Mambo 6 yatakayotawala Mdahalo wa Urais kati ya Donald Trump na Joe Biden

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Rais wa Marekani na mgombea wa chama cha Republic, Donald Trump anatarajiwa kukutana uso kwa uso na mpinzani wake, Joe Biden katika mdahalo wa kwanza wa urais unaotarajiwa kufanyika baadaye hii leo katika ukumbi wa Chuo cha Case Western Reserc, Cleveland, Ohio.

Mdahalo huo unatarajiwa kufanyika kwa muda wa dakika 90 bila kuwa na kipindi chochote cha mapumziko, kuanzia saa tatu kamili usiku kwa majira ya Ohio (Sawa na saa 10 alfajiri kwa majira ya Afrika Mashariki), ukiongozwa na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Fox News, Chriss Wallace.

Mdahalo wa leo ni wa kwanza kati ya midahalo minne inayotarajiwa kufanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa Novemba 3, kwa mujibu wa Kamisheni inayosimamia midahalo ya uraisi. Tofauti na ilivyokuwa miaka yote iliyopita, mdahalo wa leo hautahusisha wagombea hao wawili kupeana mikono, na watu wote watakaoshiriki katika mdahalo huo watalazimika kupima virusi vya corona na kuchukua tahadhari zote za kiafya kuepusha maambukizi ya virusi vya corona.

US Presidential Debate.jpg


Mambo yanayotarajiwa kutawala katika mdahalo wa leo ni Rekodi za Trump na Biden, Mahakama Kuu, Virusi vya Corona, Uchumi, Ubaguzi wa rangi, na Uadilifu katika zoezi la Uchaguzi, kwa mujibu wa Kamisheni ya Midahalo ya Urais.

Katika mdahalo huo, kila kipengele kitatengewa muda wa dakika 15, na kila mgombea ataruhusiwa kujibu swali kwa muda wa dakika 2 baada ya mwendesha mdahalo kufungua kipengele kwa kuuliza swali, kisha muda uliobaki utatumika kuendeleza mjadala kuhusu mada katika kipengele husika.

Ukwepaji kodi wa Trump
Moja kati ya mambo yanayoongeza joto la mdahalo wa leo ni suala lililoibuliwa na gazeti la New York Times siku ya Jumapili kuwa Rais Trump hakuwahi kulipa kodi kwa miaka 10 kati ya 15 kuanzia mwaka 2000, na kuwa tangu aliposhinda uchaguzi wa mwaka 2016, Trump alilipa kodi yenye thamani ya dola 750 tu.

Kampeni ya Biden ilitawaliwa na matangazo yaliyoonesha ni kwa kiasi gani waalimu, madaktari na manesi, kati ya wafanyakazi wengine, wanavyolipa kodi nyingi kuliko Trump, huku wengi wakiamini kuwa Biden atatumia hoja hiyo katika mdahalo wa leo. Hii si mara ya kwanza kwa suala la kodi ya Trump kuletwa katika mdahalo wa urais. Mwaka 2016, mgombea wa chama cha Democrat, Hillary Clinton aliwahi kusema kuwa Trump hataki kuweka wazi hesabu za kodi anayolipa, na kuwa kuna uwezekano wa ukwepaji wa kodi, kisha Trump akamjibu kwa kusema kuwa hilo ndilo jambo linalomfanya [Trump] kuwa mwerevu kuliko Clinton!

Ubaguzi wa Rangi
Ubaguzi wa rangi ni suala linalotarajiwa kuleta changamoto hasa katika mdahalo huu wa kwanza, kutokana na tofauti za wagombea hao wawili katika matukio ya ubaguzi wa rangi. Wakati Biden alionekana kuwa karibu na wahanga wa matukio ya ubaguzi wa rangi yaliyotendwa na polisi wa Marekani, Trump alitumia nguvu kubwa kulaumu vitendo vya uvunjifu wa amani na uporaji wa mali uliofanywa na waandamanaji, huku akionya kuwa kumchagua Biden ni kuchagua uvunjifu mkubwa zaidi wa amani. Biden, kwa upande wake, amesema kuwa kitendo cha Trump kushindwa kuwachukulia hatua waandamanaji wanaounga mkono utawala wa weupe mwaka 2017 ndicho kilichomshawishi kugombea urais, akisema kuwa misingi ya taifa ipo mashakani.

Kauli za Trump za upotoshaji
Rais Trump pia anafahamika kwa kutoa kauli zenye upotoshaji, na wengi wamekuwa wakijiuliza ikiwa kutakuwa na mtu atakayekuwa tayari kuhakiki kauli zake akiwa katika mdahalo huo. Lakini Mwenyekiti Msaidizi wa Kamisheni ya Uchaguzi amesisitiza kuwa hakutakuwa na mwongozaji yeyote katika mdahalo wa leo atakayekuwa akihakiki kauli za Trump pindi atakapokuwa jukwaani, lakini amesema kuwa wapo watazamaji wengi watakaokuwa wakisubiri atakachozungumza Rais Trump kwa ajili ya kuhakiki ukweli.

Chanzo: CNN
 
Sio kutumia kiingereza tu bali kunusa tu kwenye huo mdahalo hatasogea. Hana hulka na hapendi kuulizwa ulizwa vitu ambavyo vitampa wakati mgumu kuvifafanua.
People like Polepole who spent most of their time explaining what they have done mean they have done nothing. Development is something which can be seen is not invisible. They are something wrong with this regime i pray day and night for the change cos is only thing we need now
 
Trump katawala mdahalo

Biden anasahau kitu ambacho ametoka kukizungumzia muda si mrefu mpaka Trump anamkumbusha. Nadhani Biden has a memory issue

Trump ana maneno mengi katika kutackle maswari kuliko Biden
 
Trump katawala mdahalo
Biden anasahau kitu ambacho ametoka kukizungumzia muda si mrefu mpaka Trump anamkumbusha. Nadhani Biden has a memory issue
Trump ana maneno mengi katika kutackle maswari kuliko Biden
Unamsifia ila hamna kitu. Biden kafanya vizuri na alionekana kuwa alijiandaa na mdahalo. Trump anapigwa mawe mpaka anashindwa kuvumilia anaamua kuingilia muda wa mwenzake kuzungumza wakati yeye aliachiwa nafasi.
 
Unamsifia ila hamna kitu. Biden kafanya vizuri na alionekana kuwa alijiandaa na mdahalo. Trump anapigwa mawe mpaka anashindwa kuvumilia anaamua kuingilia muda wa mwenzake kuzungumza wakati yeye aliachiwa nafasi.
Trump yuko too energetic na smart alijua Wallace na Fox News ni hardcore liberals hawampendi ndio maana kila chance ya kupigwa point alidakia hata kama sio zamu yake na ku neutralize mapigo maana angekua katulia kama biden wangemvua nguo leo.
 
Trump yuko too energetic na smart alijua Wallace na CNN ni hardcore liberals hawampendi ndio maana kila chance ya kupigwa point alidakia hata kama sio zamu yake na ku neutralize mapigo maana angekua katulia kama biden wangemvua nguo leo
Sijajua CNN imetoka wapi maana moderator wa Debate alikuwa Wallace from Fox News. Fox News na wanazi wakubwa wa Trump. All in all Trump alipaniki . Biden alikuwa so presidential in his talking.
 
Sijajua CNN imetoka wapi maana moderator wa Debate alikuwa Wallace from Fox News. Fox News na wanazi wakubwa wa Trump. All in all Trump alipaniki . Biden alikuwa so presidential in his talking.
Nimekosea mkuu it was supposed to mean Fox News.
 
Back
Top Bottom