Mambo 17 yaliyosababisha kuuawa kwa Muammar Gaddafi

Niambie matibu ya mgonjwa wa Moyo Nchini India alighalimiwa kiasi gani na nchi kipindi kile ?
Hivi kabla hatujafika mbali unajua 300m $ ni sawa na shiling ngapi kibongo bongo.

Bro admit hapa kuna kosa kwa mwandishi wa awali.

Unajua uwanja wa Mkapa ama kwa mchina umejengwa kwa gharama ya sh ngapi? Ni kama dola milioni 56-60 hivi

Hivi mkuu unajua kuwa bilioni 1 ni sawa na Milioni 1000/= ,

Gharama daraja la Kigamboni zaongezeka maradufu | East Africa Television

National Stadium (Tanzania) - Wikipedia

Soma kidogo hizo link itakusaidia kujua gharama za hiyo pesa anayopewa raia mmoja kutibiwa nje ya nchi.

View attachment 1546459
 
  • Thanks
Reactions: PNC
8)Dolla 300Milioni unaijua lakini? Au ya Zimbabwe?
Yaani MTU mmoja apewe bilioni 600 Na zaidi akatibiwe?
Hizi story watu wanalishana kwenye vikao vya ghahawa zinasambaa nchi nzima.

Misri,Tunisia,Libya,Mali. Hao viongozi wao wameondolewa Na maandamano ya kumpinga raisi wao. Walioondoka kabla ya kisanga hakijawa kikubwa walipona Na nchi zao hazikupata madhara,walioshupaza shingo zao wamekufa wakipambana Na nchi kuparaganyika

Nchi za kidikteta ni vigumu kubalance story kupata habari hasi za nchi. Mf Rwanda. We unadhani kifinyo wanachokipata wapinzani bongo nchi za Afrika wanakijua sana ?
Vipi sasa kuna freedom of expression, na hali imekuwa nzuri siyo? Libya imegeuka kuwa sehemu hatari sana duniani. Hivi ni nani aliset standard ya uongozi kuwa ni lazima ifanane ya western countries? Mbona Wamarekani hawakubari mfumo wa U.K wa ufalme hata Meghan umemshinda na hakuna tatizo.
Sema hapo kwenye $300 million ama kakosea kuandika au matangopori.
 
Inawezekana mkuu ,kwani unajua ukwasi uliokuwa wa nchi ya LIBYA?.
Ndio nchi ya kwanza kabisa duniani kumlipa mshahara Raia wa nchi asiye na kazi, Ujeruman na Sweden waliiga tu baada ya kuona kumbe inawezekana.
Hapana mkuu hii ni ngumu kuingia akilini, dola milioni mia tatu ni nyingi sana.

Kwanza, matibabu ya bilioni 600+ kwa tsh ni adimu sana, naweza kusema hayapo. Afya ni ghali lakini si ghali kiasi hicho.

Pili, watu wanne tu watafanya serikali itoe dola za kimarekani bilioni 1.2, ni pesa nyingi sana hii.

Kwa ufupi ni suala lisiloingia akilini kabisa!
 
Gaddafi alikuwa dikteta, muuaji !
Alidhani Mungu kamuumba yeye tu utawala Libya...

Alivuna alichopanda, huwezi kuwafuga binadamu kama Mbwa! Binadamu ana hitaji uhuru...bila uhuru kuna siku atakunyonga tu
 
8)Dolla 300Milioni unaijua lakini? Au ya Zimbabwe?

Yaani MTU mmoja apewe bilioni 600 na zaidi akatibiwe?

Hizi story watu wanalishana kwenye vikao vya ghahawa zinasambaa nchi nzima.

Misri, Tunisia, Libya, Mali. Hao viongozi wao wameondolewa na maandamano ya kumpinga raisi wao. Walioondoka kabla ya kisanga hakijawa kikubwa walipona na nchi zao hazikupata madhara, walioshupaza shingo zao wamekufa wakipambana na nchi kuparaganyika

Nchi za kidikteta ni vigumu kubalance story kupata habari hasi za nchi. Mf Rwanda. We unadhani kifinyo wanachokipata wapinzani bongo nchi za Afrika wanakijua sana?
Ni kweli lakini hata huko Marekani madhila wanayopitia wamarekani weusi ni kiasi kidogo tu ndio yanajulikana.
 
Hakukua na freedom of expression, wapinzani walipotea , kuwekwa ndani ama kuuwa.

Gadaffi angemuandaa mrithi wake na yeye kuji wekt kando ya uongozi angebaki na heshima ya Baba wa Taifa.
Hivi wapinzani ndio watu special sana ama vp? maana naona wanatajwa wao tu kana kwamba hakuna wengine wanaopata misukosuko.
 
Mengi ya uliyoandika ni hadithi za kutunga lakini kama hadithi zingine za sungura na fisi walisema hii nayo inamafunzo. Tuchukulie kwamba yoote hayo ni kweli. Hii inatupa picha kua binadamu anathamini sana uhuru wake na demokrasia hata kama anamaisha duni/magumu kuliko kupewa vitu vya bure kama wanyama kwenye zoo, ndio maana huko Libya kukawa na maandamano ya kumpinga Gadafi hata kama ni ya watu wachache

"Mtu haishi kwa mkate tu", mwisho wa kunukuu
Ingekuwa hivyo basi hela isingekuwa na power.
 
Wakina Lissu vibaraka wa mabeberu wakaanzisha maandamano ya kumuuwa Gadadi ili wao wapate urais,badala yake sasa hapakaliki.ni moto mwanzo mwisho.
 
8)Dolla 300Milioni unaijua lakini? Au ya Zimbabwe?

Yaani MTU mmoja apewe bilioni 600 na zaidi akatibiwe?

Hizi story watu wanalishana kwenye vikao vya ghahawa zinasambaa nchi nzima.

Misri, Tunisia, Libya, Mali. Hao viongozi wao wameondolewa na maandamano ya kumpinga raisi wao. Walioondoka kabla ya kisanga hakijawa kikubwa walipona na nchi zao hazikupata madhara, walioshupaza shingo zao wamekufa wakipambana na nchi kuparaganyika

Nchi za kidikteta ni vigumu kubalance story kupata habari hasi za nchi. Mf Rwanda. We unadhani kifinyo wanachokipata wapinzani bongo nchi za Afrika wanakijua sana?
Sio bilioni 600, ni trillion 600
 
MAMBO 17 YALIYOSABABISHA KUUAWA KWA GADDAFI

1. LIBYA kulikuwa hakuna bili ya umeme, means umeme ulikuwa bure kwa raia wote

2. Libya kulikuwa hakuna Riba kwenye mikopo, Benk zote Libya zilikuwa za Umma na mikopo ilitolewa kwa raia wote tena bila Riba.

3. Gadafi alisisitiza kwamba, wazazi wake hawatapata nyumba nzuri hadi raia wote wa Libya wawe na makazi. Baba mzazi wa Gadafi amefariki wakati, yeye, mke wake na mama yake wakiishi kwenye hema.

4. Kila mfanyakazi Mpya (Mwajiriwa mpya) nchini Libya alipewa Dola za kimarekani 50,000 ili aanzie maisha.

5. Kabla ya Gadafi, kulikuwa na 25% tu ya raia wa Libya ndio walikuwa na Elimu.

6. Elimu na Huduma za Afya (matibabu) nchini LIBYA zilitolewa bure.

7. Kama Mwananchi wa LIBYA aliyehitaji kujishughulisha na kilimo, alipatiwa ardhi, nyumba, mbegu na mahitaji mengine yaliyohitajika.

8. Iwapo mwananchi wa Libya akishindwa kupata Elimu au Huduma ya Afya ndani ya LIBYA, serikali ilimsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mahitaji hayo, pia alipewa Dola milioni 300 za kimarekani kwa ajili ya gharama .

9. LIBYA, Kila raia wa LIBYA aliyenunua gari, serikali ilimwongezea nusu ya bei ya gari, means kama gari itauzwa sh milioni tano, basi raia alilipia shilingi milioni mbili na laki tano na kiasi kingine kinalipwa na serikali.

10. Bei ya Petrol nchini LIBYA ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.14

11. Libya ilikuwa haina madeni ya Nje, ilikuwa haidaiwi na nchi yoyote na ilikuwa imehifadhi dola za kimarekani bilioni 150

12. Kila mwananchi wa Libya aliyekosa ajira baada ya kuhitimu kulingana na kiwango alichofikia, Serikali ilimlipa mshahara unaokaribiana na mtu aliyeajiriwa mwenye elimu sawa na aliyonayo yeye.

13. Sehemu ya mauzo ya mafuta nchini Libya ilipelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki za kila raia wa LIBYA

14. Kila mwanamke aliyejifungua, alipewa Dola za kimarekani 5,000

15. Gharama ya mikate arobaini ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.15

16. 25% ya raia wa LBYA walikuwa na kiwango cha Elimu cha SHAHADA (a university degree)

17. GADAFFI aliaanzisha mradi mkubwa zaidi kuwai kutokea duniani, mradi wa Umwagiliaji uliojulikana kama MAN- MADE RIVER PROJECT, Mradi uliowezesha upatikanaji wa maji eneo zima la jangwa.

Kama huu uliitwa “UDIKTETA” Basi WANADEMOCRASIA wote watakwenda Motoni

USIPITE BILA KUSHARE UJUMBE HUU MZURI NA MALAZIA KWA KUCOMMENT R.I.P GADDAFI

NB: Imekopiwa mahali

===
Hizi stori zooote mnapiga aidha ni Kwasababu za kidini au hapendi vyama mbadala vya upinzani hivyo mnatumia tukio la Libya kutishia watu.

Huyo Ghadaffi ambaye misaada yake yote ulikuwa ni Misikiti ( nadani hapa 🐍🐍🐍JIWE nae kakopi ili kujipa uhalali, maana waislamu wape pesa, ubwabwa na wajengee misikiti wanakaa tuli kana maji ya mtungi hata kana wenzao wako jela kwa uonevu ). Huyo Ghafafi alileta JESHI lake Uganda likashirikiana na Askari wa Uganda kuua watanzania wenzetu ndio kila siku mnampamba humu.

Wabongo hamnazo.
 
MAMBO 17 YALIYOSABABISHA KUUAWA KWA GADDAFI

1. LIBYA kulikuwa hakuna bili ya umeme, means umeme ulikuwa bure kwa raia wote

2. Libya kulikuwa hakuna Riba kwenye mikopo, Benk zote Libya zilikuwa za Umma na mikopo ilitolewa kwa raia wote tena bila Riba.

3. Gadafi alisisitiza kwamba, wazazi wake hawatapata nyumba nzuri hadi raia wote wa Libya wawe na makazi. Baba mzazi wa Gadafi amefariki wakati, yeye, mke wake na mama yake wakiishi kwenye hema.

4. Kila mfanyakazi Mpya (Mwajiriwa mpya) nchini Libya alipewa Dola za kimarekani 50,000 ili aanzie maisha.

5. Kabla ya Gadafi, kulikuwa na 25% tu ya raia wa Libya ndio walikuwa na Elimu.

6. Elimu na Huduma za Afya (matibabu) nchini LIBYA zilitolewa bure.

7. Kama Mwananchi wa LIBYA aliyehitaji kujishughulisha na kilimo, alipatiwa ardhi, nyumba, mbegu na mahitaji mengine yaliyohitajika.

8. Iwapo mwananchi wa Libya akishindwa kupata Elimu au Huduma ya Afya ndani ya LIBYA, serikali ilimsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mahitaji hayo, pia alipewa Dola milioni 300 za kimarekani kwa ajili ya gharama .

9. LIBYA, Kila raia wa LIBYA aliyenunua gari, serikali ilimwongezea nusu ya bei ya gari, means kama gari itauzwa sh milioni tano, basi raia alilipia shilingi milioni mbili na laki tano na kiasi kingine kinalipwa na serikali.

10. Bei ya Petrol nchini LIBYA ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.14

11. Libya ilikuwa haina madeni ya Nje, ilikuwa haidaiwi na nchi yoyote na ilikuwa imehifadhi dola za kimarekani bilioni 150

12. Kila mwananchi wa Libya aliyekosa ajira baada ya kuhitimu kulingana na kiwango alichofikia, Serikali ilimlipa mshahara unaokaribiana na mtu aliyeajiriwa mwenye elimu sawa na aliyonayo yeye.

13. Sehemu ya mauzo ya mafuta nchini Libya ilipelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki za kila raia wa LIBYA

14. Kila mwanamke aliyejifungua, alipewa Dola za kimarekani 5,000

15. Gharama ya mikate arobaini ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.15

16. 25% ya raia wa LBYA walikuwa na kiwango cha Elimu cha SHAHADA (a university degree)

17. GADAFFI aliaanzisha mradi mkubwa zaidi kuwai kutokea duniani, mradi wa Umwagiliaji uliojulikana kama MAN- MADE RIVER PROJECT, Mradi uliowezesha upatikanaji wa maji eneo zima la jangwa.

Kama huu uliitwa “UDIKTETA” Basi WANADEMOCRASIA wote watakwenda Motoni

USIPITE BILA KUSHARE UJUMBE HUU MZURI NA MALAZIA KWA KUCOMMENT R.I.P GADDAFI

NB: Imekopiwa mahali

===
Mungu alivyotuuumba, alituacha tuwe huru kuchagua nini tunataka. Kuna kipindi tunafuarahia kuchagua shida badala ya raha
Kuna kipindi huwezi hata kuelewa binadamu anataka nini.
Eden kulikuwa na Matunda ya kila aina, ila tukaamua kutest lililokatazwa
Hivyo hata iweje uhuru huu wa kujaribu vitu vingine lazima uheshimiwe
 
Hizi stori zooote mnapiga aidha ni Kwasababu za kidini au hapendi vyama mbadala vya upinzani hivyo mnatumia tukio la Libya kutishia watu.

Huyo Ghadaffi ambaye misaada yake yote ulikuwa ni Misikiti ( nadani hapa 🐍🐍🐍JIWE nae kakopi ili kujipa uhalali, maana waislamu wape pesa, ubwabwa na wajengee misikiti wanakaa tuli kana maji ya mtungi hata kana wenzao wako jela kwa uonevu )alileta JESHI lake Uganda likashirikiana na Askari wa Uganda kuua watanzania wenzetu ndio kila siku mnampamba humu.

Wabongo hamnazo.
Ilete hiyo mada masheikh kuonewa kwa kuwekwa huko jela uone watu wanavyogawanyika humu kwa dini zao,hapo ndiyo unakuta mpinzani anapoungana na chama tawala.
 
Back
Top Bottom