Mambo 10 niliyojifunza 'sanaa za maonyesho' za Lowassa - Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo 10 niliyojifunza 'sanaa za maonyesho' za Lowassa - Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Candid Scope, May 30, 2015.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]
  Alalamika alimsaidia Kikwete Kampeni za urais lakini sasa yeye ametoswa

  MAMBO 10 NILIYOJIFUNZA KWENYE "SANAA ZA MAONESHO" ZA LOWASSA.


  By Malisa GJ,

  1. Asilimia zaidi ya 90% ya watu waliokuwepo uwanjani wamegharamiwa. Bodaboda walilipwa, Wanafunzi walisafirishwa, Waandishi walilipwa. Wachache walioenda kwa hiari yao walienda kushangaa tu wala sio mashabiki wa Lowassa. This is to say ikiwa Lowassa asingetumia pesa huenda uwanjani angekua yeye na familia yake tu.

  2. Wengi wanaomuunga mkono Lowassa ni "opportunists". Ni watu wanaotegemea akiingia madarakani awakumbuke. Either awape vyeo au awape unafuu kwenye biashara zao. Hakuna yeyote kwny kundi la Lowassa anayemuunga mkono kwa lengo la kuisaidia nchi.

  3. Afya ya Eddo imedhoofu sn kuweza kuwa Rais wa nchi. Alipoingia uwanjani ameshindwa kupanda ngazi za jukwaa, akasimama katikati ya ngazi kwa dakika chache kabla ya kusaidiwa kupanda. Pia anaongea kwa Shida, na mikono yake haina nguvu. Hali hii imesababisha ashindwe kushika microphone alipopewa "mike" na Kibonde.

  4. Mkutano wa Lowassa leo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Kuna watu wamepata hela ya kulipa mahari kupitia mkutano huu, kuna waliopata mitaji ya kukuza biashara zao na kuna waliopata lift za bure za kwenda Arusha kufanya mambo yao. Hii inaitwa "mbwa kala mbwa"

  5. Kutokana na maelezo ya Eddo ni wazi kuwa ana "bifu" na JK. Amekiri kuwa alimpigania sn Kikwete 1995 na 2005 lakini inavyoonekana JK amemsaliti.

  6. Akiingia madarakani atalipiza kisasi kwa wabaya wake wote hasa Samuel Sitta, Anthony Diallo na vibaraka wao wote. Ikiwa Eddo atashinda kuna dalili Sitta, Dialo, Makonda, na vibaraka wengine wa CCM wakaishia jela.!

  7. Mkutano wa leo ulikua ni mkwara wa kuionesha Kamati kuu ya chama chake kuwa ana nguvu kiasi gani, ili wasijaribu kabisa kukata jina lake wakihofia kukipasua chama.

  8. Safari ya matumaini ni safari ya matamanio. Au unaweza kuiita safari ya matumizi. Huwezi kutumia 1.4 bilion for just a single day wakati kuna watu wanakufa kwa kukosa "padadol" ya shilingi mia halafu ukasema ni matumaini. Labda matumaini ya kuuza nchi.!

  9. Ikiwa Eddo atashinda Yuko tayari kutumia rasilimali za nchi ili kulipa fadhila kwa rafiki zake waliomuunga mkono wakati wa kugombea. Kwa mfano yupo tayari kumgawia Mengi vitalu vya gesi Mtwara na kuwaacha watanzania wasinufaike na gesi yao kisa tu Mengi alimpa support kwny kugombea.

  10. Lowassa ni msanii mzuri wa sanaa za maonesho. Ametumia makundi yote mawili ktk kufanikisha azma yake. Kundi la Maskini na kundi la matajiri.Ametumia maskini kwa kuwaahidi kuwa atawabana matajiri walipe kodi ili kuboresha maisha ya maskini.

  Na ametumia matajiri akiwaahidi kuwa atawabana maskini ili wasipige kelele wakati anawagawia matajiri rasilimali za nchi. Hii ni sanaa. Ha hakika hapa Eddo ameitumia vizuri elimu yake ya sanaa ya chuo kikuu cha Dar es Salaam. (B.A in Fine &Perfoming Arts).!

  NB: Watanzania hawawezi kuruhusu kumpa nchi hii "msanii". Nchi hii inatakiwa kuongozwa na mtu "real". Na mtu real hawezi kupatikana kwingine nje ya UKAWA.!

  #SAY_NO_TO_SANAA
  #SAY_NO_TO_CCM
  #BE_REAL . #VOTE_FOR_UKAWA .
   
 2. cesallinho

  cesallinho Member

  #2
  May 30, 2015
  Joined: Jul 11, 2013
  Messages: 94
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  "Watanzania bado ni kichwa cha mwendawazimu kila msusi anataka kujifunzia vichwani mwao aina ya misuko..."
   
 3. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2015
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,800
  Likes Received: 10,383
  Trophy Points: 280
  Lowassa hawezi pewa hii nchi.....

  CCM is dying!!!
   
 4. Black Book

  Black Book JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2015
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 209
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Sidhan kama hayo umejifunzia kwenye mkutano.....Kakojoe ulale sasa!!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Uko sahihi, hata baadhi ya wabunge walioonekana kuunga mkono juhudi za upinzania bungeni kama akina Kangi Lugora leo yupo bega kwa bega na Fisadi Papa Lowasa, hii haiingii akilini mwangu na pengine ni kitu kinachotufanye tushindwe kujenga hali ya kuwaamini wanasiasa hasa wabunge mle mjengoni wanachofanya ni kwa masilahi binafsi si kwa moyo wa kujenga nchi.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Wanasiasa na wabunge wanaomwunga mkono Lowasa ni wale ambao hawakuonwa au kupata promotion kwa Kikwete, hivyo kichocheo ni kwa masilani ya nchi bali masilani binafsi. Hiyo inaonekana revange dhidi ya Kikwete. Lakini jambo la kushangaza wengi wanaomwunga mkono Lowasa hawamo kwenye kamati kuu au halmashauri kuu ya CCM. Watamteteaje Lowasa wakati hawaingii Halmashauri na kamati kuu?
   
 7. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2015
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,800
  Likes Received: 10,383
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri muda utatuambia....
   
 8. E

  Earthmover JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2015
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 13,955
  Likes Received: 4,002
  Trophy Points: 280
  ...

  .....ange mwaga mapesa kama askofu
   
 9. kichwa kikubwa

  kichwa kikubwa JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2015
  Joined: Sep 24, 2013
  Messages: 948
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 80
  Iv kwa gharama alizotumia mpaka sasa za kujinad toka ameanza, akikosa urais si atakufa kwa bp mtu huyu?
   
 10. PATOXIC

  PATOXIC Member

  #10
  May 30, 2015
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Da hii nchi hatuko serious Leo Lowassa kawa Lulu?
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kutangaza kuwashughulikia walio kinyume chake kama akina Sitta na wengine mbona ameshaweka ufa mkubwa katu halizibiki, naona hana washauri wazuri.
   
 12. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2015
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,099
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 145
  mwizi mkubwa huyu
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2015
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,754
  Likes Received: 14,551
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa hii makala kumbe ni yule Masawe Melisa anaye muabudu Slaa na Mbowe.....sijaona cha maana hapo bali hadithi za Bavicha...
   
 14. P. Majaribu

  P. Majaribu JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2015
  Joined: Jun 2, 2014
  Messages: 1,201
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Watanzania wengi bado ni vichwa maji,huyu bwana leo anaonekana ni mwema
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kumbe Lowasa ni mhitimu chuo Kikuu Dar kwa shahada ya sanaa za maonyesho? Sasa anatumia vizuri elimu ya sanaa za maonyesho kwenye kampeni zake za kisanii.
   
 16. w

  white wizard JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2015
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,517
  Likes Received: 827
  Trophy Points: 280
  yetu macho mkuu!! kwani anafanya usanii kwenye jumba la sanaa!! Anawatishia wachina kwa kuruka samasoti, tena zile za kushika na mikono chini unajibinuaaa!!!!!!!!!!!
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Jibu hoja alizoziibua si mipasho. Jenga utetezi wa hoja zako kumtetea Lowasa na nasubiri hoja zako zinisaidie kumwelewa vizuri Lowasa.
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2015
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,754
  Likes Received: 14,551
  Trophy Points: 280
  Masawe twambie afya ya Slaa
  ..
   
 19. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2015
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,373
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sitashangaa kuona anaingia Msituni. Ameshatumia hela nyingi sana na wengi wameshakula hela yake nyingi.
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa hatujasikia kwamba anakududia kugombea urais wala kutangaza nia, ikitokea hapo ndipo ulete swali kama hilo. Kwa sasa tunamjadili aliyetangaza kugombea urais Edward Ngoyai Lowasa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...