Mambo 12 ambayo yanafanya Uganda iwe tofauti na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo 12 ambayo yanafanya Uganda iwe tofauti na Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IHOLOMELA, Aug 18, 2011.

 1. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  1. Pamoja na kuwa na msongamano mkubwa wa watu katikati ya jiji la Kampala pengine kuliko ule wa Kariakoo jijini Dar, daladala muda wote iwe asubuhi au jioni hakuna KUGOMBANIA.
  2. Pamoja na kuwa na idadi kubwa kabisa ya waendesha pikipiki maarufu kama Assekido au Bodaboda, jijini Kampala ajali ni chache sana tofauti na Tanzania.
  3. Pikipiki inaweza kupakia abiria hadi wanne na kupita mbele ya trafiki bila kukamatwa tofauti na Tanzania ukipakia abiria wawili tu unapigwa faini.
  4. Wakati Tanzania inabana ajira kwa wananchi wake nchini Uganda kupika, kuuza na kunywa gogo ni halali.
  5. Pamoja na kutosumbuliwa na trafiki kwa madereva na makondakta wa daladala na mabasi ya abiria hupakia seat level tu bila kusimamisha abiria.
  6. Idadi ya nyumba nzuri za kisasa na zilizoezekwa kwa mabati nchini Uganda ni nyingi kuliko Tanzania ambapo tunadumisha utamaduni wa mababu zetu kwa mapaa ya nyasi.
  7. Wakati mamalishe na wamachinga kila kukicha nchini Tanzania ni kufuzana na askari wa jiji, Kampala unafanya biashara mahali popote bila kusumbuliwa.
  8. Wakati nchini Tanzania biashara ya mirungi ni haramu nchini Uganda inauzwa kama mchicha sokoni.
  9. Pamoja na kutokuwa na uhuru katika masuala ya kiasiasa, wananchi wake wako huru zaidi ya Watanzania wanavyowafikiria.
  10. Wakati Tanzania sinema na majarida ya ngono yanauzwa kwa kificho Tanzania jijini Kampala humwagwa hadharani huku watu wakijichagulia.
  11. Wakati polisi huwasumbua machangudoa na mashoga nchini Tanzania wenzetu Waganda kwao ni jambo la kawaida kujiuza na ushoga.
  12. Wakati nchini Tanzania kwa wastani kila baada ya kilomita 200 za Lami kuna mzani barabarani nchini Uganda madereva ambao hawajawahi kutoka nje ya nchi yao mzani wa kupima magari kwao ni kitendawili.
  Itaendelea…………………………………………………………………………..
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  13. Wakati starehe kwa tanzania inaonekana ni kukaa tu baa tena zilizojaa uswahili na kula kiti moto hususan dsm, uganda wao ni "party animals".kumbi za disco za kumwaga, bar za maana...na kwa wale wanaopenda miziki ya zamani ya 70sn 80s na 90s (old school tracks) kampala ndo penyewe maana wana kumbi za disco zinazopiga miziki hiyo tu usiku mzima.
   
 3. t

  tshaka Member

  #3
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja nifanye research leo jioni kampala!
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,724
  Likes Received: 1,231
  Trophy Points: 280
  wakati tz ni nchi ya nyerere,uganda ilikua nchi ya idd amin,...unabisha sasa
   
 5. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,234
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Ok,tunasubiri outcome.Shukran.
   
 6. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,368
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Wakati tanzania elimu ni gharama uganda ni very cheap.Wakati Tanzania inapiga vita matumizi ya lugha za makabila mashuleni na kwenye media Uganda wanadumisha.Wakati Tanzania inawanyima nguvu za kisiasa na uchumi viongozi wa mila uganda wanawasupport.NITAENDELEA.
   
 7. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 15,872
  Likes Received: 3,139
  Trophy Points: 280
  Anjenwaa .................
   
 8. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bangi je ruksa huko?
   
 9. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  &amp;lt;br /&amp;gt;&lt;br /&gt;<br />
  &amp;lt;br /&amp;gt;&lt;br /&gt;<br />
  nadhani ni ruksa maana wanavuta na hawakamatwi. Istoshe Uganda wavuta bangi na wavuta sigara sio wengi kama ilivyo Tanzania. Na inasemekana kuwa hali hii inachangiwa na aina ya chakula wanachotumia ambacho ni ndizi kina vitamin B6 na B12 pia kuna madini ya potasiamu na magineziamu ambayo hupunguza uteja. Zaidi kujua faida za ndizi soma hapa http://www.best-reviewer.com/best-review-top-20-amazing-health-benefits-bananas.htm
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,616
  Likes Received: 21,246
  Trophy Points: 280
  Interesting thread....
   
 11. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tena kumbi zao za starehe unaingia bure bila kuliupia na kuna kumbi nyingine watu wanacheza uchi
   
 12. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tena wanaongea kiganda kwa kwenda mbele
   
 13. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 503
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 80
  Iholomela uliyosema ni kweli tupu,kitu kingine ni nadra kusikia nyimbo za kikongo/hakuna au bendi zenye muelekeo wa muziki huo wao ni raga tu..
   
 14. i411

  i411 JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 795
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  kokote nitakwenda lakini bongo ndo nyumbani, kujichanganya kwetu kiaina kuna faida zake na hasara zake. lakini yote uliyosema nazani faida ni nyingi za maisha ya kibongo, kama uamini kajichanganye kwingine upeleke uswahili uone utakavyojichokea mapema.
   
Loading...