Mama Yetu Prof. Ndalichako tunaomba utangaze tarehe rasmi ya kufungua Vyuo/shule ili vijana wajiandae na gharama za usafiri. Kama Uganda ilivofanya

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
575
1,000
Baada ya Mh. Rais Magufuli kutangaza wiki ijayo kufungua michezo na Vyuo,
Sasa tunakuomba Waziri Mama Ndalichako kutoa mwongozo na kutangaza tarehe rasmi ya kufungua vyuo.

Ili kutuwezesha wazazi kuandaa gharama za hawa vijana ikiwemo nauli ya kuwapeleka vyuoni kwao.

Wenzetu Uganda tayari wameitangaza tarehe 04 June kufungua shule za misingi secondary na vyuo.

Karibu Mama tunakusubiri.
 

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,273
2,000
Akilitime Mhe Raisi alisemea "wiki ijayo mambo yakiendelea hivi nategemea kutangaza kufungua vyuo......".

Endelea kuwa na subira wiki yenyewe ndiyo hii. Kwani Naibu Waziri wa Afya amekwishaapishwa? Kama bado nadhani siku ya kuapishwa tutegemee tamko la Mh. Raisi.
 

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
575
1,000
Akilitime Mhe Raisi alisemea "wiki ijayo mambo yakiendelea hivi nategemea kutangaza kufungua vyuo......".

Endelea kuwa na subira wiki yenyewe ndiyo hii. Kwani Naibu Waziri wa Afya amekwishaapishwa? Kama bado nadhani siku ya kuapishwa tutegemee tamko la Mh. Raisi.

Huyo jamaa anaapishwa lini mkuu?
 

Ulisikia Wapi

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,791
2,000
“Ndani ya wiki mbili tutafungua shule kwa wanafunzi wanaohitimu pekee wa madarasa yote, hakutokuwa na mitihani ya muhula wa kwanza.

Shule zinapaswa kuandaa mitihani ya mwisho wa mwaka tu, wanafunzi wengine mtaendelea kuwa wavumilivu kwa sasa huku tukiangalia hali ya janga hili la corona inavyoenda”- Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom