Majoja
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 612
- 186
Huwa siiachi kamera yangu popote ninapo kwenda.
Ni ajabu na kweli lakini mama mmoja wa kihaya huko Mbezi Jogoo ameamua kuhodhi njia mto kwa madai kuwa ni eneo lake na aliuziwa.
Ni vigumu kuelewa mantiki ya mama huyo kwani majirani walio karibu na eneo hilo wamemlalamikia vikali kuhusu uamuzi wake huo, kwa vile wakati wa mvua ni kawaida kupata mafuriko yanayopita kwa wingi juu ya daraja.
Lakini mama huyo hasikii la muadhini wala muumini kwani kafunga masikio.
Malalmiko yalipozidi akatoboa matundu mawili matatu (katika picha)ili kuruhusu mafuriko.
Majirani hao wanapanga kumuona Mama Tibaijuka, Waziri wa Ardhi(ambaye vile vile ni wa kwao na huyo mama) ili kuona uhalali wa mtu kuhodhi njia ya mto.