Mambo 20 ya kumuambia mpenzi wako Kila siku

Pamoja na hayo yote uhakikishe unampa ulinzi muda wowote huyo mke wako.

Ulinzi wenyewe siyo kuwa kama baunsa bali uwe financially stable. Muda wote akihitaji pesa ipo. Hakikisha hajui stress ni kitu gani.
You are the real MVP. Your woman must be proud.
 
Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza kutumia maneno matamu. Na lazima ujue kuwa sio kila neno unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka, Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza.

Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. Watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza.

Sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unayempenda na unahitaji awe wako milele;
1. Macho yako ni mazuri, yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama.

2, Unanifanya niwe mwanaume bora, kwa hio nastahili mapenzi yako.

3. Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu.

4. Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua.

5. Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea, ghafla nakuwa mtu wa furaha.

6. Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani, lakini umenichagua mimi.

7. Hapana wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo.

8. Ninapokushika nahisi kulegea kwenye magoti.

9. Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako, ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu.

10. Siamini, maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi.

11. kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda, natamani niwe na wewe milele. yaani usife.

12. Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja.

13. Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda, nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia.

14. Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.

15. Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia, hapo hupotea kabisaaa.

16. Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi.

17. Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda.

18. Napata furaha nikiwa na wewe.

19. Napenda kutumia muda na wewe.

20. Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa.

Andaa future Acha ujinga
 
Mi sinaga huo muda wa kumsomea risala kiumbe niliyekutana naye ukubwani kama namtimizia mahitaji yake hizo mambo nitajichosha bure
 
Vijana chukueni madini, wazee tuendelee kujifukiza.....na tusiache barakoa.
Kabisa.....

Haya manejo ya wakati wa balehe

Wakongwe tukiambiwa "nakupenda" unawaza huyu "mbuzi" kaharibu wapi mpaka anakuja na mahaba haya!!!!

NB
mbuzi:- hiki ni kivumishi cha sifa wenye jinsia yao wasije kunishambulia buuureeeeee)
 
Sasa tushike lipi na tufanye yapi?

Maana wa pesa wanatuambia tutafute pesa usiku kucha wakati hata hatujui wala hatuna uhakika kama zimepotea

Akija wa dini nae anatuambia tukeshe tukiomba na kuswali

Mwalimu naye anatwambia tupige kitabu muda wote hakuna kupumzika

Wa afya nao watwambia tuzingatie mazoezi tumwage jasho kila siku kwa walau dk20

Wa milo nao ndo kabisa wanatuchanganya huyu anasema usikose papai kwenye mlo wako yule anasema tango huyu maziwa mwingine bamia yulekule ubuyu... yaani ilimradi tu

Bado tozo bado kodi bado tamthilia bado kazi bado...

Sasa wewe ndo kabisa unatuvuruga zaidi kutuambia kila siku hayo maneno (kwenye sentensi 20) tudumu nayo kuwaambia wachumba kila siku dah!
 
Tena ni kivumishi kunachosifia "ukunaji" haujakosea kabisa....upo sawa
 
Sasa tushike lipi na tufanye yapi?

Maana wa pesa wanatuambia tutafute pesa usiku kucha wakati hata hatujui wala hatuna uhakika kama zimepotea

Akija wa dini nae anatuambia tukeshe tukiomba na kuswali

Mwalimu naye anatwambia tupige kitabu muda wote hakuna kupumzika

Wa afya nao watwambia tuzingatie mazoezi tumwage jasho kila siku kwa walau dk20

Wa milo nao ndo kabisa wanatuchanganya huyu anasema usikose papai kwenye mlo wako yule anasema tango huyu maziwa mwingine bamia yulekule ubuyu... yaani ilimradi tu

Bado tozo bado kodi bado tamthilia bado kazi bado...

Sasa wewe ndo kabisa unatuvuruga zaidi kutuambia kila siku hayo maneno (kwenye sentensi 20) tudumu nayo kuwaambia wachumba kila siku dah!
Za kuambiwa changanya na zako.....!!!
 
Mpaka 20 Hakuna pesa,Anasubiria kipengere kinachotataja pesa hakuna...Ukikata simu tu Anapigiwa mwenzio.
 
Watu kumbe wameanza kupoteza muda tokea siku nyingi sana....

Ndio maana umasikini hauishi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom