Mambo gani umewahi kumuomba Mungu na akakujibu papo hapo?

Nilifanya forgery nyumbani nikaepeleka report from ya uongo baadae nika mwambia mzee wangu nahama shule nikatengeneza sababu za uongo bahati nzuri Uganda hawajali uhamisho hasa shule za private
so mzee hajui mpaka leo?vipi life la uganda?
 
Mungu anajibu.
mwaka 2014 mke wangu alikuwa mjamzito, ikafika kipindi cha kujifungua kutokana na tarehe iliyokisiwa huko kliniki. Kipindi hicho sina hata mia mbovu mfukoni nilikuwa nimenunua vitu vichache kwa ajili ya maandalizi na kulipa kodi ya nyumba hivyo mfukoni nikawa mweupe.
kusema kweli nilitamani tarehe ya kujifungua isogezwe mbele kama ingewezekana ili nijipange, nakumbuka kuna mda nakosa usingizi usiku utafikiri mimi ndio naenda kujifungua kutokana na mawazo ya kukosa hela. kuna siku moja niliamka asubuhi sana nikajiunga kifurushi cha mia tano iliyobaki kwenye mpesa ili niwapigie jamaa zangu kuwakopa hela, kila ninayempigia ananipa sababu zake za kushindwa kunikopesha. Nikaanza kuwatafuta wale wa karibu lakini kote hola, da nikachoka mwili na akili.
nikarudi nyumbani nikiwa mnyonge hata njaa sihisi, ikafika usiku wife akaanza kulalamika kuumwa tumbo hapo ndio nikazidi kuchanganyikiwa ingawa sikuwa mtu wa kanisani nikaanza kusali, nikakukumbuka mstari mmoja wa kwenye biblia kwamba Mungu anawanyeshea mvua wenye haki na waovu nikasema Mungu nikumbuke na mimi, tangu saa nane usiku sikupati usingizi tena. Asubuhi ikafika hali ikazidi kuwa mbaya mara simu yangu ikaanza kuita kuangalia naona namba ya baba nikapokea akaniuliza umeiona meseji? nikasema hapana, akasema nimekutumia laki tano mpesa kuna hela nilikuwa naisubiri siku nyingi ndio nimelipwa nikaiona nikupe na wewe kidogo, aisee kama kuna siku ambayo nilipata furaha ile ni siku moja wapo.
comment yangu ni ndefu na simu inaishiwa chaji.
Sifa,Heshima na Utukufu ni kwake
 
Mkuu niombee Nina shida yangu nahitaji Mungu anijibu sasa na sio mwezi au mwaka mwingine
Saa Tisa usiku kamili leo amka weka alarm kwenye simu ikuamshe mwambie Mungu nirehemu kiumbe wako nisiye mkamilifu nisamehe makosa yangu nisaidie maombi haya ninayokuomba ukimaliza kuomba kaoge maji ya baridi huku ukisali kuwa ninapooga maji haya yasafishe kila kinachozuia maombi yangu yasipate majibu nakiosha kwa jina la Yesu Kisha kalale usubiri matokeo
 
Kwa nini iwe saa tisa usiku wa manane na sio muda mwengine?
 
Nilikuwa na kesi ya mirathi ya marehemu mume wangu ambae sikuzaa nae lakini tulipata mafanikio kipindi kifupi. Ile kesi ilitawaliwa na upendeleo nadhani na rushwa hivyo ikaonekana mimi kama sina haki. Hakimu na watoto walikuwa wananitia maneno ya kuudhi sana kiasi siku moja nilopotoka mahakani nilijifungia chumbani kwanza nililia sana kwa uchungu kisha nikaanza kuongea na Mungu kama nipo nae pale.

Nilichokuwa namuomba niweze kuliondoa hili swala katika mawazo na nafsi yangu na Liwe kama halinihusu na kama vile hakuna nilichopoteza.

Niliomba/kuongea takriban kwa saa nzima na baada ya hapo nilipata usingizi mzito sana na nilipoamka nikajikuta ni kama mtu aliyetua mzigo sana.

Hadi hii leo ni mwaka wa 17 sikurudi tena mahakamani na nilishasahau kabisa!
MUNGU ANAJIBU ANAPOOMBWA KWA DHATI
So ukapoteza haki yako?
 
Wakati Fulani mwaka 2011 mwishoni nikiwa nafanya kazi wilayani Same mkoani Kilimanjaro , mshahara ulikatikia njiani maana waajiriwa mishahara huwa haikutani....

NYUMBANI nimemwacha wife asubuhi bila kumi kwa kumdanganya naenda job mara moja Kuna mtu Ana hela yangu then nakuletea.....

Kufika ofisini Kila mtu ninayempiga mzinga Hana na ilikaribia Christmas inabidi kufanya shopping maana nilikuwa pia na binti wa 6 years.

Nikatoka ofisini nikaenda jirani tu kidogo kwa jamaa yangu saa hiyo imekaribia saa sita.... Jamaa Ni bachelor tu na alikuwa anaandaa Ugali samaki wa lunch....... Piga mzinga Hana kitu.....

Nikawa nimekaa sebuleni kwake nimejilaza kwenye Kochi , machozi yanalenga lenga...... Nikamlilia Mungu , Mimi Ni mwenye dhambi , Sina hata chembe ya jema nafsini kwangu lakini naomba leo unisaidie.... NYUMBANI Sina kitu hata chakula Cha leo tu..... Baada ya kusali kausingizi kakaanza kuja......

Jamaa akaniamsha tupige Ugali samaki, ile nataka kunawa mikono simu kitochi yangu ikalia mlio was sms....... Kucheki......mamaamamaaa................................................. Toka tigopesa umepokea kiasi Cha shilingi 375,000#....... Na vichenchi kadhaa Kama Tigopesa Commission ya wakala..................

Kwakweli niliinuka pale na kutoka mbio moja matata sana Hadi stendi ya Same kwa Wakala nikaitoa yote then nikafululiza Hadi duka moja la vitabu vya dini pale same sokoni nikanunua Biblia ambayo Hadi Leo ninayo.............. Nikanunua na bapa moja la Konyagi na grandmalta kadhaa na vikopo vya soda.......then nikaingia sokoni pale nikachukua nyama na viungio vyake full ..........

Fika home nika-apologize kwa kuchelewa nikawapiga laki mbili na mazagamazaga........ Na soda za kupunguzia hasira.........

Nikapiga simu ofisini Nina udhuru. Nikapiga bapa langu.....maisha yakasonga.....

Nilimshukuru Mungu sana kwa Hili na ninaendelea kumshukuru maana SIJAWAHI KUWA WAKALA WA TIGO PESA ILA KWA MAAJABU NIKAPATA COMMISSION... Mimi Ni mdhambi ila aliniangalia akanionea huruma....... Na akasikiliza Sala na maombi yangu.

Kwa kweli ukiomba kwa Imani Mungu anatenda.......

Blessing
 
Wakati Fulani mwaka 2011 mwishoni nikiwa nafanya kazi wilayani Same mkoani Kilimanjaro , mshahara ulikatikia njiani maana waajiriwa mishahara huwa haikutani....

NYUMBANI nimemwacha wife asubuhi bila kumi kwa kumdanganya naenda job mara moja Kuna mtu Ana hela yangu then nakuletea.....

Kufika ofisini Kila mtu ninayempiga mzinga Hana na ilikaribia Christmas inabidi kufanya shopping maana nilikuwa pia na binti wa 6 years.

Nikatoka ofisini nikaenda jirani tu kidogo kwa jamaa yangu saa hiyo imekaribia saa sita.... Jamaa Ni bachelor tu na alikuwa anaandaa Ugali samaki wa lunch....... Piga mzinga Hana kitu.....

Nikawa nimekaa sebuleni kwake nimejilaza kwenye Kochi , machozi yanalenga lenga...... Nikamlilia Mungu , Mimi Ni mwenye dhambi , Sina hata chembe ya jema nafsini kwangu lakini naomba leo unisaidie.... NYUMBANI Sina kitu hata chakula Cha leo tu..... Baada ya kusali kausingizi kakaanza kuja......

Jamaa akaniamsha tupige Ugali samaki, ile nataka kunawa mikono simu kitochi yangu ikalia mlio was sms....... Kucheki......mamaamamaaa................................................. Toka tigopesa umepokea kiasi Cha shilingi 375,000#....... Na vichenchi kadhaa Kama Tigopesa Commission ya wakala..................

Kwakweli niliinuka pale na kutoka mbio moja matata sana Hadi stendi ya Same kwa Wakala nikaitoa yote then nikafululiza Hadi duka moja la vitabu vya dini pale same sokoni nikanunua Biblia ambayo Hadi Leo ninayo.............. Nikanunua na bapa moja la Konyagi na grandmalta kadhaa na vikopo vya soda.......then nikaingia sokoni pale nikachukua nyama na viungio vyake full ..........

Fika home nika-apologize kwa kuchelewa nikawapiga laki mbili na mazagamazaga........ Na soda za kupunguzia hasira.........

Nikapiga simu ofisini Nina udhuru. Nikapiga bapa langu.....maisha yakasonga.....

Nilimshukuru Mungu sana kwa Hili na ninaendelea kumshukuru.... Mimi Ni mdhambi ila aliniangalia akanionea huruma....... Na akasikiliza Sala na maombi yangu.

Kwa kweli ukiomba kwa Imani Mungu anatenda.......

Blessing
Mjinga wewe, ukanunua bible na bapa la konyagi at once
 
Saa Tisa usiku kamili leo amka weka alarm kwenye simu ikuamshe mwambie Mungu nirehemu kiumbe wako nisiye mkamilifu nisamehe makosa yangu nisaidie maombi haya ninayokuomba ukimaliza kuomba kaoge maji ya baridi huku ukisali kuwa ninapooga maji haya yasafishe kila kinachozuia maombi yangu yasipate majibu nakiosha kwa jina la Yesu Kisha kalale usubiri matokeo
Maj ya SAA 9 ucku kwa mkoa huu wa baridi ni ngumu
 
Back
Top Bottom