Mambo 6 Atakayoyafanya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Kwenye Ziara Yake Ya Siku 3 Mkoani Mwanza

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
MAMBO 6 ATAKAYOYAFANYA MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWENYE ZIARA YAKE YA SIKU 3 MKOANI MWANZA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan anaanza rasmi ziara ya siku 3 mkoani Mwanza kuanzia leo Jumapili Juni 13, 2021. Haya ndiyo mambo 6 atakayoyafanya.

1. Leo Jumapili Juni 13, 2021 atatembelea na kufungua kiwanda chenye mtambo wa uchenjuaji (kusafisha) wa dhahabu wa bilioni 13.2 katika eneo la Saba Saba, Ilemela.

2. Leo pia Juni 13, 2021 hiyohiyo atatembelea na kufungua Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kanda ya ziwa lenye thamani ya bilioni 42 katika Mtaa wa Bolewa, Nyamagana.

3. Kesho Jumatatu Juni 14, 2021 atatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye thamani ya bilioni 699.9 na baadae kuwasalimu wananchi wa eneo la Busisi.

4. Jumatatu hiyohiyo Juni 14, 2021 atazindua mradi wa maji ulioko wilaya ya Misungwi wa bilioni 13.2

5. Kesho pia Juni 14, 2021 hiyohiyo ataweka Jiwe la msingi kwenye mradi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka mpaka Mwanza katika eneo la Fella wenye thamani ya trilioni 3.

6. Juni 15 atahitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano mkubwa kuongea na vijana wa mkoa wa Mwanza kwa niaba ya vijana wote wa Tanzania katika uwanja wa mpira wa Nyamagana.
 
vizur kutawanya uchumi wetu sio kila kitu dar tuache kulaumu ukanda na uteam tutachelewa sn maendeleo
itasaidia kuongeza makusanyo mapato kwa serikali ikajenge mahospital na mashule
 
🙏🙏🙏
vizur kutawanya uchumi wetu sio kila kitu dar tuache kulaumu ukanda na uteam tutachelewa sn maendeleo
itasaidia kuongeza makusanyo mapato kwa serikali ikajenge mahospital na mashule
Ni jambo jema kabisa mkuu
 
Hii ni ZAWADI Kwa

Mjomba, Shangazi, Babu, Baba Mdogo, Baba, Mama, Binamu, Dada, Kaka, Shemeji, Rafiki, WiFi, kuelekea Serikali ya KAZI iendelee chagua mmoja uone KAZI!😁
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom