Mambo 7 muhimu yanayotakiwa ili website au blogu ipande kwenye Google

lembu

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
16,376
21,835
1. Taarifa za kutosha/nyingi na za kipekee unique content
2. Ukurasa unaoload kwa haraka na wenye code chache
3. Menu rahisi kwa mteja na viunganishi angalau kila paragraph
4. Kupandisha kwenye directories za nyumbani na nje kila wiki angalau directories 10
5. Kupandisha na kushirikiaha kwenye mitandao ya kihamii, forums nk angalau kila siku
6. Kuweka ulinzi kwenye website yako isitekwe nyara au kutumika kwenye uhalifu wa kimyandap
7. Kuweka monitoring system ili kujua jinsi website inavyotembelewa na pia kujua penye hitilafu ili usahihishe kabla haijaleta madhara

Ukitaka tukipatie huduma za kupamdisha website yako kwenye Google
Piga 0755646470
Email info@infocomcenter.com
 
Mwendelezo kwa ufafanuzi zaidi
Ili website au keywords za website zipande kwenye ukurasa wa kwanza wa Google, mambo kadhaa yanatakiwa kufanyika.
Ufafanuzi
Google anapandisha keywords zako juu ya zingine kwa kutoa maksi. Keywords zako zikiwa na maksi za juu kuliko zingine zote itawekwa ya kwanza. Ili kuweza kutoa maksi bila upendeleo, Google ametengeneza maswali mengi ambayo yakijibiwa vizuri kwenye webpage yako keywords husika hupewa maksi. Haya maswali ndio huitwa algorithm au rules.
Googlebot ni code ambayo ina uwezo wa kutembelea webpage na kuchukua data husika kwa ajili ya kupeleka kwenye main database ya google. Hii bot nayo imewekewa masharti au rules au algorithm itakayomuwezesha kufanya kazi yake kwa ufanisi na bila kukosea.
Sasa ili website yako iingie kwenye ushindani wa kupewa maksi nyingi kwa baadhi ya keywords zake ni lazima yafuatayo yatekelezwa kwa ufanisi zaidi:

1. Taarifa za kutosha/nyingi na za kipekee unique content:
Taarifa zenye kubeba maneno yanayotafutwa kulingana na secta husika Mfano kama ni website ya utalii iwe na full itinerary content ambayo haijakopiwa popote kwenye internet
Title ya Page iwe na full title ya product mfano
7 Day Tour to Mwanza, Serenegti and Ngorongoro
Summary ya itinerary
Halafu description ya kila siku ikianza na title halafu summary of that day
Hakikisha piach zikiwekwa ziwe optimized kwa naman ya format na size. Format ziwe jpeg au png au gif. Size isiwe zaidi ya 100KB

2. Ukurasa unaoload kwa haraka na wenye code chache:
Website yako iwe na text nyingi kuliko code. Kama code zitakuwa nyingi page yako itakuwa nzito na Googlebot au bot zingine za search engine zikija zitasubiri kidogo halafu zitaondoka bila kuikagua page yako.
Code ni pamoja na html tags, javascript na css.
Muda wa ukurasa kuload unaoshauriwa ni kati ya sekunde 2 hadi 6
Ukubwa wa ukurasa ni si zaidi ya Megabyte 2
Processes requests zinazoshauriwa ni si zaidi ya 65
Pagespeed score kuanzia 80%
Haya yote unaweza kupima kwa kutumia GTMETRIX.COM

3. Menu rahisi kwa mteja na viunganishi angalau kila paragraph:
Hakikisha men imepangiliwa ili kumpa mteja urahisi wa kujua nini iko wapi. Uwe na mfumo maalum wa kuweka menu. Weka vitu vya mhimu tu kwenye parrent buttons na zenye umuhimu mdogo kwenye child buttons. Sio lazima kila kitu kilichopo kwenye website ionekane kwenye menu. Content zingine mteja anaweza kuzipata kwa kusearch. Hakisha pia uanwekla viunganishi vya kutosha na zinazoendanan na paragraph. Kumbuka viunganishi ni sehemu ya mawasiliano kwenye page. Wateja wanapoclick kwenye links zaidi wanakupunguzia Bounce rate na Google anaheshimu sana website yenye bounce rate ndogo

4. Kupandisha kwenye directories za nyumbani na nje kila wiki:
Pandisha angalau kwenye directories 10 kila wiki.
Anza kupandisha kwenye directory ya Google, BING na Yahoo
Ya Google ni muhimu zaidi na itakuwezesha website yako kupatikana kwenye Googlemap na pia kuonekana kulia mwa Google search engine kama featured listing kama inavyooshwa hapa chini kwenye screenshot. Hii itasaidia sana kushawishi watu kutembelea website na pia kuongeza trust na reliability ya website yako. Unapolist website yako kwenye directory mbalimbali ikiwemo Google My Business hakikisha unatumia Brand name. Kama kwa mfano kampuni yako inaitwa Sunset Safaris and Travel Limited brand name hapo ni jina la kampuni yaani "Sunset Safaris and Travel Limited". Tumia jina hilohilo bila kubadilisha. Usiwe na tamaa ya keywords kwa sababu hutapata. Hata kwenye Directories zingine na social media hakikisha unatumia brand name kama unatangaza kampuni au product brand names kama unatangaza products. Asante kama umenielewa
SEO Tanzania with Webmaster Tanzania Featured.jpg


5. Kupandisha na kushirikisha kwenye mitandao ya kijamii, forums, blogs nk
Shirikisha kwenye mitandao ya kijamii angalau kila siku mara moja
Kupandisha kwenye mitandao ya kijamii haina ubishi, ukurasa wa FB au Twitter au Linkedin au Youtube au Googleplus ambao umejengwa na kufanyiwa branding pamoja na kuwa popular unaongeza kwa kiwango kikubwa reliability na trust kutoka kwa wateja watarajiwa ambao ni wapya kabisa.

6. Kuweka ulinzi kwenye website yako
Imarisha ulinzi na usalama kwenye website yako ili isitekwe nyara au kutumika kwenye uhalifu wa kimtandao.
Kazi yote ni bure kama website yako inahackiwa na kuvamiwa kwa urahisi, kufanyiwa phishing na spamming. Website ambayo haiko salama inayofamiwa ovyo ovyo huwa mara nyingi iko offline na hivyo haitapata umaarufu wowote machoni mwa search engines. Pia website zenye virusi au ambazo hazina SSL certificates zitaogopwa sio tu na wateja bali hata browsers na Search engine. Mfano kabisa Google sasa hivi anatoa maksi za upendeleo kwenye ranking kwa website zenye ssl certificate kinyume na zile ambazo hazina. Website yenye ssl certificate ukitembelea inaanza na https:// ikiwa imetanguliwa na kipicha cha kufuli iliyofunga pamoja na neno Secure kwa rangi ya kijani kibichi. Mfano mzuri ni hii website ya Jamiiforums.com

7. Weka monitoring system kwenye website yako:
Hii ni muhimu sana ili kujua jinsi website inavyotembelewa na pia kujua penye hitilafu au uhalifu ili usahihishe kabla haijaleta madhara makubwa.
Monitoring inasaidia ili kujua kama hatua unazozichukua zinazaa matunda na kwa kiwango gani. Itasaidia pia kujua ni njia zipi zinafanya kazi kwa ufanisi na zipi zinatia hasara tu ili ukaze buti kwenye njia zenye tija. Monitoring inasaidia pia kujua kama website yako haina shida na shida yeyote itakayoonekana inatatuliwa kabla aijaleta madhara kwenye website na ranking ya kwenye search engines.

Baadhi ya maeneo yanayotakiwa kufanyiwa website monitoring ni:
  1. http monitoring: hii inapima kama website yako iko online kwa kurudisha code 200. Kama haiko online inabidi urekebishe tatizo haraka aidha wewe au webmaster wako. Tool nzuri kwa hii ni Uptime Robot
  2. Traffic monitoring: Hii inatoa taarifa ya waliotembelea website wanatoka wapi, wametembelea wapi kwenye website na wamekaa muda gani. Pia utapata taarifa ya watembeleaji wapya na wanaorudi. Utajulishwa pia kiwango cha wanaoclick website yako dhidi ya wale wanaokuja na kuondoka bila kuclick popote hii ndio Bounce rate. Tool nzuri kwa hii ni Google analytic
  3. Script Monitoring: Hii inakujulisha kama scripts zipi zinatakiwa zifanyiwe update au upgade. Hii itakupa fursa ya kujua ni scripts zipi ziko obsolete yaani ziko deprecated kwa lugha ya kitaalamu (Yaani inatumia libraries ambazo hazipo supported tena. Pia itakujulisha kama script zako zimebadilishwa au kuna mpya zimeingizwa, Hii ni muhimu kwa kudhibiti hacking, phishing na script tempering ya aina yeyote. Kama unatumia Wordpress, Tool nzuri ni Wordfence plugin ni nzuri
  4. Keyword(s) Monitoring: kufuatilia keywords zako zilizopo kwenye first page ya Google punde zikihama ili ufanye kitu kurudisha. Tool nzuri kwa hii ni Uptime Robot
  5. Spam Monitoring on Emails, Comments, Registration and Traffic Flooding. Kama unatumia Wordpress, Tool nzuri ni Akismet plugin kwa coments na Jetpack kwa security zinginei
  6. Website attack monitoring, brute force, database injection, Cross-site scripting -CSS na zaidi. Kama unatumia Wordpress, Tool nzuri ni Wordfence plugin ni nzuri
Kwa maelezo zaidi
0755646470
lembu@kivuyo.com
Website: Webmaster Tanzania: Hosting, Design, Domain Registration
 
Back
Top Bottom