Mambo 30 ya kuyafahamu Kabla Hujafikisha Miaka 30

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,655
1 • Unahitaji Pesa Ili Uishi Comfortable.

2 • Watu hawajali matatizo yako. Wanajali vile unavyoweza kuwasaidia wao watatue wakwao.

3 • Kujiajiri na kuanzisha stable business ni kazi ngumu kuliko kuajiriwa. Kama wewe ni mvivu bora uajiriwe tu.

4 • Mtu hata awe mzuri vipi lazima awe na mapungufu. Ukiishi naye ndani ya wiki moja utafugundua hili.

5 • Kila mtu anapenda aishi vizuri. Lakini wachache tu ndiyo wapo tayari ku-pay price ili wafikie stage yakuishi maisha mazuri.

6 • Si lazima uwahi kuoa au kuolewa. Ni vile jamii na familia inakuwekea pressure tu.

7 • Watanzania wengi hawana uelewa katika masuala ya sales. Muulize jirani yako toka mwaka umeanza ameuza bidhaa au huduma zenye thamani kiasi gani?

8 • Tunaishi mara moja tu. Ni vema ukaishi maisha unayoyapenda kweli.

9 • Hakikisha angalau mara moja kwa mwezi unaenda nje ya mji kuepuka kelele nyingi na mvurugano wa city life. Hii itakusaidia kutoingia katika mtego wa stress. Trust me on this.

10 • Si kila mwanamke anayekukubali haraka ni cheap. Pengine naye anahisia kali juu yako.

11 • Wanasiasa hawajali lolote kuhusu wewe. Wanajali status yao tu basi.

12 • Watu wapo tayari kumsikiliza tajiri mwizi na mla rushwa na kumpuuza kijana mwerevu anayeongea ukweli.

13 • Ukitaka kuwafurahisha watu ongelea mazuri yao ukiacha yote yanayowakera.

14 • Hakuna anayejali mafanikio yako zaidi yako mwenyewe.

15 • Sex ni moja ya njia yakuondoa msongo wa mawazo.

16 • Inachukua si chini ya wiki 4 kuunda habit mpya.

17 • Hauwezi kuwa na furaha muda wote. Jifunze kuishi katika balance. Balance is key in life.

18 • Maisha Si mashindano. Trust me hakuna anayeenda kushinda mwisho wa siku. Tupo hapa kwa muda tu.

19 • No matter what you do people will judge you. Don’t give a sh*t

20 • Maisha siyo pressure. Pressure ni jamii inayoku-force uishi kama wanavyotaka wao.

21 • Average millionaire anazaidi ya vyanzo 7 vya mapato. Je wewe una source ngapi za kipato?

22 • Jukumu la mwanaume ni kumlinda mwanamke atembee katika dunia akiwa huru.

23 • Wanawake wamekuwa mhimili imara kabisa katika ku-support familia Afrika na duniani kwa ujumla. Treat them with respect.

24 • Perfect life haiwezekani. Usipoteze muda kuwa sahihi kwa kila kitu.

25 • Umeshindwa kupiga hatua katika maisha yako kwasababu umepuuza kujifunza kupitia same mistakes uliyofanya mwaka jana.

26 • Usipofurahia kampani yako binafsi hakuna mtu atakayevutia na wewe.

27 • Hakikisha una-save pesa kwa ajili ya dharura. You will thank me later.

28 • Acha kusema uongo. Msema kweli Mpenzi wa Mungu.

29 • Vyakula vinavyotokana na wanyama vinakusababishia maradhi. Kula zaidi matunda ni bora zaidi kwa Afya yako.

30 • Kuishi bila malengo ni mzigo. Soon utaona maisha hayana maana.

Ongezea ya kwako...
 
35. Haijalishi umesoma chuo bora kiasi,gani na umepata GPA kubwa kiasi gani, kama hupigi hatua na umekwama katika ajira usiyoipenda, ,unaishi maisha usiyoyafurahia basi chuo chako bora ulichosoma hakina maana na GPA yako kubwa haikusaidii chochote!
 
Katika maisha furaha ndio kitu muhimu zaidi vilivyo bakia ni mbwembwe tu kila mtu anatunga lake vijana tuna peana presha sana
 
Ushauli mzuri ila kuchanganya na kiingereza cha hapa na pale ni kama haukuwa unamaanisha, kuzungumza jambo.

35.Kingine ni kwamba vyovyote utakavyofikiria, uhai wako au mtu mwingine una thamani sana kwa watu wengine kuliko wewe mwenyewe.,mfano umefikiria kujiua-embu tafakari kuhusu mama yako na baba yako au wadogo zako.
 
37.life has no formula ....tumeumbwa tusifanane na mtu yeyote yule kila mtu ananjia zake tafuta njia zako za kutatua changamoto zako mwenyewe tuache ushamba wakutafuta siri za mafanikio za watu ...trust me hutazijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom