Mama yake Zitto Kabwe Anusurika kifo mara Baada ya kupata Ajali mbaya ya Gari hapo jana jioni..!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
MAMA mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Shida Salum amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Lindi kupata ajali mbaya. Habari ambazo zililifikia gazeti hili jana jioni muda mfupi tu baada ya kutokea kwa ajali hiyo, zilieleza kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi la nyuma wakati gari likiwa kwenye mwendo mkali.

mama+z.jpg

Kwa mujibu wa habari hizo, ingawa Mama Zitto hajaumia lakini gari hilo liliharibika vibaya kutokana na kubiringika mara kadhaa kabla ya kuangukia porini.

Mama Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Walemavu (CHAMATA), alikuwa akielekea kwenye ziara ya kikazi mkoani Lindi na alipata ajali hiyo muda mfupi baada ya kutoka kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani na RAI Jumatano, Mama Zitto alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa hajaumia.

Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Nguruku Wilaya ya Mkuranga na kwamba hakuna aliyeumia lakini gari limeharibika vibaya.

"Namshukuru Mungu kwa kunusurika na ajali hii ambayo hata hivyo nilimuona dereva akijitahidi kutuokoa, lakini ikashindikana.

Nashukuru kwani wanangu wamenitumia gari lingine na inanibidi niendelee na safari kwani kesho asubuhi (leo) ninaanza mkutano," alisema Mama Zitto.

Source: Mtanzania
 
Inshaallah salama mama!!!!!

Allah akuvue na mabalaa ya viumbe wanaoonekana na wasioonekana!!!!

Aaamiyn!!!!!!

Mytake; Muandishi wa hilo gazeti anashindwa kusema aina ya gari,number plate inasomekaje na umiliki wa gari????!!!! Hata jina la dereva???!!!

Kishamtaja Zitto basi nafsi kwatuuu!!!!!!!
 
Mungu amponye mama wa watu na kumjaza uzima tereeee!

(Ziara ya kikazi Lindi, msaliti Chitanda Lindi, tutaujua ukweli tu dunia haina siri)
 
Mungu amponye mama wa watu na kumjaza uzima tereeee!

(Ziara ya kikazi Lindi, msaliti Chitanda Lindi, tutaujua ukweli tu dunia haina siri)

Ungeenda ofisini kujua nature ya hiyo ziara!!!!!!
I thought you were one smart guy!!!!!!
 
R.I.P Chacha Wangwe...

Mzimu aw Chacha Wangwe umebisha hodi Chadema unawauliza lkulikoni wameshindwa kumkumbuka hata kwa Bango tu pale TBC wala Padri Slaa ameshindwa hata kuitisha Sala kisha kutembelea kabiri la Marehemu Kamanda Chacha Wangwe Ndio Maana Mzimu ulitimba Kahama na jawabu ameliona Chezea Mzimu wewe........
 
Mzimu wa Chacha Wangwe una huzuni kubwa juu ya kutelekezwa na kusahauliwa kabsa huku ukisema Kuwa Kama Marehemu Chacha angelikuwa Mchaga sidhani Kama angesahaulika hv !
 
Natumai tairi la gari lake halijafanyiwa hila na wahafidhina wanaozitafuta roho zao yeye na mwanawe kwa kila hila.

Wewe kaharishe kwanza ndo urudi humu kabla hujaenda hospitali ya amana kulazwa kwa kipindupindu kilichokupata.
Usichelewe maana ukianza na kutapika uhai utakuwa mashakani.Ushauri wangu kwako acha kula uchafu maana siku zako zitahesabika.Umeanza na kipindupindu inafuata amoeba
 
ccm bhana,.. Kila ishu inayotokea wanasema CDM wanahusika,.


''Kale ka usemi kasemacho mti wenye matunda ndio upigwao mawe nakaona hapa''
 
Pole mama zito. Ni wakati wakuwa makini sana huu mkizingatia maadui zenu wanawasaka kila kona. Zitto alilegezewa tairi za gari lake ni vyema kuwa makini na hawa WACHAGA.
 
Back
Top Bottom