Mambo 17 yaliyosababisha kuuawa kwa Muammar Gaddafi

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
998
MAMBO 17 YALIYOSABABISHA KUUAWA KWA GADDAFI

1. LIBYA kulikuwa hakuna bili ya umeme, means umeme ulikuwa bure kwa raia wote

2. Libya kulikuwa hakuna Riba kwenye mikopo, Benk zote Libya zilikuwa za Umma na mikopo ilitolewa kwa raia wote tena bila Riba.

3. Gadafi alisisitiza kwamba, wazazi wake hawatapata nyumba nzuri hadi raia wote wa Libya wawe na makazi. Baba mzazi wa Gadafi amefariki wakati, yeye, mke wake na mama yake wakiishi kwenye hema.

4. Kila mfanyakazi Mpya (Mwajiriwa mpya) nchini Libya alipewa Dola za kimarekani 50,000 ili aanzie maisha.

5. Kabla ya Gadafi, kulikuwa na 25% tu ya raia wa Libya ndio walikuwa na Elimu.

6. Elimu na Huduma za Afya (matibabu) nchini LIBYA zilitolewa bure.

7. Kama Mwananchi wa LIBYA aliyehitaji kujishughulisha na kilimo, alipatiwa ardhi, nyumba, mbegu na mahitaji mengine yaliyohitajika.

8. Iwapo mwananchi wa Libya akishindwa kupata Elimu au Huduma ya Afya ndani ya LIBYA, serikali ilimsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mahitaji hayo, pia alipewa Dola milioni 300 za kimarekani kwa ajili ya gharama .

9. LIBYA, Kila raia wa LIBYA aliyenunua gari, serikali ilimwongezea nusu ya bei ya gari, means kama gari itauzwa sh milioni tano, basi raia alilipia shilingi milioni mbili na laki tano na kiasi kingine kinalipwa na serikali.

10. Bei ya Petrol nchini LIBYA ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.14

11. Libya ilikuwa haina madeni ya Nje, ilikuwa haidaiwi na nchi yoyote na ilikuwa imehifadhi dola za kimarekani bilioni 150

12. Kila mwananchi wa Libya aliyekosa ajira baada ya kuhitimu kulingana na kiwango alichofikia, Serikali ilimlipa mshahara unaokaribiana na mtu aliyeajiriwa mwenye elimu sawa na aliyonayo yeye.

13. Sehemu ya mauzo ya mafuta nchini Libya ilipelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki za kila raia wa LIBYA

14. Kila mwanamke aliyejifungua, alipewa Dola za kimarekani 5,000

15. Gharama ya mikate arobaini ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.15

16. 25% ya raia wa LBYA walikuwa na kiwango cha Elimu cha SHAHADA (a university degree)

17. GADAFFI aliaanzisha mradi mkubwa zaidi kuwai kutokea duniani, mradi wa Umwagiliaji uliojulikana kama MAN- MADE RIVER PROJECT, Mradi uliowezesha upatikanaji wa maji eneo zima la jangwa.

Kama huu uliitwa “UDIKTETA” Basi WANADEMOCRASIA wote watakwenda Motoni

USIPITE BILA KUSHARE UJUMBE HUU MZURI NA MALAZIA KWA KUCOMMENT R.I.P GADDAFI


NB: Imekopiwa mahali


===
Kwa matibabu wakipelekwa nje, walikuwa wanapewa dola za kumarekani 30,000
 
8)Dolla 300Milioni unaijua lakini? Au ya Zimbabwe?

Yaani MTU mmoja apewe bilioni 600 na zaidi akatibiwe?

Hizi story watu wanalishana kwenye vikao vya ghahawa zinasambaa nchi nzima.

Misri, Tunisia, Libya, Mali. Hao viongozi wao wameondolewa na maandamano ya kumpinga raisi wao. Walioondoka kabla ya kisanga hakijawa kikubwa walipona na nchi zao hazikupata madhara, walioshupaza shingo zao wamekufa wakipambana na nchi kuparaganyika

Nchi za kidikteta ni vigumu kubalance story kupata habari hasi za nchi. Mf Rwanda. We unadhani kifinyo wanachokipata wapinzani bongo nchi za Afrika wanakijua sana?
 
Ushahidi wa haya umewahi kutolewa na mwanchi yeyote? Unaweza kutuwekea link ya mwananchi hata wa kukodiwa akikabidhiwa dola 50,000 za kuanzia maisha?

Hata Marekani taifa tajiri au Sweden Denmark na nchi nyingine tunazoambiwa zinaongoza kwa wananchi wake kuwa na furaha haya uliyoyaandika hapa hayapo.

Haya mashairi mara nyingi huandikwa na watu wanaotetea hali fulani hivi ya utawala na kujaribu kuupamba faida zake za maisha ya peponi. Hembu mtuache jamani.
 
Namba 8

Alipewa 300m $ , mkuu hiyo hela unaichukulia poa eenh.

300,000,000/= x 2360 , labda hapo mwandishi wa kwanza alikosea.
Inawezekana mkuu ,kwani unajua ukwasi uliokuwa wa nchi ya LIBYA?.
Ndio nchi ya kwanza kabisa duniani kumlipa mshahara Raia wa nchi asiye na kazi, Ujeruman na Sweden waliiga tu baada ya kuona kumbe inawezekana.
 
Mengi ya uliyoandika ni hadithi za kutunga lakini kama hadithi zingine za sungura na fisi walisema hii nayo inamafunzo. Tuchukulie kwamba yoote hayo ni kweli. Hii inatupa picha kua binadamu anathamini sana uhuru wake na demokrasia hata kama anamaisha duni/magumu kuliko kupewa vitu vya bure kama wanyama kwenye zoo, ndio maana huko Libya kukawa na maandamano ya kumpinga Gadafi hata kama ni ya watu wachache

"Mtu haishi kwa mkate tu", mwisho wa kunukuu
 
Kwa matibabu wakipelekwa nje,walikuwa wanapewa dola za kumarekani 30,000
Kwani kabla ya hospital ya JK ile ya moyo, Tz siilikuwa anaghalamia wananchi wake matibu nchini India, ni ilikuwa ni Mamillion ya Tshs..na ndio nchi maskini hii .je kwa nchi ya mafuta kama LIBYA.
 
Kuna story zingine zinakuaga zimekuzwa tu..maana yake waLibya walikua hafanyi kazi sasa

Eti hakuwapa maisha mazuri wazazi wake mpaka wanchi wote wawe na maisha bora,sasa hiyo ni akili au ni uongo wa kulaghai watu yeye akae Ikulu miaka yake yote?

Maisha mazuri kama hayo duniani kote yanaletwa na juhudi za watu wenyewe na serikali yamkini ibanwe na mambo kama mashule, hospital, maji, umeme na barabara kwisha..ila hii namba 17 it's okay hata sisi walipaswa kufanya hivyo maana uchumi wetu unategemea kilimo na si hayo madini ambayo kila siku watu wanapiga kelele, mafuta huwezi fananisha na madini ambayo yanatafutwa wakati mwingine hayaonekani, mafuta ukipata koki yake tu ya huko chini ardhini unavuna siku zote.
 
Ushahidi wa haya umewahi kutolewa na mwanchi yeyote? Unaweza kutuwekea link ya mwananchi hata wa kukodiwa akikabidhiwa dola 50,000 za kuanzia maisha?

Hata Marekani taifa tajiri au sweden denmark na nchi nyingine tunazoambiwa zinaongoza kwa wananchi wake kuwa na furaha haya uliyoyaandika hapa hayapo.

Haya mashairi mara nyingi huandikwa na watu wanaotetea hali flani hivi ya utawala na kujaribu kuupamba faida zake za maisha ya peponi. Hembu mtuache jamani
ajabu ni kwamba mkaza wa pale tripoli hawakuwai kuyajua hayo wakati wa utawala wa MG, ila walio nje na Libya wanayajua.
 
ajabu ni kwamba mkaza wa pale tripoli hawakuwai kuyajua hayo wakati wa utawala wa MG, ila walio nje na Libya wanayajua.
Uliwahi kuishi pale Tripoli mkuu? Mm ni shuhuda wa yale maisha yao mazuri.ambaye aliwahi kusoma au seminar yyte pale atushuhudie.

Nikiwa ni mgeni na sio Raia wa ile nchi niliona kabisa kuwa pale ni KANANI nchi ya maziwa na asali ijekuwa Raia halisi wa nchi.
 
Kwa kuwa umecopy mahali tunakusamehe. Siku nyingine uwe na uwezo wa kuchambua mambo. Utalishwa sana matango pori. Mfano,si kweli kwamba mtu mmoja apewe $300 m bure kwa matibabu
Niambie matibu ya mgonjwa wa Moyo Nchini India alighalimiwa kiasi gani na nchi kipindi kile ?
 
Back
Top Bottom