puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 940
- 1,847
Habar za muda huu wana JF.
Kuna mambo kwenye maisha yanatokea yanatatiza kwa namna fulani mpaka unashindwa kuelewa usimame au ukae.
Iko hivi, kuna mama yetu mdogo alietulea baada ya mama yetu kufariki. Mzee alishafariki kitambo kidogo.
Tulikuwa wadogo, kwa nafasi yake siwezi kumdharau hata kidogo kwangu ni mama.
Sasa katika pilika za maisha nikafanikiwa kujenga kakibanda kangu cha wapangaji somewhere, huyu M/mdogo aliwahigi kuolewa, lakini kwa mapenzi ya Mungu waliachana na mumewe.
Sasa nikaona siwezi kuona mama yangu anaishi nyumba za kupanga wakati mimi nina nyumba zaidi ya moja hivyo nikamwambia akakae kwenye moja ya apartment ya sehemu nilipojenga.
Changamoto, inakuja kwamba mama yangu huyu naona anavuka mipaka dizaini kama anataka kujimilikisha nyumba niliomwambia akae for free.
Leo nimewatuma mafundi wakafanye vipimo na kuanza kuchimba msingi, jambo lililonishangaza amewazuia na kuwahoji maswali kibao kana kwamba yeye ndio mmiliki. Mafundi wakanipigia, nikamuelewesha nini malengo yangu, Chakushangaza ananiambia huwezi fanya chochote hapa bila idhini yangu, kiukweli kama binadamu nilikasirika sana na sijawahi mvunjia heshima hata kwa bahati mbaya, nimejikuta naongea maneno ambayo sio mazuri.
Hivi ninavyoandika hapa ameanza kupigia simu ndugu analia anasema nimemtukana na kumdhalilisha kisa yupo kwangu.
My point ilikuwa ni kumuonesha mipaka anayotakiwa kuwa nayo yeye kama mama, angekuja kama mshauri wala tusingefika huko.
Ila kiukweli sijamtukana ila nilikuwa naongea kwa jazba. Hivi kiuhalisia kuna jambo nimekosea, nisije kosa radhi maana kwa umri alioanza kutulea ni mama yangu kabisa.
Naombeni busara zenu katika hili. Natanguliza shukrani