MAMBO 6 MUHIMU AMBAYO DAKTARI HAWEZI KUKUPA USHAURI NAYO NI HAYA HAPa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
1380036_552978928120747_261530716_n.jpg


Mambo 6 muhimu kwa binadamu huwezi kupata ushauri hu kwa Ma-Daktari ila utapata hapa Jamii Forums:

1) Binadamu anatakiwa apate mwanga wa jua unasaidia kupata Vitamin D muhimu kwa Binadamu kwa afya yako.

2) Kunywa Maji kila siku japo Mara 8 kwa siku ni nzuri kwa ajli ya afya yako na kuondosha maradhi mwilini Maji ni kinga ya kila maradhi.

3) Kupata Usingizi wa Usiku usingizi wa masaa 8 kwa usiku ni bora kwa afya yako.

4) Kupata hewa safi kila binadamu anatakiwa apate hewa safi kwa ajili ya afya yako.

5) Kufanya Mazoezi ya kukimbia au kutembea japo kwa siku kutembea kwa kilomita 5 ni bora kwa afya yako ya mwilini.

6) Kula chakula kwa wakati wake chakula chenye kuleta afya mwilini.

Huu Ushauri huwezi patakokote kule zaidi ya hapa Ukifuata huu ushauri wangu kamwe huwezi kupatwa na maradhi asanteni.
 
Ni mazoezi gani mama mjamzito anapaswa kuyafanya? Maana mim hata nikitembea kdg nackia maumivu chini ya tumbo na nachoka sana
 
5) Kufanya Mazoezi ya kukimbia au kutembea japo kwa siku kutembea kwa kilomita 5 ni bora kwa afya yako ya mwilini.
  • Je ni mazoezi gani mbadala wa mazoezi ya kukimbia na kutembea? - ambayo nawezafanya nyumbani muda wa asubuhi kabla ya kwenda kibaruani na jioni kabla ya kujipumzisha. Mzizimkavu , Fadhili Paulo
 
  • Je ni mazoezi gani mbadala wa mazoezi ya kukimbia na kutembea? - ambayo nawezafanya nyumbani muda wa asubuhi kabla ya kwenda kibaruani na jioni kabla ya kujipumzisha. Mzizimkavu , Fadhili Paulo
Piga Push up kwa uwezo wako anzia kupiga 10 kwa siku ya kwanza kila siku ongeza kidogo kidogo mpaka utakapofikia uwezo wako. Angalia picha hapo chini


Marines_do_pushups.jpg
 
Ni mazoezi gani mama mjamzito anapaswa kuyafanya? Maana mim hata nikitembea kdg nackia maumivu chini ya tumbo na nachoka sana

MziziMkavu mie na tumbo hili la miezi saba naweza kufanya mazoezi kweli??


MAZOEZI YA KUFANYA UKIWA NA UJAUZITO




pregnancymontage.jpg



Kufanya mazoezi wakati wa ujauzito kuna umuhimu mkubwa kwa afya ya mama mjamzito mwenyewe na mtoto wake ambaye bado hajazaliwa. Wanawake wengi wanatambua umuhimu wa

kula lishe bora, kuhudhuria kliniki, kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe wakati wakiwa na mimba. Lakini si wanawake wengi wanaoelewa umuhimu wa kutumia muda wao kufanya mazoezi

wakati wa ujauzito. Mazoezi yana umuhimu mkubwa kiafya wakati wa ujauzito kama ilivyo kabla ya ujauzito. Kufanya mazoezi wakati unapobeba mimba kunaleta faida kubwa wakati wa kujifungua.

Wakati wa ujauzito ni muhimu kudhibiti ongezeko la uzito wa mama. Kwa kujishughulisha mama mjamzito na kuwa na harakati humsaidia awe na afya bora na kumsaidia aweze kupitisha kipindi

cha uchungu na kujifungua kwa urahisi zaidi. Zaidi ya kumsaidia mama asiongeze uzito mkubwa wakati wa mimba, kufanya mazoezi humsaidia mama pia kurejea katika uzito wake wa kawaida kwa

urahisi baada ya kujifungua kwa kawaida au kwa uparesheni. Kwa ujumla mama mjamzito kama ambayo anavyoshauri kula chakula bora na kuwa na afya nzuri wakati wa ujauzito, hivyo hivyo

hushauriwa pia kuzingatia suala zima la kufanya mazoezi na kuchunga mwili wake usiongeze uzito mkubwa. Pia kufanya mazoezi huufanya mwili utoe mada ya endorphins, ambayo husaidia

kumfanya mama asipate matatizo ya kifikra na msongamano wa mawazo (emotional stress na depression).


Zifuatazo ni faida anazozipata mama mjamzito iwapo atafanya mazoezi:


1. Mazoezi hupunguza maumivu ya kichwa, kukosa choo na kuvimba mwili.



2. Mazoezi huongeza nguvu na kuupa mwili stamina.



3. Mazoezi hukufanya ujisikie vizuri na kukufanya uwe katika hali ya furaha.



4. Mazoezi hupunguza maumivu ya mgongo na huimarisha mifupa ya mgongo, makalio na mapaja na kuifanya iwe na uwezo wa kuvumulia vyema uzito wa mimba.


5. Mazoezi husaidia huongeza mtiririko wa damu na hewa katika ngozi na kuifanya ngozi yako ionekane nzuri.


6. Mazoezi hutayarisha mwili wako uwe tayari kwa ajili ya kuhisi uchungu kwa muda mfupi na kujifungua kwa urahisi.


7. Mazoezi hufanya mwili wako urudi upesi katika muonekano wake wa kawaida baada ya kujifungua.


8. Mazoezi humsaidia mama mjamzito apate usingizi kwa wepesi na kulala vyema.


Hata hivyo mama majamzito anashauriwa kabla ya kuanza kufanya mazoezi apate ushauri wa daktari na kuhakikisha kuwa hana matatizo ambayo kwa kufanya mazoezi pengine

yakahatarisha mimba yake. Kwa wale waliokuwa wakifanya mazoezi kabla ya kubeba mimba wanashauriwa kuendelea na mazoezi yao lakini kwa kuwa waangalifu na kwa

kiwango kidogo. Lakini kwa wale ambao walikuwa hawafanyi mazoezi hawaruhusiwi kufanya aina zote za mazoezi wakati wa ujauzito. Mazoezi kama vile kuogelea (kwa wale

anaojua kuogelea), kutembea na yoga ni miongoni mwa mazoezi yanayoshauriwa wakati wa ujauzito. La muhimu ni mama mjamzito kutokaa tu na kujiepusha na uvivu na pengine

kwa kufanya shughuli zake tu za kawaida ambazo mama huwa anazifanya nyumbani kila siku ikawa inatosha kuwa mazoezi yake na akaongeza kwa kutembea kidogo ( walking)

kila jioni. Kutembea ni mazoezi salama na rahisi kwa kila mama mjamzito na yanayojulikana na kila mtu na kuweza kufanywa mahala popote. Ni bora kama unaweza

fanya mazoezi na mwenza wako, rafiki au hata ndugu na jamaa yako ili uweze kufurahia zaidi mazoezi hayo. La muhimu ni kufuata maelekezo ya daktari kwani si kila mama

mjamzito anaruhusiwa kufanya mazoezi wakati wa ujauzito kutokana na sababu tofauti. Baadhi ya mazoezi ambayo yana madhara kwa afya ya mama mjamzito na kwa mtoto

hayaruhusiwi kabisa kufanywa wakati wa ujauzito. Mazoezi hayo ni kama vile mazoezi ya aerobic, ski, kupanda mawe, kupanda farasi na mengineyo kama hayo. Iwapo unaishi

katika miji iliyoendelea basi unaweza kupata kwa urahisi vituo maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi mama wajawazito, na katika vituo hivyo kwa kawaida wakina mama

wajawazito hukusanyika na kufanya mazoezi kwa pamoja. Lakini kama uko katika miji ambayo vituo hivyo hakuna usife moyo, na jitahidi kufanya mazoezi hayo peke yako huku ukishirikiana na familia yako.


 
5. Kufanya Mazoezi ya kukimbia au kutembea japo kwa siku kutembea kwa kilomita 5 ni bora kwa afya yako ya mwilini.

...kwa hili nina wapongeza sana SUMATRA kwa baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar tumejikuta tunafanya mazoezi bila kutaka, "baada ya kufunga kituo cha daladala cha posta ya zamani...!

"well done SUMATRA"
 
  • Je ni mazoezi gani mbadala wa mazoezi ya kukimbia na kutembea? - ambayo nawezafanya nyumbani muda wa asubuhi kabla ya kwenda kibaruani na jioni kabla ya kujipumzisha. Mzizimkavu , Fadhili Paulo

Nunua kamba ya bukta na tshit na raba!! Alafu ukimaliza kanunue KAMBA!! Tumia kama dakika 20 au nusu saa kwa siku(asubuhi au jion) kuruka kamba Hii itakusaidia sana mkuu!!
 
Back
Top Bottom