Mama wa Kambo, tujadiliane hili!

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
497
Jamani wapwa na mabinam,nisameheni kama nitakua nimewakata stimu zenu,maana wengi wanataka wakija hapa wasome vinavyohusu 'kule chini tu',hata hivyo matokeo ya kwenda chumvini,infii,kusoma plate number,sijui demu wangu anatoka maji na yote tunayojadili humu ni WATOTO!

Hii habari hapo chini nimeisoma juzi na nililia sana na nimekuwa nikimuwaza sana huyu mtoto hadi watu wangu wa karibu wamegundua sina furaha sababu sipati jibu kwa nini malaika wa Mungu kama huyu anyanyasike hivi?

Mim nawaomba wapwa tushauriane na tujadiliane ni jinsi gani tutasaidia kupunguza kunyanyasika kwa watoto kama huyu hapo chini sababu wao kama wao hawana uwezo wa kujisaidia lakini kwa vile hapa ni House of Great Thinkers nina amini tunaweza kupata ufumbuzi.

Kwangu mimi hili ni tatizo kubwa sana na linausononesha moyo wangu!

LOVE YOU ALL!​

hebu soma hii

Mtoto huyu anaitwa Hans ni mkazi wa Tabata hapa Dar,siku tatu zilizopita yalikumta makubwa kutoka kwa mama yake wa kambo anaeishinae.Hans alikuja hapa Dar toka mwezi wa tatu akitokea Morogoro kwa mama yake mzazi na kuja hapa Dar kwa baba yake mzazi kwa ajili ya shule na matunzo mengine.Hans kwa sasa ana miaka 9 tu na anasoma shule ya msingi Tabata.

Kama unavyomuona pichani Hans t shirt aliyovaa imetapakaa Damu...

Hans ana mawazo na sura yake haina matumaini ni kama mtu aliyekata tamaa.Wiki iliyopita Hans alitoka shule na shule ilikuwa imefunga akarudi nyumbani na ripoti yake ya mtihani akampa mama yake wa kambo.matokeo yake yalikuwa mazuri maana yupo 10 bora.Baada ya kuingia ndani akabadilisha nguo na akaenda kucheza na watoto wenzie.Baadae mama anamuita na kumfungia chumbani kilichofuata ni kipigo kwa madai kuwa ameiba heha.Hela ambayo Hans hajui ni tsh ngapi inayosemekana kaiba.

Alipigwa mpaka akang'atwa mikononi kama unavyomuona na kifuani,akapigwa mpaka na skuna kichwani na damu zikaanza kumtoka masikioni.Baada ya kupigwa sana majira ya saa moja jioni yule mama akamfukuza nyumbani na Hans akatoka nyumbani pasipokujua hata anakokwenda.
Wakati haya yakitokea baba mzazi hakuwepo,hivyo akaondoka nyumbani hapo kilichotokea majira ya saa nne usiku akaonekana Kipawa akiwa amelala kibarazani kwa mtu aliyetupa habari hii.Ndio kumuuliza kilichotokea na kusimulia yaliyompata mpaka kufika hapo.Ikabidi wamchukue wamlete Tabata ambapo yeye Hans hakuwahata akijua ni upande gani wa Tabata alichoshika ni shule anayosoma shule ya msingi Tabata.

Hapo pichani ni alama ya meno kifuani,basi wale walimuokota wakamripoti kwa wajumbe wawili wa eneo la Tabata nao wakamripoti polisi.Kesho yake ikabidi wampeleke shule ili iwe rahisi kuwapata wazazi wake.Kufika shule wakakutana na baba yake mzazi ambae nae alikuwa akimtafuta mwanae.Wajumbe wakamwambia baba inabidi twende polisi tulipotoa ripoti ya kumuokota huyu mtoto...basi walipofika polisi,polisi wakamuweka ndani yule baba wa mtoto wakamwambia mkewe akija pale kituoni ndio watamuachia na kumkamata mke wake kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya huyo mtoto.

Hapo pichani ni damu zilikuwa zinatoka sikioni na hapo zimeganda.
Hans anasema ni kawaida sana yeye kupigwa na huyo mama wa kambo na mara nyingi humng'ata.

Kichwani ni majeraha yaliyotokana na kupigwa na skuna....duuh yaani huyu mama sijui alikuwa kamdhamiria nini mwana wa mwenzie???!!!

Hans alipatiwa matibabu,mpaka sasa sijui kinaendelea nini tutafatilia halafu tutakwambia nini kilijiri baada ya hapo.
Thanks to Dina Marios
 
Asaidiwe akaripoti ustawi wa jamii, ngo's za haki za binadamu na wizara husika. Kwa kuanzia aende kwa WEO (ward executive office) kuna idara za mambo ya jamii. Hayo mambo yanatokea sana ila ukienda mbeze unasaidiwa
 
Pole zangu zote kwa huyu mtoto kwanza.

Swala la wazazi kuachana mara nyingi wanaoathirika ni watoto.Sisi wazazi inabidi tuwe waangalifu sana tunapofanya haya maamuzi na kama hakuna njia yoyote ya kutatua matatizo yetu ya ndoa zaidi kupeana talaka basi swala la watoto liwe la kwanza kujadiliwa.

Kweli sio wazazi wote wa kambo wana roho mbaya kwa watoto wao wa kambo lakini mara nyingi sio rahisi pia kwa wao kutoa mapenzi ya dhati kwa hawa watoto.Kabla hatujafanya maamuzi ya kuwakaribisha watoto wetu kuishi na mama/baba wa kambo tujaribu kushauriana kwanza ndani ya nyumba.Najua sio rahisi mwenzako kukukatilia usimlete mtoto wako kwa maneno lakini ni rahisi sana kukupa jibu la hapana kwa njia ya vitendo au wewe ukamsoma tu kwa kuangalia uso wake wakati mnajadiliana hili swala.

Tukishaona kwamba mwenzetu hana furaha huyu mtoto kuishi hapo ni vizuri tutafute hata ndugu wa karibu ambaye yuko tayari kukaa na mtoto wako kama mama/baba mzazi hana uwezo wa kukaa nae.mara nyingi huu mzigo wa watoto wetu huwa tunawatupia bibi/babu zetu, huko huwa wanapata mapenzi safi sana na kudekezwa juuu lakini sio wote tuliokuwa na bibi/babu ambao wako hai pia.

Ushauri wangu kwa wazazi wenzangu kabla hatujafanya kitendo au vitendo vyovyote ambavyo tunajua kinaweza kuharibu ndoa zetu au uhusiano wetu ni vizuri tukawafikiria watoto wetu kwanza.Mtoto anahitaji mapenzi ya wazazi wote wawili bila kuingiliwa au kuzidiwa na upande wowote ule hili kuapata malezi bora na misingi bora ya maisha.
 
Dah, ...imeniuma sana hii, huyo mama wa kambo anastahili kula mkong'oto mpaka atie adabu.
Na huyo baba'ke Hans siku zote hajajua machungu ya mwanawe? Jinga kabisa!
 
arsene ingawa we ni mpinzani wangu dimbani lakini hapa nakupa heko umeongea mambo ya maana sana...wazazi wa siku hizi too selfish wao wanajali ya kwao tu bila kuangalia mtoto atapata effects zipi kutokana na maamuzi yao! cheusi please mama naomba kama utaweza ufuatilie updates za huyu mwana kisha ututonye.....mapenzi yanaongelewa sana humu lakini ndo hayohayo yanaumiza watu wengine ambao ni very innocent...am so moved na story ya huyu mtoto....inshaallah mungu amtangulie
 
Inasikitisha sana na inauma sana...na ingependeza sana kama mtoa hoja angekuja na mapendekezo badala ya kutaka mjadala kwenye issue kama hii

a small change on the heading could make this thread thread touching
 
Dah, ...imeniuma sana hii, huyo mama wa kambo anastahili kula mkong'oto mpaka atie adabu.
Na huyo baba'ke Hans siku zote hajajua machungu ya mwanawe? Jinga kabisa!

Kuna taratibu na sheria! Kuchukua uamuzi mkononi is not clever!
 
duh hili mama ni lipompopo kweli
chuki ya nini sasa kwa mtoto
nyau kweli hili
 
Nilisoma hii hbr kwa Dina machozi yamenitoka aisee ss kuna hii nyingine mtoto ameponea chupuchupu kuibiwa jamni!! Mungu tusaidiee
 
Jamani wapwa na mabinam,nisameheni kama nitakua nimewakata stimu zenu,maana wengi wanataka wakija hapa wasome vinavyohusu 'kule chini tu',hata hivyo matokeo ya kwenda chumvini,infii,kusoma plate number,sijui demu wangu anatoka maji na yote tunayojadili humu ni WATOTO!

Hii habari hapo chini nimeisoma juzi na nililia sana na nimekuwa nikimuwaza sana huyu mtoto hadi watu wangu wa karibu wamegundua sina furaha sababu sipati jibu kwa nini malaika wa Mungu kama huyu anyanyasike hivi?

Mim nawaomba wapwa tushauriane na tujadiliane ni jinsi gani tutasaidia kupunguza kunyanyasika kwa watoto kama huyu hapo chini sababu wao kama wao hawana uwezo wa kujisaidia lakini kwa vile hapa ni House of Great Thinkers nina amini tunaweza kupata ufumbuzi.

Kwangu mimi hili ni tatizo kubwa sana na linausononesha moyo wangu!

LOVE YOU ALL!​

hebu soma hii

Mtoto huyu anaitwa Hans ni mkazi wa Tabata hapa Dar,siku tatu zilizopita yalikumta makubwa kutoka kwa mama yake wa kambo anaeishinae.Hans alikuja hapa Dar toka mwezi wa tatu akitokea Morogoro kwa mama yake mzazi na kuja hapa Dar kwa baba yake mzazi kwa ajili ya shule na matunzo mengine.Hans kwa sasa ana miaka 9 tu na anasoma shule ya msingi Tabata.

Kama unavyomuona pichani Hans t shirt aliyovaa imetapakaa Damu...

Hans ana mawazo na sura yake haina matumaini ni kama mtu aliyekata tamaa.Wiki iliyopita Hans alitoka shule na shule ilikuwa imefunga akarudi nyumbani na ripoti yake ya mtihani akampa mama yake wa kambo.matokeo yake yalikuwa mazuri maana yupo 10 bora.Baada ya kuingia ndani akabadilisha nguo na akaenda kucheza na watoto wenzie.Baadae mama anamuita na kumfungia chumbani kilichofuata ni kipigo kwa madai kuwa ameiba heha.Hela ambayo Hans hajui ni tsh ngapi inayosemekana kaiba.

Alipigwa mpaka akang'atwa mikononi kama unavyomuona na kifuani,akapigwa mpaka na skuna kichwani na damu zikaanza kumtoka masikioni.Baada ya kupigwa sana majira ya saa moja jioni yule mama akamfukuza nyumbani na Hans akatoka nyumbani pasipokujua hata anakokwenda.
Wakati haya yakitokea baba mzazi hakuwepo,hivyo akaondoka nyumbani hapo kilichotokea majira ya saa nne usiku akaonekana Kipawa akiwa amelala kibarazani kwa mtu aliyetupa habari hii.Ndio kumuuliza kilichotokea na kusimulia yaliyompata mpaka kufika hapo.Ikabidi wamchukue wamlete Tabata ambapo yeye Hans hakuwahata akijua ni upande gani wa Tabata alichoshika ni shule anayosoma shule ya msingi Tabata.

Hapo pichani ni alama ya meno kifuani,basi wale walimuokota wakamripoti kwa wajumbe wawili wa eneo la Tabata nao wakamripoti polisi.Kesho yake ikabidi wampeleke shule ili iwe rahisi kuwapata wazazi wake.Kufika shule wakakutana na baba yake mzazi ambae nae alikuwa akimtafuta mwanae.Wajumbe wakamwambia baba inabidi twende polisi tulipotoa ripoti ya kumuokota huyu mtoto...basi walipofika polisi,polisi wakamuweka ndani yule baba wa mtoto wakamwambia mkewe akija pale kituoni ndio watamuachia na kumkamata mke wake kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya huyo mtoto.

Hapo pichani ni damu zilikuwa zinatoka sikioni na hapo zimeganda.
Hans anasema ni kawaida sana yeye kupigwa na huyo mama wa kambo na mara nyingi humng'ata.

Kichwani ni majeraha yaliyotokana na kupigwa na skuna....duuh yaani huyu mama sijui alikuwa kamdhamiria nini mwana wa mwenzie???!!!

Hans alipatiwa matibabu,mpaka sasa sijui kinaendelea nini tutafatilia halafu tutakwambia nini kilijiri baada ya hapo.
Thanks to Dina Marios

Straight legal action should be taken for assault,inflict of body injury of minor pia deprive of right to live in good condition(child is living in dangerous enviroment)in which at the end of the day that child will be effected physcological in all of his life.
 
Sidhani,lazima baba atakuwa amefunguka macho.

amechelewa, nusura akute kaput. Japo ni usumbufu nivema kama akina baba mkitoka kwenye ze bingwa muwe munachungulia watoto wamelalaje/wameshindaje.
 
Ukiona hivyo hilo jimama lina historia nzito ya kuporomosha mimba kienyeji, kwa hiyo limeshakuwa ligumba na lina roho sugu ya mauaji kuliko askari wa kivita!

Mi kwa mtazamo wangu hapo, kosa kubwa lipo kwa baba, maana sikuona sbb ya yeye kumleta mwanae hapo nyumbani hali a kuwa anafahamu fika kuwa anafuga jinamizi, angeweza kumsomesha na kumtunza mwanae hata akiwa huko huko Moro.

Suluhisho la kesi km hii, huyo jinamizi wa kike awajibishwe na sheria, na ikiwezekana km huo baba anampenda mwanae kweli basi amtwange talaka 8 tena barabarani mbele ya mjumbe na mashahidi wote, na asipewe hata nafasi ya kurudia chochote nyumbani, huyo ni shetani la mguu mmoja!

Machozi yananitoka bila kujua, inauma sana!
 
Back
Top Bottom