Mambo 7 ambayo CCM ikifanya yaweza kujiokoa; vinginevyo...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa miezi kadhaa sasa baada ya Uchaguzi tumeona juhudi kadhaa za Chama cha Mapinduzi kujiokoa au niseme kujinusuru. Juhudi hizi zimelenga hasa katika kurudisha "imani" ya wananchi kwa Chama cha Mapinduzi, imani ambayo wananchi wanaonekana kuipoteza kama ilivyoonekana wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Uchaguzi Mkuu uliopita umewathibitishia wana CCM kuwa kama hawakuona haja ya kubadilika kabla ya wakati huo basi haja hiyo imenguruma kama radi baada ya uchaguzi na kuiweka CCM katika uchaguzi usioepukika; kubadilika au kuvunjika.

Mengi tuliyoyaona yamefikiria na kubuniwa na wana CCM wenyewe katika kujaribu "kujichunguza". Mengi ya haya kwa watu wengine yameendelea kuwa kama kichekesho kwani haionekani kugusa hasa kiini cha mgogoro uliopo kati ya wananchi na chama kinachowatawala; mgogoro ambao hauwezi kukoma kwa vitisho, nguvu za dola, au kupuuzia. Vitisho, nguvu za dola na kupuuzia vilifanya kazi kwa muda tu lakini baada ya wananchi wa Tanzania kuvuka mpaka wa woga na ujasiri na kukipita kizingiti cha kutokujali vitu hivyo vimebakia kama masalia ya zana za ujima ambazo sehemu yake ni katika jumba la makumbusho.

Bahati mbaya sana CCM katika kujisafisha wameshindwa kuwauliza wakosoaji wake kutoa maoni na hivyo wamebakia wao wenyewe ndani kwa ndani wakipeana maoni, kupepeana kwa kuulizana na kutulizana kwa kubebana huku wakichekeana na kukumbatiana katika kujiridhissha kuwa mambo yataenda na kuwa mazuri. Kwa vile nimeona kuwa hakuna mtu ndani ya CCM atawaambia ninachowaambia hapa nimeona nijitolee tu bila kuombwa kuwapa mawazo ya nini wafanye ili waweze kujiokoa na wasipofanya kuangamia kwao kuko dhahiri, kwaja kwa haraka, na kutawavunja kusababisha CCM iparaganyike kama sehemu ile ya unabii inavyosema. Bahati mbaya sana (kama naweza kusema ni bahati mbaya) hakuna mtu aliyeweza kukwepa neno la unabii likashatoka.

Kuanzia simulizi la Kigiriki la Odepus hadi filamu inayocheza ya Panda 2 tunaweza kuona jinsi gani neno likitamkwa lilivyo huenda likatimia na hakuna mtu wa kuweza kubaadilisha japo vitu mbalimbali vyaweza kufanywa vikabadilika bila kubadilisha matokeo kwani once fate has set its course, no one can escape from its condemning and unforgiving hands. Ndio maana nimesema kuwa mambo yafuatayo yakifanyika CCM "yaweza" kujiokoa... sijui kama ITAWEZA kujiokoa. Labda itapunguza tu ukali wa fate.

1. IKUBALI MAKOSA, IOMBE RADHI TAIFA NA KUKIRI UBOVU WAKE

Katika mchakato wa hatua 12 za kuacha ulevi hatua ya kwanza kabisa ya kukiri kwamba mtu hakuwa na uwezo dhidi ya kileo. Yaani, kukubali udhaifu na makosa ya mtu kwani sifa ya kwanza ya mlevi ni kuwa hakubali kuwa ni mlevi; huweza kujiita "anakunywa kidogo tu" au "anaweza kuacha wakati wowote" n.k Hadi pale atakapokubali kuwa ni mlevi ndipo hatua za kujinusuru zinapoanza. CCM vivyo hivyo. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (siyo Mzee mmoja Nyerere!) alikuwa na uwezo huu wa kujiangalia na kujikosoa. Kinyume na imani na uongo unaonezwa siku hizi kuwa Nyerere alikuwa hashauriki ukweli wa historia unaonesha kuwa ni kiongozi pekee wa Tanzania ambaye aliwahi kubadilisha mwelekeo wa mambo kadha wa kadha na kukiri kukosea - siyo baada ya kutoka madarakani bali akiwa madarakani. Aliandika mojawapo ya vijitabu vyake maarufu kiitwacho "TUJISAHIHISHE". CCM ni lazima ianze hapo. Iandae waraka wa kina wenye kuanisha na kutuelezea mapungufu ya utawala wake na ni wapi wamekosea na makosa hayo yamesababisha nini. Ni lazima wakubali kuwa wamekuwa walevi wa madaraka.

2. IWE TAYARI KULIPA GHARAMA YA MAKOSA HAYO
Sasa, haitoshi kwa CCM kutuambia tu imekosea au ina udhaifu; lazima iwe tayari kulipa gharama ya makosa hayo - hata ikiwa ni gharama yoyote ile. Pasipo kuwa tayari kulipa gharama au kuhofia gharama ni kutokuwa wa kweli katika dhana nzima ya kujitengeneza. Ndio maana wengine wetu tumepuuzia na kukejeli wazo la "kujivua gamba" kwa sababu dhana nzima haijaonesha kama CCM iko tayari kulipa gharama ya uamuzi huo. Matokeo yake CCM imebakia kucheza mchezo wa "kidali po" na watuhumiwa wa ufisadi huku wakinyosheana vidole kama wanaoogopana. Bila kuwa tayari kulipa gharama CCM haiwezi kubadilika.

3. IKUBALI KUWA NDOGO LAKINI MAKINI NA BORA

CCM inajivunia wanachama wengi zaidi nchini; lakini ni kwa kiasi gani inajivunia wanachama makini na bora zaidi? Sasa hivi kuna hali ya kuwaona wana CCM wote kama wanachama wa chama ambacho tayari kimeharibika na watu wameamua kufa nacho tu. Mabadiliko ya kweli yatahusisha kujimega - siyo kujivua gamba - na kusababisha kuondoka kwa kikundi cha wana CCM. Katika hili naamini CCM ni lazima iwe tayari kujisafisha kwa kuwaondoa wanachama siyo tu waliothibitishwa kuwa ni mafisadi bali hata ambao wanatuhumiwa kuwa ni mafisadi. Zamani CCM ya Nyerere haikujali mtu alikuwa ni nani, amefanya nini kwa chama au vipi lakini kama alikuwa ni tatizo kwa taifa au chama hakuvumiliwa. Orodha ya watu walioondolewa ni kubwa na wengine ndio walikuwa "vigogo" wa enzi hizo; nani atamsahau Kambona? Nani atamsahau Chifu Fundikira? Leo hii CCM ina watu wanaosababisha matatizo kwa taifa na CCM yenyewe lakini hakuna mwenye uwezo wa kutaka watu hao waondolewe - kwa kuogopa kuonekana siyo demokrasia. Demokrasia ni pamoja na kuchukua maamuzi ya wazi, ya makusudi na yaliyolengwa kuliokoa taifa. Katika kufanya hivyo kuna watu wapungua na vikaragosi vyao lakini CCM itabakia na watu makini na bora na kurudisha mvuto wake. Hili naweza uklisema kwa chama kingine chochote ambacho kinajikuta kwenye migogoro.

4. IBADILI MFUMO WA KUMPATA MGOMBEA WA URAIS MAPEMA ZAIDI

Mojawapo ya matatizo tunayoyaona sasa hivi ndani ya CCM (na yanasubiri kutokea ndani ya CHADEMA) ni mfumo wa kumpata mgombea wa Urais. Maneno na kelele zote tunazozisikia sasa zinatokana namfumo mbovu wa kumpata mgombea wa Urais. CCM inaweza kujikuta inatuliza kelele na migongano ya ndani endapo tu itaamua kubadilisha mfumo wake wa kumpata mgombea wa Urais na hili likafanyika mapema zaidi. Mtindo mzuri ni ule ambao utarudisha uamuzi kwa wanachama na siyo kwa Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mfumo ambao ungefuata mtindo wa Primaries ambapo wagombea wangeruhusiwa kuandaa ilani zao wakaziuza kwa wanachama mikoani na mwishowe kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wale ambao wameweza kuhimiri ushindani kwenye primary wanakuja na kuomba kura za watu wa mikoani na kuuza ajenda zao huku wakishindanishwa ndani ya chama - kwa kupitia midahalo na mikutano ya pamoja - na hatimaye kura zinapigwa kumpata mgombea wa CCM na wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Kimsingi hakutakuwa na "mgombea pekee" tena na itaweka utaratibu mzuri wa kumpata mgombea mwenza vile vile kwani yeyote atakayeshinda atatakiwa kumteua mgombea mwenza wake kutoka upande mwingine wa Muungano ambaye atapitishwa na huo Mkutano Mkuu. Bila kutatua tatizo hili la Mgombea wa Urais CCM itaendelea kutengeneza makundi ya kudumu na yenye visasi. Nikiri kuwa wazohili siyo langu bali linatoka kwenye "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania".

5: VIONGOZI WAKE WAKUTANE NA WACHADEMA NA UPINZANI

Mojawapo ya mambo ambayo ni ya kusikitisha sana na yanayoonesha uwezo mdogo wa Rais Kikwete kuongoza - na ninamaanisha hivyo - ni kushindwa kwake kujaribu au kutaka kukaa pamoja na viongozi wa upinzani na kujadili masuala ya mustakabali wa taifa na badala yake kutumia kila nafasi kukoleza tofauti zetu kwa maneno na vitendo ambavyo havisadii kujenga umoja zaidi ya kuzidi kutufanya tuchague pande mbili tofauti. Kabla ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi na miezi michache baadaye nimetoa wito kuwa Kikwete akutane na viongozi wa Chadema na kuwasikiliza na wao kumsikiliza na hatimaye kuja na mambo ya kuweza kukubaliana.

Sijui ni nani anayemshauri na sijui ni kina nani wanamuzia lakini kama ni yeye mwenyewe basi kuanguka kwa CCM kunakolezwa naye kwani tofauti za kisiasa zina kawaida ya kuzaa chuki za kisiasa; chuki za kisiasa huzaa visasi vya kisiasa na visasi vya kisiasa huzaa vuguru za kisiasa. Hii ni kanuni ya kudumu ya mahusiano kati ya siasa na tofauti za kisiasa katika jamii. Tulipofika sasa ni kwenye genge la maangamizi na kwa kadiri ya kwamba uongozi wa CCM hautaki kukaa chini na Chadema kukubaliana mambo mbalimbali ili kuweza kutengeneza mazingira mazuri basi ndivyo hivyo hivyo tofauti za kisiasa zinazidi nchini. Uamuzi wa kujaribu kuzima tofauti za kisiasa kwa kutumia vyombo vya dola, vitisho au unyanyasaji hautafanikiwa kwani mtu ambaye utu wake umedharauliwa na yeye ametwezwa hana cha kupoteza tena. CCM na serikali yake isifikirie hata kidogo kuwa kuwanyanyasa kina Zitto, Mbowe, Slaa n.k kunawaharibia sifa la hasha. Kinaanza kuwapeleka kwenye kona ya msimamo mkali.

Hakuna watu ambao wako mild kisiasa kama Zitto, as an intellectual and an influential political figure in the country, Zitto anazidi kusukimizwa kuwa na msimamo mkali dhidi ya CCM na akija kuchukua msimamo huo wazi CCM itajikuta pabaya zaidi. Mambo waliyoyafanya baada ya uchaguzi, kumkamata kwa madai ya kuingilia kazi za polisi na kukamatwa tena hivi juzi Singida kunanifanya nielewe kuwa CCM wanataka maadui zaidi na siyo marafiki; na wakimkosa Zitto na watu wengine kama marafiki na kuwaweka upande wa maadui CCM itajikuta inajichimbia zaidi na zaidi katika kaburi la kuangamia kwake.

Hakuna ujanja, CCM ni lazima ifanye mkutano wa pamoja na uongozi wa Chadema pasipo masharti au kutishana bali katika hekima na roho ya umoja wa kitaifa. Wasipokutana sasa watalazimishwa kukutana wakati michirizi ya machozi inatiririka katika mashavu ya Watanzania. Watabakia kutafuta wa kuwalaumu!

6. [censored]
7. [censored]


Nimesema ni mambo ambayo yanaweza tu kusaidia CCM kujiokoa, hayahakikishi kuwa itajiokoa. Lakini yakifanyika Taifa litanufaika hata kama CCM haitaokoka. Yaani, hata CCM isipookoka baada ya kufanya haya yote, Tanzania itaokoka. Hili ni bora zaidi. Bora chama kimoja kife kuliko taifa zima kuangamia.
 
asante mm kwa thread yako nzuri but mapendekezo yako ni magumu mno hasa kwa ccm na chadema.

Kwa jinsi wananchi wanavyoichukia ccm ukifanya nao urafiki jua na wewe umechukiwa, na wakijua kuwa unafanya vikao na unakutana nao basi wanachama na wapenz wa chama wanakuwa na wasiwasi na wewe. Hii imetokana na kwamba viongozi wengi wa upinzani wamerubuniwa kwa pesa na kuamia ccm. Mfano kabouru aliyekuwa kiongozi chadema. So pendekezo la ccm na chadema kuzungumza ni gumu sana sio kwa ccm peke yao bali na kwa chadema pia. Wafuasi wanachama na wapenzi wa chadema hawataki kusikia kuwa kuna urafiki kati ya cm na chadema.
 
ahsante mkubwa kwa nondo za ukweli, ila CCM ni sikio la kufa ...... Nimeipenda hii ni bora chama kimoja kufa kuliko taifa zima kuangamia
 
asante mm kwa thread yako nzuri but mapendekezo yako ni magumu mno hasa kwa ccm na chadema.

Kwa jinsi wananchi wanavyoichukia ccm ukifanya nao urafiki jua na wewe umechukiwa, na wakijua kuwa unafanya vikao na unakutana nao basi wanachama na wapenz wa chama wanakuwa na wasiwasi na wewe. Hii imetokana na kwamba viongozi wengi wa upinzani wamerubuniwa kwa pesa na kuamia ccm. Mfano kabouru aliyekuwa kiongozi chadema. So pendekezo la ccm na chadema kuzungumza ni gumu sana sio kwa ccm peke yao bali na kwa chadema pia. Wafuasi wanachama na wapenzi wa chadema hawataki kusikia kuwa kuna urafiki kati ya cm na chadema.

of course najua CCM hawawezi kufanya haya; lakini tumeyaweka wazi ili wasije kusema kuwa "hawakufikiria".
 
of course najua CCM hawawezi kufanya haya; lakini tumeyaweka wazi ili wasije kusema kuwa "hawakufikiria".
Asante kwa mtazamo wako wenye mlengo mmoja umeanza vizuri ila umemaliza vibaya sana ukaonesha itikadi yako wazi,nasi hatuangalii umeanzaje bali unamalizaje
 
Great article as usual! CCM wanajiona masharobaro hawawezi kufanya hayo. Ndo mwisho wao!
 
Katika yote hapo juu nadhani kila mtu atafikiria gumu ni lile la CCM kukutana na CHADEMA, lakini kwa nnavyifahamu hii CCM ya leo hakyanani gumu ni lile la kwanza kabisa KUKUBALI MAKOSA, these guys won't, and never will. Maana wao (Viongozi wa CCM na washauri) kukubali makosa basi moja kwa moja wanaamini itamuharibia mwenyekiti, itamdhoofisha na kumpotezea umaarufu kwa wananchi (utadhani bado anao).

Tatizo kubwa la CCM na ni la kihistoria ni MWENYEKITI. CCM ni mwenyekiti, ndani ya miaka yote hii toka 1977 CCM wameshindwa kutofautisha chama na mwenyekiti. Bado wako kule kule kwenye kudumisha fikra, mawazo na maamuzi ya mwenyekiti. Sasa tatizo limekuja mwenyekiti ndiyo kama mnavyomuona. Nchi iko kwenye auto pilot lakini tunasubiri neema na busara za mwenyekiti.Hiivyo basi Mkjj ulitakiwa kuweka "censored" kuanzia no. 2 mpaka 7.
 
Mkuu Nyambala,nakubaliana na ww hata mwenyekiti akiamua mambo ya ajabu watakuabaliana ili tu wasionekane wanampinga ,ndio maana suala la kuwatosa wanaokigharimu chama linakuwa gumu hapo ndipo wazo la MM litakapo shindwa la kukubali makosa na kulipa gharama kwa yale waliotenda,CCM ya leo haina Mwenyekiti ambae anauwezo wakuamua na kusema kwa sauti yenye msisitizo na akaonekana anamaana na lile analolisema.ndio maana hata waliochini yake wanafanya wapendavyo wakijua hakuna wakuwauliza,usishangae siku moja Mwenyekiti akaahilisha kikao kwa vile Swaiba wake hajafika kwenye kikoa.
 
Mimi nimependa kitu kimoja ktk makala yako "kuwa Chadema inashindwa kujitofautisha na CCM katika mambo mengi". Ukichunguza sana baada ya chadema kuwa chama kikuu cha upinzani, nilitegemea kuwa ingeanzsiha mara moja utoaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa wananchi ikiwa na lengo la kuwafanya wananchi kutambua na kuelewa kwa kina wajibu wa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63.-(2) Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

Kutokana na hilo chadema inawaacha wabunge wake wakishiriki kalamu mbili ambazo zilimshinda fisi; Wakati wabunge wake wakitamani sana kuonekana wakiisimamia Seikali ipasavyo, jambo ambalo linahitaji mbunge atumie muda wake mwingi akifanya utafiti na ufuatiliaji wa utendaji wa serikali katika kukusanya na kutumia fedha na raslimali mbali mbali; wakati huo huo wanatumbukia katika mtego wa CCM wa mbunge ambaye ni tarishi wa kupikea maendeleo kutoka serikalini kuu, mawaziri n.k na kuyafikisha jimboni kwa lengo la kuwafurahisha wananchi ili wamchague tena.

Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa wabunge wa CDM hawataweza kufanikisha kalamu yoyote vizuri na kutimiza matarajio ya wananchi, japokuwa wengi wao wanaonyesha uwezo mkubwa sana wa kuisimamia Serikali,jambo ambalo si wananchi wengi wakiappreciate kama utarishi wa kupokea maendeleo kutoka serikali kuu na kuyafikisha jimboni. Baada ya kudanganya wananchi kuwa imewatema mafisadi CCM, licha ya wabunge wa CCM kushindwa kutimiza wajibu wa mbunge ipasavyo na badala yake kutimiza utarishga wa maendeleo ya jimbo moja moja; wananchi wataona kuwa wabunge wa CDM walishindwa kuleta maendeleo waliyoahidi na hivyo kuwatosa.

CHADEMA inapaswa kuiga mfano wa Mhe Benjamin William Mkapa ambaye baada ya kuingia madarakanai kwa kuuza ilani ya CCM ya mwaka 1995, mapema kabisa alitangaza hadharani kuwa ilani hiyo haitekelezeki na akapanga mipango yake mipya kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo chini yake Serikali ya Tanzania ikaanza kulipa madeni ya nje jambo ambalohalikuwemo katika ilani hiyo. Serikali yake iliheshimika kwa wafadhili na kufanikiwa kukopeshwa na kupatiwa misaada iliyowezesha kukuza uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei katika kipindi chote cha utawala wake, japokuwa yalikuwepo mapungufu kadhaa.

Hivyo CHADEMA inatakiwa kuwaelimisha watanzania mapema iwezekanavyo kuwa mfumo wa mbunge kutoa kipaumbele katika maendeleo ya jimbo na kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuisimamia Serikali kwa kuunga mkono na kupigia makofi kila hoja ya Serikali ndio maaan Tanznaia ni inakuwa katika kundi la nchi maskini zaid hapa duniania licha ya raslimali tulizonazo. Aidha ubinafsi wa kupendelea jimbo atkalo ni sawa na rushwa kwa wananchi ili wamchague kwa kuwa majukumu yake ni kuisimamia Serikali yenye wajibu wa kuwatumikia watanzania wote ili hatimaye Serikali iweze kupata mapato mengi zaid ya kuwahudumia watanzania wote kinyume na hali ilivyo sasa ambapo fedha zinafujwa ovyo, madini yanasombwa ovyo, raslimali zetu zinzhmishwa kiholela n.k.

CHADEMA inapaswa kuwaelimisha watanzania kuwa mfumo ulioasisiwa na CCM wa kuwapima wabunge kwa kutegemea maendeleo waliyopelekea katika majimbo wanayotoka ulikuwa na lengo la kudhoofisha dhana ya "KUISIMAMIA SERIKALI".Mana halisi ya "mbunge" ni kuwa wananchi katika jimbo fulani wanapatiwa kiti kimoja katika bunge ambalo lina wajibu wa kuisimamia Serikali ambayo kwa mujibu wa Katiba ndio yenye mamlaka ya kukusanya, kupanga na kutumia fedha, madini na raslimali zote za Tanzania kwa manufaa ya wananchi wote na sio wa jimbo moja moja.

Chini ya mfumo huo mbovu ili mbunge aweze kupata maji, barabara, shule n.k katika jimbo lake hulazimika kuwapigia magoti mawaziri, makatibu wakuu n.k huko wizarani na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ambao kwa pamoja alipaswa kuwasimamia kama mwakilishi wa wananchi. Sasa kama mbunge atapokea upendeleo kutoka kwa watu anaopaswa kuwasimamia, atawezaje kutimiza majukumu yake ya kuwasimamia?.

Ni kutokana na mapungufu haya, hivi sasa hapa nchini fedha za umma, mali za umma, madini na raslimali zote za Tanzania hazina watu wa kuhakikisha vinatumika kwa kadri ya matarajio ya wananchi kutokana na wabunge kugeuzwa matarishi wa maendeleo ya jimbo moja moja, hali hii inawaacha viongoizi, watumishgi wa Serikali pasipo kuwa na usimamizi wa moja kwa moja kutoka kwa wananchi na hiki ndicho chanzo cha umaskini wa wwatanzania na Tanzania.

Katika utoaji huo wa elimu ya uraia CHADEMA pia inapaswa kuhakikisha wananchi wanapata ufahamu wa namana ya kutimiza shauku na lengo lao la kuchagua mtu/watu wa kuwaletea maendeleo yaani kuchagua watu ambao watakuwa na kauli ya mwisho katika fedha/mafungu ambazo yatatumika kuleta maendeleo katika majimbo yao k.m kupitia katiba mpya wananchi waelimishwe umuhimu wa kupendekeza mfumo wa Serikali za miitaa ambazo wananchi wanamchagua meya ambaye ni mtendaji badala ya utaratibu wa sasa ambao halmashauri zinakuwa chini ya wakurugenzi wenye kauli ya mwisho juu ya matumizi ya fedha.

Mfano halisi wa hali hii ni bajeti ya 2011/12 ambapo zaidi ya Shs Trilioni 6 zitapelekwa katika halmashauri za wilaya zilizo chini ya wakurugenzi na wawakilishi wa wanancdhi yaani wabunge na madiwani wakiwa na sauti ndogo sana kuhusu matumizi ya fedha hizo. Sasa katika mazingira haya maendelo wananchi wanayoyatarajia yatakujaje pasipokuwepo msimamazi wa wananchi?

Wananchi wanataraji maendelo kutoka huko na mbunge na diwani ilihali fdha na mafungu yapo chini ya mtu mwingine aliye chini ya Serikali Kuu. Matokeo yake ni wizi a ufisadi wa kutisha. Kwa maneno mengine watanzania wengi hawatambui kuwa licha ya shauku yao ya kuchagua watu wa kuwaletea maendeleo kama vile wabunge na madiwani, viongozi hawa ni wa kisiasa zaidi. Mfumo unapaswa kubadilishwa ili watanzania wachague watendaji kama vile meya mtendaji ambaye atakuwa ndiye kiongozi na muwajibikaji mkuu katika halmashauri.

Endapo Chadema itashindwa kufanya haya si ajabu wabunge wake wengi wakashindwa kurejea bungeni na ikashindwa kuongeza idadi ya wabunbge wake katika uchaguzi wa 2015 kutokana wapiga kura kukosa elimu ya uraia ya kutosha kujua wanatakiwa kufanya nini ili hatimaye taifa liweze kupata maendeleo kwa pamoja na sio jimbo moja moja. Ikumbukwe kuwa CCM inashamiri kutokana na ujinga wa wananchi ndio maana kutoka 1992 imekata kuwapatia wananchi elimu ya uraia.
 
Mzee wangu ni kipindi kidogo kwa kuwa nina majukumu ya hapa na pale ila kuwa nimesoma vizuri sana makala yako ni kweli kabisa kuwa CCM haya mambo ndio yanakiwezesha CCM kushinda uchaguzi hivyo kuwa kufanya hivyo kunaweza kufanya CCM kushindwa kama vile wanaposema kuwa ni ngumu sana kuja na mikakati na pia CCM kuacha kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi na ndio maana kuna ulazima wa kuachana nayo kabisa CCM na itakuwa vizuri sana kama ikishindwa uchaguzi kabisa
 
Nasita kuona hili ndani ya ccm yetu ila kama tungelikuwa na uvccm yenye mashiko na kutujali ccm ingelithubutu kwenda kwenye primaries na wakapigiwa kura....hii ingelisaidia sana kuvifanya vyombo vya usalama kujitenga na dola mapema na kuwa huru kiutendaji....., media nazo zingejiweka hadharani kuwa zimeegemea mrengo upi baadala kuwa wanafiki kama sasa, sitaki namtaka...., nakumbuka utawala wa bill clinton king ndie alikuwa reporter wa cnn alipoingia bush king akaondolewa na sasa obama white house sasa karejea king tena--uhuru wa mwanahabari ndani ya media moja ku side anakoamini
 
SIJAKUELEWA KABISA, umekula unga wa ndele? nyeusi unaiita nyeupe na nyeupe unaiita nyeusi!!!!!!!! Sijui kama umejibu hoja, au umepinga hoja? AU unajibu mapigo? Mzee Mwanakijiji ametoa wazo na hoja zake juu ya nini kifanyike labda kitakinusuru CCM, wewe watanabe unakuja na CDM, Sijaelewa. Hebu mawazo yako yapost kama new topic
 
Mwanakijiji, hapa umejenga dhana au unajaribu kutoa ushauri? Hakuna hata moja ulilosema linatekelezeka. Kuyatekeleza madai yako maana yake ni kuwa CCM ikubali kufa na hilo haliwezekani na wala halitatokea. Hoja yako ya mwisho ya kukaa na wapinzani ingeleeta maana sana kama wapinzani wenyewe wangekuwa na umoja. CCM haiwezi kukaa na chama kimoja kimoja kujadili mustakabali wa nchi mnachotakiwa wapinzani kukomaa kisiasa ili mtengeneze ajenda moja ijadiliwe vinginevyo itakuwa ni kupoteza muda.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
safi saana watu kama ninyi kumi na tano Tanzania itafika mbali sana .......laiti kama ungekua kule marekani ningekupa cheo cha usenator....lakini kwa kitanzania na kupa HONGERA sana ndugu yangu...kwa kweli inapendeza saaana!!
 
SIJAKUELEWA KABISA, umekula unga wa ndele? nyeusi unaiita nyeupe na nyeupe unaiita nyeusi!!!!!!!! Sijui kama umejibu hoja, au umepinga hoja? AU unajibu mapigo? Mzee Mwanakijiji ametoa wazo na hoja zake juu ya nini kifanyike labda kitakinusuru CCM, wewe watanabe unakuja na CDM, Sijaelewa. Hebu mawazo yako yapost kama new topic

Nilikuwa na wazo hilo la CDM kujitofautisha na CCM, lakini baada ya kuwa MMJ alilitaja katika makala yake nikona ni vyema badala ya kuanzisha thread mpya niweke maoni yangu hapo hapo. Hivyo napokea usharui nimefungua thread mpya
 
safi saana watu kama ninyi kumi na tano Tanzania itafika mbali sana .......laiti kama ungekua kule marekani ningekupa cheo cha usenator....lakini kwa kitanzania na kupa HONGERA sana ndugu yangu...kwa kweli inapendeza saaana!!
 
ila hili la NNE Mtu wangu nazani ni mtihani.
Maana hata yooooooote yaliyompata na yanayompata Mh.EDDIE NI mnyukano wa 2015

maana jamaa nyota yake iko juu sana.

lkn ngoja tuone. AHSANTE KWA U chambuzi wako wa kina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom