Mambo ambayo Jafar Haniu unapaswa kuyapa kipaumbele chaneli 10

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,066
2,000
Naam na yawe mambo 8...

Mods msiunganishe uzi huu.

Haniu fanya yafuatayo:-
1. Programming - Channel hii ina vipindi vingi local labda kuliko channel yoyote ya TV Tanzania lakini vipindi havijapangiliwa vipo hobelahobela.

2. Ubora wa picha - hili ni tatizo sugu hapo Channel Ten picha ni mbovu mno vipindi ni vizuri lakini picha mbovu braza...nakupa mfano kipindi cha Hamza Kasongo kikiwa Ch10 kilikuwa na content nzuri ila ubora chini mnoo huko kiliko sasa kinavutia kwa ubora. ..channel ten ina vipindi vizuri kabisa ila picha hazishawishi kabisa kutazama...Nashauri fedha alizotoa Mwenyekiti Dkt JPM uziwekeze first and foremost kununua mitambo ya kisasa Digital itakayowezesha ubora wa picha unaweza kuwa inspired na mitambo ya TV1 Tanzania just pay a courtesy visit kwa rafiki yako MUKHSIN MAMBO pale Tv1 ni kiongozi pale ujifunze aina ya mitambo wanayotumia au pay a courtesy visit pale NBS Channel ya UGANDA ukaone aina ya mitambo wanayotumia wana picha bora sana wale miongoni mwa TV stations za EA zenye quality ya juu ya picha. Cameras yes unaweza kuzihitaji lakini nadhani sio kipaumbele kuliko mitambo...mathalani picha za STATE HOUSE ulikotokea zikitumwa wakazitumia Ch10 kwenye bulletin bado zinakuwa mbovu wakati zile huwa always ni HD. Tfdhl zingatia kununua mtambo mpya wa transmission ndipo zifuate kamera etc
YOU NEED A MILLION PIXELS ili CHANNEL TEN iwe ya mfano kama mnavyopania.

3. Graphics- zamani nilipokuwa nafanya kazi kwenye media niliwahi kufanya kazi briefly hapo Ch 10 walikuwa na Mac PCs za kutosha ila hapakuwepo kabisa competent graphics designers...hakuna haja ku-import graphics kutoka Kenya kv logo wakati tuna vijana wamebobea kwenye graphics designing...shindanisha kupata designers wazuri.

3. Graphics zibadilishwe na ziwe kiwango-hiyo rejuvenation plan iwe classic na ya kiwango.

4. Set za studio zibadilishwe- Ch10 iachane na kutumia set za chroma keying kwa sababu kwanza hazina ubora (kuna flickering za kutosha) nashauri jengo jipya mnalotafuta liwe na space ya kutosha ili muweze ku-design multiple studios kv ya news,vipindi vya mahojiano ya ana kwa ana,entertainment pgms,sports nk...mkuu Haniu live set ni nzuri sana na unaweza kubadilisha tu Background kadri utakavyo.

5. Muda wa news ubadilishwe uwe saa 2. Msiogope ushindani saa 1 watu wengi wanakuwa barabarani shindaneni na wakongwe wenzenu hakuna cha kuogopa.

6. Presence ya Ch10 kwenye social networks itiliwe maanani eg active website, na social media pages both on Twitter, Instagram etc

7. Branding - yaani niamini kuna vijana wanaweza kuwa hawaifahamu Ch10 kwa sababu ya lower branding, hili ndilo lengo la idara ya Sales and Marketing wafanye kazi ya kui brand channel...logos ziwe everywhere kwenye microphones za news na programs, leaflets, banners, ma-concert, kusponsor events,kuruhusu live forums zirushwe Ch10 mfano symposiums za vyuo etc

8. Quality iwe motto yenu- ili kufanya ch10 ipendwe na vijana ubora uwe kipaumbele.

Nawatakia kila la kheri na sina shaka J.Haniu utaiondoa Channel ten hapo ilipo sasa. Kila la kheri

N'yadikwa

Narudia tena : mods msiuunganishe huu uzi ni barua ya wazi kwa Jafar Haniu.Sent using Jamii Forums mobile app
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
7,515
2,000
Hayo yooote uliyoyaandika ni ya maana mno ila huu ushauri wako utachukuliwa na mbao tv na sio Chanel ten wao watakuwa kama TBC tu hovyohovyo
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
3,994
2,000
Wasisahau kuweka kipindi cha'TUNATEKELEZA' kama wale wenzao wa TBC.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom