Mambo 10 hatari ambavyo hupaswi kufanya au kurudia katika maisha yako yote!

Apr 18, 2012
95
213
22282112_898323403652946_6458905696794434194_n.jpg

Kufanya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa. Huu ni msemo wa zamani sana lakini bado una ujumbe mkubwa sana kwetu.

Haya mambo 10 ninayaoenda kuyazungumza katika makala hii kama ulishafanya moja ya tabia hizi basi usirudie tena. Ni hatari sana sio kwako tu na hata kwa watu wengine. Na kama hujawahi kufanya, hongera sana, mshukuru Mungu wako na endelea kumuomba akuepushe nayo.

Napenda sana hii nukuu, "Endesha kama mmiliki gari na sio mmiliki wa barabara. Ukipanga chumba, usiishi kama umepanga nyumba nzima. Usisubiri mpaka uione sura ya kifo ndio ubadilike". Kuna watu hawatabadilika mpaka tu pale watakaponusurika kifo.

Kuna vitu vingi sana ambavyo huwezi kuvibadilisha. Moja wapo ni "mabadiliko". Kubadilika ni lazima sio muhimu. Na bora ubadilike mwenyewe kuliko kubadilishwa na maisha.

Aonaye mapungufu fulani katika maisha yake na hachukui hatua yoyote kufidia hayo mapungufu huyo mtu ni pungufu.

Kama hujawahi kufanya haya mambo, usijaribu, ni hatari kuliko jehanamu. Na kama unafanya, huu ni wakati wa kubadilika. Na kama uliwahi kufanya usirudie tena.

Ni mambo gani hayo? Haya hapa...

1. Kuhifadhi Vinyongo.

Ukiweka chuki, roho mbaya dhidi ya mtu au watu fulani unajiumiza wewe mwenyewe na nafsi yako. Kuweka chuki moyoni mwako ni sawa na kunywa sumu ukidhani kuwa atakufa mtu mwingine. Faridi Kubanda husema hivi, "Chuki humchoma aliyeihifadhi". Chuki ni ujinga ambao huzaa uovu utakaokunyima furaha kwenye maisha yako. Samehe, sahau, kua kisha endelea na maisha yako. Kusameha na kusahau ni dalili ya utu uzima, kutokusamehe ni dalili ya utoto. Inatosha kuwa mtoto, ni wakati wa kuwa mtu mzima.

2. Kuairisha Airisha Mambo.

Unapanga kufanya kitu fulani kwa muda fulani, muda huo ukifika unapanga tena kufanya muda mwingine. Unapanga kuanzisha biashara mwezi ujao, mwezi ujao ukifika huanzishi unapanga kuanzisha mwezi mwingine. Unapanga kwenda mahali fulani kesho, kesho ikifika huendi mpaka mwaka unaisha. Hii sio hatari ndogo ni hatari kubwa mno. Unaweza ukazeeka unapanga tu bila kufanya na hii ndio huleta tofauti kati ya masikini na watu waliofanikiwa. Watu waliofanikiwa hupanga na kufanya. Masikini hupanga bila kufanya.

3. Kujilinganisha na watu wengine.

Jikubali wewe mwenyewe, jiamini, ona kwamba unaweza. Ukijkubali wewe ndipo watu wengine watakukubali. Pia kujilinganisha na watu wengine ni kujinyima furaha. Kila mtu alizaliwa akiwa wa pekee na wa tofauti kwa hiyo hata ufanyeje wewe utaendelea kuwa wewe na yule ataendelea kuwa yule. Upekee ni uzuri, utofauti ni nguvu. Jivunie kuwa wewe na sio mtu mwingine.

4. Starehe & Anasa Kupitiliza.

Utumiaji wa pombe, sigara, madawa ya kulevya. Ngono, hivi ni vitu ambavyo huweza kukufanya sio uwe masikini bali ufe masikini. Anasa, starehe ni dhambi na mshahara wa dhambi ni........... Badilika, achana ma tabia chafu, pia mshauri na mwenzio kuacha haya mambo. "Maisha ni kama mshumaa uwakao kwenye upepo uvumao sana, usipoyalinda unayapoteza. Linda maisha yako".

5. Kupinga Kitu Ambacho Unajua Ni Kweli.

Sisemi tusiwe wadadisi au tusiulize maswali au tusitafiti mambo kwa mapana zaidi, hapana. Nachotaka kusema ni kwamba, hata kama umejaliwa uwezo wa kubadilisha uongo kuwa ukweli na watu wakakubali hilo sio jambo la kujivunia sana. Wajuaji wako wengi sana na ubishi wa sifa wakati mwingine haufai. Usimbishie mtu eti tu kwa sababu unamzidi umri, eti tu kwa sababu unamzidi cheo au elimu au nguvu, ni vibaya sana. Hili ni kosa kubwa sana. "Ukweli unaweza ukautupa motoni na usiungue". Hata ufanyeje hutaweza kuuficha ukweli kama ambavyo huwezi kulificha jua.

7. Uvivu & Uzembe.

Ukitaka kuwa masikini, ukitaka kufa masikini ni rahisi sana. Kuwa mvivu, kuwa mzembe. Sikuwahi kuona wala kusikia mtu mvivu, mtu mzembe mwenye mafanikio ya maana. Thomas A. Edson, mgunduzi wa bulb, alikuwa akilala masaa manne tu, Paul Mashauri, mhamasishaji kutoka Tanzania huwa anaamka saa kumi na nusu alfajiri kila siku. Aliko Dangote, tangu mwaka 1978 mpaka leo anafanya kazi masaa zaidi ya 16 kila siku, P. Did, mwanahiphop tajiri namba moja duniani aliwahi kuwa anafanya kazi masaa 17 kila siku. Uvivu ni ujinga uletao umasikini katika maisha ya mwanadamu.

8. Kusema Ndiyo Kwa Kila Kitu.

Ukiwa mtu wa ndiyo kwa kila kitu jiandae kukosa kila kitu. Watu wanaosema ndiyo kwa kila kitu hukosa kila kitu.Unachohitaji ni msimamo na kulinda heshima yako wewe kama binadamu. Usifanye kila kitu kwa sababu fulani anafanya, usinywe pombe kwa sababu fulani anakuambia unywe. Jifunze kusema hapana kwa lile jambo ambalo unaona sio zuri kwako na kwa wengine. Usiishi ndani ya mawazo ya mtu maisha ni mafupi Sana, sikiliza moyo wako fuata moyo wako kisha tumia akili yako ipasavyo. Watu wengi wamekuwa wajinga kwa sababu ya kuwa kama polisi. "Yes sir, yes sir, .... Hii ni mbaya sana. 'Yes Sayers Archive Nothing".

9. Kuogopa Kushindwa.

Plato aliwahi kusema hivi; "Tunaweza kumsamehe mtoto anayeogopa giza la usiku lakini hatuwezi kumsamehe mtu mzima anayeogopa mchana". Kuogopa kushidwa ni kikwazo kikubwa sana katika maisha ya kiutu uzima. Kuogopa kushindwa ni kushindwa. Kutokuogopa kushindwa ni kushinda. Jay Z anasema kwamba, "siogopi kufa, ila naogopa kutokujaribu". Fanya ushindwe, lakini usishindwe. "The only war won or lost, can be described" ~Nelson Mandela.

10. Kutokujifunza.

Kadri unavyojifunza ndivyo unavyojua jinsi gani hujui. Tatizo sio gharama ya Kitabu, tatizo ni gharama utakayolipa baada ya kutokusoma hicho kitabu. Sisi ni matokeo ya vile tunavyojifunza kwa hiyo kama hujifunzi wewe sio chochote.

---------------Ahsante Sana----------------
 
Hapa Tanzania mambo hatari ni
1. Kumuombea Lissu
2. Kuvaa tisheti inayomuombea Lissu
3. Kujadili mambo ya Lissu
4. Kumchangia damu Lissu
5. Kumchangia hela ya matibabu Lissu n.k.
 
Good
 
Hapo kwenye kuhifadhi vinyongo kwa kweli vinatula mnoo. Unakuta hata humu JF kuna watu wanawawekea wenzao vinyongo wala hatujuani kisa tuu labda alicomment kitu hukukipenda n.k
 
Back
Top Bottom