvua kubwa
Mnamo mwaka 2008 nilikuwa katika moja ya shughuli za utafutaji katika Kijiji kimoja kinaitwa MKANYAGENI huko Tanga. Tulikuwa katika mapori fulani huko tukichana mbao. Lakini siku mbele baadae nilianza kuumwa na homa kali Sana. Jamaa zangu wakaamua kuniruhusu na kurudi mjini ili nisije nikawafia kule.

Safari ilikuwa Ni ndefu na ni ya mguu, nilitembea kilomita kadhaa na hatimae nikashindwa kabisa kutembea kutokana na kuishiwa nguvu.

Nikiwa nimekaa chini sijui cha kufanya, angani ilitanda mvua moja kubwa Sana, dakika chache baadae ikaanza kunyesha. Pale nilipo hapakuwa na nyumba wala sehemu yoyote ya kujizuia na mvua.

Kiukweli niliamua kumwambia Mwenyezimungu kana kwamba naongea na mtu. Nikasema "Ewe Mwenyezimungu, nakuomba uizuie mvua hii mpaka ntakapofika mjini kwani Kama ikininyeshea hapa hakika sitoweza hata kutembea"

Basi mvua ile ilikata na nilijikongoja mpaka kufika pale MKANYAGENI majira ya saa 2 usiku tangu saa 10 jioni.

Nilipofika tuuuu, aisee mvua iliachiwa sijapata ona... Daaah nkasema kweli Mungu yupo.

2. Chakula cha hapo kwa hapo.
Mwaka 2015, siku moja nikiwa sina hata mia mbovu. Mipango yangu yote imepinda. Njaa inaniuma sijakula siku nzima mpaka nikafikia hatua ya kulegea kwa njaa.

Niliamua kumwambia Mungu nisaidie, nitakufa na hii njaa mimi mja wako.

Nilitoka kuelekea nisikokujua, lakini baada ya dakika kadhaa niliamua kurudi tu geto.

Aisee kitu cha kushangaza WALLAAHI nilimkuta mtoto wa jirani pale mlangoni kwangu akinisubiri na akiwa ameshika bakuli ya wali.. kwa kudai kuwa amepewa na mama yake aniletee... Nilishangaa Sana maana huyo mama wala Sina mazoea nae wala HAKUWA jirani wa karibu...

Nkasema kweli Mungu amejibu maombi. Asante sana Mungu.

3. Kuokoka ka kufumaniwa na mke wa mtu.

Hii ilikuwa ni mwaka 2017... Sitosahau.

Nikiwa ndani kwa mtu na mke wake.. Jamaa hakuwa mji ule kabisa alikuwa kikazi mji mwingine. Lakini hammad ghafla tukasikia sauti za honi ya gari getini ikimaanisha kuwa msela ameshafika.... Yule mama alikwenda kufungua geti nikiwa nimejificha nyuma ya friji nikisali maombi yote.

Mara mprado huo ndani mzee kaingia..

Daah kumbe alisahau simu mfuko wa mbole katika duka flan huko mjini, ikabidi awashe tena gari arudi kuchukua kwa ajili ya matumizi ya kesho.

Nafkiri mbio nilizotoka nazo pale Ni zaidi ya BOEING 787. Na ikawa mwisho wa kudate na Iile shuga mamy. Hakika mzee angenikamata Ningekufa tu.

Acheni wake za watu hata wakijirahisisha.

Ila jaman MUNGU ANAJIBU MAOMBI kwa aombae kwa dhati.
Miaka kadhaa nyuma nikiwa Safarini Kikazi kwenda Mwanza nikapitia Moro kwa Bi Mkubwa kumsabahi na kulala home kwa siku mbili tatu maana nilikuwa na Private Car.
Kesho yake jioni Bi Mkubwa akanipeleka nje ya Mji kwenda kuangalia Shamba / Kiwanja ambacho nilikinunua Baadae.
Mara baada ya kumaliza kuangalia Shamba hamad Funguo za Gari sizioni,nilikuwa nimevaa Jeans yangu moja mfuko mmoja wa mbele kwa ndani ulikuwa umetoboka.
Sikukumbula niliweka mfuko gani ila nikahisi ntakuwa niliweka kwenye huo mfuko.
Tukaanza kutafuta kuanzia nilipo park Gari,Kumbuka giza lilishaingia na tuko Mashambani, Gari New Model,huwezi kuchonga funguo kiholela Mpaka uende through Manufacturer na kazini wanajua Mwanaume niko Safarini Mwanza.
Tafuta na kutafuta hamna kitu.
Bi Mkubwa akaanza ku Panic, Mzee mwenye Shamba ka Panic,anaogopa, Akaja kijana wake wa Maziwa kusaidia kutafuta, mimi Simu yangu charge imeisha hivyo torch imezimika.
Kijana akaja na torch.
Nikamwambia Mungu, wewe wajua hizi funguo nilipozidondosha, naomba uniongoze nizipate, nikamuweka Kijana Mbele na torch Mimi nyuma kwenda katika Manyasi nilipokuwa nakagua shamba, kufika katikati nikahisi nimeona kitu cheusi,akili ya mwanzo ikaniambia ni kinyesi cha Ng'ombe tu,nikapiga hatua kuendelea, lakini kuna kitu kikaniambia hebu rudi hatua moja nyuma uangalie vizuri.
Kurudi that was the Car Key
Lile tukio ni dogo ila liliiikuza sana Imani.
yangu juu ya uwezo wa Mungu.
Rest in Peace my Bi Mkubwa, Shamba nililonunua kwa ajili yako wala hukulifaidi
 
Mungu acha aitwe Mungu

Ipo hivi, nilienda kuchakata demu wangu kwao si nkajisahau bwana hadi mida ya jioni ambapo hiyo mida mama yake ndo huwa anarudi kutoka job( huyu mama ni mkali balaa yani kukutia kisu hashindwi).

Mara tukamuona mdogo mtu anakuja mbio oooh mama anakuja, hatujajiandaa kwa lolote Mara huyo tunamuona kwenye dirisha anapita ili aingie ndani dah hiyo siku nilidata aisee!

Kilichofanyika pale demu kanichukua mpaka chumbani kwa mama yake kwenya mabegi akatoa manguo akanambia lala juu ya mabegi halafu akafunika juu zile nguo halafu demu hakuondoka hapo akajifanya kama anatafuta nguo.

Mama mtu kaingia chumbani kwake kamkuta mtoto mtu kama anatafuta nguo kumbe mimi nipo kwa ndani basi wakasalimiana halafu mama mtu akaanza yani wewe mbona nguo umeharibu hivyo mtoto kajibu nilikuwa natafuta nguo yangu ila sijafanikiwa na ndo naendelea kuitafuta dadeq yani ndani humo nililia machozi kwa Mungu, yani niliomba kila sala na nkaapa uzinzi naacha.

Mara mtoto akaanza mama amekuja hapa mama flani amenambia ukija tu uende anakuita (sasa hapa sijui alikuwa anadanganya au ilikuwa ukweli maana sikufanikiwaga kumuuliza) mama yake kaanza yani si aje tu mimi nimechoka kipindi hicho wapo chumbani nkasema leo nafia humu Mara nasikia anabadilisha nguo anamwambia mtoto wake aah ngoja tu niende daah aisee sikuamini yani alovyoondoka tu demu kanichomoa kanitoa yani miguu inatetemeka balaa aisee Mungu huyu acheni aitwe Mungu

Mungu ni mwema kila saa japo sisi binadamu tunamtenda kila kukicha ila haachi kutuonesha ukuu wake
Amen, always God is good.
 
Basi bwana, iko hivi mwaka 2012 nikiwa kidato Cha sita niliishiwa kabisa hela ya matumizi. Kila nikiomba hela nyumbani wanasema hawana. Mimi hapo Sina kila kitu.
Siku moja usiku nikamuomba mungu anijalie nipate japo hata sh. 1000. Ilipofika asubuhi nikaingia darasani Kama kawaida, mchana tukaenda kula.
Kama mjuavyo baada ya kula mtu huhitaji kwenda haja kubwa. Nikaianza safari ya kwenda msalani ee bwana wee njiani nikakutana ma 2000, nakwambia nilimshukuru mungu balaa. Ile buku mbili ilinisaidia Sana. Hakika mungu Ni mwema Sana.
 
Pole sana mkuu... Apumzike kwa amani
Miaka kadhaa nyuma nikiwa Safarini Kikazi kwenda Mwanza nikapitia Moro kwa Bi Mkubwa kumsabahi na kulala home kwa siku mbili tatu maana nilikuwa na Private Car.
Kesho yake jioni Bi Mkubwa akanipeleka nje ya Mji kwenda kuangalia Shamba / Kiwanja ambacho nilikinunua Baadae.
Mara baada ya kumaliza kuangalia Shamba hamad Funguo za Gari sizioni,nilikuwa nimevaa Jeans yangu moja mfuko mmoja wa mbele kwa ndani ulikuwa umetoboka.
Sikukumbula niliweka mfuko gani ila nikahisi ntakuwa niliweka kwenye huo mfuko.
Tukaanza kutafuta kuanzia nilipo park Gari,Kumbuka giza lilishaingia na tuko Mashambani, Gari New Model,huwezi kuchonga funguo kiholela Mpaka uende through Manufacturer na kazini wanajua Mwanaume niko Safarini Mwanza.
Tafuta na kutafuta hamna kitu.
Bi Mkubwa akaanza ku Panic, Mzee mwenye Shamba ka Panic,anaogopa, Akaja kijana wake wa Maziwa kusaidia kutafuta, mimi Simu yangu charge imeisha hivyo torch imezimika.
Kijana akaja na torch.
Nikamwambia Mungu, wewe wajua hizi funguo nilipozidondosha, naomba uniongoze nizipate, nikamuweka Kijana Mbele na torch Mimi nyuma kwenda katika Manyasi nilipokuwa nakagua shamba, kufika katikati nikahisi nimeona kitu cheusi,akili ya mwanzo ikaniambia ni kinyesi cha Ng'ombe tu,nikapiga hatua kuendelea, lakini kuna kitu kikaniambia hebu rudi hatua moja nyuma uangalie vizuri.
Kurudi that was the Car Key
Lile tukio ni dogo ila liliiikuza sana Imani.
yangu juu ya uwezo wa Mungu.
Rest in Peace my Bi Mkubwa, Shamba nililonunua kwa ajili yako wala hukulifaidi
 
Mengi sana ila mara ya mwisho niliomba nifanikiwe upande wa masomo kwa ufupi nilichoomba kilikua 100% perfect ila hii hitokea nikiwa serious na hiko kitu
 
mimi ilinitokea nilipewa mtihani mgumu kweli kweli chuoni sikujua naanzia wapi nikamwomba mungu nikasikia sauti inaniambia tizama ubaoni nikaona notisi za majibu yote ya maswali zimeandikwa ubaoni nikawa nanyanyua kichwa naangalia ubaoni nakopi kama ilivyo hadi msimamizi wa mitihani akawa ananikodolea macho ananishanga shangaa nikaibua na A KWENYE HILO SOMO

NILIPOMALIZA KUANDIKA YAKAFUTIKA YENYEWE
Mmmh like serious?..hii ni zaidi ya miracle
 
Mimi naona Ni uwezo tu aliotupa Mungu, kuwa ubongo wetu umegawanyika sehemu kuu mbili. Subconscious Mind & Conscious Mind.

Kazi kubwa hapa nikuwa ubongo wa matendo yasiyo ya HIYARI Ni pamoja na kufanyia kazi Yale yote uliyoyawaza kuwa ya kweli bila kujali Ni mabaya au mazuri.

Na ikiwa utaamini huwa yanatokea Kama muujiza, Na hapa huwa inashauriwa uyaandike na kubandika ukutani kwako ili yajirudie rudie kichwani yafanyiwe kazi.

Waliosoma THE POWER OF YOUR SUBCONSCIOUS MIND watanielewa vizuri. Ila kifupi UBONGO wa binadamu una nguvu za maajabu kuliko tunavyojua. Fikiria leo upewe dk tano kwa hiyari yako uendeshe matendo yote yasiyo ya hiyari Kama uyeyushaji wa chakula, kupumua,kupepesa macho,mapigo ya moyo nk Ni wazi kuwa hakuna atakayeweza.

Tuna nguvu za ajabu Sana ndani yetu Ila hatujui kuzitumia na wanaojua hawaziamini. "THE MAGIC POWER OF SUBCONSCIOUS MIND WITHIN YOU HAVE TREASURE"
 
Attachments

  • Subconscious Mind Power How to Use the Hidden Power of Your Subconscious Mind ( PDFDrive.com ).pdf
    554.1 KB · Views: 33
Back
Top Bottom