Mamalia mpya agunduliwa Tanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Wazungu wana vituko vyao, ati leo wao ndio wanautangazia ulimwengu kuwa wamegundua mamalia mpya. Hivi haka kamnyama hakuna aliyewahi kukaona huko Tanzania?
 
1. Hii habari tayari ilikuwa hapa ingeunganishwa iwe moja!

2. Sii ndo ndo hawa wazungu walisema 'walivumbua' hata Mt. Kilimanjaro 1890s?
 
Wazungu wana vituko vyao, ati leo wao ndio wanautangazia ulimwengu kuwa wamegundua mamalia mpya. Hivi haka kamnyama hakuna aliyewahi kukaona huko Tanzania?
Ndo tabia yao hiyo, si mnakumbuka wanavyosema walivyovumbua Mlima Kilimanjaro wakati kila siku wachagga walikuwa wanauona, na kwenda kutambika huko au Ziwa Nyanza wakati wasukuma, wahaya, wajaluo, nk kila siku walikuwa wanavua samaki pale!,na kinachonipandisha hasira zaidi wakabadilisha na jina la ziwa hili na kuliita Victoria (Malkia wao ambaye hana faida yeyote na wazawa wa eneo hilo!) Mimi binafsi kupingana na huo ujinga wao siku zote naliita lile ziwa kwa jina lake halisi yaani "Ziwa Nyanza" na siyo Victoria!!,
Hebu fikiria leo hii M-bantu aenda USA na Mississipi auite (Mtemi) Milambo, au River Danube uite River Mkwawa je watakubali au Mto Thames wa Uingereza uitwe Kinjeketile je watakubali?
 
Sometimes najaribu kufikiria ni kiasi gani hawa wazungu wanatuonaga hamnazo! I agree with you. Labda na sisi tupeleke petition kwa wanaohusika ili hili ziwa libadilishwa jina, mbona walibadili jina la uwanja wetu wa kimataifa overnight?! It can be done.
 
....au sijaelewa, yaani kule Uingereza kuna river Kinjeketile?!!!

joke..
 
Ishu hapa ni documentation.. of koz katika mfumo wao (wazungu)
 
Mwanakijiji umenikuna,

Unanikumbusha nilivyoenda American Museum of Natural science kuna sehemu walionyesha wanyama wa Tanzania waksema kuwa hawakujulikana kwenye sayansi mapaka miaka ya karibuni.Mimi nikasema wangeandika "Western Science" kwa sababu kusema "science" kuna tangaza kuwa huko Tanzania hatukuwa na "science" yetu.

Very condescending indeed, in the midst of all the political correctness.They are too deep in this dominance philosophy to even notice things like that.

Katika style hiyo hiyo wamegundua Marekani, wamekuwa wa kwanza kupanda Mlima Everest (ingawa walitumia tour guide, you wonder about the tour guide and his people) wamegundua Nile and Lake Nyanza and all that jazz.Full of it!
 
Topic hii inanikumbusha mbali zaidi, miaka ile ya Ugunduzi, Chagula's nerve, Mianzi water pipes, Tanzanite, Oldivai Goji, n.k.

Lakini kubwa zaidi ni mapungufu ya vyuo vyetu vikuu kutokuwa na kumbukumbu na kukosa uhusiano na jamii, utakuta research nyingi hazina impact kwenye jamii inayowazunguka.
 
Sasa hapa ndipo shule za Watanzania zinapotia aibu, kwani wazungu watachukua huyo mnyama na Watanzania hata wasimsikie kabisa. Mh I wish hata Sokoine University wangechangamkia hiyo research ili jamii ifaidike hata na huo ugunduzi basi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom