'Mama yetu Anna Makinda njoo utusaidie, tunadhalilika huku wanao!!!'

Rose Mayemba

JF-Expert Member
May 7, 2012
721
1,017
Tangu tume ya uchaguzi itangaze chaguzi kwenye nafasi zilizoachwa wazi vilio vya aina hii vilianza kusikika kwenye jimbo la Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano...

Mama yetu uko wapi?

sisi wanao hatulali huku. kila tunapopita tunazomewa, tumekuwa kama wageni kwenye ardhi yetu wenyewe, Shangazi na Mjomba walikuja kutujulia hali lakini hakuna nafuu yoyote, utadhani walikuja kutonesha donda lililouguzwa muda mrefu.

Mama yetu uko wapi?

Jirani zetu kila siku tunawaona na sura za furaha, mama na baba zao huwajulia hali kila kunavyokucha, wamekuwa ni mahodari hawashikiki na mpaka sasa watu wamepoteza imani kabisa na familia yetu, hakuna hata anayejaribu kuja kuomba maji ya kunywa,

ee mama yetu mpendwa...

Hata waliokuwa karibu yetu anatoroka mmoja mmoja, nyumba imekuwa ya moto, wote wamehamia kwa jirani yetu, hawataki hata kutusikia.
Hii yote ni kwasababu umetutupa sana mama, watu wanadhani pengine ulishakufa, wengine wanatuulizia wanadhani upo ndani umelala kwa maradhi, kumbe upo nchi ya mbali, wanaobahatika wanakuona tu kwenye vyombo vya habari.

Mama rudi nyumbani...

Deni ulilotuachia ni kubwa na sasa tunadaiwa kila mahali, uliowakopa wameanza kuja sasa kutudai, wametangaza mnada kuuza vyombo vyote vilivyopo sebuleni, na wana mpango hata wa kunadi vitanda vyetu vya kulalia.

Nakusihi sana mama...
Tayari aibu yetu inafahamika na kila mtu, njoo urudishe madeni utatukuta tunalala nje, tena kwenye virago

..................
 
unaanza kujipendekeza kwa mama wa watu aibu yako umbea mwingine kwa mwanamke ni aibu kubwa sana umeondoka lini machame umehamia jimboni kwa makinda wewe kaa migombani kwenu tu basi.
 
kwa sasa mtajivika hata nguo na makabila ambayo siyo ya kwenu kwa lengo la kujipendekeza kwa watu lakini kizuri ni kwamba watu walishawajua mzimu wa zitto na sera za ubaguzi zinawatesa daima kazi mnayo tena ngumu kweli nendeni mkapigie magoti zitto ili kuondokana na dhambi.
 
nimekusamehe kwani hujui utendalo.....
 
unaanza kujipendekeza kwa mama wa watu aibu yako umbea mwingine kwa mwanamke ni aibu kubwa sana umeondoka lini machame umehamia jimboni kwa makinda wewe kaa migombani kwenu tu basi.

si kosa lako maama akili yako inawaza wamachame tu....
 
Huna lolote njaa tu mwache mama wa watu acheze muziki bana huko najua kwa alivyowadanganya hata na kuwaloga hata akiwatukana hamtafanya lolote maana hamjui zuri na baya nyie maana ana miaka 30 bungeni lakini hajawafanyia lolote lakini bado mnawapenda
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom