Mambo 10 muhimu ya kuzingatia ili kupunguza gharama za ujenzi

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,697
Watu wengi wamejikuta katika hali ngumu ya kifedha au hata kukwama katika ujenzi kutokana na kushindwa kuweka mikakati mizuri ya kupunguza gharama za ujenzi.

Kwa kutambua umuhimu wa ujezi, na kwa kutambua kuwa ujenzi ni jambo linalogharimu fedha nyingi; nimeona ni vyema nikushirikishe mambo 10 muhimu unayoweza kuyazingatia ili uweze kupunguza gharama za ujenzi.

1. Chagua kiwanja bora
Uchaguzi sahihi wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi ni jambo muhimu sana. Watu wengi hujikuta wakitumbukia kwenye gharama kubwa za ujenzi kutokana na uchaguzi duni wa kiwanja.

Hebu fikiri ukinunua kiwanja sehemu ambayo ni mkondo wa maji au udongo wake unatitia; hili litakulazimu kutumia gharama kubwa zaidi ili kukifanya kiwanja hicho kifae kwa ujenzi, gharama ambazo zingeweza kuokolewa kama ungefanya uchaguzi sahihi wa kiwanja.

2. Chagua ramani nzuri na rahisi
Ni wazi kuwa watu wengi wanajenga nyumba kila kukikucha lakini siyo wote wanaojenga nyumba zenye ramani sahihi na bora.

Pamoja na sababu kuwa suala hili linatokana na ukosefu wa elimu sahihi juu ya masuala ya ujenzi; ramani mbaya huwagharimu watu wengi fedha nyingi na mwishowe haziwapi nyumba walizozihitaji.

Kwa mfano; ramani za nyumba za Ulaya (Hasa maeneo ya baridi) huwezi kuzijenga kwenye maeneo ya Afrika yenye joto. Inaweza kuwa ni ramani nzuri sana lakini ikawa na vitu vingi vinavyoongeza gharama zisizokuwa za msingi. Vivyo hivyo ramani ya rafiki yako inaweza isiwe bora kwako.

Hivyo, hakikisha unachagua ramani nzuri na rahisi ambayo utaweza kuitekeleza vyema bila kukutengenezea mzigo mkubwa wa gharama.

3. Fanya utafiti wa kutosha
Kukurupuka na kuanza kufanya jambo ni suala baya sana. Utafiti katika suala la ujenzi ni jambo muhimu sana litakalokuwezesha kupunguza gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa.

Unapaswa kutafiti yafuatayo:
  • Bei za bidhaa na vifaa vya ujenzi
  • Mafundi bora
  • Vifaa bora na vya bei nzuri
  • Teknolojia za kisasa kwenye ujenzi, n.k.

Ukitafiti kwa kina masuala tajwa hapo juu pamoja na mengine yanayohusiana nayo, kwa hakika utapunguza gharama za ujenzi ambazo zingepotea kutokana na kutokuwa na uelewa sahihi.

4. Tumia vifaa mbadala
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika sekta ya ujenzi, kumekuwepo na vifaa pamoja na malighafi mbalimbali ambazo zinarahisisha ujenzi, zinaokoa gharama za ujenzi pamoja na kulinda mazingira.

Hivi leo zipo mbao maalumu, matofali au hata vifaa vya jamii ya vigae ambavyo vinaokoa gharama za ujenzi maradufu kuliko vifaa vya kawaida. Ikiwa utajikita kutumia vifaa hivi basi utaweza kupunguza gharama zisizo za lazima kwenye ujenzi.

5. Simamia vyema manunuzi na ujenzi
Watu wengi wamejikuta wakipoteza fedha nyingi sana kwenye miradi yao, hasa miradi ya ujenzi kutokana na kukosa usimamizi mzuri.

Niimeona watu wakijenga nyumba kwa simu na kuishia kupata hasara kubwa. Fundi anakuambia leta mifuko 10 ya saruji kumbe ni minne tu inahitajika; fundi anakuambia ametumia kitu fulani kumbe ametumia kilicho dhaifu ili apate pesa yake ya mfukoni.

Ni muhimu kuhakikisha unasimamia manunuzi vyema pamoja na ujenzi kwa ujumla na si kumkabidhi fundi kila kitu.

6. Chagua msimu sahihi wa ujenzi
Siyo kila majira yanafaa kwa ajili ya ujenzi; inakupasa kuchagua msimu sahihi unaofaa kwa ajili ya ujenzi.

Ni wazi kuwa majira kama vile ya mvua nyingi siyo rafiki kwa ujenzi; hii ni kutokana na sababu ya changamoto za usafirishaji wa malighafi za ujenzi pamoja na changamoto ya mafundi kutokuweza kufanya kazi wakati mvua ikinyesha.

Suala hili linaweza kutengeneza gharama za ziada ambazo hazikutarajiwa kama vile kuongezeka kwa gharama za usafirishaji pamoja na ununuzi wa vifaa kama vile turubai; gharama ambazo zingeweza kuepukwa ikiwa msimu wa ujenzi ungechaguliwa vyema.

7. Tafuta fundi sahihi
Hivi leo kuna mafundi wengi, lakini si wote ni mafundi bora. Kwa ajili ya kwenda kwa mazoea au kutokana na kukosa uelewa, watu wengi wamejikuta wakitumia mafundi ambao huwasababishia gharama kubwa za ujenzi.

Hebu fikiri ukifanya kazi na fundi anayekosea kila kitu; ni wazi kuwa kazi itakuwa ni kujenga na kubomoa ili kurekebisha makosa.

Suala hili litakusababishia kutumia pesa nyingi zaidi kwa ajili ya marekebisho; ilihali pesa hizo ungeziokoa kama ungechagua fundi bora.

8. Fanya baadhi ya mambo wewe mwenyewe
Ukiruhusu kufanya kila kitu kwenye ujenzi kwa kutegemea mtu anayehitaji malipo utajitengenezea gharama kubwa sana katika ujenzi wako.

Kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya wewe mwenyewe au wanafamilia wako; mambo kama vile maandalizi ya awali ya kiwanja, kumwagilia maji sehemu iliyojengwa; kukusanya vipande vya mawe au tofali, n.k.

Kwa kufanya mambo kama haya au hata zaidi kulingana na uwezo wako utapunguza sana gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa. Kumbuka! Linda tu usifanye kitu kinachohitaji ujuzi wa kitaalamu usiokuwa nao kwani kinaweza kuleta matatizo makubwa baadaye.

9. Tumia tena malighafi
Kuna kauli isemayo “mafundi ni waharibifu”; mara nyingi mafundi hupenda kutumia vitu hovyo hovyo bila kujali gharama yake.

Mafundi watakata mbao mpya ili tu kupata kipande kidogo wanachokihitaji kuliko kuunga vipande viwili; wanaweza pia kuvunjavunja matofali au kukatakata mabati mapya ili kupata kipande wanachotaka kuliko kutafuta kipande cha zamani kwa ajili ya eneo husika.

Hivyo basi, ili kupunguza gharama za ujenzi, hakikisha unasimamia matumizi ya rasilimali zilizobaki au zilizokwisha kutumika. Vipande vya matofali, mabaki ya mawe, misumari ya zamani, au vipande vya bati vinaweza kutumika sehemu nyingine na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.

10. Zingatia kanuni za ujenzi
Kuna kanuni kadha wa kadha za ujenzi ambazo zisipozingatiwa zinaweza kusababisha hasara kubwa au ongezeko kubwa la gharama za ujenzi.

Masuala kama vile unyeshaji wa sehemu iliyojengwa kwa saruji, uchanganyaji wa saruji, muda wa ujenzi, n.k. Ni baadhi tu ya mambo muhimu sana.

Kwa mfano nyumba isiponyeshwa vizuri ni lazima itapata nyufa na itatengeneza gharama zaidi za marekebisho; kwa mfano pia nyumba ikilazamishwa kujengwa harakaharaka kuliko muda stahiki ni lazima itapata dosari mbalimbali ambazo zitagharimu fedha zaidi kuzirekebisha Na kupelekea Mambo yako kurudi nyuma.
 
Ayo yapo tu ila Kama wakupigwa utachaka tu.

Itoshe kusema Mimi huwa nampatia fundi vifaa akitoa boko halambi hata mia yangu muda mwingine ukatili unasaidia
 
Imeeleweka hii, kwenye kipengele no.9 "Tumia tena malighafi" hii ilishawahi kunifanya kushikana mashati na fundi wangu tukiwa site.
 
Yani tuseme ukweli kama unataka ujenzi mzuri kubali garama tu ukiwa nafundi mzuri inatosha kila kitu atafanya kama yake
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla.Njoo ofisini kwetu TEGETA tukuhudumie kwa gharama nafuu sana:-
2*2 fut12=2500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=5000
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=13500
1*10fut 18 fisher board( treated)=15500
2*4 fut18(treated)=9500
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu
 
Naweza kuunganisha hii nyumba na sijaacha matoleo ILI iwe ya kisasa na Lengo ni kuiongeza chumba cha kulala na dinning room na kupanua jikon, pamoja nipate na store, . Ilivyo kwasasa ndio hivyo Ktk picha na ramani ya sasa ndio hiyo iliyozungushiwa rangi nyekundu na ninavyoitaji iwe ni hiyo ramani ambayo haina rangi
Iwe ya box kama hiyo chini
Msaada kwa wale wataalam na wazoefu Ktk ufundi
IMG-20210430-WA0016.jpg
IMG-20210430-WA0015.jpg
Polish_20210430_125304636.jpg
IMG_20210414_143642_846.jpg
Polish_20210501_020633021.jpg
Polish_20210501_020911361.jpg
 
Attachments

  • IMG-20210430-WA0024.jpg
    IMG-20210430-WA0024.jpg
    77.2 KB · Views: 31
Tunauza mbao kwa bei ya jumla.Njoo ofisini kwetu TEGETA tukuhudumie kwa gharama nafuu sana:-
2*2 fut12=2500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=5000
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=13500
1*10fut 18 fisher board( treated)=15500
2*4 fut18(treated)=9500
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu
Nashitaji Mbao 2x4 Futi
20 zenye dawa. Unazo? Bei gani
 
Naweza kuunganisha hii nyumba na sijaacha matoleo ILI iwe ya kisasa na Lengo ni kuiongeza chumba cha kulala na dinning room na kupanua jikon, pamoja nipate na store, . Ilivyo kwasasa ndio hivyo Ktk picha na ramani ya sasa ndio hiyo iliyozungushiwa rangi nyekundu na ninavyoitaji iwe ni hiyo ramani ambayo haina rangi
Iwe ya box kama hiyo chini
Msaada kwa wale wataalam na wazoefu Ktk ufundiView attachment 1769576View attachment 1769578View attachment 1769579View attachment 1769580View attachment 1769581View attachment 1769582
Aliyekucholea nyumba ya mwanzo vipimo vidogo sana. Anyway badiliasha na kutanua kama unaweza
 
Hiyo iache kama ilivyo itakuwa ya mtumishi aka servant kota. Mbele yake jenga hiyo nyumba ya ndoto yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom