Mama wa mkoani aliyejifanyia upasuaji na kumtoa mtoto tumboni

Sandiego

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
1,289
2,076
Sumbawanga:
Kama kuna ujasiri, alichofanya Joyce Kalinda (32) mkazi wa kitongoji cha kalya kata ya kirando wilaya ya nkasi mkoa wa rukwa cha kujifanyia upasuaji mwenyewe na kutoa mtoto tumboni

Mwanamke huyo ambaye huo ni uzazi wake wa nane pamoja na ndugu zake wamezungumza na gazeti la mwananchi walipokuwa wakisimulia jinsi tukio hilo lisilo la kawaida lilivyotokea

Siku ya tukio takribani saa kumi alfajiri Joyce alianza kuhisi uchungu akiwa anatokea nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mkunga wa jadi hivyo kuamua kwenda kituo cha afya kirando kwa ajili ya kujifungua lakini hakufanikiwa.

Licha ya kupokewa vizuri na muuguzi wa zamu, alipotakiwa kusubiri ili wenzake ambao walikuwa wametoka kujifungua wahudumiwe, aliinuka kitandani nakutoka nje ya wodi.
Ndugu zake aliokuwa ameambatana nao akiwamo wifi yake, Rosemary Sokoni walipomuhoji kuhusu kuwa nje ya wodi aliwajibu kuwa alikuwa anafanya mazoezi ili aweze kujifungua salama, lakini muda mfupi baada ya ndugu zake kuondoka nayewalitoroka

Akisimulia jinsi alivyootoroka na kufikia hatua ya kujifanyia upasuaji, Joyce alisema kwanza aliona mtu aliyevaa kitu kama kanzu na kofia hospitalini hapo akimuagiza "nenda kachukue wembe katika dishi uliokuwa umeuandaa kwa ajili ya kumkatia mtoto kitovu kisha lete " alifanya hivyo

Alidai kuwa mtu huyo alimshika mkono na kumwambia ''nifuate '' walitoka katika lango la kuingilia hospitalini na kuelekea nyumbani kwao umbali wa mita 250 kutoka kilipo kituo hicho.

Waliambatana na mtu huyo hadi nyumbani kwake na akiwa nje ya nyumba hiyo, alipewa maelekezo ya kuvua nguo zake na kujichana tumboni kuanzia chini kidogo ya kifua na kumtoa mtoto akiwa hai.

Anadai wakati akifanya tukio hilo hakusikia maumivu yoyote lakini baada ya kumtoa mtoto, ndipo akili zilpoanza kumjia, alimfunika mtoto kwa nguo zake.

Joyce anasimulia kuwa baada ya tukio hilo, ghafla mtu huyo alitoweka. Anasema kulipo pambazuka alipita mama mmoja ambae ni jirani yao aliyekuwa akienda kumwagilia bustani, na baada ya kumuona mama yule alimchukua na kumuingiza ndani ya nyumba yake huku akimtania ''wewe unapenda kujifungulia ndani ''

Baada ya mama huyo kuondoka, alimuagiza mtoto wake aitwae Lunus Sindani (12) kumuita shangazi yake ili aende kumsaidia kwa kuwa hali yake kiafya ilibadilika.

Anasema wakati akimsubiria wifi yake, alianza kurudishia baadhi ya vitu vya ndani vilivyokuwa vimetoka kama vile utumbo kwa kutumia mikono yake.

Baada ya kufika wifi yake Rosemary (27) alieleza alimkuta wifi yake akiwa amelala chali na mtoto akiwa mapajani na awali alifikiri kuwa alijifungua akiwa hapo nyumbani.

Alikwenda kwa mkunga wa jadi aliyepo jirani na alipofika mkunga huyo aliwaeleza kuwa tatizo hilo ni kubwa hivyo kutoa rai kuwa taarifa itolewe kwa mwenyekiti.

Baada ya taarifa watu walifika na kumchukua kwa machela iliyowekwa godoro hadi kituo cha afya. Wakati wote huo sehemu ya utumbo, mfuko wa uzazi, kondo la nyuma na mtoto vilikuwa nje na kitovu cha mtoto kilikuwa hakijakatwa.

Kaka wa mzazi huyo Amosi Mweupe (37) anasema alipokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa akihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Licha ya kusema kuwa yeye si msemaji Dk Gideon Edwin alidokeza kuwa walipambana kwa nafasi yao kuokoa maisha ya mama huyo na kwa hilo walifanikiwa.

Mganga mkuu wa Mkoa waRukwa Boniface Kasululu alisema hana uhakika kama mama huyo alipatwa na kichaa cha mimba wakati akisubiri kujifungua kwani walimpokea akiwa timamu.

Mkazi wa Kirando, Maufi Mzindakaya alisema tukio hilo ni la aina yake na lilisababisha shauku ya watu kutaka kumfahamu mwanamke huyo

Chanzo gazeti la mwananchi :
 
Eti akaanza kurudisha vitu vya ndani kama utumbo kwa kutumia mikono yake!!! Duhh!!

Yani kama sinema vile!
 
Uongo huu kujipasua mwenyewe unadhani rahisi..au mnajua mzazi anapasuliwaje.?

Kupasua kunaenda step by step ,layer kwa layer mpaka kufikia ndani.

Hii inaipusha kukata mishipa ya damu na mtu kupoteza damu hatimaye kufa.

Na wanalenga eneo husika..mfano kizazi wanalenga kule chini. Sasa huyu anasema kaambiwa anza kujikata kifuani kushuka chini haha.

Halafu kiwenmbe hakiko imara kukata mwili mnene wa mtu hadi kufika mbali ndani.
 
Juzi kuna mpuuzi mwingine huko nje yeye kamchelewesha mkewe hospitali matokeo yake kajifungua akiwa kwenye gari huku jamaa anapiga picha na kushare kwa mtandao kila hatua.

PUNBAVU SANA, KIZAZI HIKI.
 
Kuna watu ni majasiri sana tena sio mchezo kabisa, huyu mama na yule jamaa wa kusini aliyejikata kikojolea na kidole afu anahojiwa damu zinavuja yuko comfortable kashika na kipisi cha kikojoleo chake aiseee Mungu aliumba viumbe wake aisee
 
Back
Top Bottom