Mambo ambayo Serikali ya awamu ya tano imeyafanyia kazi baada ya kubandikwa hapa JamiiForums

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,799
Ni mengi yameletwa hapa jukwaani kwa muda mrefu na kwa awamu tofauti tangu zama za utawala wa Mr. Clean a.k.a Ben Mkapa ambapo jukwaa hili lilianza rasmi likijulikana kwa jina la @JamboForums.

Alipoingia Mkwere a.k.a Jakaya Kikwete, naye aliendelea kupitia pitia

JamiiForums ambapo mengi aliyafanyia kazi ikiwemo ile kesi ya mama kudhulumiwa nyumba na jina papaa msofe.

Utawala wa Magufuli nao hauko nyuma kwenye kuokoka mawili matatu, na Tayari wazo la Pascal Mayalla la kutaka twitter ifungiwe tayari limesha fanyiwa.

Hebu wenzangu tuyaorodheshe na mengine ambayo yanafanyiwa kazi kutokana na kubandikwa hapa jukwaani.
Allah msikh
 
Na kutaka jamii forum kuipoteza kabisa Tanzania lakini imeshindikana.

Achange karata zake vizuri, kwa style hii ameshindwa labda a change information.
 
Jiwe hana mapenzi kabisa na social media platforms zote. Jamiiforums ndiyo usiseme kabisa, na ndiyo maana mmiliki wake amepewa makesi lukuki kwa kutukingia kifua na kuendelea kuficha IDs zetu
 
Sio rahisi kuitenga JF na Serikali kwani Members wake wengi ni Watanzania ambao ni watumishi, au Wana ndugu ambao ni watumishi au viongozi au wenye ndugu ambao ni viongozi hivyo jambo likiandikwa hapa ni rahisi kufanyiwa kazi, kwani ID hizi zimetupa uhuru wa kuwasilisha mambo kwa kina kuliko sehemu nyingine yeyote.

Binafsi nimeshuhudia mambo mengi sana yakizungumzwa hapa ama yatokee ama yafanyiwe kazi na serikali.

1. Nimeshuhudia utabiri wa Mgombea nafasi ya Urais kwa 2015 ukitokea.

2. Nimeshuhudia utabiri wa mgombea urais kwa Chadema ukitokea (binafsi pia niliandika mada 2016).

3. Utabiri wa vurugu za kinondoni ( refer Aquilina's case) nakumbuka nilitoa angalizo.

4. Utabiri wa Chadema kuwa na Mbunge mmoja 2020 ( Nakumbuka pia hii)

Looh ni Mengi Sana kwa kweli.

Binafsi niwashukuru Sana waanzilishi wa JF kwani tumepata platform ya kutoa yaliyomo mioyoni na akilini mwetu beyond the physical limits.

Thanks JF.
 
Jiwe hana mapenzi kabisa na social media platforms zote. Jamiiforums ndiyo usiseme kabisa, na ndiyo maana mmiliki wake amepewa makesi lukuki kwa kutukingia kifua na kuendelea kuficha IDs zetu
Kesi ya JF imeanza tangu awamu ya nne na sio ya tano.

Yapo mengi sana yamefanyiwa kazi, hususan ya kufichua ubadhirifu!

Tumeona viongozi wakibadilishwa na wakati mwingine tumeona teuzi!

Tatizo limeanza pale JF ilipobadilika kutoka "The Home of Great Thinkers" ikawa ni jukwaa la kuwaporomoshea matusi watawala mpaka na familia zao.

Pia mambo yaliharibika pale ambapo ilionekana JF ikilalia upande wa chama pinzani na kuiporomoshea matusi CCM!

I real miss the "original JF" I wish ingerudishwa tuijenge nchi yetu! Bado hatujachelewa!!!
#bringbackourjamiiforum

Queen Esther
 
Ni mengi yameletwa hapa jukwaani kwa muda mrefu na kwa awamu tofauti tangu zama za utawala wa Mr. Clean a.k.a Ben Mkapa ambapo jukwaa hili lilianza rasmi likijulikana kwa jina la @JamboForums...
Habari na wanahabari kuwekwa kundi la wakwamisha maendeleo
 
Ni mengi yameletwa hapa jukwaani kwa muda mrefu na kwa awamu tofauti tangu zama za utawala wa Mr. Clean a.k.a Ben Mkapa ambapo jukwaa hili lilianza rasmi likijulikana kwa jina la @JamboForums.

Alipoingia Mkwere a.k.a Jakaya Kikwete, naye aliendelea kupitia pitia

JamiiForums ambapo mengi aliyafanyia kazi ikiwemo ile kesi ya mama kudhulumiwa nyumba na jina papaa msofe.

Utawala wa Magufuli nao hauko nyuma kwenye kuokoka mawili matatu, na Tayari wazo la Pascal Mayalla la kutaka twitter ifungiwe tayari limesha fanyiwa.

Hebu wenzangu tuyaorodheshe na mengine ambayo yanafanyiwa kazi kutokana na kubandikwa hapa jukwaani.
Allah msikh
Mpambe wa rais wa Zanzibar Uzi nilileta mwenyewe kwanini amekaa muda mrefu sasa amebadilishwa
 
Back
Top Bottom