Mambo 15 ya kufanya kama serikali ya Magufuli inataka kuendeleza viwanda Tanzania

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,179
7,330
Pengine sio yote yanafaa... lakini mengi yatasaidia

1. Kwa miaka 5 serikali ielekeze nguvu kuinua viwanda vya bidhaa za chakula, hivyo...

2. Serikali itoe ruzuku kwa uendelezwaji wa viwanda vya chakula kwa miaka 5, mathalani...

3. Serikali iondoe kodi zote katika vifungashio vya bidhaa za chakula kwa miaka 5, kwa mfano...

4. Makopo ya metal na plastiki, chupa za plastiki na glass, karatasi za nylon na za kawaida ihakikishwe zinazotengenezwa nchini au kuagizwa zipatikane kwa bei rahisi, kufanikisha hilo...

5. Kwa miaka 5 serikali itoe ruzuku kwa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya chakula, kwa mfano...

6. Kwa miaka 5 gharama za umeme kwenye viwanda vya vifungashio vya chakula ziwe nusu ya gharama za kawaida, kisha...

7. Serikali ihamasishe bidhaa zote za chakula, hasa vilivyo rahisi kusindika na kuwa packed visiuzwe bila kuwa packed, kwa mfano...

8. Unga wa mahingi, Unga wa ngano, Mchele, Maharage/kunde, Nyama, Samaki, mayai na baadhi ya matunda viuzwe vikiwa packed, ili...

9. Biashara yake iwe rasmi zaidi na uuzaji nje ya nchi uwe rahisi zaidi, na pia...

10. Serikali iendeleze masoko ya ndani ya vyakula kwa kuyaboresha kimiundombinu na kuyarasimisha, tena...

11. Serikali ihamasishe kufunguliwa na kusambaa kwa super markets, lakini pia bidhaa zote za chakula vilivyosindikwa na kufungwa nchini visilipishwe VAT kwa miaka 5, vile vile...

12. Serikali ifungue mashamba makubwa ya mazao ya chakula kama mahindi, ngano, alizeti, maharage, mtama, miwa na mpunga, kwa kuyaendeleza hadi kiwango cha kuwa tayari kupanda mbegu (kusafisha pori, kutoa visiki na inapolazimu kuweka miundombinu ya umwagiliaji), kisha...

13. Iyakodishe mashamba hayo kwa watu walioomba na kupatiwa mafunzo, huku wahitimu wa vyuo mbalimbali wakipewa kipaumbele, ambapo...

14. Watakaokodisha mashamba hayo wataingia mikataba na wenye viwanda vya kusindika na kufungasha chakula ambao nao watakuwa na mikataba na wenye super na mini super markets, bila kusahau...

15. Serikali iimarishe maabara za TFDA kuhakikisha vyakula vyote vinavyosindikwa na kufungashwa na viwanda vyetu, pia vinavyoagizwa nje ya nchi vinakuwa na ubora unaotakiwa.

Naomba kuwasilisha
 
Kama angalau 90% ya wana jukwaa hili wangekuwa wana mawazo positive kama yako, tusingekuwa kama tulivyo (INGAWA INAWEZEKANA BAADHI YA VITU ULIVYOVISEMA SI RAHISI KUTEKELEZEKA), ila kuna jamaa mmoja alileta uzi humu akidai kuna utafiti unaonesha asilimia kubwa ya vijana mtandaoni wanaandika pumba tupu wala hamna la maana wanalowaza. Ngoja tuone michango, pengine inaweza kutupa picha fulani hivi!
 
Nimeipenda hii sana pia serekali ianze kufocus kwenye viwanda vya kati ikiwemo vya alizeti,unga,nguo na vingine ambavyo uendeshaji wake na uanzishwaji wake sio gharama kubwa hii itasaidia kuongeza kipato kwa vijana pamoja na kuwa na ajira za uhakika..
 
uzi mzuri sana lakini tukae tujue,nchi hii watu hawapo kama unavyowaza wewe unataka nchi ijikwamue na wananchi wake ,lakini wao wapo wanataka kufanyiwa matambiko kama mizimu na kuombwa
 
Nimeipenda hii sana pia serekali ianze kufocus kwenye viwanda vya kati ikiwemo vya alizeti,unga,nguo na vingine ambavyo uendeshaji wake na uanzishwaji wake sio gharama kubwa hii itasaidia kuongeza kipato kwa vijana pamoja na kuwa na ajira za uhakika..

Nyongeza wangetoa pia kipaombele kwa wazawa wa eneo husika kwa mitaji na pembejeo za kilimo na viwanda na elimu ya ujariamali kuliko kumaliza nguvu nyingi kuwaondoa wazawa katika maeneo yao na kuwa dhamini wawekezaji ambao mpaka sasa hawana tija yoyote kwa taifa hili masikini.
 
Kama angalau 90% ya wana jukwaa hili wangekuwa wana mawazo positive kama yako, tusingekuwa kama tulivyo (INGAWA INAWEZEKANA BAADHI YA VITU ULIVYOVISEMA SI RAHISI KUTEKELEZEKA), ila kuna jamaa mmoja alileta uzi humu akidai kuna utafiti unaonesha asilimia kubwa ya vijana mtandaoni wanaandika pumba tupu wala hamna la maana wanalowaza. Ngoja tuone michango, pengine inaweza kutupa picha fulani hivi!

Hiyo asilimia 90 umeenda mbali sana, wangalau asilimia 50 kama tutaweza kuwa na mawazo ya kujenga. Kwenye mawazo ya huyu jamaa naona amelenga kwenye viwanda na kilimo. Mimi nijikite kwenye kwenye kilimo maana ndio msingi wa hivyo viwanda. Kwa bahati mbaya sana mimi ni mkulima, madhila tunayokutana nayo sio mchezo. Nitoe angalizo kwani mpaka sasa sisi wakulima tunaendelea na shughuli hii kama wito na sio kupata faida. Huku kwenye kilimo serekali isiposhusha bei ya pembejeo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na mazao hafifu, na pia waangalie hao watakaokuwa na viwanda wanunue bidhaa za mkulima kwa bei yenye maslahi kwani kuna maslahi duni sana kwenye kilimo, kiasi kwamba sisi wenye wito tu ndo tunaendelea kulima. Nina mashaka sana watu watawekeza zaidi kwenye viwanda na kusahau sehemu nyeti ya kilimo ambayo ndio inatoa malighafi ya hivyo viwanda. Ni vema kwanza tukahakikisha kama alivyopendekeza mleta mada tuwe na mashamba kwa usimamizi wa serekali na kipaombele tupewe wakulima ambao tayari tunalima kwani tuna uzoefu na mapenzi na kilimo, kisha wapewe hao wasomi, maana iwapo utawapa hao wasomi kama sehemu ya kutoa ajira bila kuangalia mapenzi yao kwenye kilimo, ni rahisi sana wao kukwamisha shughuli hizo kwani sioni wakiwa wavumilivu kwenye changamoto za kilimo.
 
Serikali ifanye haya:

1. Tuanze na viwanda vya huduma za kila siku ie Chakula, Malazi na Makazi.

2. Kuwe na mfumo unaorahisisha upatikanaji wa mitaji.
 
Mawazo yako supa, hata mimi huwa nashangaa mtu anaanzisha thread hapa nzuri tu alakini atapokelewa kwa kejeli, matusi, dharau na kadhalika.
Umesahau jambo moja kubwa zaidi. Nchi haiwezi kuendelea kiviwanda kama haiwezi kulinda viwanda vyake vya ndani kutoka na ushindani wa bidhaa za aina hiyohiyo zinazotoka nje ya nchi. Mara nyingi watu wana hisia siku zote kuwa bidhaa za nje ni bora kuliko za ndani, hii ni kwa nchi zote hata Ulaya. Uthibiti imara wa bidhaa kutoka nje ndio suala la msingi ili kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za ndani. Hapa naitupia lawama wizara wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji. Hawajaja na sera ya kulinda bidhaa za ndani zilizopo. Kwa mfano, kuna umuhimu gani wa kuagiza sementi, kanga na vitenge? Bidhaa hizi zikithibitiwa viwanda vyetu vitafufuka na kuongeza uzalishaji maana soko lipo. (Ninaelewa masharti ya soko huria ya WTO, lakini mbona wenzetu wanafanya?). Ni mbinde kuagiza gari mpya ya nje nchini India, wanalinda viwanda vyao vya magari maana na wao wanatengeneza.
 
Tuko, uko sawa kabisa, ila sasa watekelezaji wanawaza kisiasa zaidi ya kiutendaji. Kila utakapojaribu kufanya jambo lolote utakutana na chombo ambacho tayari kipo na kinatekeleza masuala ya kisiasa zaidi ya utaalamu.
Ukisoma mikakati mingi iliyowahi kupangwa na serikali ni mizuri sana ila utekelezaji unaangukia pabaya.
 
Pengine sio yote yanafaa... lakini mengi yatasaidia

1. Kwa miaka 5 serikali ielekeze nguvu kuinua viwanda vya bidhaa za chakula, hivyo...

2. Serikali itoe ruzuku kwa uendelezwaji wa viwanda vya chakula kwa miaka 5, mathalani...

3. Serikali iondoe kodi zote katika vifungashio vya bidhaa za chakula kwa miaka 5, kwa mfano...

4. Makopo ya metal na plastiki, chupa za plastiki na glass, karatasi za nylon na za kawaida ihakikishwe zinazotengenezwa nchini au kuagizwa zipatikane kwa bei rahisi, kufanikisha hilo...

5. Kwa miaka 5 serikali itoe ruzuku kwa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya chakula, kwa mfano...

6. Kwa miaka 5 gharama za umeme kwenye viwanda vya vifungashio vya chakula ziwe nusu ya gharama za kawaida, kisha...

7. Serikali ihamasishe bidhaa zote za chakula, hasa vilivyo rahisi kusindika na kuwa packed visiuzwe bila kuwa packed, kwa mfano...

8. Unga wa mahingi, Unga wa ngano, Mchele, Maharage/kunde, Nyama, Samaki, mayai na baadhi ya matunda viuzwe vikiwa packed, ili...

9. Biashara yake iwe rasmi zaidi na uuzaji nje ya nchi uwe rahisi zaidi, na pia...

10. Serikali iendeleze masoko ya ndani ya vyakula kwa kuyaboresha kimiundombinu na kuyarasimisha, tena...

11. Serikali ihamasishe kufunguliwa na kusambaa kwa super markets, lakini pia bidhaa zote za chakula vilivyosindikwa na kufungwa nchini visilipishwe VAT kwa miaka 5, vile vile...

12. Serikali ifungue mashamba makubwa ya mazao ya chakula kama mahindi, ngano, alizeti, maharage, mtama, miwa na mpunga, kwa kuyaendeleza hadi kiwango cha kuwa tayari kupanda mbegu (kusafisha pori, kutoa visiki na inapolazimu kuweka miundombinu ya umwagiliaji), kisha...

13. Iyakodishe mashamba hayo kwa watu walioomba na kupatiwa mafunzo, huku wahitimu wa vyuo mbalimbali wakipewa kipaumbele, ambapo...

14. Watakaokodisha mashamba hayo wataingia mikataba na wenye viwanda vya kusindika na kufungasha chakula ambao nao watakuwa na mikataba na wenye super na mini super markets, bila kusahau...

15. Serikali iimarishe maabara za TFDA kuhakikisha vyakula vyote vinavyosindikwa na kufungashwa na viwanda vyetu, pia vinavyoagizwa nje ya nchi vinakuwa na ubora unaotakiwa.

Naomba kuwasilisha

Tuanze na agro processing factories, viwanda vya nguo, katani,na ngozi, 2. Food products value addition - kama kusaga na kupaki unga, kukoboa na kupaki mchele, kubangua na kupaki korosho, ku- process fruit juices, kuongezea thamani mazao kama nyanya, vitunguu etc.
 
Namuomba Mungu huu uzi uendelee kujadiliwa kwa kutumia akili hivi hivi. Wote tuseme amin! Tanzania haifikii malengo kwa sababu ya mimi na wewe na yeye. Kama wewe ukiwa na mawazo kama mleta mada na wachangiaji hapo juu, na mimi nikibadilika na kutumia akili ni rahisi kumbadilisha yeye na kufanikisha mambo ya msingi.
 
Katika uchumi wa masoko ni nguv za soko 'demand and supply' zitakazoamua nini kifanyike, kiwanda gani kiwekwe wapi.

Serikali inaweza kuingia kati sio kwa yenyewe kujenga na kumiliki viwanda bali kwa kupitia fisical and monetary policies.

Equation ya irving fisher iliyoboreshwa (neo classical) ya PT=MV inaeleza zaidi.
Katika sera ya viwanda tunapaswa kuwa na vision ambayo itatuambia tu focus kwenye mambo gani kwa malengo yapi.
Nchi kama Tanzania ambayo inaingiza ndani bidhaa nyingi kuliko inazotoa nje inapaswa kujiimarisha kwenye bidhaa zinazotoka nje tena zinazotuingizi fedha za kigeni zinazochukuliwa na world bank kama hard currencies.
Sasa kabla ya kutengeneza vision yetu tunapaswa tuangalie potential yetu katika huu uwanja kisha tuangalia comperative na competitive advantage kwenye soko la dunia.
Niishie hapa kwanza kwa sasa.
 
7. Serikali ihamasishe bidhaa zote za chakula, hasa vilivyo rahisi kusindika na kuwa packed visiuzwe bila kuwa packed, kwa mfano...

Hili no Saba Sio lazima tusubiri sana, vyakula vyote viuzwe packed, serikali ipunguze kodi Za plastiki Kama ulivosema. Mimi ninauthamini mchango wako sana.

Na sijui kwanini sisi Ni masikini, wenzetu wanapata order ya bidhaa zao kuuza nje kwakua wameziboresha.
 
Kwenye viwanda wandugu hatuta take off kama ndege. It will be a step by step process.
Na hapa lazima uongozi wa juu uonyeshe kuhonor professions.
Niliposikia general tire inaanzishwa kwa hoja ya kisiasa nilisikitika sana na hapo hapo nikajua kusema serikali ya magufuli ni ya viwanda ni dhambi.
You can afford to go labour intensive with crude technology against a competitor who goes capital intensive.
If we need industries we have to work on the basics first, lay a foundation and take it one step at a time.

Mimi nnakuhakikishia ukifungua chicken processing plant Tanzania ya kuprocess kuku laki moja kwa siku, hautamaliza miezi mitatu kuku wote Tanzania watakuwa wameisha.
The same kwenye haya maharagwe na korosho mnayosemea.
You can compete globally without economies of scale and you cant achieve these economies of scale with small scale industries.
You cant attract big investors in an environment where you can give asurance of raw material availability over long term.
Jamani, industries is pure work, profession, no magic
 
Tuanze na agro processing factories, viwanda vya nguo, katani,na ngozi, 2. Food products value addition - kama kusaga na kupaki unga, kukoboa na kupaki mchele, kubangua na kupaki korosho, ku- process fruit juices, kuongezea thamani mazao kama nyanya, vitunguu etc.
Ugumu wa hivi viwanda ni gharama za umeme na gharama za packaging materials. Hapo ndipo serikali inatakiwa iweke boost...
 
Mawazo yako supa, hata mimi huwa nashangaa mtu anaanzisha thread hapa nzuri tu alakini atapokelewa kwa kejeli, matusi, dharau na kadhalika.
Umesahau jambo moja kubwa zaidi. Nchi haiwezi kuendelea kiviwanda kama haiwezi kulinda viwanda vyake vya ndani kutoka na ushindani wa bidhaa za aina hiyohiyo zinazotoka nje ya nchi. Mara nyingi watu wana hisia siku zote kuwa bidhaa za nje ni bora kuliko za ndani, hii ni kwa nchi zote hata Ulaya. Uthibiti imara wa bidhaa kutoka nje ndio suala la msingi ili kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za ndani. Hapa naitupia lawama wizara wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji. Hawajaja na sera ya kulinda bidhaa za ndani zilizopo. Kwa mfano, kuna umuhimu gani wa kuagiza sementi, kanga na vitenge? Bidhaa hizi zikithibitiwa viwanda vyetu vitafufuka na kuongeza uzalishaji maana soko lipo. (Ninaelewa masharti ya soko huria ya WTO, lakini mbona wenzetu wanafanya?). Ni mbinde kuagiza gari mpya ya nje nchini India, wanalinda viwanda vyao vya magari maana na wao wanatengeneza.
Ni kweli mkuu

Mara nyingi tunashindwa kwenye ushindani kutokana na gharama

Kwenye viwanda gharama kubwa zipo
1. Teknolijia
2. Nishati
3. Man power
4. Malighafi
5. Kodi
6. Usafirishaji kupeleka sokoni

Nchi kama China inakiwa na viwanda shindani kutokana na kuwa na gharama ndogo kwenye namba 1-3.

Sisi tunaumia zaidi na namba 2. Lakini tunakuwa na faida walau kwa soko la ndani kwa kupungua gharama za namba 6. Kwa hiyo serikali ikitaka kuwezesha viwanda vya ndani vianze na kupata momentum waweke msaada hapo namba 2 na 5...
 
Ugumu wa hivi viwanda ni gharama za umeme na gharama za packaging materials. Hapo ndipo serikali inatakiwa iweke boost...
Tuko kikubwa zaidi ambacho umekisahau ni uboreshwaj wa bidhaa za ndani. nikimaanisha kwamba kila bidhaa inayozalishwa nchini toka kiwandani iwe na ubora wa kimataifa si tu kwa std za kibongo ili sasa watu warudishe imani kwa bidhaa za ndani.
lakin pia tunahitaj sasa muundo wa elimu hasa katika ngazi za vyuo vikuu utoke kwenye tafiti za baseline surveys uende kwenye industrial applied research hii, itatupa nafasi zaid ya kuwa na vitu bora zaid na pia itatoa mwanya wa kuwa na bidhaa nyingi zaid kwan wataalam wa uzalishaj wataongezeka.
 
Ni kweli mkuu

Mara nyingi tunashindwa kwenye ushindani kutokana na gharama

Kwenye viwanda gharama kubwa zipo
1. Teknolijia
2. Nishati
3. Man power
4. Malighafi
5. Kodi
6. Usafirishaji kupeleka sokoni

Nchi kama China inakiwa na viwanda shindani kutokana na kuwa na gharama ndogo kwenye namba 1-3.

Sisi tunaumia zaidi na namba 2. Lakini tunakuwa na faida walau kwa soko la ndani kwa kupungua gharama za namba 6. Kwa hiyo serikali ikitaka kuwezesha viwanda vya ndani vianze na kupata momentum waweke msaada hapo namba 2 na 5...
na ishu kubwa Tuko sio technology kwan sio mara zote ile teknolojia mpya ikawa bora zaid. mie naona mapungufu yapo kwenye innovation zaidi. sioni kama kwenye hii nchi kuna nafasi ambayo mwanafunzi anapewa nafasi ya kuwa innovative. tutasingizia technolojia ila ubunifu wetu uko wapi?

teklojia itakuja tu ikiwa watu ni wabunifu tusi rely kwenye technology importation tu manake hata iyo sio lazima kwamba ikafit huku kwetu kwan inakuja kwa gharama kubwa sana.
 
Ugumu wa hivi viwanda ni gharama za umeme na gharama za packaging materials. Hapo ndipo serikali inatakiwa iweke boost...
gharama za packaging zionatokana na malighafi na production process............
bado tukipewa room we can manage this kwa kufanya recycling, kutumia by-products nk.
ujue majuzi nilikuwa na mtu mmoja tunaongea nae mtyu mkubwa sana toka TPDC ujue nilimshangaa sana alipokuwa anasema eti field ya mafuta na gesi haihitaj wataalam wengi kiiivyo. eti inahitaj pesa tu.

ukiangalia kwa upana akili ya mtu kama huyu ni mtu mbinafsi na hili ndo tatizo kwa nchi hii, hata wenye viwanda watakuwa wabinafsi tuu
 
Hiyo asilimia 90 umeenda mbali sana, wangalau asilimia 50 kama tutaweza kuwa na mawazo ya kujenga. Kwenye mawazo ya huyu jamaa naona amelenga kwenye viwanda na kilimo. Mimi nijikite kwenye kwenye kilimo maana ndio msingi wa hivyo viwanda. Kwa bahati mbaya sana mimi ni mkulima, madhila tunayokutana nayo sio mchezo. Nitoe angalizo kwani mpaka sasa sisi wakulima tunaendelea na shughuli hii kama wito na sio kupata faida. Huku kwenye kilimo serekali isiposhusha bei ya pembejeo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na mazao hafifu, na pia waangalie hao watakaokuwa na viwanda wanunue bidhaa za mkulima kwa bei yenye maslahi kwani kuna maslahi duni sana kwenye kilimo, kiasi kwamba sisi wenye wito tu ndo tunaendelea kulima. Nina mashaka sana watu watawekeza zaidi kwenye viwanda na kusahau sehemu nyeti ya kilimo ambayo ndio inatoa malighafi ya hivyo viwanda. Ni vema kwanza tukahakikisha kama alivyopendekeza mleta mada tuwe na mashamba kwa usimamizi wa serekali na kipaombele tupewe wakulima ambao tayari tunalima kwani tuna uzoefu na mapenzi na kilimo, kisha wapewe hao wasomi, maana iwapo utawapa hao wasomi kama sehemu ya kutoa ajira bila kuangalia mapenzi yao kwenye kilimo, ni rahisi sana wao kukwamisha shughuli hizo kwani sioni wakiwa wavumilivu kwenye changamoto za kilimo.
Mkuu nadhani siku moja tuweke uzi wa kilimo hapa tuudadavue sawasawa...

Lakini kikubwa ni kwamba Watanzania wengi (pengine zaidi ya 95%) wanaoanza ujasiriamali wana mitaji isiyozidi milioni 1.

Sasa mtu akikupa pori la kilimo lenye miti na visiki shilingi milioni moja inayosha hadi kutoa visiki kwenye eka moja tu. Hujalima, hujanunua mbegu, hujapanda nk.

Lakini hiyo milioni moja inatosha kwa eka 3 hadi 5 kwa shamba ambalo tayari limeng'olewa visiki na linafaa kupiga trekta.

Ndio maana nikapendekeza serikali iyaendeleze mashamba hadi level ya kung'oa visiki kisha ikodishe kwa wajariamali.

Watu wengi wanakimbilia kufungua viduka maana kuna mtu keshajenga jengo, kaweka umeme nk anakikodoshia fremu. Hebu fikiria mtu una milioni 1 kisha ipewe kakiwanja kapo location nzuri ya biashara, kisha uambiwe ufungue hapo duka... yaani ujenge jengo, uweke miondombinu yake, kidha ununie bidhaa uuze. Milioni moja inatosha? Lakini ukipewa fremu milioni moja unaanza mdogo mdogo.

Sasa hiyo ndio inayotokea kwenye kilimo. Watu wana mitaji kiduchu... anaenda mvomero ananunua pori eka 5 kwa laki 2 anaona kafanikiwa... lakini hadi siku uvune kitu kwenye hilo pori sio chini ya milioni 3 itahitajika kila ekari.... ndio maana vijana wanabanana mijini kufungua viduka...

Nchi nzima sehemu zenye mashamba yaliyoendelezwa kupata eneo la kukodisha ni ngumu saana maana demand ni kubwa.... nenda dakawa, kibaigwa, kiteto, monduli nk... nenda kyela mashamba ya mpunga yenye miundombinu ya umwagiliaji... wanakodidha hadi kwa laki na nusu kwa mwaka na bado huwezi kupata....

In short; serikali ijenge "fremu" za mashamba ikodishie wakulima...
 
Back
Top Bottom