Mama yake hawezi kukubali nimuoe akifahamu hali yangu ya kiuchumi

Sam Drive

Member
Dec 27, 2020
22
32
Ilikuwa asubuhi moja nazungumza na mpenzi niliyekuwa nafikiria kumuoa nikamuuliza kuwa endapo mzazi wake atafahamu hali yangu ya kiuchumi, kuwa ni ya chini je atakubali nimuoe?

Akasema hawezi kukubali, na hata nikienda kujitambulisha nisiseme ukweli kuhusu hali yangu ya kiuchumi.

Binafsi sioni kama ni sawa kwangu naona kama sitakubaliwa vile nilivyo...kama itahusisha kudanganya kuhusu uwezo wangu...ni bora kuahirisha na kuendelea kutafuta yule ambaye tutakubaliana kwa hali zote.

Maoni yenu wakuu
 
kwani mama take ndio unayemlala au kumuoa hadi utafute mwingine na kwanai unatafutwa kukubaliwa na wazazi wake au ni mchumba ndio akukubali yeye, sasa unamuacha kwa sababu gani??
Sioni kama n sawa kufanya jambo bila wazazi pande zote kuridhia
 
Ilikuwa asubuhi moja nazungumza na mpenzi niliyekuwa nafikiria kumuoa nikamuuliza kuwa endapo mzazi wake atafahamu hali yangu ya kiuchumi, kuwa ni ya chini je atakubali nimuoe?

Akasema hawezi kukubali, na hata nikienda kujitambulisha nisiseme ukweli kuhusu hali yangu ya kiuchumi.

Binafsi sioni kama ni sawa kwangu naona kama sitakubaliwa vile nilivyo...kama itahusisha kudanganya kuhusu uwezo wangu...ni bora kuahirisha na kuendelea kutafuta yule ambaye tutakubaliana kwa hali zote.

Maoni yenu wakuu
Mbona kama umekata tamaa? Kijana tafuta pesa qumer haziami.
 
Mh hapo Ni kazi hata ukidanganya Ni km utakuwa umejitwika mzigo flani hivi upande wa mke wako,Bora useme ukweli tu.
 
Acha ufala ...Badala ya kutafuta unayeendana Naye ..Bora utafute pesa uwe Bora zaidi Usipende kuishi kwenye unyonge ..Ukadhani kuwa mnyonge ndo kuwa real
 
Nimekutukana bonge moja la mtusii! Huna akili hata kidogo wewe. Hapo unakwenda kuanzisha Familia na Ukoo wako wewe mwenyewe, unaogopa kwenda ukweni kwenu kisa pesa! Nenda, wakikukataa usiondoke kinyonge wala kujutia kwenda pale. Toka zako rudi kwako fanya maisha yako.
 
Kuwa mjanja...huo mzigo mbebeshe mwenyewe huyo bibie. Mwambie unampenda sana na uko tayari kumuoa ila hauna mpango wa kudanganya kuhusu hali yako na kujikweza kwa namna yoyote ile.

Mpe yeye maamuzi ya nini kifuate. Kama anakupenda na anataka muoane then jukumu la kuwaweka wazazi wake kwenye mstari liwe lake.
 
Well said
 
Huyo mpenzi wako nae ana matatizo, usimsikilize, wewe kuwa muwazi na usifiche hali yako kwa huyo Mzazi wake.

Kama huyo Mzazi wake hatokukubalia, wewe achana nao na uendelee na maisha yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom