Mambo 10 yaliyopo Ulaya, hasa hasa Sweden, pengine kwako ni mageni, na ungependa kuyafahamu

FAJES Mbona hujawaambia kwamba mtoto unapompeleka mtoto dagis (daycare) unampeleka yeye tu kama yeye, labda na kanguo ka kumbadilisha tu ila mahitaji yake mengi yooooote mpaka diapers atapata huko huko?
 
Wadangaji sina experience nao ila itakuwa kwa kiasi kidogo maana karibia kila mtu ana uwezo wa kujiingizia kipato. Kuhusu biashara ya ngono, Kwa Sweden, anayenunua ni kosa, ila anayetoa huduma (Mwanamke) si kosa kwake. Huwa sijui mantiki ya hii sheria kwamba Mwanamme anakuwa guilt ila Mwanamke hawi guilt kwenye prostitution. Kwa Uholanzi kujiuza ni haki ya kila mtu. Kuna sehemu kabisa huko Amsterdam wana-mama waakuwa kwenye jumba lenye vioo wanajiuza kama unavyoona bidhaa kwenye maduka.
Inaitwa Red light street
 
Wakuu, heshima kwenu.!

Kama ilivyo ada, JF ni kisima cha habari, stories, ucheshi na mengineyo. Ili kuifanya JF iendelee kuwa kisima cha taarifa, naomba nami leo ku-share mawili matatu kuhusu mada tajwa hapo juu.

1) Kwa muda wote niliopo huku, miaka mitatu sasa, nimesafiri na kutembea maeneo mbalimbali. Safari za muda mrefu na fupi. Kwakweli sijawahi kushuhudia ajali ya barabarani. Simanishi kuwa ajali hazipo kabisa, ila ni kwa kiwango kidogo sana. Kwa mujibu wa utafiti wangu mfupi usio rasmi, nimegundua hii inatokana na sababu zifuatazo,

i) Leseni za udereva zinatolewa kwa njia ambayo ipo high secured. Yaani hata kama una leseni ya bongo, na una experience ya kuendesha kwa miaka 10, lazima ufanyiwe majaribio kabla ya kupewa leseni ya huku. Endapo utakosea hata kosa moja tu wakati wa majaribio, mfano kuchelewa kuwasha indicator kabla ya kukata kona, au ukaendesha gari huku umeegesha mkono dirishani kama ifanyikavyo bongo, hakika hautapewa leseni na inabidi urudie tena majaribio. Aidha, leseni mpya zinatolewa kwa mafunzo ambayo lazima uwe very compentent. Kwa ufupi wakuu ni kwamba, leseni hazitolewi kama njugu.

ii) Ikibainika umeendesha gari huku umekunywa pombe kwa kiasi kisichoruhusiwa, fine yake inaweza kukaribia nusu ya kipato chako cha mwezi. Kuna baadhi ya magari, hususan magari ya makampuni, ili uweze kuliendesha, lazima ufanye test ya kucheki kama umekunywa pombe. Usipofanya hiyo test ambayo ipo kwenye mfumo wa gari, hiyo gari haitoondoka wala kuwaka.

iii) Magari yote yanayotembea barabarani lazima yakaguliwe kila mwaka ili kujua kama bado yanakidhi vigezo vya kuwa barabarani.

iv) Njia nyingi hasa high way, ni one-way. Hizi ni barabara hasa zinazotoka mji mmoja kwenda mwingine. Baadhi ya miji, hata barabara za ndani zina mfumo huu. Yaani magari yanayoenda upande mmoja hayakutani na yanayokuja upande mwingine. Madereva wanafahamu nachomaanisha.

v) Barabara zina standard kiwango cha juu. Yaani ikitokea uharibifu tu mahala, haraka sana inafanyiwa marekebisho.

2) Kwa muda wa miaka mitatu sasa, tangu niwepo huku (Sweden na Uholanzi), hakuna hata sekunde moja ambapo umeme na maji vimekatika. Hebu imagine huko Kilosa, Ileje, Nyapande, Nkasi, Ludewa, Liwale, Ngara, Uvinza, Makete kuwe na access ya umeme na maji ndani ya nyumba 24 hours/7 days. Maisha yangekuwaje? Raha si raha? Ha ha haa.!

3) Intrnent ni huduma muhimu kwa kila nyumba kama ilivyo umeme na maji. Namanisha kuwa, kila nyumba imeungunishiwa mfumo wa kupata internet.

4) Huduma za Elimu na Afya kwa Sweden ni bure. Elimu kwa Uholanzi unalipia kidogo, ila siyo gharama kubwa kivile.

5) Sweden ukiwa mgonjwa ukapelekwa hosp unapatiwa na huduma ya chakula. Ni bure, haulipii. Muhimu uwe mkazi au raia. Pesa zinatoka kwenye Tax unayolipa. Hapa ndipo kuna hoja kwamba, wanalipa Tax kubwa, mfano kwenye mji ambao huwa naishi, Tax ni almost 30% ya kipato chako.

5) Shughuli zote zimewekwa kwenye mfumo rasmi chini ya makampuni. Kwa ufupi hakuna eti ile kusema hii kazi i.e anapewa fundi locally na kuanza kujenga kwa kuwatafuta vibarua mtaani kienyeji. Namanisha kuwa, kila kazi, iwe ni kupanda maua, kupaka rangi, usafi, kusafisha vioo kwenye majumba n.k zipo kwenye mfumo rasmi. Na kila anayefanya kazi anaajiriwa katika mfumo rasmi. Nadhani hii njia inafanya hizi nchi za wenzetu kila mtu kuhakikisha analipa kodi.

6) Kila anayeajiriwa, hata iwe non-professional job, kwa kiasi kikubwa, mshahara anaolipwa mtu unamwezesha kukidhi maisha katika standard ya kawaida. Yaani anaweza kula chakula, kulipia rent, usafiri, n.k kwa mwezi mzima na akabakisha chenji kidogo. Nasisitiza kuwa ni kwa kiasi kikubwa, kulingana na uexperience niliyonayo. Huenda kuna baadhi ya kazi (zitakuwa chache sana) mtu anaweeza kulipwa below the standard. Wenzetu wana standard za mishahara kwa nchi nzima. Siyo kila mtu kujipangia tu.

7) Train na mabasi ya Public ndani na nje ya mji yana ratiba zinazofahamika. Mfano, kila baada ya robo saa gari inapita kwenye kituo. Kuwe na abiria ama hakuna abiria muda ukifika basi lazima liondoke/kusafiri kama ilivyopangwa. Hii ni kwa sababu, Serikali ina- provide subsdy kwenye sekta za usafiri. Kwahiyo kama kampuni itapata hasara, serikali inafanya ku-top up ili sekta hiyo iendelee ku-survive.

8) Hakuna masuala ya mfanyakazi wa ndani kumuangalia mtoto ama mtu mzee kama bongo. Hii ni kwa sababu, mama akijifungua, mama anapewa maternity leave na baba anapewa partenity leave ambapo kwa ujumla wake vikichanganywa inafikia mwaka mmoja. Hivyo mtoto atalelewa na wazazi mpaka afikishe mwaka mmoja. Baada ya hapo anapelekwa kwenye baby care center ambako anapelekwa asubuhi na kuchulkuliwa mchana. Kwa Wazee, akishafikisha umri wa kutojiweza, anapelekwa kuhudumiwa kwenye community center ambako pension yake itatumika kumuhudumia.

9) Kiwango cha ukosefu wa ajira ni kiasi kidogo sana. Yaani si rahisi kukuta mkazi yupo home muda mrefu bila kazi yoyote. Sisemi kuwa hakuna wasiokuwa na ajira, ila ni kwa kiasi kidogo sana. Suala la gharama za maisha ni jukumu la baba na mama. Sio kama sisi eti kazi ya kutafuta mahitaji ni suala la baba peke yake. Huku suala la usawa linafanyika kwa vitendo. Hii mada ya usawa nitaijadili siku nyingine.

10) Pamoja na kodi kubwa wanayokatwa (atleast 30%), ila jamaa wanafaidi sana kodi yao. Yaani unakuta Serikali inampatia mzazi kiasi flani cha pesa kwa ajili ya huduma ya mtoto anapozaliwa mpaka anapokuwa mkubwa. Ha ha haa. Kwa lugha fupi ni kuwa, kila mtoto analipwa kiasi flani cha pesa mpaka afikishe umri mkubwa. Siyo kiasi kikubwa, ila kinamwezesha kuishi.

Kwa leo naomba niishiea hapa. Leo nimezungumzia upande wa +ve side, siku nyingine nitazungumzia -ve side pia. Haya niliyosema simanishi kuwa nchi za Ulaya wanaishi kama Mbinguni, na kwenyewe kuna shida zake nyingi tu.

Kama kuna mahala nimeteleza kidogo, basi ni sahihi kukosolewa na kurekebisha jambo ambalo naweza kuwa nime-overlook. Ila nilichokisema kina uhalisia mkubwa zaidi ya 90% maana ni mambo niliyoyaona na kusimuliwa.

NB: Siasa za huku kwa kiasi kikubwa, zimejikita kwenye sera za kupunguza wahamiaji ( Yaani malalamiko kuwa wahamiaji ni wengi yamekuwa makubwa sana miongoni mwa raia). Siasa nyingine zimejikitia kwenye masuala ya mabadilkiko ya Tabia ya nchi (Climate change). Yaani sisi Afrika tukiwa tunataka labda kuandamana kwa ajili ya kupatiwa huduma za msingi za maisha, huku wenzetu wameanza kuandamana kushinikiza Serikali zao zichukuwe hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi . Naomba hii iwe mada ya siku nyingine pia.

Ahsanteni.
Wenzetu wanaishi sisi tunasurvive
 
Ndiyo kwa Sweden mtoto akiwa na miaka 15 anaruhusiwa kuanya mapenzi na mtu wa rika lake. Isipokuwa kunasheria inayowalinda wasiwe kwenye mahusiano na mtu mzima. Japo watoto wengi wa shule hasa Sweden wanaanya sana mapenzi na rika lao pia vijana walio kwenye miaka ishirini na kitu.
Kuna wakimbizi wengi toka Middle East. Hawa wamekuwa wanawapitia sana vibinti vya shule. Watoto wengi wameharibika wakiwa shule wanavuta sigara na bangi. Kwao wanaweza wasielewe au wakaelewa lakini mtoto ndo anamaamuzi. Kuna sheria watoto chini ya miaka 18 hawezi nunua sigara au pombe dukani. Lakini wapo wengi sana wananunua kwa kuwatumia vijana wakubwa kwenye miaka 20 na kitu. Kisha uvuta nao na hata kunywa pombe nao. Mida ya jioni yanayoendelea ni aibu. Hawaoni shida kukuta wanasex kwenye Park, shuleni maeneo ya kupumzika na hata kanisani maliwatoni, au ktk lounge.

Watoto wengi hasa hao ma teenager, wanapenda sana kuchill, sigara haziwatoki midomoni, kuna baadhi uacha shule wakipenda kujirusha kwanza na maisha.
Siku za mwanzo jambo la kwanza kabisa lililonishangaza ni kuona namna wasichana wanavuta sigara kwa kiasi kikubwa. Nikadhani baridi inachangia ila naona imekuwa kama culture. Pombe pia wanapiga si mchezo. Japo si za kulewa. Uzuri Mkuu, kwa Sweden huwezi kununua pombe kama unavyopenda. Kuna maduka maalumu ya kununua pombe. Nadhani wangeacha iwe huru nguvu kazi ingeathirika sana kwa watu kunywa pombe na kushindwa kufanya kazi.

Kuhusu Sex mkuu naona pia ni kama culture sasa. Yaani wao wanafundishwa masuala ya reproductive health wakiwa bado wadogo. Hii ina advantages na disadvantages pia. Ndio maana kufanya abortion ni legal na haki ya mwanamke hata bila ridhaa ya Mzazi au Mpenzi wake. Maana huwezi kumuona binti mdogo mjauzito. Nadhani abortion na exposure ya early reproductive health vinawasaidia sana. Lasivyo kungekuwa na mimba nyingi za utotoni.
 
FAJES Mbona hujawaambia kwamba mtoto unapompeleka mtoto dagis (daycare) unampeleka yeye tu kama yeye, labda na kanguo ka kumbadilisha tu ila mahitaji yake mengi yooooote mpaka diapers atapata huko huko?
Mkuu ujue huwa nikisoma comments nyingi huko Quora wanapasifia sana Sweden kwa kuwa na system bora zaidi Duniani ya kulea mtoto na maternity + peternity leave. Ila kwakweli wapo juu sana. Yaani unazaa mtoto unapewa pesa na Serikali za kumtunza mtoto mpaka anakuwa mkubwa. Duh. Japo kodi ni kubwa ila wananufaika sana. Ndio maana Waarabu wa Asia, Wasomalia, Ethiopians na Eritreans wanachangamkia fursa hiyo. Unakuta wanazaa watoto wengi mpaka inakuwa tishio kwa wazawa wenye nchi yao. H aha haaa.
 
Mbona ndugu zetu Wasomali hujawataja?😁😁
Yani hayo mataifa wamefanya kuzaa kama mtaji. Hawajihangaishi kusoma hata SFI tu wala kutafuta kazi. Wanasubiria hela za social na monthly allowance za watoto.😏

Tukirudi kwenye issue ya watoto (kuanzia maternity/paternity leave, daycare, shule etc)na kama mmoja wa watu waliofaidi hiyo system kama mtoto na kama mzazi, acha tu wasifiwe kwasababu they deserve it!!! Na kodi wakate tu maana social services zote zinazotolewa na serikali ni FIRST CLASS. Hakuna longolongo wala ubabaishaji.
 
Umenikumbusha kitu mkuu. Ile kitu nyingine inaitwa tax return. Nyinyi wenye kazi za kudumu na uhakika wa kuishi Sweden on permanent basis unaweza usiielewe vizuri hii kitu faida yake maana mnapata return kidogo huenda isifike hata 1000kr. Ila ukifanya kazi za vibarua na ukawa hauna kazi ya permanent unaweza kupata tax return hadi 20,000 kr. Kwakweli Wazungu acha waitwe Wazungu tu. Japo ssi Waafrika tunawarushia sana mawe Wazungu ila mie huwa naita hizo ni chuki binafsi na athari za kung'ang'ania historia za ukoloni tu. Ila jamaa wapo mbali sana kwenye systems za kuendesha maisha ya mwanadamu, ukiachana na changamoto za hapa na pale.
 
Ndugu yangu katika hiyo namba 2 Hadi chozi la huzuni limenitoka. Hapa tulipo CCM wametukatia maji tokea 26/10/2021 hadi leo hii 20/11/2021 hakuna dalili ya maji kutoka yaani ni changamoto tupu.

Imagine ndugu yangu tunatamanije kuwa katika taifa lenye maisha ya pepo kama hilo?! Kwa maisha tunayoishi hapa Tanzania kiukweli kama kuna kwenda mbinguni au motoni basi watanzania nadhani tumeshatumikia 80% ya adhabu maana hawa wajaalaaana wanachofanya watajibia siku ya kiama mbwa hawa MUNGU mwenye neema awalaani wote.
taratibu kaka karibu sweden tubebe boksi, huku Kalmar kamji kadogo kusini huku, ni peponi kwa ujumla
 
Mbona ndugu zetu Wasomali hujawataja?😁😁
Yani hayo mataifa wamefanya kuzaa kama mtaji. Hawajihangaishi kusoma hata SFI tu wala kutafuta kazi. Wanasubiria hela za social na monthly allowance za watoto.😏

Tukirudi kwenye issue ya watoto (kuanzia maternity/paternity leave, daycare, shule etc)na kama mmoja wa watu waliofaidi hiyo system kama mtoto na kama mzazi, acha tu wasifiwe kwasababu they deserve it!!! Na kodi wakate tu maana social services zote zinazotolewa na serikali ni FIRST CLASS. Hakuna longolongo wala ubabaishaji.
Itakuwa unamiaka zaidi ya 10 huko Sweden, Mkuu
 
Umenikumbusha kitu mkuu. Ile kitu nyingine inaitwa tax return. Nyinyi wenye kazi za kudumu na uhakika wa kuishi Sweden on permanent basis unaweza usiielewe vizuri hii kitu faida yake maana mnapata return kidogo huenda isifike hata 1000kr. Ila ukifanya kazi za vibarua na ukawa hauna kazi ya permanent unaweza kupata tax return hadi 20,000 kr. Kwakweli Wazungu acha waitwe Wazungu tu. Japo ssi Waafrika tunawarushia sana mawe Wazungu ila mie huwa naita hizo ni chuki binafsi na athari za kung'ang'ania historia za ukoloni tu. Ila jamaa wapo mbali sana kwenye systems za kuendesha maisha ya mwanadamu, ukiachana na changamoto za hapa na pale.
I can imagine mtu unavyochekelea kama ukirudishiwa kiwango kikubwa hivyo.🤗🤗

Wenzetu wanaelewa kwamba kuna watu ambao ,ndio wamelipa tax, ila kutokana na kipato chao hawakupaswa kulipa that much. Yani system yao inam[I]favor[/I] mwananchi kwa kila hali na kila namna. Sisi sasa.....😱😱
 
Ndugu yangu katika hiyo namba 2 Hadi chozi la huzuni limenitoka. Hapa tulipo CCM wametukatia maji tokea 26/10/2021 hadi leo hii 20/11/2021 hakuna dalili ya maji kutoka yaani ni changamoto tupu.

Imagine ndugu yangu tunatamanije kuwa katika taifa lenye maisha ya pepo kama hilo?! Kwa maisha tunayoishi hapa Tanzania kiukweli kama kuna kwenda mbinguni au motoni basi watanzania nadhani tumeshatumikia 80% ya adhabu maana hawa wajaalaaana wanachofanya watajibia siku ya kiama mbwa hawa MUNGU mwenye neema awalaani wote.
Pamoja na shida zote hizi bado group letu tulivyokuwa huko wote tulikumbuka bongo.
 
iii) Magari yote yanayotembea barabarani lazima yakaguliwe kila mwaka ili kujua kama bado yanakidhi vigezo vya kuwa barabarani.
Hapa kwetu yanakaguliwa yakiwa nyumbani na ithibati inatolewa hata mkiwa bar
 
Back
Top Bottom