Mama Zitto Kabwe amkampenia JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Zitto Kabwe amkampenia JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Mar 1, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  • Asema hana mpinzani

  na Deogratius Temba

  JITIHADA za kuhakikisha Rais Kikwete anaendelea kukubalika kwa wananchi na kuchaguliwa zinazidi kushamiri ambapo mama wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Zitto Kabwe ametangaza kuwa hakuna mtu yeyote mwenye kufaa nafasi hiyo hivi sasa.

  Mama huyo, Shida Salum, ambaye ni mwenyekiti wa walemavu, alitangaza kumuunga mkono Kikwete juzi kwenye viwanja vya Temeke, jijini Dar es salaam, alipokuwa kwenye mkutano wa Aman Forum.

  Alisema Rais amefanya kazi nzuri ya kuimarisha amani na kuwatetea walemavu hivyo ni vema Watanzania wakampa fursa ya kuongoza kwa kuwa wanasiasa waliopo hivi sasa iwe wa CCM au wa vyama vya upinzani hawajafikia viwango vya kuwania urais.

  “Ninasema hivi; hakuna mtu anayeweza kuwatetea walemavu kama Rais Kikwete, amewakamata wauaji wa maalbino, na sasa anatutetea zaidi, kura zote za urais ni kwa Rais Kikwete, wapinzani watapata za ubunge tu!” alisema.

  Aliongeza kuwa wapinzani wanapaswa kujiandaa kumsimamisha mgombea urais mwaka 2015 ili kuepuka matokeo mabaya wanayoweza kuyapata iwapo watamsimamisha mgombea wa urais ili kukabiliana na Kikwete.

  Mkutano huo ambao uliongozwa na Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Walid Aman Kaborou, na pia kuhudhuriwa na wajumbe kutoka vyama vya Tanzania Labour (TLP) na NCCR- Mageuzi, limewashambulia viongozi wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) kuwa ni wachochezi.

  Akizungumza kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na watu wachache, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alisema amejiunga na taasisi ya Aman Forum, kwa sababu amegundua kuwa nchi ina tatizo hasa unapofikia wakati wa uchaguzi wa urais.

  “Kuna kundi la watu lina njama za kumdhuru au kumsambaratisha Rais Kikwete na serikali yake, wajue kuwa wakifanya hivyo hawatakuwa wamekidhuru chama tawala bali ni Watanzania wote, mimi nimeamua kujiunga na Amani Forum, ili sasa nitangaze vita na kundi hilo,” alisema Mrema.

  Mrema alibainisha kuwa ameamua kuitetea nchi na hajahongwa wala kununuliwa na mtu yeyote kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakimtuhumu.

  Aidha, aliwashambulia makada wa CCM na viongozi wastaafu walioshiriki kuchangia hoja katika tamasha la kumuenzi hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika katika ukumbi wa Karimejee mwishoni mwa mwaka jana kuwa ni wachochezi na wanatakiwa kukamatwa kwa sababu hawana heshima kwa rais wa nchi.

  “Kuna tamasha la Mwalimu Nyerere, makada wa CCM wamelitumia kama kichaka cha kuendesha uhaini hawa walinunuliwa; wamesema Kikwete amezungukwa na wezi, wanamtukana rais? Nyie CCM mnamtusi kiongozi wenu anayewapeperushia bendera?”

  Mrema ambaye aliwahi kuibua kashfa ya ufisadi wa kuibiwa kwa sh bilioni 900, ambayo ilimhusisha pia Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alisema katika miaka minne, Rais Kikwete amefanya mambo makubwa ikiwepo kuruhusu wasaidizi wake wajiuzulu, kwa kuhusishwa.

  “Hivi mnamtaka afanye maamuzi gani mazito, wakati amekubali rafiki yake aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ajiuzulu? Serikali si imewajibika? Mnasema mtamtosa kwa kosa gani alilofanya Rais Kikwete?

  Mrema aliendelea kusema kuwa suala la ufisadi hata Baba wa Taifa alilishindwa kwa sababu baadhi ya viongozi waliokuwa wakifanya naye kazi walipohusishwa na ufisadi aliwahamisha au kuwaongezea majukumu badala ya kuwawajibisha.

  “Mwingira aliuza ndege ya serikali, mbona Nyerere alimhamisha na kumpa ukuu wa mkoa wa Arusha? Balozi Mustafa Nyang’anyi alinunua kivuko kibovu Mwalimu akampa ubalozi wa Marekani; Rais Kikwete amewapeleka watu mahakamani ninyi mnasema mtamtosa!” alishangaa Mrema.

  Mrema aliyekuwa amefuatana na baadhi ya viongozi wa chama chake makao makuu, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Hamad Tao, aliendelea kusema kuwa hajanunuliwa, na Rais Kikwete, lakini atahakikisha anampigia debe ili ashinde urais Oktoba mwaka huu.

  “Watanzania tuache uongo, unafiki na uzandiki, sijanunuliwa na Rais Kikwete, mbona Seif anayempigia debe Rais Karume kuwa aongezewe muda hamsemi amenunuliwa? Ninasema kura zote za urais ziende kwa Rais Kikwete!” aliongeza.

  Naye Walid Kaborou, ambaye ni mwenyekiti wa taasisi hiyo, alisema wanaosimama na kusema kuwa Rais Kikwete atoswe wanazungumzia kazi ambayo hawajawahi kuifanya. “Hawa hawajawahi kuwa marais leo wanasema rais atoswe; hao Mwalimu Nyerere Foundation kati yao nani aliyewahi kuwa rais? Hao ni wachochezi na kwa uchochezi kama huo hatuwezi kufika!” alisemea Kaborou.
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huyu mama kwani ana nguvu gani kisiasa? Naona haishi ktk vyombo vya habari wakati wabunge wengine mama zao wamesettle tu kulikoni?
   
 3. annamaria

  annamaria Senior Member

  #3
  Mar 1, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Muache aseme.Ni haki yake ya kidemokrasia na kikatiba..
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  wapinzani wetu
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Simply clueless.
  Lakini ni kipi cha kutegemea kutoka kwa watu wasiojua dunia ilipo?? Yaani ni kama kusema mtu aliyezaliwa na kukua huko kwa wahadzabe, upeo wake lazima uendane na mazingira yake.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Wenu? Wewe na nani mkuu?
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Usisahau kua ni hizi hizi katiba na demokrasia ndio zilizotufikisha hapa tulipo. Nchi isiyo na matumaini.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mi-danganyika bwana ati kisa Mh. Zitto ni public figure... sasa inatulazimisha tuone kwamba pia mama yake ni public figure... I hate vichwa maji!
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  na wewe!
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Mar 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Si mshangai, maana kama mwanae aliweza kuhongwa na kina RA, wewe unategemea hajui radha ya kujiunga na magenge ya ufisadi wa TZ, Kaonjeshwa asali na Zito sasa anaamua na yeye akachonge mzinga, kwa maslahi ya kifamilia.
  mwaka huu wa uchaguzi tutayasikia na kuyaona mengi.
   
 11. p

  pruzangi Member

  #11
  Mar 1, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muda utafika na TZ ita ondokana na Ufisadi
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ufisadi upo kwa sababu ya mfumo wenyewe uliopo. As it is sioni kama kuna mtu anayejali kwamba tunao mfumo unaozalisha, kulea na kuukingia kifua ufisadi. Sasa sijui kama unaelewa magnitude ya kuundoa ufisadi mkulu.
   
 13. M

  Mchili JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Njaa mbaya. Mrema nae!!!!!!!!! aibu
   
 14. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Zitto na Mamake are cheap politicians who can be bought (and they have) by any1 na wataimba mbeleko ya bwanao
   
 15. D

  Donrich Senior Member

  #15
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mama katumia haki yake ya msingi ya kuonyesha political feeling zake...
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Mkuu umetokota kabisa, unajua kinachokusumbua ni ujuha kwa kudhani unajua. Uliyoyaandika hapa ukiambiwa thibitisha utaweza? mbona mkuu post yako hii haina mashiko. Yaani thinking capacity yako imefikia hapa! kwa hiyo na wewe unalaumu kwa sababu umekosa nafasi ya kuhongwa na RA au?

  Naomba nikuulize Mr. Nguvu, unapoweka vidole kwenye keyboard ya PC yako huwa unaruhusu vidole vibonye keyboard vikienda simultenously na brain yako, au vinabonya tu ubongo huwa umeachwa nyuma?kwa kukusaidia njia hizi zote sio nzuri!!

  Fikiri kwanza kabla ya kuandika, huone kama ulichoandika kina make sense au kujaza post tu kutokana na chuki zako kwa Zito! hakuna mtanzania yeyote wa rika na mwenye akili timamu wa namna yeyote not even mbwa kama umefuga ambaye anaweza akafaidika kwa njia yeyote na post hii uliyoituma not even your mother kama unaona kuna uhusiano wa mtu na mama yake!

  I suggest kwa kukusaidia ilikuwa wakati mzuri wako kujadili hali ya wapinzani nchini mwetu, allegations zako hizi za kusingizia watu hazijengi. kama husingizii weka uthibitisho.period!
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Alichosema Shida Salum kasema lile analoona sahihi kwake, kwani wapinzani hawasimamishi mtu mwaka huu huku bara. Amezungumza reality iliyopo kwa sasa ambapo watu wanaoona kakosea kusema ukweli waseme nani anafaa kuwa rais tumpigie kura.

  My problem na statement hizi za Shida Salum ni kuwa , hata kama alichosema ni kweli, lakini hakijengi upinzani, yeye kama mpinzani na wengine wote wakwepe kabisa aina yeyote ya statement ambayo zina ipa sifa CCM na watendaji wake. Ukisema JK anafaa then hata wabunge wanafaa kitu ambacho si kweli.

  Ili tatizo ni kubwa sana kwa vyama, mbowe ameishawahi kumfagilia JK, Mrema ndiyo kila siku, leo Shida Salum, kesho utasikia Mtikila list will go on and on....

  Then at the end of the day tunajiona tuna CCM kama chama kikuu, vyama vyote vya upinzani ni matawi tu ya CCM.!!!
   
 18. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Weberoya,

  Habari za weekend? Lini Mbowe alimfagilia JK na katika issue gani?
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Mar 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Waberoya kazini.
  Umekasirika ?
  matusi ni kieelezo cha malezi duni, lishe mushkeri.....labda tatizo la afya ya akili .....pole kijana.
  mpe salamu Zito na mamae wameisha neemeka na dhambi mbaya kuliko zote, dhambi ya usaliti.
  Miezi kumi nyuma , mama Zito alikua mmoja kati ya kinamama waliotuaminisha kua JK ni Rais Bomu, leo anaibuka kutuaminisha kuwa huyu mheshimiwa Rais wetu ni wakufaa kuongezewa miaka mitano, kuna jambo nyuma ya pazia Waberoya, unless kama haikustui..afya ya akili ipo shakani.
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Dear Selous; nilichoandika na nadhani umenielewa post yangu nzima , kuwa statement zozote zinazotolewa na vyama vya upinzani juu ya CCM na JK lazima ziwe critical.

  Mbowe alisema JK avunje baraza la mawaziri, sentensi hii kwako Selous utakuwa umenielewa haraka sana nina maanisha nini. Ukisema leo hii JK avunje baraza la mawaziri, maana yake; JK ni mzuri, anafaa, wanaomwangusha ni mawaziri. Na je akishavunja bara za la mawaziri si atapata sifa? akipata sifa Chadema itashikaje nchi? still unataka usimame kugombea urais??. Ningeweza kueleza hili over and over. Yaani aligeuka kuwa consultant wakati tumemuweka awe mbele kuiondoa CCM, kuna statement nyingi sana ambazo utakuta wapinzani wanaongea wakidhani wanajenga kumbe wanaharibu. Mbaya zaidi kwa chadema ili shadeclare JK ni fisadi; leo hii anabadilika na kuwa msafi kiasi cha kumwabia avunje baraza la mawaziri

  Habari iko humu humu JF, ebu jikumbushe hiyo thread. However nimependa ulivyouliza swali lako

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/47458-jk-vunja-baraza-la-mawaziri-mbowe.html

  nadhani nimejaribu kujibu

  cheers
   
Thread Status:
Not open for further replies.
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...