Mamba mkubwa auawa hotelini jijini Mwanza

Chris14

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
3,076
2,176
Kwa habari niliyopata hivi punde :

Inasemekana Mamba ameuawa pembezoni mwa hoteli ya Tilapia jijini Mwanza leo mchana.

=====

Mamba huyu ameuawa kwa kupigwa risasa na Maliasili baada ya kuibuka katika eneo la kivuko cha kwenda Hifadhi ya Saanane pale Capri point wilayani Nyamagana mkoani Mwanza na hivyo kuleta taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

8b56da22a9283cb6ac3f312dcf9bd0dc.jpg


7e33e2b4ad30a503ed2c18b9889f9a90.jpg


10c85ba24285dca6a0bb38f84fc63b66.jpg
 
Yaani sisi Waswahili suluhisho letu la kwanza kwa kila tatizo siku zote ni kuua tu.

Sidhani kama kulikuwa na juhudi zozote za kumkamata na kumrudisha alipotoka, sisi ni kuua tu.

Mwizi tukimkamata na kumdhibiti bado tunaishia kumuuwa, hata kama wangesaidia taarifa muhimu za kuwakamata wenzake.
 
Mbona USA wanaingia mpaka swimming pool lakini wanawakamata na kuwapeleka sehemu za mbali?
Kwanini wamuuwe?
Hebu maliasili watoe mafunzo kwa wananchi kwamba pindi wanapoona mnyama wapigiwe na kuja kumkamata
Kumshika Mamba ni rahisi sana
Inasikitisha kwa kweli
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom