Mamba Aiangusha Ndege Kongo, 20 Wafariki

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Mamba Aiangusha Ndege Kongo, 20 Wafariki
5061966.jpg

Mabaki ya ndege iliyoangushwa na mambaMonday, October 25, 2010 2:35 AM
Watu 20 wamepoteza maisha yao nchini Kongo baada ya ndege waliyokuwamo kuanguka toka angani baada ya mamba aliyeingizwa kinyemela ndani ya ndege hiyo kuchoropoka na kuleta kizazaa kikubwa ndani ya ndege.Abiria aliyetaka kumsafirisha mamba wake kinyemela kwa kumficha mamba huyo ndani ya begi na kuingia nalo ndani ya ndege amesababisha vifo vya watu 20.

Ni mtu mmoja tu kati ya watu 21 waliokuwemo ndani ya ndege huyo ndiye aliyenusurika maisha yake.

Kwa mujibu wa abiria huyo aliyeponea chupu chupu kupoteza maisha yake, mamba huyo aliyekuwa amefichwa ndani ya begi na kuingizwa kinyemela ndani ya ndege nchini Kongo alisababisha mtafaruku mkubwa ndani ya ndege na kupelekea ndege kuanguka.

Mamba huyo alichoropoka toka kwenye begi wakati ndege ndogo ya abiria iliyotengenezwa nchini Czech aina ya Let 410 ilipokuwa angani ikitoka mji wa Kinshasa kuelekea Bandundu.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika wakati mamba huyo alipoanza kuranda randa ndani ya ndege na kupelekea abiria waviache viti vyao kusalimisha maisha yao.

Wahudumu wa ndani ya ndege walikimbilia ndani ya chumba cha marubani na kufuatiwa na baadhi ya abiria ambao nao waliamua kuitumia nafasi hiyo kusalimisha maisha yao.

Inasemekana kuwa ndege hiyo ilianguka toka angani kutokana na uzito ndani ya ndege kuelemea upande mmoja.

Ndege hiyo iliangukia kwenye nyumba iliyopo maili chache toka kwenye uwanja wa ndege ambao ndege hiyo ilipanga kutua.

Mamba aliyesababisha ajali hiyo alitoka salama salimini toka kwenye mabaki ya ndege hiyo lakini aliuliwa kwa kuchomwachomwa na kisu na watu waliojitokeza kuwaokoa majeruhi wa ajali hiyo.
 
Du!! Jamani ,
Ni hadithi ya kusitisha na kuchekesha. sasa watu wenye hasira nao wakamuuwa mamba. he Africa bado tuna kazi du.:smile-big::smile-big:
 
Kwa kweli ni ajabu na kweli. Hii inaonyesha ni jinsi gani Africa tulivyo wababaishaji maana hapo inaonekana kuna mazingira ya rushwa rushwa hadi mamba kuingi ndani ya ndege.
 
Hao watu walikuwa waoga mno. mamba wa kutosha kwenye begi awashinde kukontrol? ni ujinga wa hali ya juu sana ndo umewauwa. angalined dicovery channel national geograph za DSTV. Iy is ver easy kumdhibit mamba hasa mdogo
 
Hao watu walikuwa waoga mno. mamba wa kutosha kwenye begi awashinde kukontrol? ni ujinga wa hali ya juu sana ndo umewauwa. angalined dicovery channel national geograph za DSTV. Iy is ver easy kumdhibit mamba hasa mdogo

unaweza kukuta alikuwa kenge na isitoshe wenyewe mambo ya balance hawayajui so hata wakikaa wote upande mmoja wanaona poa tu
 
This is like a joke!! aaaiiigh! RIP na hizi ndege zikianza kuanguka basi ndio kama msimu! maana jana moja bado kidogo ianguke (Quantas), leo Cuba sijui na hawa wasanii wenzetu wa Congo! Africans need to be serious, :nono:Jeeeeeeeeeeeeeeeez!!!
 
Huyu 'Chalii' aithee mbona maandishi yake yamekaa kimzaa kimzaa sana wakati ni vitu vya kusikitisha.
baada ya mamba aliyeingizwa kinyemela ndani ya ndege hiyo kuchoropoka na kuleta kizazaa kikubwa ndani ya ndege.

mamba huyo aliyekuwa amefichwa ndani ya begi na kuingizwa kinyemela ndani ya ndege nchini Kongo alisababisha mtafaruku mkubwa ndani ya ndege na kupelekea ndege kuanguka.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika wakati mamba huyo alipoanza kuranda randa ndani ya ndege na kupelekea abiria waviache viti vyao kusalimisha maisha yao.

Wahudumu wa ndani ya ndege walikimbilia ndani ya chumba cha marubani na kufuatiwa na baadhi ya abiria ambao nao waliamua kuitumia nafasi hiyo kusalimisha maisha yao.
Yaani kama namuona huyo mamba alivyochoropoka ghafla na mstuko wa abiria na hizo fujo alizo alizowafanyia huyo mamba angani 'haki-ya-mungu' mpaka watu kukimbilia kwenye pilot's cabin, alafu tena anaongezea ilikuwa kizazaa hizi abari za kusikitisha yeye anaona kama story ya utani.

anyway R.I.P
 
pole sana wenzetu wakongo kwa maafa hayo.but who should be blaimed ? airport management-security department or who,simply i don't understand.there should be some one to be charged of this offence,come on, may be airport sreening system is outdated can't even see.....or corruption....????.
Almight God to rest their soul in peace.
Amen.:nono::A S angry::bowl::doh:
 
Kweli huko DRC kitu usalama wa anga na maisha ya binadamu ni zero kabisa. Hata cockpit inaingilika kirahisirahisi tu? Hawana habari kabisa na marekebisho ya milango ya cockpit yaliyosisitizwa baada ya Septemba 11 (2001)? Ndio maana tunakosa hoja za kujitetea wazungu wanapopiga marufuku ndege zetu kwenye anga zao. :A S angry:
 
Duh Afrika kweli kuna mambo. Hii inanikumbusha Nigeria nao wana ujinga kama huo eti mtu anaruhusiwa kupanda kwenye ndege na kuku! Yaani unamwona abiria wa karibu yako ana kuku kwenye kikapu kamshikilia. Inatia aibu kwa kweli.
 
Back
Top Bottom