Mambo 70 muhimu ya wananchi yaliyofutwa katika Katiba Inayopendekezwa

uswaa

Member
Mar 4, 2014
55
20
1. Kupunguzwa kwa madaraka ya rais
Wananchi walipendekeza madaraka makubwa ya Rais hasa ya uteuzi yapunguzwe na ziundwe taasisi za kikatiba za kumshauri rais kabla hajafanya teuzi. Wananchi walipendekeza pia baada ya rais kumteua kiongozi basi itabidi mteuliwa huyo Bunge limthibitishe.
Katiba Inayopendekezwa imeyafuta haya yote na imemwongezea Rais madaraka.

2. Kutenganisha mamlaka ya mihimili ya dola
Wananchi walipendekeza uhuru zaidi kwa Bunge na mamlaka zaidi kwa Bunge kuisimamia, kuiwajibisha na kuishauri Serikali. Pendekezo hili linaenda sambamba na kutenganisha Serikali na Bunge, hali ambayo iko sasa. Rasimu ya Warioba ililipa Bunge mamlaka zaidi kuisimamia Serikali na hata pale ambapo Bunge lingekataa bajeti au muswada mbaya wa Serikali mara kadhaa, rais asingeliweza kulivunja Bunge. Wananchi walisema sana mawaziri wasitokane na wabunge, ili wabunge wafanye kazi ya uwakilishi pekee na mawaziri watumie weledi wao kumsaidia rais kazi za Serikali.
Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti haya.

3. Kumwajibisha mbunge
Rasimu ya Warioba iliwapa wapiga kura uwezo wa kuwawajibisha wabunge kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nao wakati wowote kama wakienda kinyume na masilahi ya wananchi katika jimbo husika. Wananchi walijiuliza kama mbunge ni mtumishi wao, iweje hayuko katika kituo cha kazi kwa miezi kadhaa na wasiweze kumwajibisha mpaka miaka mitano? Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti haya.

4. Vyanzo vya mapato vya kuaminika
Kuwapo kwa vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakavyogharimia mambo ya Muungano ambayo yamepunguzwa kutoka 22 hadi 7 lilikuwa pendekezo ambalo hata taasisi za Serikali zilipendekeza. Katiba Inayopendekezwa imerudisha mapato ya Muungano kama Katiba ya Mwaka 1977 na kwa kufanya hivyo tumerudi kwenye mgogoro wa msingi, kuchukua kodi tatu, ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa na mapato kutoka Zanzibar ni kuiua Zanzibar na kuifanya ishindwe kumudu matumizi yake ya ndani kwa mambo yasiyo ya Muungano na vivyo hivyo kwa Tanganyika.

5.Muundo wa shirikisho lenye mamlaka kamili
Kwa miaka nenda rudi tumekuwa na kitendawili cha ni muundo gani wa Muungano Jamhuri yetu inao. Kitendawili hiki kimeelezwa na wengi akiwamo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Rasimu ya Warioba iliweka kwa mara ya kwanza Muundo Jamhuri ya Muungano kuwa ni wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili, nchi moja na yenye Serikali tatu. Kilichoongezwa ni na Rasimu ya Warioba ilikuwa Bunge na Serikali ya Tanganyika na siyo nchi ya Tanganyika kama ambavyo wengi wameaminishwa hivyo. Katiba Inayopendekezwa imerejesha na kuudhoofisha zaidi muundo wa Serikali mbili, kwa kuifanya Tanganyika au Tanzania Bara kuwa ndiyo Jamhuri ya Muungano na Zanzibar kuwa na mamlaka zaidi kwa mambo yasiyo ya Muungano ikiwamo kujiunga na jumuiya za kimataifa.

6. Kupunguza ukubwa wa Serikali
Wananchi walionesha kutofurahishwa na ukubwa wa Serikali unaopelekea matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi. Walipendekeza uwapo wa Serikali ya Muungano iliyo imara, yenye ufanisi na ndogo. Rasimu ya Warioba ilisema idadi ya mawaziri isizidi 15.
Katiba Inayopendekezwa inasema mawaziri wasizidi 40, pendekezo hili halina uhalisia kwa sababu Serikali ya Muungano itashughulika na mambo ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika/ Tanzania Bara na kuifanya kuwa kubwa zaidi na hivyo kuhitaji mawaziri zaidi ya 40, kiufupi pendekezo hili halitekelezeki.

7. Tume ya Uhusiano na Uratibu
Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha kunakuwapo uhusiano mzuri, mawasiliano na uratibu wa serikali zote tatu chini ya Mamlaka ya Serikali ya Muungano na kupitia Tume ya Uhusiano na Uratibu. Bunge Maalumu lilishindwa kuelewa mantiki ya pendekezo hili na Katiba Inayopendekezwa imelivuruga kabisa, kutoka pendekezo la Warioba la "Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali" hadi "Tume ya Uratibu wa Mambo ya Muungano" katika Katiba Inayopendekezwa.

8.Kupunguza ukubwa wa Bunge
Wananchi walizungumzia pia ukubwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na gharama zinazoambatana nalo na wakapendeza Bunge dogo na lenye ufanisi mkubwa. Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalumu likasema wabunge wasipungue 340 na wasizidi 390.

9. Ukomo wa vipindi vya ubunge
Wananchi walizungumzia nafasi za ubunge kuhodhiwa na watu fulani kwa miaka nenda rudi na wakapendekeza ifike mahali kuwe na ukomo ili kuleta uwakilishi mpana na mabadiliko. Rasimu ya Warioba iliweka ukomo wa vipindi vya ubunge kuwa vitatu na kuwa na ukomo wa miaka 15 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Bunge Maalumu na Katiba Inayopendekezwa wamefuta pendekezo hili.

10. Kuwapo kwa tunu za Taifa
Wananchi walipendekeza uwapo wa tunu za Taifa katika Katiba, tunu hizi ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa. Raia wa Tanzania walikuwa na wajibu wa kuheshimu tunu hizi lakini Katiba Inayopendekezwa imezifuta tunu hizi.

11. Maadili na miiko ya viongozi
Wananchi walizungumza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya jamii, watumishi na viongozi wa umma, wengi wakisema Katiba iainishe maadili na miiko ya viongozi wa umma ambayo kwayo tutawawajibisha. Katiba Inayopendekezwa imesema maadili na miiko kwa viongozi (mathalan kutenganisha biashara na uongozi ili kuepusha mgongano wa masilahi), isiwamo kwenye Katiba bali ikawekwe kwenye sheria.

12. Masharti yasiyoweza kubadilishwa na Bunge
Rasimu ya Warioba iliweka masharti ya kuzuia Bunge kubadili baadhi ya masharti mahususi ya Katib, ibara ya 119 isipokuwa kwa ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni (mathalan malengo makuu ya Taifa, haki za binadamu n.k. Pia, bahati mbaya tulisahau kuweka na Sura ya tatu juu ya maadili). Masharti yote ya Ibara hii yamefutwa isipokuwa Muundo wa Muungano na Uwapo wa Jamhuri ya Muungano.

13. Kuwapo kwa Tume Huru ya Uchaguzi
Wananchi walizungumza umuhimu wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi za Jamhuri ya Muungano. Ilisisitizwa juu ya umuhimu wa tume kugawa majimbo ya uchaguzi na kwamba mwenyekiti wa tume na makamu wake wathibitishwe na Bunge ili kuwapa uhalali wa kitaifa, pendekezo hili limefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

14. Usawa wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume
Kuwapo uwiano wa uwalikishi wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima kwa mazingira ya sasa. Uwiano kati ya wanawake na wanaume katika vyombo mbalimbali vya dola hasa vile vya kutunga sheria limeendelea kuwa tatizo nchini na lililokaa kwa muda mrefu.

Wananchi na hasa wanawake na baadhi ya wanaume walipendekeza uwiano ulio sawa katika kufikia fursa hasa ukizingatia wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa. Rasimu ya Warioba ilipendekeza katika kila jimbo kutakuwa na wabunge wawili, wa kike na wa kiume, Katiba Inayopendekezwa imefutilia mbali pendekezo hili muhimu

15. Kuanzishwa kwa mgombea huru
Haki ya wananchi kushiriki shughuli za umma imekuwa ikizuiwa siku nyingi na kwamba ushiriki katika shughuli za umma kama kiongozi wa kuchaguliwa inapaswa kuwa haki ya msingi ya mwananchi yeyote yule. Rasimu ilitoa haki ya mgombea huru bila vikwazo, Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti magumu ambayo hakuna mtu anayeweza kuyatimiza kirahisi, kitendo hiki siyo sawa.

16. Msaada wa kisheria kwa wananchi
Wananchi walieleza kutokuridhishwa kwao na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji huo na wakapenda huduma ya msaada wa kisheria liwe suala la kikatiba kwa mwananchi yeyote yule na serikali iwajibike kutoa h
Katiba Inayopendekezwa imesema wananchi hawatakuwa na haki ya kudai huduma hii kokote nchini, hata mahakama hazitaweza kusikiliza mashauri ama Serikali imetoa haki hii au haikutoa haki hii rejea Ibara ya 21.

17. Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi
Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi atekeleze kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

18. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Wananchi Tanzania
Tume ya Warioba ilipendekeza kuwapo kwa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti haya licha ya wapiganaji kupendekeza utaratibu wa kusimamia masilahi yao kikatiba.

19. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi
Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itakayokuwa na jukumu la kusimamia utumishi wa Jeshi la Polisi. Katika uajiri wa askari wa Jeshi la Polisi, Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itazingatia kanuni na misingi ya utumishi iliyoainishwa katika Katiba hii
Wiki iliyopita tulianza kukuletea mambo 70 muhimu ya wananchi yaliyofutwa katika Katiba Inayopendekezwa. Mambo haya yalikuwa kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Joseph Warioba. Leo tunaendelea na maeneo mengine 20.

20. Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi
Rasimu ya Warioba ilipendekeza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia (a) Viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake; (b) Ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu; (c) Kanuni za uwazi na uwajibikaji; na (d) Kukuza uhusiano na jamii. Warioba akaendelea kusema, Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya nchi washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.

Misingi hii yote imefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

Mambo 70 muhimu ya wananchi yaliyofutwa katika Katiba Inayopendekezwa

21. Kuhusu Wabunge wa Kuteuliwa
Wananchi walipendekeza Rais asiwe na mamlaka ya kuteuwa wabunge na baadhi ya sababu zao ni Kutekeleza kikamilifu dhana ya mgawanyo wa madaraka. Kuwa na wabunge wanaotokana moja kwa moja na ridhaa ya wananchi kupitia kura zao na kuwa na wabunge walio huru katika kutekeleza majukumu yao. Rasimu ya Warioba ilipendekeza katika Ibara ya 113(2)(b) kumpa Rais nafasi ya kuteua wabunge watano wanaowakilisha watu wenye ulemavu na ikumbukwe kwamba wabunge hawa watano wanachaguliwa na watu wenye ulemavu wenyewe na Rais anafanya kazi ya kuwateua, hii ni tofauti na Rais kuwateua yeye mwenyewe. Ukisoma kifungu cha 45(2) utaona utaratibu wa kisheria unawekwa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki katika nafasi za uwakilishi.
Katiba Inayopendekezwa katika Ibara ya 129(2)(c) inampa Rais uhuru wa kuchagua wabunge wasiozidi kumi kutoka watu wenye sifa ya kuwa wabunge. Pendekezo hili ni kinyume na maoni ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma na kukiuka msingi wa wabunge kuwa wawakilishi wa wananchi moja kwa moja.

22. Kuhusu sifa ya kielimu kwa mbunge
Rasimu ya Warioba ilipendekeza sifa mojawapo ya kuwa mbunge ni kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne na ajue kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Baadhi ya sababu za kuunga mkono pendekezo hili ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na changamoto zilizoko katika sekta za uchumi, elimu na utandawazi ipo haja ya mbunge kuwa na elimu ya kutosha kuweza kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko haya.

Katiba Inayopendekezwa inapendekeza sifa mojawapo ya kuwa mbunge ni kujua na kusoma lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Pendekezo hili liko mbali kabisa na chini ya kiwango cha maoni ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma.

23.Nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Kikatiba
Rasimu ya Warioba ilipendekeza kuwako na nafasi kikatiba za Makatibu Wakuu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi katika utumishi wa umma kama watakavyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma. Kila Katibu Mkuu atakuwa kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Serikali aliyopangiwa na Rais na atashika nafasi ya madaraka ya Katibu Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.

Rais anaweza, kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma, kumteua mtumishi mwandamizi katika Utumishi wa Umma kuwa Naibu Katibu Mkuu. Kila Katibu Mkuu atakuwa mshauri wa mwisho kwa Waziri kwa masuala yote ya utendaji na atatoa ushauri kwa Baraza la Mawaziri katika vikao na Kamati zitakazoitishwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu hatashika madaraka yake hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi zake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

24. Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu
Rasimu ya Warioba ilipendekeza kuwapo kikatiba kwa Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ambayo itakuwa na majukumu ya kuchambua na kulishauri Baraza la Mawaziri juu ya masuala mbalimbali kabla ya kuwasilishwa na kufanyiwa uamuzi na Baraza hilo na itatekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.

Katiba Inayopendekezwa imefanikiwa kufuta msharti hayo yote mahususi licha ya kwamba huu ulikuwa wakati muafaka wa kuiimarisha sekta ya utumishi wa umma kikatiba ili iendelee kutuhudumia wananchi ikiwa na ari, kujiamini na kutenda kwa weledi pasina ya kuvurugwa na mara kadhaa na wanasiasa wabaya.

25. Malengo mahususi ya kiuchumi
Masharti yafuatayo katika malengo mahususi la kiuchumi yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa;-kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini

kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halaliinayompatia kipato kuweka utaratibu wa usimamizi wa kiuchumi nauandaaji wa mipango, kuwezesha malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kutekelezwa.

26. Haki ya kutokuwa mtumwa
Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwa yanapiga marufuku mtu kulazimishwa kufanya kazi bila hiari yake, hii ni kinyume na sheria na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.

27. Uhuru wa habari na vyombo vya habari
Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti "pokonyezi" (claw-back clauses) kwenye ibara ya Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari. Rasimu ya Warioba inatoa wajibu kusambaza habari na taarifa kwa wananchi. Katiba Inayopendekezwa inatoa wajibu wa kusambaza habari na taarifa sahihi na za ukweli kwa wananchi.

Kuweka maneno taarifa sahihi na za ukweli ni kuminya haki hii, Katiba inapasa kuweka msingi na sheria ingetoa ufafanuzi. Kuweka hapa kutapelekea kutumika kifungu hiki ndivyo sivyo. kuzingatia miiko ya taaluma ya uandishi na utangazaji wa habari ni suala la sheria na kanuni, na ikumbukwe ulimwengu wa leo hautegemei pekee wanataaluma wa habari kutoa habari, kifungu hiki kitaminya haki hii. Kwa kuweka maneno haya katika masharti ya ibara hii, Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari uko mashakani kabisa.

28. Haki ya Elimu na Kujifunza
Wananchi walipendekeza kutolewa kwa elimu bora ya msingi bure na bila vikwazo ikiwemo kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu.

Masharti yafuatayo yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa:-
Kila mtu ana haki ya: kupata fursa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo;
kupata elimu bora ya msingi bila ya malipo na inayomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea naelimu ya ngazi inayofuatia au kuweka msingi wa kuanzakujitegemea; kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu.

29. Haki ya Mtoto
Wananchi walipendekeza kutolewa ulinzi zaidi kwa haki za mtoto na Rasimu ya Katiba Mpya Toleo la Pili iliweka masharti yaliyoelekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa Kisheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoakipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa na kufanya haki zilizowekwa katika Ibara hii kuwa kiini macho.

30.Haki za watu wenye Ulemavu
Wananchi na hasa watu wenye ulemavu walipendekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki kwenye nafasi za uwakilishi.

Katiba inayopendekezwa imeondoa jukumu hili na tafsiri yake ni kwamba wawakilishi wa watu wenye ulemavu wataendelea kuteuliwa pasina ya kuwa na msingi wa kikatiba na kisheria kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawachagua wawakilishi wao tofauti na sasa.

31. Haki za wanawake
Wananchi waliotoa maoni hasa wanawake na wanaume walipendekeza kwa sauti moja kuona haki za wanawake zinalindwa, zinahifadhiwa, zinatolewa na kutekelezwa kwa wakati na mamlaka za nchi. Wananchi walipendekeza kuona wanawake wanalindwa dhidi ya unyonyaji na ukatili. Katiba Inayopendekezwa siyo tu imefuta kifungu kinachomlinda mwanamke dhidi ya unyonyaji bali pia imefuta masharti elekezi yaliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ambayo yalikuwa yanazielekeza Mamlaka za nchi kuweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, heshima, usalama na fursa za wanawakewakiwemo wajane.

33. Wajibu wa Raia
Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti yaliyokuwemo katika Rasimu ya Warioba juu ya mamlaka ya Bunge kutunga sheria kwa ajili ya kuwawezesha raia kutekeleza masharti ya ibara hii. Kufuta masharti hayo ni kuacha Katiba bila utaratibu mzuri wa kuhakikisha raia wanawajibika kwa taifa letu.

34. Hifadhi ya Haki za binadamu

Katiba Inayopendekezwa imefuta haki na uhuru ambao umeainishwa katika mikataba ya kikanda na ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambazo Jamhuri ya Muungano imeridhia. Huu ni mfano mbaya kabisa hasa kwa Taifa linaloheshimu haki za binadamu kama zilivyoainishwa katika mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.
 
wamebadili kanuni wenyewe,wamejadili wenyewe,wamepiga kura wenyewe na kucheza disco ya ukumbi wa bunge wenyewe.
 
Duh.. watanzania wachache sana tuyajuayo haya. Wengi wai wakishapewa khanga, kofia na ma t. Shirt ndo basiiiiiii
 
Mungu tusaidie, nchi yetu inanuka kila kona. Ila hata kiimani ktk dini zetu haisemi watu kuwa wapole hv, ipo siku Tz itaamka kutoka usingizini/ gizani na woga utaisha....hakuna atakayejali kuumia wala kufa. Kila jambo lina mwanzo na mwisho
 
Umesema mambo 70.Hayo ni 34. Hauzingatii ukweli.Viongozi wengi anaowachagua rais inabidi wathibitishwe na bunge. Nashangaa tu katika rasimu resident magistrate hajatajwa.Ipo tu Mahakama ya juu na Mahakama ya Rufaa.
 
Duh.. watanzania wachache sana tuyajuayo haya. Wengi wai wakishapewa khanga, kofia na ma t. Shirt ndo basiiiiiii
Kudai kuwa Watanzania hawawezi kuganya maamuzi yao bila khanga au kofia ni kutudharau na kutudhalilisha. Tumeamua kwa umoja wetu kwa hiari yetu kupokea Katiba iliyopendekezwa na bunge letu likiwakilisha wapiga kura wote kwa wingi wa kura zao. Kama una hoja 70 hizo ni zako zitafutie kura.
 
Huu ni uongo mkubwa. Kuhusu madaraka ya Rais kupunguzwa usisahau kwamba serkali inaihimili mitatu: bunge, mahakama, na serkali chini ya Rais. Kutaka Bunge limtawale Rais ni kosa kuwa, ni kuingilia mhimili huo. Kwa nini kila uteuzi wa Rais upitishwe na Bunge? Kumbuka Rais anachaguliwa na Watanzania milioni 25 huku mbunge wa Mji Mkongwe anachaguliwa na wapiga kura 3,000. Kuhusu kutenganisha bunge na serkali eti mawaziri wasiwe wabunge kwa nini wawakil8shi wa bunge wasiwatumikie wananchi kwenye serkali? Dunia nzima wabunge ni mawaziri. Mbunge huwajibishwa kwemye uchaguzi miaka mutano mitano, si kwa zomeazomea ya ukawa. Hakuna haja ya ukomo, ubunge si ajira. Kama sotaki uendelee sitakupa kura yangu.
 
Nimeyapata kwenye ukurasa wa facebook: Nayaweka hapa, pia kama attachment; bado unayatetea?

MAMBO 20 MUHIMU YA WANANCHI YALIYOTUPWA NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA. UNATAKA KUUJUA UKWELI BASI SOMA HAPA NA MJULISHE MWENZIO

Katiba Inayopendekezwa ina mapungufu makubwa na imeyatupilia mbali maoni muhimu ya wananchi kama yalivyotolewa na wananchi wenyewe kama ifuatavyo;-

1. Kupunguzwa kwa madaraka ya Rais

Wananchi walipendekeza madaraka makubwa ya Rais hasa ya uteuzi yapunguzwe na ziundwe Taasisi za kikatiba za kumshauri Rais kabla hajafanya teuzi. Wananchi walipendekeza pia baada ya Rais kumteua kiongozi basi itabidi mteuliwa huyo Bunge limthibitishe. Katiba inayopendekezwa imeyafuta haya yote na imemuongezea Rais madaraka.

2. Kutenganisha Mamlaka ya Mihimili ya Dola

Wananchi walipendekeza uhuru zaidi kwa Bunge na mamlaka zaidi kwa Bunge kuisimamia, kuiwajibisha na kuishauri Serikali. Pendekezo hili linaenda sambamba na kutenganisha serikali na Bunge, hali ambayo iko sasa. Rasimu ya Warioba ililipa Bunge mamlaka zaidi kuisimamia Serikali na hata pale ambapo Bunge lingekataa bajeti au muswada mbaya wa serikali mara kadhaa, Rais asingeliweza kulivunja Bunge. Wananchi walisema sana Mawaziri wasitokane na wabunge, ili wabunge wafanye kazi ya uwakilishi pekee na mawaziri watumie weledi wao kumsaidia Rais kazi za Serikali.

3. Kumwajibisha Mbunge

Rasimu ya Warioba iliwapa wapiga kura uwezo wa kuwawajibisha Wabunge kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nao wakati wowote (Recall Powers) kama wakienda kinyume na maslahi ya wananchi katika jimbo husika. Wananchi walijiuliza kama mbunge ni mtumishi wao, iweje hayuko katika kituo cha kazi kwa miezi kadhaa na wasiweze kumwajibisha mpaka miaka mitano?

4. Vyanzo vya Mapato vya kuaminika

Kuwepo kwa vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakavyogharimia mambo ya Muungano ambayo yamepunguzwa kutoka 22 hadi 7 lilikuwa pendekezo ambalo hata taasisi za serikali zilipendekeza. Pendekezo la Katiba Inayopendekezwa imerudisha mapato ya Muungano kama Katiba ya Mwaka 1977, na kwa kufanya hivyo tumerudi kwenye mgogoro wa msingi, kuchukua kodi tatu, ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa na mapato kutoka Zanzibar ni kuiua Zanzibar na kuifanya ishindwe kumudu matumizi yake ya ndani kwa mambo yasiyo ya Muungano na vivyo hivyo kwa Tanganyika.

5. Muundo wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili

Kwa miaka nenda rudi tumekuwa na kitendawili cha ni muundo gani wa Muungano Jamhuri yetu inao. Kitendawili hiki kimeelezwa na wengi akiwemo Baba wa Taifa Mw. J.K Nyerere. Rasimu ya Warioba iliweka kwa mara ya kwanza Muundo Jamhuri ya Muungano kuwa ni wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili na lenye Serikali 3.

6. Kupunguza ukubwa wa Serikali

Wananchi walionesha kutofurahishwa na ukubwa wa serikali unaopelekea matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi. Walipendekeza uwepo wa serikali ya muungano iliyo imara, yenye ufanisi na ndogo. Rasimu ya Warioba ilisema idadi ya mawaziri isizidi 15, Katiba Inayopendekezwa inasema Mawaziri wasizidi 40

7. Tume ya Uhusiano na Uratibu

Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha kunakuwepo uhusiano mzuri, mawasiliano na uratibu wa serikali zote tatu chini ya Mamlaka ya Serikali ya Muungano na kupitia Tume ya Uhusiano na Uratibu. Bunge Maalum lilishindwa kuelewa mantiki ya pendekezo hili na Katiba Inayopendekezwa imelivuruga kabisa, kutoka pendekezo la Warioba la “Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali” hadi “Tume ya Uratibu wa Mambo ya Muungano” katika Katiba Inayopendekezwa.

8. Kupunguza ukubwa wa Bunge

Wananchi walizungumzia pia ukubwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na gharama zinazoambatana nalo, na wakapendeza bunge dogo na lenye ufanisi mkubwa. Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema Wabunge 390.

9. Ukomo wa vipindi vya ubunge

Wananchi walizungumzia nafasi za ubunge kuhodhiwa na watu fulani kwa miaka nenda rudi na wakapendekeza ifike mahali kuwe na ukomo ili kuleta uwakilishi mpana na mabadiliko. Rasimu ya Warioba iliweka ukomo wa vipindi vya ubunge kuwa vitatu na kuwa na ukomo wa miaka 15 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Bunge Maalum na Katiba Inayopendekezwa wamefuta pendekezo hili.
10. Kuwepo kwa Tunu za Taifa (Core Values)

Wananchi walipendekeza uwepo wa tunu za Taifa (core values) katika katiba, tunu hizi ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa. Raia wa Tanzania walikuwa na wajibu wa kuheshimu tunu hizi lakini Katiba Inayopendekezwa imezifuta tunu hizi.

11. Maadili na Miiko ya Viongozi

Wananchi walizungumza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya jamii, watumishi na viongozi wa umma, wengi wakisema Katiba iainishe Maadili na miiko ya viongozi wa umma ambayo kwayo tutawawajibisha. Katiba Inayopendekezwa imesema Maadili na Miiko kwa viongozi (mathalani kutenganisha biashara na uongozi ili kuepusha mgongano wa maslahi), isiwemo kwenye Katiba bali ikawekwe kwenye Sheria.

Rasimu ya Warioba iliweka masharti ya kuzuia Bunge kubadili baadhi ya masharti mahususi ya Katiba (entrenched provision) ibara ya 119 isipokuwa kwa ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni (mathalan Malengo Makuu ya Taifa, Haki za Binadamu n.k. Na bahati mbaya tulisahau kuweka na Sura ya 3 juu ya Maadili). Masharti yote ya Ibara hii yamefutwa isipokuwa Muundo wa Muungano na Uwepo wa Jamhuri ya Muungano.

13. Kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi

Wananchi walizungumza umuhimu wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi za Jamhuri ya Muungano. Ilisisitizwa juu ya umuhimu wa Tume kugawa majimbo ya uchaguzi na kwamba Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake wathibitishwe na Bunge ili kuwapa uhalali wa kitaifa, pendekezo hili limefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

Kuwepo uwiano wa uwalikishi wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima kwa mazingira ya sasa. Uwiano kati ya wanawake na wanaume katika vyombo mbalimbali vya dola hasa vile vya kutung sheria limeendelea kuwa tatizo nchini na lililokaa kwa muda mrefu. Wananchi na hasa wanawake na baadhi ya wanaume walipendekeza uwiano ulio sawa katika kufikia fursa hasa ukizingatia wanawake ndio wazalishaji wakubwa. Katiba Inayopendekezwa imefutilia mbali pendekezo hili muhimu.

15. Kuanzishwa kwa Mgombea Huru

Haki ya wananchi kushiriki shughuli za umma imekuwa ikizuiwa siku nyingi na kwamba ushiriki katika shughuli za umma kama kiongozi wa kuchaguliwa inapaswa kuwa haki ya msingi ya mwananchi yeyote yule. Rasimu ilitoa haki ya mgombea huru bila vikwazo, Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti magumu ambayo hakuna mtu anayeweza kuyatimiza kirahisi, kitendo hiki sio sawa.

16. Msaada wa Kisheria kwa Wananchi

Wananchi walieleza kutokuridhishwa kwao na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji huo na wakapenda huduma ya msaada wa kisheria liwe suala la kikatiba kwa mwananchi yeyote yule na serikali iwajibike kutoa huduma hiyo. Katiba Inayopendekezwa imesema wananchi hawatakuwa na haki ya kudai huduma hii kokote nchini, hata mahakama hazitaweza kusikiliza mashauri ama Serikali imetoa haki hii au haikutoa haki hii rejea Ibara ya 21.

17. Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi

Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi atekeleze kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa

18. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Wananchi

Tume ya Warioba ilipendekeza kuwepo kwa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti haya licha ya wapiganaji kupendekeza utaratibu wa kusimamia maslahi yao Kikatiba.

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la
Jamhuri ya Muungano litazingatia (a) viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake; (b) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu; (c) kanuni za uwazi na uwajibikaji; na (d) kukuza mahusiano na jamii. Warioba akaendelea kusema, Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya Nchi Washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi. Misingi hii yote imefutwa na Katiba inayopendekezwa

UKISOMA MPAKA HAPA HAKIKISHA NA MWENZAKO ANAPATA UJUMBE HUU

Humphrey Polepole
December 8, 2014 ·
 
Attachments

  • MAMBO 20 MUHIMU YA WANANCHI YALIYOTUPWA NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA.doc
    46.5 KB · Views: 167
mtumie kwenye email yake basi mkuu, maana thread hii umetuondoa kabisa wengine
 
Huu ni uongo mkubwa. Kuhusu madaraka ya Rais kupunguzwa usisahau kwamba serkali inaihimili mitatu: bunge, mahakama, na serkali chini ya Rais. Kutaka Bunge limtawale Rais ni kosa kuwa, ni kuingilia mhimili huo. Kwa nini kila uteuzi wa Rais upitishwe na Bunge? Kumbuka Rais anachaguliwa na Watanzania milioni 25 huku mbunge wa Mji Mkongwe anachaguliwa na wapiga kura 3,000. Kuhusu kutenganisha bunge na serkali eti mawaziri wasiwe wabunge kwa nini wawakil8shi wa bunge wasiwatumikie wananchi kwenye serkali? Dunia nzima wabunge ni mawaziri. Mbunge huwajibishwa kwemye uchaguzi miaka mutano mitano, si kwa zomeazomea ya ukawa. Hakuna haja ya ukomo, ubunge si ajira. Kama sotaki uendelee sitakupa kura yangu.
Jalibu kuangalia hili jambo kwa mapana yake: Hivi kama kazi ya mbunge moja wapo ni kuikosoa serikali je mheshimiwa waziri kama mbunge anaweza kuikosoa serikali ambayo yeye ni sehemu yake? kama kwa mujibu wa kanuni za serikal za kidemocrasia mihimili hii 3 yaani Bunge, Mahakama N excutive(serikali) inatakiwa kutokuingiliana katika utendaji wake, Huoni kuwa raisi kupewa madalaka ya kumteua jaji mkuu tayari kapewa nguvu ya kuiingilia mahakama? kama Rais akiteua wabunge baadhi( tuchukulie 20) Harafu wabunge wengine wa kuchaguliwa wa chama tawala wakapewa nafasi ya uwaziri na naibu wa waziri. Huoni kwamba miongoni mwa hao wote yaaani wabunge wa kuteuliwa na hao wengine ambao wameingizwa katika serikali watakuwa hawana uwezo tena wa kuikosoa serikal ambayo inaongozwa na raisi aliyewapa nafasi hizo? Liangalie hili jambo kizarendo kabisa! kumpa mamlaka rais ya kuteua wabunge na mawaziri kutoka katika bunge ni sababu ya bunge kushindwa kufanya shughuli zake!!!!!!
Nasikitika nchi yangu!! watu tunafanya maamuzi kwa kuzingatia faida zetu zitakazo tokana na maamuzi hayo!
uko wapi uhuru wa mahakama haswa pale ambapo mtuhumiwa ni mtu wa upande wa serikal?
Fikilia vizuri kizarendo kabisa na uwe na Hofu ya Mungu kama unamcha kweli!
 
Nimeyapata kwenye ukurasa wa facebook: Nayaweka hapa, pia kama attachment; bado unayatetea?

MAMBO 20 MUHIMU YA WANANCHI YALIYOTUPWA NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA. UNATAKA KUUJUA UKWELI BASI SOMA HAPA NA MJULISHE MWENZIO

Katiba Inayopendekezwa ina mapungufu makubwa na imeyatupilia mbali maoni muhimu ya wananchi kama yalivyotolewa na wananchi wenyewe kama ifuatavyo;-

1. Kupunguzwa kwa madaraka ya Rais

Wananchi walipendekeza madaraka makubwa ya Rais hasa ya uteuzi yapunguzwe na ziundwe Taasisi za kikatiba za kumshauri Rais kabla hajafanya teuzi. Wananchi walipendekeza pia baada ya Rais kumteua kiongozi basi itabidi mteuliwa huyo Bunge limthibitishe. Katiba inayopendekezwa imeyafuta haya yote na imemuongezea Rais madaraka.

2. Kutenganisha Mamlaka ya Mihimili ya Dola

Wananchi walipendekeza uhuru zaidi kwa Bunge na mamlaka zaidi kwa Bunge kuisimamia, kuiwajibisha na kuishauri Serikali. Pendekezo hili linaenda sambamba na kutenganisha serikali na Bunge, hali ambayo iko sasa. Rasimu ya Warioba ililipa Bunge mamlaka zaidi kuisimamia Serikali na hata pale ambapo Bunge lingekataa bajeti au muswada mbaya wa serikali mara kadhaa, Rais asingeliweza kulivunja Bunge. Wananchi walisema sana Mawaziri wasitokane na wabunge, ili wabunge wafanye kazi ya uwakilishi pekee na mawaziri watumie weledi wao kumsaidia Rais kazi za Serikali.

3. Kumwajibisha Mbunge

Rasimu ya Warioba iliwapa wapiga kura uwezo wa kuwawajibisha Wabunge kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nao wakati wowote (Recall Powers) kama wakienda kinyume na maslahi ya wananchi katika jimbo husika. Wananchi walijiuliza kama mbunge ni mtumishi wao, iweje hayuko katika kituo cha kazi kwa miezi kadhaa na wasiweze kumwajibisha mpaka miaka mitano?

4. Vyanzo vya Mapato vya kuaminika

Kuwepo kwa vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakavyogharimia mambo ya Muungano ambayo yamepunguzwa kutoka 22 hadi 7 lilikuwa pendekezo ambalo hata taasisi za serikali zilipendekeza. Pendekezo la Katiba Inayopendekezwa imerudisha mapato ya Muungano kama Katiba ya Mwaka 1977, na kwa kufanya hivyo tumerudi kwenye mgogoro wa msingi, kuchukua kodi tatu, ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa na mapato kutoka Zanzibar ni kuiua Zanzibar na kuifanya ishindwe kumudu matumizi yake ya ndani kwa mambo yasiyo ya Muungano na vivyo hivyo kwa Tanganyika.

5. Muundo wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili

Kwa miaka nenda rudi tumekuwa na kitendawili cha ni muundo gani wa Muungano Jamhuri yetu inao. Kitendawili hiki kimeelezwa na wengi akiwemo Baba wa Taifa Mw. J.K Nyerere. Rasimu ya Warioba iliweka kwa mara ya kwanza Muundo Jamhuri ya Muungano kuwa ni wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili na lenye Serikali 3.

6. Kupunguza ukubwa wa Serikali

Wananchi walionesha kutofurahishwa na ukubwa wa serikali unaopelekea matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi. Walipendekeza uwepo wa serikali ya muungano iliyo imara, yenye ufanisi na ndogo. Rasimu ya Warioba ilisema idadi ya mawaziri isizidi 15, Katiba Inayopendekezwa inasema Mawaziri wasizidi 40

7. Tume ya Uhusiano na Uratibu

Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha kunakuwepo uhusiano mzuri, mawasiliano na uratibu wa serikali zote tatu chini ya Mamlaka ya Serikali ya Muungano na kupitia Tume ya Uhusiano na Uratibu. Bunge Maalum lilishindwa kuelewa mantiki ya pendekezo hili na Katiba Inayopendekezwa imelivuruga kabisa, kutoka pendekezo la Warioba la “Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali” hadi “Tume ya Uratibu wa Mambo ya Muungano” katika Katiba Inayopendekezwa.

8. Kupunguza ukubwa wa Bunge

Wananchi walizungumzia pia ukubwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na gharama zinazoambatana nalo, na wakapendeza bunge dogo na lenye ufanisi mkubwa. Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema Wabunge 390.

9. Ukomo wa vipindi vya ubunge

Wananchi walizungumzia nafasi za ubunge kuhodhiwa na watu fulani kwa miaka nenda rudi na wakapendekeza ifike mahali kuwe na ukomo ili kuleta uwakilishi mpana na mabadiliko. Rasimu ya Warioba iliweka ukomo wa vipindi vya ubunge kuwa vitatu na kuwa na ukomo wa miaka 15 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Bunge Maalum na Katiba Inayopendekezwa wamefuta pendekezo hili.
10. Kuwepo kwa Tunu za Taifa (Core Values)

Wananchi walipendekeza uwepo wa tunu za Taifa (core values) katika katiba, tunu hizi ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa. Raia wa Tanzania walikuwa na wajibu wa kuheshimu tunu hizi lakini Katiba Inayopendekezwa imezifuta tunu hizi.

11. Maadili na Miiko ya Viongozi

Wananchi walizungumza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya jamii, watumishi na viongozi wa umma, wengi wakisema Katiba iainishe Maadili na miiko ya viongozi wa umma ambayo kwayo tutawawajibisha. Katiba Inayopendekezwa imesema Maadili na Miiko kwa viongozi (mathalani kutenganisha biashara na uongozi ili kuepusha mgongano wa maslahi), isiwemo kwenye Katiba bali ikawekwe kwenye Sheria.

12. Masharti yasiyoweza kubadilishwa na Bunge

Rasimu ya Warioba iliweka masharti ya kuzuia Bunge kubadili baadhi ya masharti mahususi ya Katiba (entrenched provision) ibara ya 119 isipokuwa kwa ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni (mathalan Malengo Makuu ya Taifa, Haki za Binadamu n.k. Na bahati mbaya tulisahau kuweka na Sura ya 3 juu ya Maadili). Masharti yote ya Ibara hii yamefutwa isipokuwa Muundo wa Muungano na Uwepo wa Jamhuri ya Muungano.

13. Kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi

Wananchi walizungumza umuhimu wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi za Jamhuri ya Muungano. Ilisisitizwa juu ya umuhimu wa Tume kugawa majimbo ya uchaguzi na kwamba Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake wathibitishwe na Bunge ili kuwapa uhalali wa kitaifa, pendekezo hili limefutwa na Katiba Inayopendekezwa.

14. Usawa wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume

Kuwepo uwiano wa uwalikishi wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima kwa mazingira ya sasa. Uwiano kati ya wanawake na wanaume katika vyombo mbalimbali vya dola hasa vile vya kutung sheria limeendelea kuwa tatizo nchini na lililokaa kwa muda mrefu. Wananchi na hasa wanawake na baadhi ya wanaume walipendekeza uwiano ulio sawa katika kufikia fursa hasa ukizingatia wanawake ndio wazalishaji wakubwa. Katiba Inayopendekezwa imefutilia mbali pendekezo hili muhimu.

15. Kuanzishwa kwa Mgombea Huru

Haki ya wananchi kushiriki shughuli za umma imekuwa ikizuiwa siku nyingi na kwamba ushiriki katika shughuli za umma kama kiongozi wa kuchaguliwa inapaswa kuwa haki ya msingi ya mwananchi yeyote yule. Rasimu ilitoa haki ya mgombea huru bila vikwazo, Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti magumu ambayo hakuna mtu anayeweza kuyatimiza kirahisi, kitendo hiki sio sawa.

16. Msaada wa Kisheria kwa Wananchi

Wananchi walieleza kutokuridhishwa kwao na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji huo na wakapenda huduma ya msaada wa kisheria liwe suala la kikatiba kwa mwananchi yeyote yule na serikali iwajibike kutoa huduma hiyo. Katiba Inayopendekezwa imesema wananchi hawatakuwa na haki ya kudai huduma hii kokote nchini, hata mahakama hazitaweza kusikiliza mashauri ama Serikali imetoa haki hii au haikutoa haki hii rejea Ibara ya 21.

17. Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi

Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi atekeleze kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. Masharti haya yamefutwa na Katiba Inayopendekezwa

18. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Wananchi

Tume ya Warioba ilipendekeza kuwepo kwa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Katiba Inayopendekezwa imefuta masharti haya licha ya wapiganaji kupendekeza utaratibu wa kusimamia maslahi yao Kikatiba.

19. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi

Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itakayokuwa na jukumu la kusimamia utumishi wa Jeshi la Polisi. Katika uajiri wa askari wa Jeshi la Polisi, Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itazingatia kanuni na misingi ya utumishi iliyoainishwa katika Katiba hii

20. Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi

Rasimu ya Warioba ilipendekeza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la
Jamhuri ya Muungano litazingatia (a) viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake; (b) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu; (c) kanuni za uwazi na uwajibikaji; na (d) kukuza mahusiano na jamii. Warioba akaendelea kusema, Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya Nchi Washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi. Misingi hii yote imefutwa na Katiba inayopendekezwa

UKISOMA MPAKA HAPA HAKIKISHA NA MWENZAKO ANAPATA UJUMBE HUU

Humphrey Polepole
December 8, 2014 ·
Naipenda hiyo ya Mkuu wa Polisi "afanye jazi yake bila upendeleo". Hii iliwekwa na CUF wakiamini kuwa hawatatawala hata siku moja. Ni hoja nzuri, lakini kwa nini iishie kwa mkuu wa polisi? Jaji je? Askofu? Katibu Kata? Gavana Benki Kuu? Mengi? Mufti? Mwenyekiti wa CUF? Shangazi? Captain wa Yanga?Katiba inatakiwa isiwe na macho, Mzee Warioba aliburuzwa na kina Baregu akajichanganya akatunga ya kuzuia CCM.
 
Back
Top Bottom