Mambo 30 Yanayokuonesha Kuwa Sasa Umri Umeenda:

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,469
281
Mie simo..

1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi
2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani
3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe
4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini
5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala
6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa
7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club
8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei
9. Idadi ya t-shirt na jeans inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo
10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu Polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua
11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako
12. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi
13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu
14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwalisha makombo
15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana
16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala
17. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulimalima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura
18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh. ngapi?"
19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba
20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Guardian, Daily News, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani
21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati
22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"
23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati
24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa
25. Ukimwona rafiki yako ana ujauzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"
26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja
27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako
28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei, na mfumo mbovu wa utawala
29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi
30. Kwa wanawake utaanza kuona vijana wanakukimbia na kwa wanaume utaanza kuona vibinti vinakupapatikia sana.

Ukiona una robo ya sifa hizi 30 basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma.
 
Basi ntakuwa nshazeeka kitambo mie..manake i've scored 25 out of 30

AshaDii
wewe vipi? .. saa haijafika kumi kasarobo?
 
mmmh, hilo nalo neno, naogopa kuzisoma zote maana .......................................
 
Basi ntakuwa nshazeeka kitambo mie..manake i've scored 25 out of 30

AshaDii
wewe vipi? .. saa haijafika kumi kasarobo?

Mie 30/30! Lol... Tena inaongezeka nyingine... Unakuta kijana ambae ni mkubwa kabisa anauliza, Hivi Michael Jordan/ Tupac ama Mariah Carey ndio akina nani?

In the sense your favorite music stars kwa sasa nyimbo zao zinajulikana kama zilipendwa! :A S shade:

Mie ninataka kujua King'asti, TIMING, Asprin, Kaizer, FP , nyumba kubwa, Kongosho na wengine wana score ngapi hapa... Lol!
 
Last edited by a moderator:
Mie hayo yamenitokea more than 15 yrs back, unaweza imagine how kikongwe am I.

Umenichekesha sana dadaangu...
Ujue kuna wakati wanangu wanashangaa ninavyofuatilia utabiri wa hali ya hewa..mara nikija na magazei home ni sunday news na the guardian....kichekesho zaidi hata mpira siku hizi sijui unavyokwenda! Zamani gani Simba ashinde au afungwe nisijue???...

mimi hayo yote nilishayapitia long time....
lakini mbona naona kama muda haujanitupa sana? au najipa moyo?
 
Lol! Naona hapa bragging ya nani zaidi inaanza! You can be all that... Ila tambua inatakiwa unishikmoo mimi! :biggrin:
huu mjadala huwa hauishagi, i.e. hakuna anayekubali kushindwa, mkiongozwa na mimi........
kuna sehemu tuliishia kukubaliana either tushikamooniane wote, au hakuna kushikamooniana
 
Umenichekesha sana dadaangu...
Ujue kuna wakati wanangu wanashangaa ninavyofuatilia utabiri wa hali ya hewa..mara nikija na magazei home ni sunday news na the guardian....kichekesho zaidi hata mpira siku hizi sijui unavyokwenda! Zamani gani Simba ashinde au afungwe nisijue???...

Na uki embrace... Unajisikia raha saana.... Kuna raha yake utu uzima. Vijana wachache sana wanabahatika kufika age zetu. Ni kuomba tu Mungu kubahatika kuishi maisha kama ya akina Chinua Achebe. Unafariki pale ambapo inaonekana umemaliza kazi zako hapa ulimwenguni...
 
Dah...
umri kwangu uliyoyoma when I was 22 kumbe... Ambapo in addition to hizo 20 nilizoscore wakati huo, pia nilibadili kasumba ya kwenda makonset ya bongofleva nikawa naenda live bands za zilipendwa...
 
Hakuna kushikamoana bora

La sivyo, mtanishkamoo wote except Dark City

huu mjadala huwa hauishagi, i.e. hakuna anayekubali kushindwa, mkiongozwa na mimi........
kuna sehemu tuliishia kukubaliana either tushikamooniane wote, au hakuna kushikamooniana
 
Last edited by a moderator:
mimi hayo yote nilishayapitia long time... lakini mbona naona kama muda haujanitupa sana? au najipa moyo?

Nimeipenda hii... Kuna kitu huwa tunasahau. Muda hautupiti kabisa... Ila unaweza pitwa na baadhi ya matendo. So kama wewe ni teenager, unaishi ki teenager, ukiwa mtu mzima unaishi ki utu uzima. Kulalamika kuwa muda umekutupa hiyo hai apply kabisa! Lol

Ndio mana kwa wengine, the more unakuwa the more you feel good.

huu mjadala huwa hauishagi, i.e. hakuna anayekubali kushindwa, mkiongozwa na mimi........
kuna sehemu tuliishia kukubaliana either tushikamooniane wote, au hakuna kushikamooniana

ha ha ha! Hiyo si mbaya kwa kweli...
 
Denial FP, you are in denial

Mie nimeamua kukubaliana na hali

Nikicheka siku hizi pempeni ya macho mistari ya wrinkles inajaa, mwanzoni nilikuwa najitahidi sana kunywa maji ili isitokee. Mwishowe nimeamua ku-surrender

mimi hayo yote nilishayapitia long time....
lakini mbona naona kama muda haujanitupa sana? au najipa moyo?
 
Ha ha ha ha ha, ha ha ha, you wish.:-*

Usinione na utaahira humu, kuna kitu naficha

Kongosho... Unaweza kuwa mengi sana humu ndani! But hata ujitahidi namna ipi, 'Utahira' haupo kabisa! Kuna kufanya vitu kwa fun na kufanya vitu kama ulivyo. Sio kazi ndogo kuwepo siku zote hizi Jf hadi leo unachanganya wengi kama ni me ama ke... Lol!
 
Back
Top Bottom