Mama Wema afunguka kuhusu Wema kurudiana na Diamond

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,378
Licha ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuibuka na kukanusha sakata lao la kurudiana, bado madai ya wawili hao kutoka kwa siri yamekuwa yakishika kasi kiasi cha kumfanya mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu naye kulazimika kufungukia taarifa hizo.




Wema Sepetu na Mama Yake
MADAI YA KURUDIANA


Watu walio karibu na mastaa hao wanadai kuwa, siyo siri, Wema na Diamond wanakutana wanapohitajiana ila ni vigumu kukiri kwa kuwa kila mmoja ana mtu wake.

Watoa ubuyu hao walizidi kufunguka kuwa, isingekuwa rahisi watu kuvumisha kitu ambacho hakipo na kitendo cha mitandao mingi ya kijamii kulianika hilo kinaashiria kuwa kuna jambo nyuma ya pazia.

“Wema ameibuka na kusema hajarudiana na Diamond ila wanashirikiana katika kazi tu, sasa sisi tunawaona wakijivinjari kwa siri na usitarajie kwamba yupo atakayekiri maana Wema yuko na Idris (Sultan) na Diamond yupo na Zari…

“Lakini pia mitandao mingi ya kijamii inaandika huku wakiweka viashiria vya kurudiana kwao, sasa kama wao wanabisha, wabishe tu lakini sisi ndiyo tunaujua ukweli na ipo siku wataumbuka,” alisema mtu wa karibu wa Wema ambaye anadai alimshuhudia Diamond kwa macho yake akiingia chumbani kwa Wema.

UZALENDO WAMSHINDA MAMA WEMA

Kufuatia maneno kuzidi kuenea mithili ya moto wa kifuu kuhusu Wema na Diamond kurudiana kwa siri, Ijumaa lilizungumza na mama Wema aliyewahi kuonesha dhahiri kutotaka mwanaye kuwa na Mbongo-Fleva huyo na kwa mara ya kwanza alifunguka kilichomo moyoni mwake.

Mama huyo ambaye umri umekwenda lakini bado anaonekana ‘yumo’ alisema kuwa, haamini hayo yanayosemwa na watu kwamba Wema karudi kwa Diamond kwa kuwa ingekuwa hivyo yeye angekuwa ameshagundua.

“Kwanza niseme tu kwamba, sidhani na wala sitarajii mwanangu kurudiana na Diamond. Ni kitu ambacho hakiwezi kutokea, ninachoona hapo ni mambo ya uzushi ya kwenye mitandao.

“Ninachojua mimi, Wema yuko kwenye ulimwengu mwingine wa kimapenzi, arudi kwa Diamond kwa kipi? Ana maisha yake mengine anayoyafurahia na hivyo kusema kamrudia Diamond hainiingia akilini.

“Najua wengi walidhani hivyo baada ya Wema kuposti kitu f’lani kumhusu Diamond kwenye mtandao lakini najua alifanya vile ili kuwakata vilimilimi waliokuwa wakimtukana na kudhani ana bifu na Nasibu,” alisema mama huyo.

AMPEKENYUA MAMA DIAMOND

Licha ya kwamba ni muda mrefu mama huyo hajawahi kumzungumzia mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ tangu wakati ule alipokuwa akimponda Diamond kuwa hata kwa dawa hawezi kumuoa binti yake, safari hii amempekenyua kwa kudai kuwa hamjui na hata akikutana naye hawezi kumtambua.

Mama Wema alisema hayo baada ya kupewa madai kwamba, anajifanya hajui kuwa mwanaye amerudiana na Diamond wakati hivi karibuni walionekana pamoja nyumbani kwa mama Wema maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.

“Niseme tu kwamba mama Diamond simjui, hata leo nikikutana naye siwezi kumtambua labda anishtue, ila nimpongeze tu kwa uzalendo aliouonesha hivi karibuni wa kumposti Wema akiwa na Idris kwenye ile shoo ya Black Tie na kuandika maneno yaliyoonesha uzalendo,” alisema mama Wema.
 
Wema keshalipa mtu aandike huu upuuzi!
Huyu mama si mzima. Kiakili Atakuwa ktk group la walioanza la kwanza mwaka 1999
 
  • Thanks
Reactions: irk
Mmh mama wema jamani ana mdomo yule mwanamke majiran zake sinza wanamuogopa, huyu mama ndo kiboko ya sandrah , mama diamond anajifanya mswahili lakini mama wema ni yale mashangingi ya sinza ya 90's enzi zake na mama hasheem walitikisa sana sinza, mama ana mdomo mchafu utafikir kinaniliu cha shilole
 
Mbna watu wanahangaika sana n chibu inamaana mganga wa wema ndio kamwambia bi mkubwa kua chibu atamrudia mwanae ili kurudisha ile nyota ya wema ambayo chibu aliiba......akili za mama n mtoto kma za mganga wa jadi
 
Ingekuwa kuna sheria labda ya kuandika uongo..kampuni hiyo ya udaku ingesha kwishilia mbali.

Mfy...
 
Ah ahahh ananikumbusha vichambo tulivyokua tunapewa na binamu yangu Dinazarde, kama ingekua kuacha umbea ni kile kipindi aiseh mtu unachambwa mpaka unachanganyikiwa ,nakumbuka kuna kipindi binamu alikua anachambwa mpaka anaji quote na kujitukana mwenyew jaman nikukumbuka nacheka sana dah
haaaa binamu utanivunja mbavu..
Dinazarde alikua ana jiquote mwenyewe... hapo ushachambwa na watu kama 7....akili imedata.... nimekumbuka nimechekaje
siku hizi tumetulia sana
 
haaaa binamu utanivunja mbavu..
Dinazarde alikua ana jiquote mwenyewe... hapo ushachambwa na watu kama 7....akili imedata.... nimekumbuka nimechekaje
siku hizi tumetulia sana
Ahaa dah nimemis sana kile kipindi aiseeh, hizo ban sasa kila siku tunazinywa, dah siku hiz naona wadau wako busy, ila kile kipindi hapana aiseeh tulizidisha umbea kwa kweli,ahaha ahaha namis sana enzi zetu zike
 
haaaa binamu utanivunja mbavu..
Dinazarde alikua ana jiquote mwenyewe... hapo ushachambwa na watu kama 7....akili imedata.... nimekumbuka nimechekaje
siku hizi tumetulia sana
tukizidiwa vichambo tunaitana pm kuulizana huyo anayetuchamba nani, kuna kipindi nilikua nachambwa na watu kumi halafu hakuna wa kunitetea basi da nilikua nadata naishia kutukana na. Kulambwa ban
 
Alieleta hii nyuzi kalipwa na wema kwani Dada yule kashindikana amebaki kuonga na ili awe kwenye midomo ya watu wao wanaosoma magazeti ya udaku
 
Back
Top Bottom