Uganda: Mwanamke Mariam Nabatanzi mwenye miaka 39, azaa watoto 44 na mume mmoja. Alianza kuzaa akiwa na miaka 13!

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701


Wakati jamii ikihimizwa kuhusu masuala ya uzazi wa mpango ambao utawawezesha kuwa na watoto wachache ili waweze kumudu kuwapatia mahitaji muhimu ikiwamo elimu, malazi, mavazi na chakula, mwanamke mmoja nchini Uganda ameweka rekodi ya kuwa na watoto wengi zaidi.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 huenda ndiye mwenye watoto wengi zaidi barani Afrika ambapo amezaa jumla ya watoto 44 kwa mume mmoja, lakini hadi sasa watoto 38 pekee ndio wapo hai.

Akielezea hali hiyo alisema kuwa amekuwa akijifungua mapacha wengi mara kwa mara na hivyo kufanya idadi kubwa ya watoto, lakini kwa upande wake alitamani kuwa na watoto 6 pekee.

Mama huyo ambaye anaonekana bado ana uwezo wa kuzaaa watoto wengine amesema kuwa mara kadhaa amekwenda hospitali ili afunge uzazi lakini wataalamu wa afya wamemwambia kuwa ana mayai mengi na hivyo ni hatari kwa afya yake kufanya hivyo.

Watoto hao kwa siku moja hula 7kg za maharage, 24kg za unga, na 2.5kg za sukari.Wakati jamii ikihimizwa kuhusu masuala ya uzazi wa mpango ambao utawawezesha kuwa na watoto wachache ili waweze kumudu kuwapatia mahitaji muhimu ikiwamo elimu, malazi, mavazi na chakula, mwanamke mmoja nchini Uganda ameweka rekodi ya kuwa na watoto wengi zaidi.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 huenda ndiye mwenye watoto wengi zaidi barani Afrika ambapo amezaa jumla ya watoto 44 kwa mume mmoja, lakini hadi sasa watoto 38 pekee ndio wapo hai.

Akielezea hali hiyo alisema kuwa amekuwa akijifungua mapacha wengi mara kwa mara na hivyo kufanya idadi kubwa ya watoto, lakini kwa upande wake alitamani kuwa na watoto 6 pekee.

Mama huyo ambaye anaonekana bado ana uwezo wa kuzaaa watoto wengine amesema kuwa mara kadhaa amekwenda hospitali ili afunge uzazi lakini wataalamu wa afya wamemwambia kuwa ana mayai mengi na hivyo ni hatari kwa afya yake kufanya hivyo.

Watoto hao kwa siku moja hula 7kg za maharage, 24kg za unga, na 2.5kg za sukari.

screenshot-%3Ca%20href=

0fgjhs232qe4gflh1.4ac1d594%2B%25281%2529.jpg


=====

Bayyo said;
Mwacheni Mungu aitwe Mungu, ndivyo unavyoweza kusema.

Mwanamke mmoja nchini Uganda aitwaye Mariam (39) amezaa watoto 44, watoto 38 wakiwa hai. Madaktari wanasema bado ana uwezo wa kufyatua watoto wengine. Anaweza kuweka rekodi ya dunia kuwa mwanamke aliyezaa watoto wengi bila kutumia madawa/njia za kisasa kwenye kutafuta uzazi, tofauti na wenzetu wazungu.

Mwanamke huyo aliolewa akiwa mdogo akiwa na miaka 13, baada ya kulazimishwa na wazazi wake kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya mila na desturi za kiafrika. Amekuwa na kawaida ya kuzaa mapacha... mfano uzao wa kwanza alijifungua watoto 6, uzao wa pili watoto 5.

Amezaa watoto hao wote akiwa na MME moja.

MSOSI: kila siku unga debe kg 24, maharage kg 7, sukari 2.5kg, mikate mingi tu.

Analala au kupumzika masaa kama 4 au 5 kwa ajili ya kuhangaika na watoto wake, kwani mme wake hana time kutunza familia, sanasana mume alikuwa anampiga na kumtesa kama ilivyo wanaume wa kabila la wakurya, huku akimwita nguruwe kwa kuzaa watoto wengi badala ya kusaidiana kulea.

Cha kushangaza mwanaumme huyohuyo anapiga gemu pekupeku afu anamwita mkewe nguruwe,, wanaume tumwogope Mungu.

SHULE: Watoto wengi hawajaenda shule, ada ni shida sana.

UJUMBE WAKE: Anawaasa wazazi wasiwaoze watoto wao mapema kama ilivyofanyika kwake. Zaidi wanaume wawajibe kwenye familia zao. Lakini pia wanawake wasitelekeze au kutupa watoto.

MY TAKE: Huyu mwanamke anastahili tuzo. Kwanini huyo mwanamke asiingie kwenye kitabu cha rekodi ya dunia???

MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU.

Source: AZAM TV[/QUOTE]
 
Hata kama angeanza kuzaa ana mwaka mmoja bado hiyo idadi ni kubwa!

Maana kubeba mimba ni miezi tisa ambayo nikikaribisha naweza kusema ni sawa na mwaka mmoja!

Enewei sijaelewa tofauti ya umri wake na idadi ya watoto alionao
 
enewei sijaelewa tofauti ya umri wake na idadi ya watoto alionao
baba yake alikuwa na watoto 45, kwa wanawake wengi, ila alizaa wengi maana kila mimba ni mapacha sio chini ya wawili. Huyu mama inasemekana wengi ni mapasha tena wale watatu watatu, wanne au wawili... na hawana baba wa kueleweka wengi hawajawahi kuwaona baba zao
 
baba yake alikuwa na watoto45, kwa wanawake wengi, ila alizaa wengi maana kila mimba ni mapacha sio chini ya wawili. Huyu mama inasemekana wengi ni mapasha tena wale watatu watatu, wanne au wawili... na hawana baba wa kueleweka wengi hawajawahi kuwaona baba zao
alaa kama kuna hao twins na triplets nimeelewa sasa, ahsante mitale na midimu
 
Back
Top Bottom