Mambo 7 ambayo CCM ikifanya yaweza kujiokoa; vinginevyo...

Mzee mwanakijiji,<br />
Unajua kuna mlevi wa pombe na Alcoholic! <br />
Mlevi wa pombe hulewa pindi anapokunywa tu,
M'bwia unga hapo ni ccm au viongozi wa ccm? maana kama unakusudia ccm, utakuwa umekosea kwani sidhani kama hizo nyimbo za ufisadi ulitaja ni ktk sera za ccm! labda useme 'viongozi wa ccm', naam! hapo utakuwa umepatia¡ lakin nadhan hilo ni tatizo la watu wachache (si wote ndio mafisadi),hivyo basi twaweza pembua kati ya chuya na mchele, au ndo yale yale ya "samaki..."
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa miezi kadhaa sasa baada ya Uchaguzi tumeona juhudi kadhaa za Chama cha Mapinduzi kujiokoa au niseme kujinusuru. Juhudi hizi zimelenga hasa katika kurudisha "imani" ya wananchi kwa Chama cha Mapinduzi, imani ambayo wananchi wanaonekana kuipoteza kama ilivyoonekana wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Uchaguzi Mkuu uliopita umewathibitishia wana CCM kuwa kama hawakuona haja ya kubadilika kabla ya wakati huo basi haja hiyo imenguruma kama radi baada ya uchaguzi na kuiweka CCM katika uchaguzi usioepukika; kubadilika au kuvunjika.

Mengi tuliyoyaona yamefikiria na kubuniwa na wana CCM wenyewe katika kujaribu "kujichunguza". Mengi ya haya kwa watu wengine yameendelea kuwa kama kichekesho kwani haionekani kugusa hasa kiini cha mgogoro uliopo kati ya wananchi na chama kinachowatawala; mgogoro ambao hauwezi kukoma kwa vitisho, nguvu za dola, au kupuuzia. Vitisho, nguvu za dola na kupuuzia vilifanya kazi kwa muda tu lakini baada ya wananchi wa Tanzania kuvuka mpaka wa woga na ujasiri na kukipita kizingiti cha kutokujali vitu hivyo vimebakia kama masalia ya zana za ujima ambazo sehemu yake ni katika jumba la makumbusho.

Bahati mbaya sana CCM katika kujisafisha wameshindwa kuwauliza wakosoaji wake kutoa maoni na hivyo wamebakia wao wenyewe ndani kwa ndani wakipeana maoni, kupepeana kwa kuulizana na kutulizana kwa kubebana huku wakichekeana na kukumbatiana katika kujiridhissha kuwa mambo yataenda na kuwa mazuri. Kwa vile nimeona kuwa hakuna mtu ndani ya CCM atawaambia ninachowaambia hapa nimeona nijitolee tu bila kuombwa kuwapa mawazo ya nini wafanye ili waweze kujiokoa na wasipofanya kuangamia kwao kuko dhahiri, kwaja kwa haraka, na kutawavunja kusababisha CCM iparaganyike kama sehemu ile ya unabii inavyosema. Bahati mbaya sana (kama naweza kusema ni bahati mbaya) hakuna mtu aliyeweza kukwepa neno la unabii likashatoka.

Kuanzia simulizi la Kigiriki la Odepus hadi filamu inayocheza ya Panda 2 tunaweza kuona jinsi gani neno likitamkwa lilivyo huenda likatimia na hakuna mtu wa kuweza kubaadilisha japo vitu mbalimbali vyaweza kufanywa vikabadilika bila kubadilisha matokeo kwani once fate has set its course, no one can escape from its condemning and unforgiving hands. Ndio maana nimesema kuwa mambo yafuatayo yakifanyika CCM "yaweza" kujiokoa... sijui kama ITAWEZA kujiokoa. Labda itapunguza tu ukali wa fate.

1. IKUBALI MAKOSA, IOMBE RADHI TAIFA NA KUKIRI UBOVU WAKE

Katika mchakato wa hatua 12 za kuacha ulevi hatua ya kwanza kabisa ya kukiri kwamba mtu hakuwa na uwezo dhidi ya kileo. Yaani, kukubali udhaifu na makosa ya mtu kwani sifa ya kwanza ya mlevi ni kuwa hakubali kuwa ni mlevi; huweza kujiita "anakunywa kidogo tu" au "anaweza kuacha wakati wowote" n.k Hadi pale atakapokubali kuwa ni mlevi ndipo hatua za kujinusuru zinapoanza. CCM vivyo hivyo. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (siyo Mzee mmoja Nyerere!) alikuwa na uwezo huu wa kujiangalia na kujikosoa. Kinyume na imani na uongo unaonezwa siku hizi kuwa Nyerere alikuwa hashauriki ukweli wa historia unaonesha kuwa ni kiongozi pekee wa Tanzania ambaye aliwahi kubadilisha mwelekeo wa mambo kadha wa kadha na kukiri kukosea - siyo baada ya kutoka madarakani bali akiwa madarakani. Aliandika mojawapo ya vijitabu vyake maarufu kiitwacho "TUJISAHIHISHE". CCM ni lazima ianze hapo. Iandae waraka wa kina wenye kuanisha na kutuelezea mapungufu ya utawala wake na ni wapi wamekosea na makosa hayo yamesababisha nini. Ni lazima wakubali kuwa wamekuwa walevi wa madaraka.

2. IWE TAYARI KULIPA GHARAMA YA MAKOSA HAYO
Sasa, haitoshi kwa CCM kutuambia tu imekosea au ina udhaifu; lazima iwe tayari kulipa gharama ya makosa hayo - hata ikiwa ni gharama yoyote ile. Pasipo kuwa tayari kulipa gharama au kuhofia gharama ni kutokuwa wa kweli katika dhana nzima ya kujitengeneza. Ndio maana wengine wetu tumepuuzia na kukejeli wazo la "kujivua gamba" kwa sababu dhana nzima haijaonesha kama CCM iko tayari kulipa gharama ya uamuzi huo. Matokeo yake CCM imebakia kucheza mchezo wa "kidali po" na watuhumiwa wa ufisadi huku wakinyosheana vidole kama wanaoogopana. Bila kuwa tayari kulipa gharama CCM haiwezi kubadilika.

3. IKUBALI KUWA NDOGO LAKINI MAKINI NA BORA

CCM inajivunia wanachama wengi zaidi nchini; lakini ni kwa kiasi gani inajivunia wanachama makini na bora zaidi? Sasa hivi kuna hali ya kuwaona wana CCM wote kama wanachama wa chama ambacho tayari kimeharibika na watu wameamua kufa nacho tu. Mabadiliko ya kweli yatahusisha kujimega - siyo kujivua gamba - na kusababisha kuondoka kwa kikundi cha wana CCM. Katika hili naamini CCM ni lazima iwe tayari kujisafisha kwa kuwaondoa wanachama siyo tu waliothibitishwa kuwa ni mafisadi bali hata ambao wanatuhumiwa kuwa ni mafisadi. Zamani CCM ya Nyerere haikujali mtu alikuwa ni nani, amefanya nini kwa chama au vipi lakini kama alikuwa ni tatizo kwa taifa au chama hakuvumiliwa. Orodha ya watu walioondolewa ni kubwa na wengine ndio walikuwa "vigogo" wa enzi hizo; nani atamsahau Kambona? Nani atamsahau Chifu Fundikira? Leo hii CCM ina watu wanaosababisha matatizo kwa taifa na CCM yenyewe lakini hakuna mwenye uwezo wa kutaka watu hao waondolewe - kwa kuogopa kuonekana siyo demokrasia. Demokrasia ni pamoja na kuchukua maamuzi ya wazi, ya makusudi na yaliyolengwa kuliokoa taifa. Katika kufanya hivyo kuna watu wapungua na vikaragosi vyao lakini CCM itabakia na watu makini na bora na kurudisha mvuto wake. Hili naweza uklisema kwa chama kingine chochote ambacho kinajikuta kwenye migogoro.

4. IBADILI MFUMO WA KUMPATA MGOMBEA WA URAIS MAPEMA ZAIDI

Mojawapo ya matatizo tunayoyaona sasa hivi ndani ya CCM (na yanasubiri kutokea ndani ya CHADEMA) ni mfumo wa kumpata mgombea wa Urais. Maneno na kelele zote tunazozisikia sasa zinatokana namfumo mbovu wa kumpata mgombea wa Urais. CCM inaweza kujikuta inatuliza kelele na migongano ya ndani endapo tu itaamua kubadilisha mfumo wake wa kumpata mgombea wa Urais na hili likafanyika mapema zaidi. Mtindo mzuri ni ule ambao utarudisha uamuzi kwa wanachama na siyo kwa Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mfumo ambao ungefuata mtindo wa Primaries ambapo wagombea wangeruhusiwa kuandaa ilani zao wakaziuza kwa wanachama mikoani na mwishowe kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wale ambao wameweza kuhimiri ushindani kwenye primary wanakuja na kuomba kura za watu wa mikoani na kuuza ajenda zao huku wakishindanishwa ndani ya chama - kwa kupitia midahalo na mikutano ya pamoja - na hatimaye kura zinapigwa kumpata mgombea wa CCM na wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Kimsingi hakutakuwa na "mgombea pekee" tena na itaweka utaratibu mzuri wa kumpata mgombea mwenza vile vile kwani yeyote atakayeshinda atatakiwa kumteua mgombea mwenza wake kutoka upande mwingine wa Muungano ambaye atapitishwa na huo Mkutano Mkuu. Bila kutatua tatizo hili la Mgombea wa Urais CCM itaendelea kutengeneza makundi ya kudumu na yenye visasi. Nikiri kuwa wazohili siyo langu bali linatoka kwenye "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania".

5: VIONGOZI WAKE WAKUTANE NA WACHADEMA NA UPINZANI

Mojawapo ya mambo ambayo ni ya kusikitisha sana na yanayoonesha uwezo mdogo wa Rais Kikwete kuongoza - na ninamaanisha hivyo - ni kushindwa kwake kujaribu au kutaka kukaa pamoja na viongozi wa upinzani na kujadili masuala ya mustakabali wa taifa na badala yake kutumia kila nafasi kukoleza tofauti zetu kwa maneno na vitendo ambavyo havisadii kujenga umoja zaidi ya kuzidi kutufanya tuchague pande mbili tofauti. Kabla ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi na miezi michache baadaye nimetoa wito kuwa Kikwete akutane na viongozi wa Chadema na kuwasikiliza na wao kumsikiliza na hatimaye kuja na mambo ya kuweza kukubaliana.

Sijui ni nani anayemshauri na sijui ni kina nani wanamuzia lakini kama ni yeye mwenyewe basi kuanguka kwa CCM kunakolezwa naye kwani tofauti za kisiasa zina kawaida ya kuzaa chuki za kisiasa; chuki za kisiasa huzaa visasi vya kisiasa na visasi vya kisiasa huzaa vuguru za kisiasa. Hii ni kanuni ya kudumu ya mahusiano kati ya siasa na tofauti za kisiasa katika jamii. Tulipofika sasa ni kwenye genge la maangamizi na kwa kadiri ya kwamba uongozi wa CCM hautaki kukaa chini na Chadema kukubaliana mambo mbalimbali ili kuweza kutengeneza mazingira mazuri basi ndivyo hivyo hivyo tofauti za kisiasa zinazidi nchini. Uamuzi wa kujaribu kuzima tofauti za kisiasa kwa kutumia vyombo vya dola, vitisho au unyanyasaji hautafanikiwa kwani mtu ambaye utu wake umedharauliwa na yeye ametwezwa hana cha kupoteza tena. CCM na serikali yake isifikirie hata kidogo kuwa kuwanyanyasa kina Zitto, Mbowe, Slaa n.k kunawaharibia sifa la hasha. Kinaanza kuwapeleka kwenye kona ya msimamo mkali.

Hakuna watu ambao wako mild kisiasa kama Zitto, as an intellectual and an influential political figure in the country, Zitto anazidi kusukimizwa kuwa na msimamo mkali dhidi ya CCM na akija kuchukua msimamo huo wazi CCM itajikuta pabaya zaidi. Mambo waliyoyafanya baada ya uchaguzi, kumkamata kwa madai ya kuingilia kazi za polisi na kukamatwa tena hivi juzi Singida kunanifanya nielewe kuwa CCM wanataka maadui zaidi na siyo marafiki; na wakimkosa Zitto na watu wengine kama marafiki na kuwaweka upande wa maadui CCM itajikuta inajichimbia zaidi na zaidi katika kaburi la kuangamia kwake.

Hakuna ujanja, CCM ni lazima ifanye mkutano wa pamoja na uongozi wa Chadema pasipo masharti au kutishana bali katika hekima na roho ya umoja wa kitaifa. Wasipokutana sasa watalazimishwa kukutana wakati michirizi ya machozi inatiririka katika mashavu ya Watanzania. Watabakia kutafuta wa kuwalaumu!

6. [censored]
7. [censored]


Nimesema ni mambo ambayo yanaweza tu kusaidia CCM kujiokoa, hayahakikishi kuwa itajiokoa. Lakini yakifanyika Taifa litanufaika hata kama CCM haitaokoka. Yaani, hata CCM isipookoka baada ya kufanya haya yote, Tanzania itaokoka. Hili ni bora zaidi. Bora chama kimoja kife kuliko taifa zima kuangamia.
Sikio la kufa halina dawa!...
 
Mmmh, si hawa CCM ninaowafahamu!

As long as sehemu kubwa ya watanzania watanedelea kuwa wajinga, CCM itaendelea kupeta. Ukumbuke kuwa zamani tulisema rasilimali ya myonge ni umoja, lakini siku hizi tumeona kuwa raslimali ya CCM ni ujinga wa watanzania waliowengi. I do not see that fact changing any time soon.

Unachosema mwanakijiji ni kuwa CCM kwanza inaze kujiangalia na ufusadi. Angalia safu ya uongozi wa chama, nani si fisadi na nani anaweza kumnyoshea kidole mwingine. Imefika wakati wanasema wazi hakuna aliyemsafi kuliko mwingine, that means wote ni wachafu. Nani atamsafisha mwenzie?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom