Mambo 2 yanayotatanisha kwenye hoja za viongozi wote wa Chadema waliojiuzulu na yanayowaumbua

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
utata juu ya wote waliojiuzulu chadema
.

Mimi kwenye Elimu ya shule za secondary mpaka high school na kuendelea niliopt kusoma masoma ya arts ikiwepo Lugha nk. kwa mantiki hiyo, nikichukua tamko la M/kiti wa Temeke, nikilinganisha na M/kiti Feki wa matawi ya Chadema mwanza, halafu nikiMalizia na m/kiti wa mkoa Singida na wengineo akiwepo Chatanda kama wewe ni mtaalam wa Lugha utagundua mambo yafuatayo.

Mosi, Staili ya uandishi kuanzia kichwa cha habari fonti inayotumika, upangaji wa aya mfumo wa uwasilishaji hoja au kwa ujumla tunasema staili ya uandishi ni ya mtu moja tu. Swali ni kwa nini na mtu huyo ni nani?

Pili, Hoja au tuhuma zinazotolewa zinafanana na msisitizo wake pia unafanana sana kiasi kwamba mwandishi huyo siyo mzuri hata wa kubadilisha lugha ili afiche malengo yake. Je kwanini na nani???

Tatu, kuanzia press kubwa ya Dsm, uchomaji wa ofisi za Chadema Arusha, Tamko la Mwanza na Singida nyuma yake utawakuta UVCCM wakiratibu. swali ni kwa nini na kwa ufadhili na mwongozo wa nani??

Nne, leo nimepata mahali taarifa zisizo rasmi kuwa kuna fungu la Sh mil 5 na kuendelea za kuwapa viongozi wa chadema nchi nzima. Sasa sina hakika kama hawa waliotangaza uamuzi wa kujiuzulu wamefikiwa na mafungu ya ccm au ni dhamiri zao. Time will tell.

Kwa kuhitimisha, matamko haya kuandikwa na mtu moja na kusomwa na watu wengine, pengine kwa kulipwa fedha kama fununu zinavyodai, kufanana kwa hoja za wanaojiuzulu na uwepo wa uvccm nyuma ya mikakati hiyo, kunanifanya niamini kuwa huu ni mchezo wa intelijensia fulani feki ambayo kiukweli ni mchezo wa danganya toto.- hadanganyiki mtu hapa.

Akili za kuambiwa nikichanganya na zangu, napata jawabu kuwa huu ni mkakati wa ccm. Chadema tutuvuka haya majaribu ni madogo sana kwangu. Aluta continua.

Hii hoja ya mdau nayo ina mashiko ukiunganisha dots ya malalamiko ya Mwigulu Fb.

Haya matamko anayaandika mwigulu na alikuwa anayasambaza kwa id yake ya taswira hapa jamii forum lakini hili la singida ametumia id mpya lakini rudi kwenye mabandiko yake ya nyuma aliyokuwa akijiripoti wakati akiwa marekani na moja aliyorusha akimlisha mtoto utaona aya na fonts zinafanana.
 
Mkuu Awenda, hacheni kuwaongelea tena hawa watu, sibili tu siku 14 zifike tuwaondoe kabisa katika vichwa vyetu. Mnapoendelea kuwajadili wanaona kama wamewaumiza. Hacha waendelee na propaganda zao na CCM yao. Their days in Chadema are numbered. Hivi hazijafika bado!
 
Huhitaji kutumia akili sana kujua yanayoendelea nyuma yake kuna Mafisadi wa CCM hasa Mwigulu nchemba ndiyo mratibu mkuu wa hii kitu.
 
Japo tumechelewa tangu tulipowagundua 2010, sasa lazima waondoke.
 
mkuu @Mikael P. Aweda kwanza napenda kukueleza kuwa yawezekana kuwa wanatumiwa na CCM, lakini umeshawahi kukaa na kufikiri kuwa kwanini mtu kama Mwenyekiti wa mkoa Singida, ambaye amejitolea kwa hali na mali ili CDM isonge mbele, Nyumba yake, sanduku la posta, na hata resource nyingine, leo hii awe ametumiwa na CCM? Kuna push factors gani ambazo zimepelekea hilo.
Tafakari! Chukua hatua
 
mkuu, tuwe wakweli mie naamini akina zzk wana makosa ila hata uongozi wetu uliobaki una makosa pia. kimsingi tuhuma hizi hazijaanza leo, zimekuwepo toka enzi za akina marehemu chacha wangwe, kafulila, Juliana shonza nk tukubali ukweli, tuhuma nyingi za msingi zimekuwa zikijirudia sasa sina hakika kama kujirudia huku ni bahati mbaya au vp!! nikuulize swali, (kuhusu ubaguzi) mh lema alilipuka hapa jf bila kupitia vikao na taratibu za ndani ya chama kama katiba yetu ya mwaka 2006 ibara ya 10 inavyoelekeza na hakufanywa chochote na uongozi - je hii ilikuwa ni kupitiwa kwa kamati kuu?! kwa kweli baadhi yetu tunapenda mabadiliko, lakini kuwe na HAKI na USAWA miongoni mwa wanachama wote.....tunataka demokrasia halisi ndani ya chama ili kujitofautisha na maccm.
 
Mnamkweza bure Mwigulu. Hana uwezo huo.Mnajihelewesha kuyadadavua mambo na kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo ndani ya CHADEMA. Ni kama mtu mshirikina: Akiumwa kihwa anafikiria mchawi ni jirani yake , tumbo halikadhalika, mavuno kidogo sababu ni ileile jirani mchawi, akisikia kelele juu ya paa ni mhawi tu, hana sababu nyingine.
Huhitaji kutumia akili sana kujua yanayoendelea nyuma yake kuna Mafisadi wa CCM hasa Mwigulu nchemba ndiyo mratibu mkuu wa hii kitu.
 
mkuu, tuwe wakweli mie naamini akina zzk wana makosa ila hata uongozi wetu uliobaki una makosa pia. kimsingi tuhuma hizi hazijaanza leo, zimekuwepo toka enzi za akina marehemu chacha wangwe, kafulila, Juliana shonza nk tukubali ukweli, tuhuma nyingi za msingi zimekuwa zikijirudia sasa sina hakika kama kujirudia huku ni bahati mbaya au vp!! nikuulize swali, (kuhusu ubaguzi) mh lema alilipuka hapa jf bila kupitia vikao na taratibu za ndani ya chama kama katiba yetu ya mwaka 2006 ibara ya 10 inavyoelekeza na hakufanywa chochote na uongozi - je hii ilikuwa ni kupitiwa kwa kamati kuu?! kwa kweli baadhi yetu tunapenda mabadiliko, lakini kuwe na HAKI na USAWA miongoni mwa wanachama wote.....tunataka demokrasia halisi ndani ya chama ili kujitofautisha na maccm.
gastone mkuu nimependa maswali yako maana hata mimi nimeuliza maswali ambayo yanataka kushabihiana na hayo. Binafsi ninachokiona hapa ni kuwa kuna tatizo la msingi, mimi nimewahi kuwa mwanachama wa YUNA, ambapo kuna watu wanaitwa waanzilishi, Author members, katiba ilikuwa kwa staili ambayo hawa jamaa ndo wenye maamuzi ya mwisho, wengi wa wanachama hao kwasasa ni viongozi wa CDM na wachache ni wa CCM. Ilikuwa dhambi kubwa kuliko zote ni kuhoji matumizi, utasikia next time hatukuchagui kwenda Nairobi kwenye EARMUN na kadhalika, hivyo mi nadhani kuna haja ya kuangalia kwa undani jambo hili. Hata hivyo wahenga walisema vita vya panzi furaha kwa.....
 
Last edited by a moderator:
mkuu, tuwe wakweli mie naamini akina zzk wana makosa ila hata uongozi wetu uliobaki una makosa pia. kimsingi tuhuma hizi hazijaanza leo, zimekuwepo toka enzi za akina marehemu chacha wangwe, kafulila, Juliana shonza nk tukubali ukweli, tuhuma nyingi za msingi zimekuwa zikijirudia sasa sina hakika kama kujirudia huku ni bahati mbaya au vp!! nikuulize swali, (kuhusu ubaguzi) mh lema alilipuka hapa jf bila kupitia vikao na taratibu za ndani ya chama kama katiba yetu ya mwaka 2006 ibara ya 10 inavyoelekeza na hakufanywa chochote na uongozi - je hii ilikuwa ni kupitiwa kwa kamati kuu?! kwa kweli baadhi yetu tunapenda mabadiliko, lakini kuwe na HAKI na USAWA miongoni mwa wanachama wote.....tunataka demokrasia halisi ndani ya chama ili kujitofautisha na maccm.
Mkuu nakukumbusha na HENRY KILEWO KWENYE BLOG YAKE
 
mkuu @Mikael P. Aweda kwanza napenda kukueleza kuwa yawezekana kuwa wanatumiwa na CCM, lakini umeshawahi kukaa na kufikiri kuwa kwanini mtu kama Mwenyekiti wa mkoa Singida, ambaye amejitolea kwa hali na mali ili CDM isonge mbele, Nyumba yake, sanduku la posta, na hata resource nyingine, leo hii awe ametumiwa na CCM? Kuna push factors gani ambazo zimepelekea hilo.
Tafakari! Chukua hatua
Hata Naibu Katibu Mkuu, CHADEMA since 16 Years old.
Fedha fedheha Mkuu, kuna watu wanasaliti Ndoa zao walizozijenga kwa Mikono yao wenyewe
 
Mkuu huu mkakati wa ccm utapita tuu. Wewe subiri siku 14 zikamilike ndio utaona kuwa samaki awezi kutishiwa na mawimbi ya Bahari. ZZT karibu atasaulika katika jamii ya Watanzania.
 
Mkuu huu mkakati wa ccm utapita tuu. Wewe subiri siku 14 zikamilike ndio utaona kuwa samaki awezi kutishiwa na mawimbi ya Bahari. ZZT karibu atasaulika katika jamii ya Watanzania.

Wote waliokengeuka watarudi kwenye mstari TU, ila waliokamatwa na NGOZI ndio wezi sweka segerea wale. CHADEMA TAMU bana hata kutamka tu YATOSHA
 
Wewe boot licker.. unatumiwa na wachagga! Wenzako wamejitambua, wamejitoa kwenye mtandao!

Hivi wachagga wamefanya kitu gani hadi wanachukiwa kama wasomali hapa tanzania? Hakuna post yako ambayo umewaongelea vizuri wachagga walikufanyaje?
 
Hata Naibu Katibu Mkuu, CHADEMA since 16 Years old.
Fedha fedheha Mkuu, kuna watu wanasaliti Ndoa zao walizozijenga kwa Mikono yao wenyewe

Hata mchawi anamtoa kafara mwanae.sembuse na kusaliti CDM chezea rupiaeee
 
Back
Top Bottom