Elections 2015 Mambo 10 niliyojifunza 'sanaa za maonyesho' za Lowassa - Arusha

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
lowasa5.jpg
Aamonduli8.jpg

Alalamika alimsaidia Kikwete Kampeni za urais lakini sasa yeye ametoswa

MAMBO 10 NILIYOJIFUNZA KWENYE "SANAA ZA MAONESHO" ZA LOWASSA.


By Malisa GJ,

1. Asilimia zaidi ya 90% ya watu waliokuwepo uwanjani wamegharamiwa. Bodaboda walilipwa, Wanafunzi walisafirishwa, Waandishi walilipwa. Wachache walioenda kwa hiari yao walienda kushangaa tu wala sio mashabiki wa Lowassa. This is to say ikiwa Lowassa asingetumia pesa huenda uwanjani angekua yeye na familia yake tu.

2. Wengi wanaomuunga mkono Lowassa ni "opportunists". Ni watu wanaotegemea akiingia madarakani awakumbuke. Either awape vyeo au awape unafuu kwenye biashara zao. Hakuna yeyote kwny kundi la Lowassa anayemuunga mkono kwa lengo la kuisaidia nchi.

3. Afya ya Eddo imedhoofu sn kuweza kuwa Rais wa nchi. Alipoingia uwanjani ameshindwa kupanda ngazi za jukwaa, akasimama katikati ya ngazi kwa dakika chache kabla ya kusaidiwa kupanda. Pia anaongea kwa Shida, na mikono yake haina nguvu. Hali hii imesababisha ashindwe kushika microphone alipopewa "mike" na Kibonde.

4. Mkutano wa Lowassa leo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Kuna watu wamepata hela ya kulipa mahari kupitia mkutano huu, kuna waliopata mitaji ya kukuza biashara zao na kuna waliopata lift za bure za kwenda Arusha kufanya mambo yao. Hii inaitwa "mbwa kala mbwa"

5. Kutokana na maelezo ya Eddo ni wazi kuwa ana "bifu" na JK. Amekiri kuwa alimpigania sn Kikwete 1995 na 2005 lakini inavyoonekana JK amemsaliti.

6. Akiingia madarakani atalipiza kisasi kwa wabaya wake wote hasa Samuel Sitta, Anthony Diallo na vibaraka wao wote. Ikiwa Eddo atashinda kuna dalili Sitta, Dialo, Makonda, na vibaraka wengine wa CCM wakaishia jela.!

7. Mkutano wa leo ulikua ni mkwara wa kuionesha Kamati kuu ya chama chake kuwa ana nguvu kiasi gani, ili wasijaribu kabisa kukata jina lake wakihofia kukipasua chama.

8. Safari ya matumaini ni safari ya matamanio. Au unaweza kuiita safari ya matumizi. Huwezi kutumia 1.4 bilion for just a single day wakati kuna watu wanakufa kwa kukosa "padadol" ya shilingi mia halafu ukasema ni matumaini. Labda matumaini ya kuuza nchi.!

9. Ikiwa Eddo atashinda Yuko tayari kutumia rasilimali za nchi ili kulipa fadhila kwa rafiki zake waliomuunga mkono wakati wa kugombea. Kwa mfano yupo tayari kumgawia Mengi vitalu vya gesi Mtwara na kuwaacha watanzania wasinufaike na gesi yao kisa tu Mengi alimpa support kwny kugombea.

10. Lowassa ni msanii mzuri wa sanaa za maonesho. Ametumia makundi yote mawili ktk kufanikisha azma yake. Kundi la Maskini na kundi la matajiri.Ametumia maskini kwa kuwaahidi kuwa atawabana matajiri walipe kodi ili kuboresha maisha ya maskini.

Na ametumia matajiri akiwaahidi kuwa atawabana maskini ili wasipige kelele wakati anawagawia matajiri rasilimali za nchi. Hii ni sanaa. Ha hakika hapa Eddo ameitumia vizuri elimu yake ya sanaa ya chuo kikuu cha Dar es Salaam. (B.A in Fine &Perfoming Arts).!

NB: Watanzania hawawezi kuruhusu kumpa nchi hii "msanii". Nchi hii inatakiwa kuongozwa na mtu "real". Na mtu real hawezi kupatikana kwingine nje ya UKAWA.!

#SAY_NO_TO_SANAA
#SAY_NO_TO_CCM
#BE_REAL . #VOTE_FOR_UKAWA .
 
"Watanzania bado ni kichwa cha mwendawazimu kila msusi anataka kujifunzia vichwani mwao aina ya misuko..."

Uko sahihi, hata baadhi ya wabunge walioonekana kuunga mkono juhudi za upinzania bungeni kama akina Kangi Lugora leo yupo bega kwa bega na Fisadi Papa Lowasa, hii haiingii akilini mwangu na pengine ni kitu kinachotufanye tushindwe kujenga hali ya kuwaamini wanasiasa hasa wabunge mle mjengoni wanachofanya ni kwa masilahi binafsi si kwa moyo wa kujenga nchi.
 
Lowassa hawezi pewa hii nchi.....

CCM is dying!!!

Wanasiasa na wabunge wanaomwunga mkono Lowasa ni wale ambao hawakuonwa au kupata promotion kwa Kikwete, hivyo kichocheo ni kwa masilani ya nchi bali masilani binafsi. Hiyo inaonekana revange dhidi ya Kikwete. Lakini jambo la kushangaza wengi wanaomwunga mkono Lowasa hawamo kwenye kamati kuu au halmashauri kuu ya CCM. Watamteteaje Lowasa wakati hawaingii Halmashauri na kamati kuu?
 
Wanasiasa na wabunge wanaomwunga mkono Lowasa ni wale ambao hawakuonwa au kupata promotion kwa Kikwete, hivyo kichocheo ni kwa masilani ya nchi bali masilani binafsi. Hiyo inaonekana revange dhidi ya Kikwete. Lakini jambo la kushangaza wengi wanaomwunga mkono Lowasa hawamo kwenye kamati kuu au halmashauri kuu ya CCM. Watamteteaje Lowasa wakati hawaingii Halmashauri na kamati kuu?

Ngoja tusubiri muda utatuambia....
 
Iv kwa gharama alizotumia mpaka sasa za kujinad toka ameanza, akikosa urais si atakufa kwa bp mtu huyu?

Kutangaza kuwashughulikia walio kinyume chake kama akina Sitta na wengine mbona ameshaweka ufa mkubwa katu halizibiki, naona hana washauri wazuri.
 
Iv kwa gharama alizotumia mpaka sasa za kujinad toka ameanza, akikosa urais si atakufa kwa bp mtu huyu?

yetu macho mkuu!! kwani anafanya usanii kwenye jumba la sanaa!! Anawatishia wachina kwa kuruka samasoti, tena zile za kushika na mikono chini unajibinuaaa!!!!!!!!!!!
 
Sitashangaa kuona anaingia Msituni. Ameshatumia hela nyingi sana na wengi wameshakula hela yake nyingi.

Atakusanya wamasai na sime zao vijijini wakee macho maana hawa wameshalalamikiwa sana kuvamia vijiji vya wakulima.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom