Mambo ambayo yanatakiwa kupiganiwa na vijana wanaojitambua mwaka 2017

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kijana wazalendo wa nchi yao na kijana wa wasaka tonge, kijana mzalendo huwa amekomboka kifikra na anapambana kuondoa mfumo ambao unakandamiza haki za watu tofauti na kijana anaesaka uongozi ndani ya serikali anaepigania Fursa na Ajira.

Tunapoukaribisha mwaka 2017 kuna mambo ambayo vijana wanamabadiliko wote Tanzania tuyapiganie ili kulinda utu, haki na Heshima ya nchi yetu, na hapa ndio Mwanzo wakupata vijana kama wakina Steven Bhiko wa Tanzania wa kukupigania taifa letu.

Vijana wana Mabadiliko tunakibarua kizito ambacho vijana wenzetu wa south Africa walitua mzigo wa mapambano dhidi ya utu wao baada ya kupambana kwa zaidi ya miaka 50 kupigania utu wao heshima pamoja thamani ya Uafrika watu.

Wao walifanikiwa kwa sababu ya kuondoa uoga kuona thamani ya nchi na utu wao haiwezi kulingana na thamani ya Damu na uhai wao, kwa hiyo basi tunapo elekea Mwaka 2017 tunatakiwa kujua kila kipindi kinapigania Uhuru wake sasa tunatakiwa kupigania uhuru wetu.

Sasa sisi kama vijana wana MabadilikoTanzania Kuna mambo tunatakiwa kuyafanya kwa ajili ya kukumbukwa na vizazi vyetu vizavyo kama vijana wa South Africa wanavyokumbukwa Leo kwa kupigania Uhuru wao mambo ya kupigania mwaka 2017 ni kama yafutayo;-

Tume huru ya uchaguzi ili ndio jambo la kwanza ambalo kila kijana mpenda mabadiliko unatakiwa aliwekee kipaumbele chake mwaka 2017 ni aibu sana sisi kama vijana kusubiria kushinda wakati tume ya Uchaguzi yote niwateule wa Rais kuanzia Mtendaji wa Mtaa au kijiji mpaka mwenyekiti wa tume taifa tena cha kushangaza ni makada kwa hiyo tunatakiwa kupigania hili sio kwa maneno kwa vitendo.

Bunge live Kuwaona wawakilishi wetu wanachokifanya kwenye vikao vya maamuzi ni haki yetu wote bila kujali vyama vyama vyao sasa tutajuaje mbunge wangu kero ya maji nilimtuma ameiongelea ni maana kazi ya wabunge sio kujenga barabara bali ni kuiambia Serikali watumie kodi zetu kuleta barabara kwa hiyo tusiwaona wabunge wetu wanafanya nini tutegemee uwakilishi mbovu wa wabunge kusaini posho tu na kufanya starehe hii ni kazi nyingine ya vijana mwaka 2017.

Kupigania Demokrasia hii ni kazi ya vijana kuwa mstari kutetea katiba inapovunjwa kukatazwa kwa Mikutano ya vyama vya siasa ni ishara ya kukanyagwa Demokrasia kuwa hivyo basi kijana aejielewa yuko tayari mda wowote kutetea katiba ya nchi yake inapovyunjwa na hii ni kazi ya vijana mwaka 2017.

hakuna haki hakuna usawa kama wewe ni kijana wa kitanzania upo na umekaa kimya basi ujue umekubalia na wapokonya haki mwaka 2017 ni Mwaka wa kutoka kwenye Social Media (Facebook na watsapp) na kuacha kulalamika na kupigania kwa vitendo mambo hayo.

Wakina Karl max na Fedrick Angel waliandika vitabu vya Communist Manifesto na Das Capital kuupinga ubeberu lakini Mao Tse Tung na Vladimir Lenin waliweka kwa vitendo wakauondoa ubeberu, vitendo vinamanufaa zaidi kuliko maneno Mwaka 2017 tuufanye ni Mwaka wa vitendo.

Asanteni sana.
 
Vijana kama wewe ni tunu ya taifa.Akina Ben Saanane(kila la kheri huko aliko) walianza mapambano japo kwa namna nyingine.
Mapambano hayo yalipaswa kuongozwa na wingi ya vijana wanaharakati au wanachama wa upinzani.
Kama kweli mtaamua,mtabarikiwa ila muwe na akili kama nyoka wa kwenye biblia.
 
2017 ni mwaka kupigania kipengele naamba 3.2.C kibadilishwe katika katiba yetu pendwa ya Chadema.
tmp_7809-_20161227_210717-1443663799.JPG
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kijana wazalendo wa nchi yao na kijana wa wasaka tonge, kijana mzalendo huwa amekomboka kifikra na anapambana kuondoa mfumo ambao unakandamiza haki za watu tofauti na kijana anaesaka uongozi ndani ya serikali anaepigania Fursa na Ajira.

Tunapoukaribisha mwaka 2017 kuna mambo ambayo vijana wanamabadiliko wote Tanzania tuyapiganie ili kulinda utu, haki na Heshima ya nchi yetu, na hapa ndio Mwanzo wakupata vijana kama wakina Steven Bhiko wa Tanzania wa kukupigania taifa letu.

Vijana wana Mabadiliko tunakibarua kizito ambacho vijana wenzetu wa south Africa walitua mzigo wa mapambano dhidi ya utu wao baada ya kupambana kwa zaidi ya miaka 50 kupigania utu wao heshima pamoja thamani ya Uafrika watu.

Wao walifanikiwa kwa sababu ya kuondoa uoga kuona thamani ya nchi na utu wao haiwezi kulingana na thamani ya Damu na uhai wao, kwa hiyo basi tunapo elekea Mwaka 2017 tunatakiwa kujua kila kipindi kinapigania Uhuru wake sasa tunatakiwa kupigania uhuru wetu.

Sasa sisi kama vijana wana MabadilikoTanzania Kuna mambo tunatakiwa kuyafanya kwa ajili ya kukumbukwa na vizazi vyetu vizavyo kama vijana wa South Africa wanavyokumbukwa Leo kwa kupigania Uhuru wao mambo ya kupigania mwaka 2017 ni kama yafutayo;-

Tume huru ya uchaguzi ili ndio jambo la kwanza ambalo kila kijana mpenda mabadiliko unatakiwa aliwekee kipaumbele chake mwaka 2017 ni aibu sana sisi kama vijana kusubiria kushinda wakati tume ya Uchaguzi yote niwateule wa Rais kuanzia Mtendaji wa Mtaa au kijiji mpaka mwenyekiti wa tume taifa tena cha kushangaza ni makada kwa hiyo tunatakiwa kupigania hili sio kwa maneno kwa vitendo.

Bunge live Kuwaona wawakilishi wetu wanachokifanya kwenye vikao vya maamuzi ni haki yetu wote bila kujali vyama vyama vyao sasa tutajuaje mbunge wangu kero ya maji nilimtuma ameiongelea ni maana kazi ya wabunge sio kujenga barabara bali ni kuiambia Serikali watumie kodi zetu kuleta barabara kwa hiyo tusiwaona wabunge wetu wanafanya nini tutegemee uwakilishi mbovu wa wabunge kusaini posho tu na kufanya starehe hii ni kazi nyingine ya vijana mwaka 2017.

Kupigania Demokrasia hii ni kazi ya vijana kuwa mstari kutetea katiba inapovunjwa kukatazwa kwa Mikutano ya vyama vya siasa ni ishara ya kukanyagwa Demokrasia kuwa hivyo basi kijana aejielewa yuko tayari mda wowote kutetea katiba ya nchi yake inapovyunjwa na hii ni kazi ya vijana mwaka 2017.

hakuna haki hakuna usawa kama wewe ni kijana wa kitanzania upo na umekaa kimya basi ujue umekubalia na wapokonya haki mwaka 2017 ni Mwaka wa kutoka kwenye Social Media (Facebook na watsapp) na kuacha kulalamika na kupigania kwa vitendo mambo hayo.

Wakina Karl max na Fedrick Angel waliandika vitabu vya Communist Manifesto na Das Capital kuupinga ubeberu lakini Mao Tse Tung na Vladimir Lenin waliweka kwa vitendo wakauondoa ubeberu, vitendo vinamanufaa zaidi kuliko maneno Mwaka 2017 tuufanye ni Mwaka wa vitendo.

Asanteni sana.
Kama ulikuwa na kapoint kidogo mwanzoni, walewale. kumbe hukuwa unaongea na vijana wote wa kitanzania, ulikuwa ukiongea na vijana makada wa vyama vya siasa tu tena haswa Bavicha.

Lakini, hayo yasingekuwa tatzo sana, ningekuunga mkono tu, ila najiuliza kwanza, hivi ni kweli kuliona bunge au demokrasia ndo kilio kikuu cha watz? Haswa akina mjomba village?

Nadhani mtu ukiwa na dai la msingi na ni la haki, utashinda. Sasa akina Max na Mao na wengine walitaka kuwaondoa mabeberu, sa mbona we unataka tupiganie kurudi kwao?

Uhuru sawa, lakini upi haswa? Lazima tujipange vyema ili tupiganie mara moja na kwa umilele. Biko angekuwepo leo, angejiunga na akna Malema na mapigano yangeendelea. Sisi adui wetu haswa ni yupi? Sipingi wazo la katiba mpya wala tume huru, ila hivyo tu tukishavipata tutakuwa tumeshatatua yote?
 
Mavijana yenyewe ndo haya ya buku saba ma nafiki yanajipendekeza ili yapate ukuu wa wilaya
 
Back
Top Bottom