Mambo 6 yasiyoweza kusameheka kirahisi katika ndoa/mahusiano

Sikujua kama bado Watanzania tunaamini uchawi!

Mlienda kwa mganga na nyie ndio akafanikiwa "kunyofoka" kwa yule dada au?

Ni stori ndefu Gaijin...bt kifupi tu na sie tulimpandia hukohuko, otherwise bro alishapotea, na kuna picha majirani walimpiga jamaa katoka ofisini dem kamwambia aoshe vyombo, bro kachuchumaa anaosha vyombo, inasikitisha sana
 
Heheh samahani najua hili la uchungu kwako lakini limenichesha sana!

Na kilichonichekesha ni ile watu kuona mtu anaosha vyombo ni kupotea......

Kweli binaadamu tunafoutiana.

Ila pia hongereni kwa kumuokoa bro wenu
 
SMU

Hivi mwanadani wako anajua mapato yako yote na vipi yanatumika

* Nikijitazama bill yangu ya viatu asiione kamwe maana anaweza zimia.
Anajua mapato yote(sina vyanzo vingi kivile!). Na matumizi yote yanayozidi tzs 100,000 (mara nyingi namshirikisha kwa taarifa au uamuzi) lakini hata kama akitaka kujua mapato na matumizi yote mpaka shilingi moja bado anayo acess na record zangu (generally narecord kila kinachoingia na kutoka kila siku!)
 
Hongera kwa kuwa muwazi na kuwa organized vya kutosha kuweza kuweka record ya matumizi.

Ni njia moja nzuri sana ya kuhakikisha huendi nje ya uwezo wako, na rahisi kupaona pa kubana matumizi ikihitajika kufanya hivyo
 
Heheh samahani najua hili la uchungu kwako lakini limenichesha sana!

Na kilichonichekesha ni ile watu kuona mtu anaosha vyombo ni kupotea......

Kweli binaadamu tunafoutiana.

Ila pia hongereni kwa kumuokoa bro wenu

Anyway inachekesha bt its so painful to ma bro...na ukiacha matusi anayoyarusha kwa yule dada mwingine, na mengineyo, ndo nahoji kwanini wadada wanakuwa na roho za kishetani hivi, mbona wanaume wapo wengi tu. Kwani we Gaijin huamini uchawi?
 
Hongera kwa kuwa muwazi na kuwa organized vya kutosha kuweza kuweka record ya matumizi.

Ni njia moja nzuri sana ya kuhakikisha huendi nje ya uwezo wako, na rahisi kupaona pa kubana matumizi ikihitajika kufanya hivyo
Asante...nashukuru Mungu nimeweza kujidiscipline vizuri...mwazo nilikuwa najaribu kufanya mwisho wa mwezi lakini nikawa najikuta vitu vingi nakuwa nimesahau na hivyo kushindwa kubalance mapato, matumizi na pesa iliyopo mkononi/benki...lakini baade nikajilazimisha kufanya kila siku, na nimefanikiwa kufanya hivyo kwa miaka kadhaa sasa. Utaratibu huu umenisaidia sana kujua ni sehemu gani pesa inatumika zaidi na kufanya marekebisho kwa kadri ninavyoweza.
 
Anyway inachekesha bt its so painful to ma bro...na ukiacha matusi anayoyarusha kwa yule dada mwingine, na mengineyo, ndo nahoji kwanini wadada wanakuwa na roho za kishetani hivi, mbona wanaume wapo wengi tu. Kwani we Gaijin huamini uchawi?

Mimi uchawi naona kama ni kitu kilichopo dunia nyengine sio hii hii nnayoishi mie.

Siwezi kumuona mtu anafanya "mambo ya ajabu" au "kuumwa" nikashuku kuwa ni uchawi.
 
1.Domestic violance
(hii siwezi huvumilia hata chembe,tokea nione mtu kapewa kilema hadi leo nimeapa hii kitu siiwezi)
2.Cheating/Mtoto wa nje
(hivi kwangu ni kitu kimoja,itategemea mtoto alimpata kabla au baada but havyo havivumiliki
3. Accounts za siri na mipango ya siri(itategemea na agreementa tulizopeana mwanzo,otherwise i wont trust him)
4.Ulevi na madawa (hii nitajitahidi kumpeleka therapy,hapa sitomtupa)
5.Inlawas,hawa nita deal nao tu
Labda wawe extreme na yeye awe ame base sana kwao
 
Hususan ikiwa hukujua kuwa upo kwenye mtihani na mtoa mtihani anakuchanganya hujui mambo matano au sita!

Kwa kweli imebidi nicheke na kwenda kulipitia swali; mwanzoni nilitaka kuweka mambo matano kumbe nikajikuta nimefikisha sita. Nikagundua wakati mwingine hata walimu wanafelisha wanafunzi!
 
Jaribu kuangalia mambo haya sita na uyapange kwa uzito wake wa kusameheka - yaani namba 1 likiwa ni zito kabisa kusameheka hadi 6 jepesi zaidi kusameheka. Yaani lile la kwa 1 kimsingi linaweza kabisa kuvunja uhusiano (definitely) na lile la 6 laweza kushtua au kutikisa kidogo (most probably) lakini linaweza likapita katika historia na watu wakadumu. Ukipenda unaweza ukaelezea kwanini namba zako zivyo hivyo vilivyo.

Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)

Unaweza kupanga yote 6 au kupanga makubwa matatu (your top three). Siji kama wanaume na wanawake tunashindwa kusamehe vitu vile vile au la.

MMM
1. Ulevi/matumizi ya madawa ya kulevya,ni kero na uwezekano wa kuwa responsible unapungua. Ni tatizo sana kwangu, labda sababu situmii kilevi cha aina yeyote, hasameheki kabisa.

2. Account za siri(mipango isiomshirikisha mwenza), Kamwe halisameheki sababu atakuwa anaplan kujenga palestina wakati mie najenga Israel, tutakuwa hatuna common oblectives kimaisha.

3. Kimada/affair za nje, hili litategema msimamo wake ni nini juu yangu. Kama ananitambua na kuniheshimu as a wife na kimada ananiheshimu, I can take it na kuendelea kuishi naye. So its 50/50 kuetegemea na tabia ya mwenza wangu

4. Kuingiliwa na wakwe, halisumbui hata kidogo, piga marufuku kija kwangu ni kuwatembelea huko waliko wao na kuwasaidia wakiwa huko huko. No problem at all.

5. Mtoto wa nje, sioni tatizo liko wapi, ni kumchukua haraka akiwa na mwaka mmoja namchanganya na wakwangu na kuwalea kwa mapenzi yote. Inasaidia kwa mwenza kutulia kimawazo akiona watoto wake wote pamoja na kuua connection na mzazi mwenzie. Kuiba upendo wa mtoto wa nje kutoka kwa mama yake mzazi kuja kwangu. Kufanya watoto wote wajione kitu kimoja sabaabu hata ukimkataa mtoto wa nje wa mumeo hauwezi badili ukweli ni wake na ataendelea kuwa wake na ana haki zake. Hata wazazi tukifa watoto watakuwa kitu kimoja na wasaidiana wao kwa wao. Mara nyingi vitu hivi huleta shida sana kwenye mirathi wanaishia kuuza mali zote kwa kutoelewana au kuona wengine ni intruders.
 
6. Violence, kama anawapiga wa mtaani mie hayanihusu kabisa, ila kwetu akina tata mwanamke kupigwa na mpenzi ni part ya mapenzi jamani.
 
6. Violence, kama anawapiga wa mtaani mie hayanihusu kabisa, ila kwetu akina tata mwanamke kupigwa na mpenzi ni part ya mapenzi jamani.

Hapo sikubaliani napo hata kidogo.

Akinipiga namfikisha kwenye vyombo vya sheria kisha afunge virago sitaki hata kumuona tena.
 
1.Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
Hapa wala hamna majadiliano...leo unaletewa mtoto kesho ngoma.Sijui nayo atasubiri mpa ikule ndo akwambie umgonjwa!!?
2.Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
Nampakia vitu vyake ...namsindikiza mpaka nje alafu namtakia maisha mema huko kwa kimada.
3.Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
Kofi moja la shavu when things are heated is forgiveable...kipigo cha kuniachia makovu/kunipa manundu HAPANA.
4.Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
Kama hasaidiki kwenye swala zima la kuacha basi inabidi tuagane maana itakua kero kwangu.Besides...sitaki mtoto wa mtu anifie mikononi kwa madawa ya kulevya.
5.Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
Well kama tulikubaliana kushirikishana kila kitu hapo ni imani yangu kwake itashuka maana sitojua kama kuna mengine ananificha.I mean sihitaji kujua ana ngapi maana sio zangu ni zake ila nikijua tu kwamba ana acc NBC...CRDB na Benki ya Posta inatosha.Kama hatukukubaliana hivyo haitonisumbua.
6.Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
Hili dogo sana na linatatulika kwahiyo halihitaji kusamehe wala kutokusamehe.

1. Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
(hili halina mjadala-Halikubaliki)

2. Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
(hili nalo vile vile-Halikubaliki)

3. Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
(Hili atafikishwa na polisi pia, sheria za nchi zichukue mkondo wake)

4. Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
(Hili I will try kumsaidia kidogo, ikishindikana basi)

5. Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
(Hii ni non-factor as far as si extreme. Wazazi wake wanampenda na nitawachukulia tu kama watu wazima, na ku deal nao)

6. Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
(Hili halinikeri hata kidogo. Namshauri atafute wakili wa kumtunzia will yake tu, akifa mali yende kwa nani)

red and bolded: Hiyo ndo siwezi kusamehe kabisa kabisaaaaaaaa! Hayo mengine mbona yanatokeaga tu ila kuniletea katoto ili hali na mimi nna uwezo, mweeee, lazima uhame.
 
1.Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
Hapa wala hamna majadiliano...leo unaletewa mtoto kesho ngoma.Sijui nayo atasubiri mpa ikule ndo akwambie umgonjwa!!?
2.Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
Nampakia vitu vyake ...namsindikiza mpaka nje alafu namtakia maisha mema huko kwa kimada.
3.Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
Kofi moja la shavu when things are heated is forgiveable...kipigo cha kuniachia makovu/kunipa manundu HAPANA.
4.Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
Kama hasaidiki kwenye swala zima la kuacha basi inabidi tuagane maana itakua kero kwangu.Besides...sitaki mtoto wa mtu anifie mikononi kwa madawa ya kulevya.
5.Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
Well kama tulikubaliana kushirikishana kila kitu hapo ni imani yangu kwake itashuka maana sitojua kama kuna mengine ananificha.I mean sihitaji kujua ana ngapi maana sio zangu ni zake ila nikijua tu kwamba ana acc NBC...CRDB na Benki ya Posta inatosha.Kama hatukukubaliana hivyo haitonisumbua.
6.Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
Hili dogo sana na linatatulika kwahiyo halihitaji kusamehe wala kutokusamehe.

Upele mwingi mwilini mkunaji kaota kucha ndefu, kazi ipooooo!
 
Mtoto wa nje kwa nini halisameheki wakati tunajua wenza wetu wanacheat? Sifurahii ila sioni kama halisameheki. Je mwenza akikuletea UKIMWI inakuaje whan you are sure na uaminifu wako?

Kweli nifafanulieni mie hapa ni bichwamaji kwenye hili.
Mi naona faida tu, napata wa kunisaidia na kazi ndani au labda sababu nililelewa na step sistaz wawili ana mzazi wangu haku-complicate kabisa kuwakubali, alituchanganya na kutulea na sasa wote ni kitu kimoja.
 
Inaumiza sana kuona neno 'mtoto wa nje' linakipaumbele sana katika sababu sita za MMJ
Inaumiza kwa sababu mimi ni 'mtoto wa nje'
Je 'mtoto wa nje' sio mtoto kama walivyo watoto wengine?
Je 'mtoto wa nje' hana haki ya kuwafahamu watoto nusu yake wa baba yake?
Je 'mtoto wa nje' ndiye aliyepelekea baba/mama kufanya aliyofanya
Je haiwezekani kabisa ni sababu ya 'udhaifu' wako wewe ndio ikapelekea baba/mama kuwa na 'mtoto wa nje'
Kwa hali ilivyo siku hizi, magonjwa ya kifo, mpaka kuwe na 'mtoto wa nje' lazima kuwe na sababu ya msingi ya kujadiliwa katika familia
Wazo langu, Suala la affair nje litenganishwe kabisa na 'cheating (hiki kinaweza kuwa kitendo cha haraka sana au hata oral au dhamira tu kama busu ndani mdomoni kabla hata ya tendo), lakini inapofikia kuzaliwa kwa sisi kina 'karume-kenge' mtupe heshima yetu hivyo basi 'mtoto wa nje' iongezwe kama namba 7.
 
Back
Top Bottom