Mambo 6 yasiyoweza kusameheka kirahisi katika ndoa/mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo 6 yasiyoweza kusameheka kirahisi katika ndoa/mahusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 2, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Jaribu kuangalia mambo haya sita na uyapange kwa uzito wake wa kusameheka - yaani namba 1 likiwa ni zito kabisa kusameheka hadi 6 jepesi zaidi kusameheka. Yaani lile la kwa 1 kimsingi linaweza kabisa kuvunja uhusiano (definitely) na lile la 6 laweza kushtua au kutikisa kidogo (most probably) lakini linaweza likapita katika historia na watu wakadumu. Ukipenda unaweza ukaelezea kwanini namba zako zivyo hivyo vilivyo.


  Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
  Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
  Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
  Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
  Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
  Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)

  Unaweza kupanga yote 6 au kupanga makubwa matatu (your top three). Siji kama wanaume na wanawake tunashindwa kusamehe vitu vile vile au la.

  MMM
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  1. Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
  (hili halina mjadala-Halikubaliki)

  2. Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
  (hili nalo vile vile-Halikubaliki)

  3. Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
  (Hili atafikishwa na polisi pia, sheria za nchi zichukue mkondo wake)

  4. Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
  (Hili I will try kumsaidia kidogo, ikishindikana basi)

  5. Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
  (Hii ni non-factor as far as si extreme. Wazazi wake wanampenda na nitawachukulia tu kama watu wazima, na ku deal nao)

  6. Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
  (Hili halinikeri hata kidogo. Namshauri atafute wakili wa kumtunzia will yake tu, akifa mali yende kwa nani)
   
 3. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hayasameheki Africa au Marekani na Ulaya? Mbona mtaani kwetu hayo ni mambo yanayotokea karibu kila wiki na maisha yanaendelea tu kama kawa
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  leo hii usipoyasamehe haya utaishi na nani???
   
 5. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  1. Mtoto wa nje 2. Violence 3. Cheating 4. Account za siri 5. Ulevi 6. Wakwe
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Una akili kama mchwa.
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hivi tayari tunatakiwa sote turidhike mwanamme kuwa na mtoto wa nje, affair, na awe violent?

  Kweli Mungu humpa mtu kile anachokitarajia
   
 8. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,918
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Mtoto wa nje mama ake anamsubmbua sana bro. infact alizaa na wadada 2, ila huyo mwingine alikuwa mchawi na akamfanya bro bushoke..tulivyotrace na kugundua, bro akafanikiwa kunyofoka kwa yule mdada...na akahama mkoa, akawa anakaa na yule mwingine. Kazi sasa ipo kwa yule dada mchawi... sidhani kama bro au sisi wandugu tutamsamehe huyu dada...Hivi wadada mbona mnakuwa na roho za kishetani hivi??
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,980
  Trophy Points: 280
  vipi ukigundua mumeo ana uhusiano na dume jenzake? Tena mumeo ndio kafanywa mwanamke wa hilo lidume?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Sikujua kama bado Watanzania tunaamini uchawi!

  Mlienda kwa mganga na nyie ndio akafanikiwa "kunyofoka" kwa yule dada au?
   
 11. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  yote kwangu yanasameheka inategemea ......................!
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Yote hayo na mengineyo yanasemeheka na maisha yanaendelea ... hata maadiko matakatifu yanaelekeza hivyo... assuming pia kama ndoa yenyewe ina utakatifu..

  God Bless

  BE ( Kabashana - Parish)
   
 13. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mi naweza samehe yote inategemea tu nimejulishwa wakati gani na je nimegundua mwenyewe au amenitubu kwangu mwenyewe na sababu za yeye kufanya alichofanya ila kitu sitakaa nisamehe ni dharua kwangu
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Mnajua watu wengine mnafeli mitihani kirahisi kweli..
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika kwa nini umechagua hayo sita tu (mimi nadhani kuna mengine pia). Hata hivyo katika hayo sita nikianzia gumu zaidi, yanakaa hivi:
  1. Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating) na Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine - haya kwangu mimi yana uzito sawa na adhabu yake/uamuzi ni moja tu.
  2. Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva - siwezi kulala na mlevi kitanda kimoja
  3. Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence) - Hili nalo ni zito kweli, linakuwa namba tatu kama linatokea mara moja, kama linatokea mara kwa mara, linabeba uzito sawa na hayo ya namba moja
  4. Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts - Jepesi kama pesa inayoingia huko sio ile ninayoitoa kwa ajili ya matumizi ya wote hapo nyumbani
  5. Kuingiliwa na wakwe(in-laws intrusion)/wazazi - Hili linakuwa jepesi kama tu ni wakwe wenyewe ndio wanaingilia, lakini sio mmoja wetu kuwaalika kuingilia (hili litanipa tabu na linabeba uzito wa namba mbili)
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hususan ikiwa hukujua kuwa upo kwenye mtihani na mtoa mtihani anakuchanganya hujui mambo matano au sita!
   
 17. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Ndo hapo sasa? You better live alone...hii dunia yetu ambayo kila kukicha kuna jipya ipo kazi kumpata mtu asiyekuwa na tatizo hata moja katika hayo.
   
 18. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kama huu ulioutoa hapa, nina hakika hata wewe mwalimu wangu unaweza kukutoa jasho kuupasi
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Maelekezo ya huu mtihani yanachanganya pia.......ulitaka 'watahiniwa' tuyapange hayo mambo 6 (5?) kulingana na uzito wake ama tuyape alama 1 mpaka 5 kulingana na zito wake?
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  SMU

  Hivi mwanadani wako anajua mapato yako yote na vipi yanatumika


  * Nikijitazama bill yangu ya viatu asiione kamwe maana anaweza zimia.
   
Loading...