Mbali na kampeni zenye maneno matamu na ahadi kabambe kutoka vyama vya upinzani lakini Watanzania walio wengi hawaviamini vyama vya upinzani kwa sababu zifuatazo;
1. Wananchi wengi hawaviamini vyama vya upinzani kutokana na kutokukomaa lakini pia kukosekana kwa hazina ya viongozi walioiva kuongoza nchi.
Hivyo wananchi bado wana hofu na mashaka makubwa kuwapigia Kura vyama vya upinzani, wanachi wana hisi kuwapa nchi wapinzani ni sawa sawa na kumkabidhi bunduki mtoto mdogo.
2. Wananchi wengi hawaviamini vyama vya upinzani kutokana na baadhi ya vyama vya upinzani kuwa na "UBIA" na mataifa ya kibeberu, hivyo wananchi wana hofu juu ya usalama wa rasilimali zao, wanahisi ubia huo unalengo la kukaribisha unyonyaji wa rasilimali zetu. yaani inawezekana baadhi ya vyama vina malengo ya siri na washirika wa kibeberu.
3. Ukali wa matamshi yatolewayo na baadhi ya vyama vya upinzani, wananchi wengi wanawasiwai juu ya kauli kali zinazotolewa na vyama vya upinzani ambazo zinaashiria au kuchochea vurugu na kutisha amani ya wananchi, wananchi wengi wamezoea amani na utulivu.hawataki purukushani za vyama vya upinzani.
4. Utitiri wa wagombea wa kiti cha uraisi, tofauti na chaguzi zilizo pita mwaka huu 2020 kumekuwa na idadi kubwa ya wagombea kiti cha uraisi kwa vyama vya upinzani, ambapo kila chama kina nia ya kuing'oa CCM, sawa tunaweza kusema ndio kukomaa kwa demokrasia lakini unapo dhamiria kukiondoa chama kikubwa na kikongwe kama CCM chenye umri wa miaka 43 hamna budi kuunganisha nguvu kinyume chake ni sawa sawa na kutaka kuuangusha/kukata mbuyu kwa kutumia kiwembe, wananchi wengi wanaamini kuwa hakuna chama cha upinzani kitakacho simama peke yake na kikafanikiwa kuiangusha CCM.
5. Wanachi wengi wanaamini kuwa uhakika wa AMANI yao na UTULIVU wao unapatikana chini ya utawala wa CCM na sio vyama vya upinzani. uthibitisho wa hayo ni kutokana na uzoefu kuanzia TANU na kisha CCM . wananchi wengi wana tathimini na kubaini kuwa bado chama mbadala zaidi ya ccm hakijapatikana.
Zaidi ya miaka 68 nchi imetulia tuliii hivyo hakuna haja ya chama kingine. Ni kazi ngumu sana kuiangusha CCM sio mwaka huu tu wa 2020 bali hata miaka 50 ijayo bado itakuwa vigumu hadi pale patakapo patikana wapinzani imara na walio iva kuiongoza nchi.