Mambo 6 kuhusu Majeruhi ajali ya Wanafunzi Arusha waliofatwa na Ndege kupelekwa Marekani

REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,925
14,895
Screen-Shot-2017-05-13-at-11.41.41-PM.png

Ajali ya basi dogo la Wanafunzi Karatu Arusha iliua 32 weekend iliyopita na kuacha Majeruhi watatu ambao wamekua wakitibiwa kwenye Hospitali ya mkoa wa Arusha, Mount Meru.

Mbunge wa Singida kaskazini Lazaro Nyalandu amekua mstari wa mbele kuhakikisha watoto hawa wamesaidiwa kimatibabu pamoja na kisaikolojia ambapo juzi May 11 aliongea na AyoTVna millardayo.com Arusha.

1. ‘Ninapenda kutangaza kwa furaha kubwa sana kwamba tumefanikiwa kupata Ndege kubwa inayoweza kutumika kama ‘AMBULANCE‘ angani na inaondoka North Carolina Marekani kuja moja kwa moja Kilimanjaro Tanzania kuwachukua hawa majeruhi’ – Nyalandu

2. Baada ya taarifa hizo, Ndege hiyo yaSamaritan Purse DC 8 N782SP imewasili Kilimanjaro Tanzania leo May 13 2017 ikiwa na Marubani wanne na Wahudumu wake 7 tayari kuwabeba Majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwenye matibabu.

Screen-Shot-2017-05-13-at-10.45.14-PM.png

Mmoja wa Marubani wa Ndege hiyo akiwa na Mbunge Lazaro Nyalandu kwenye uwanja wa Ndege KIA.

Rubani wa Ndege hiyo amewaambia Waandishi kwenye uwanja wa ndege Kilimanjaro (KIA) kwamba wataondoka kesho na watasimama Cape Verdekuweka mafuta na kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia kesho yake usiku.

Screen-Shot-2017-05-13-at-10.54.08-PM.png

Tayari Wazazi wa watoto hao watatu wameshapata VISA za kuingia Marekani pamoja na watoto wao na wako tayari kwa safari.

3. Ndege hii imetolewa na shirika laSAMARITAN’S PURSE (mfuko wa Msamaria) linalosimamiwa na mtoto wa Mwinjilisti mkubwa wa Marekani Franklin Graham, familia yao baada ya kupelekewa habari za kilichotokea kwenye ajali ya Karatu walikubali kuituma ndege hiyo kutoka Marekani kuja kuwachukua Majeruhi Tanzania.

Screen-Shot-2017-05-13-at-11.31.51-PM.png

Mwinjilisti Franklin Graham

4. Kwenye Ndege hiyo kuelekea Marekani itawabeba Mama wa watoto hao watatu, itawabeba pia Nesi mmoja na Daktari mmoja wa Kitanzania ambao wataendelea kuwahudumia watoto hao ndani ya ndege hiyo yenye uwezo wa kutoa huduma kama Ambulance pia.

5. Ndege hiyo ikishatua North Carolina,SAMARITAN’S PURSE wameandaa Ndege nyingine ambayo pia inaweza kufanya kazi kama AMBULANCE angani iitwayo AIR AMBULANCE na kuwachukua hadi jimbo la Iowa ambako Hospitali ya Mercy imekubali kuwatibu Wagonjwa hawa bure kwa muda wote watakaohitaji matibabu.

Screen-Shot-2017-05-13-at-11.38.20-PM.png

6. ‘Tukiwa Marekani tutakua na haki ya kuangalia kinachoendelea ambapo Watanzania na marafiki wa Tanzania wataopenda kuchangia kwa M-PESA na njia nyingine wataruhusiwa, tayari shule 3 za Arusha Braeburn Internation, St. Costantine na International School of Moshi zimejiunga kuandaa mfuko ambao utatumika kuwachangia’ – NYALANDU
 
Ndege kama hiyo inaitwaje na inauzwa sh Ngapi
 
kwani Bombardier isingeweza kuwasafirisha hawa watoto kuliko ndege hii ikawafuata kwa gharama kubwa, any way mungu akubariku mh nyalandu kwa
msaada wako. pia mungu awaponye haraka majeruhi hawa
 
Mkuu,
Kumbuka ajali ile viti vilingoka ndani ya basi hivyo majeruhi wengi wamevunjika sehemu mbalimbali na kupata mipasuko ya ndani ya mwili. Hivyo ndege maalumu ya ambulance itasaidia wafike huko bila kuongezewa maumivu au majeraha yanayoweza kupatikana wakikaa ktk ndege ya kawaida wakati wa safari ndefu inayohitaji mipango mingi inayozingatia mahitaji maalum ya abiria majeruhi.
 
Heri wamepewa msaada na wageni, ingekua n wa hapa nchini, ungekua siasa nahc ungepelekwa mpk bungeni, ndo mana wale vimbelembele wote kimya,
Mungu yu mwema
 
Back
Top Bottom